Eeeeh banaa wee tayari umeshajiunga mara!... haya na Mzee Mwanakijiji yumo au?
Halafu masuala ya majimbo nyinyi mnasemaje?
Mahakama ya kadhi??
Sera yenu ya ardhi na mikataba ya madini ipo vipi?
Rev.
Ok mkuu wangu unaweza nambia tofauti inayowatenganisha mrengo wa TTTP na mirengo mingine (kushoto na Kulia) hasa inapokuja ktk maswala ya jamii..what are the Values, Athics kwani wataalam husema:- In civilized life, law floats in a sea of ethics. Each is indispensable to civilization. Without law, we should be at the mercy of the least scrupulous; without ethics, law could not exist.
Kwa hiyo ni lazima ukanyage nyayo za watu hapa..
Una tafsiri vipi Uzawa, Ushoga, maswala ya ndoa, mirathi, haki za kuabudu..Ni kwa kiwango kipi kwa sababu hadi leo huwa nashindwa sana na ile haki ya watu kuabudu dini waitakayo..mathlan, Je naweza kuabudu dini ya kiasili inayo lenga imani ya mizimu na Uchawi!
Tutafafanua na kuelezea sera zetu kadiri tunavyo nakshanaksha na kukamilisha hatua za usajili. Mengi yaliyo kwenye misimamo yetu hayatofautiana na mengi yenye msingi wa kutumikia Tanzania na kwa manufaa ya Watananzania mliyoyasoma hapa jamvini. Maswali ya sera tungelipenda kuyajibu kwa kirefu ili kupunguza ambiguity maana ni maswala nyeti.
Katika mfumo bora wa kiutawala, Sheria lazima zifuatwe na Wananchi na wanaotunga Sheria na dhamana ya kutunga Sheria ni lazima wafanye kazi kwa kutimiza wajibu na majukumu yao.
Kilichotokea Tanzania ni kuvunjwa kwa Sheria na Wananchi wake na kukosekana kwa kuwajibika kwa waliopewa dhamana ya kulinda na kuhakikisha kuwa Sheria na Kanuni zinafuatwa.
PPTL katika safari yake ya kujenga Taifa, itahakikisha kuwa Sheria, Kanuni na Katiba ndio dira za nchi na si utashi wa mtu mmoja mmoja au vikundi maalum.
Hivyo, kabla ya kuanza kushughulikia ipaswavyo yaliyopita ya kuhujumu nchi, kazi ya kwanza itakuwa ni kuhakikisha kuwa Sheria, Kanuni na Katiba zinafanya kazi kwa haki na zinavyopaswa, bila kuteterekea kutokana na msukumo wa kisiasa, hujuma au namna yoyote ile ambayo lengo ni kutafuta mianya ya kukiuka Sheria, Kanuni na Katiba.
Kisha kwa ridhaa na dhamana ambayo PPTL imepewa, PPTL itafuatilia kwa kutumia kitana kila kitu kinachogusa uchumi wa Tanzania kuwa kuangalia mapengo na matatizo yaliyotokea na kuhakikisha hatua madhubuti zinachukuliwa kuziba mianya ya kuhujumu nchi na hatua kali za kisheria na kikatiba zitachukuliwa dhidi ya yeyote yule ambaye amevunja sheria, kanuni na kukiuka Katiba.
Hivyo kwa mifano hiyo mitatu, naamini kuwepo kwa mfumo bora na uongozi imara, PPTL itaweza kutatua matatizo ya kale na yajayo kwa kuyafanyia kazi na kutoa maamuzi ya haki kwa kutumia Sheria, kanuni na muongozo wa Kikatiba.
Lakini tusifanye Utani wakuu zangu hii ya Rev kweli imekaa sawa?
Kwa nini mkuu wangu usijiunge na chama fulani kisha toka humo ukakua kisiasa kabla hutafikia maamuzi kama haya. Kuanzisha chama kipya inachukua nguvu kubwa sana tena fedha nyingi sana unaweza kufilisika kabisaaa kuwavuta maskini wenye njaa.
Mchungaji heshima mbele. Kwanza nakupongeza kwa uamuzi wako huo. We need more people who actually dare to walk the walk rather than talk the talk. i want to come up with some constructive words to help you and your new party so please allow me to sleep on it. Very soon I will come with my advice and suggestions.
Eeeeh banaa wee tayari umeshajiunga mara!... haya na Mzee Mwanakijiji yumo au?
jina linaloeleweka na mass ni advantage...
umeuliza swali la msingi sana. Hata hivyo naomba uwe na subira kidogo, ni mengi kuelezea na ni mengi tunajiandaa nayo. Swali lako linajibika, ila ni vyema kama litajibiwa kirefu ili kuondoa mwanya wa kutokuelewa. Mwenyekiti bado anajibu maswali ya wadau wengine mbalimbali waliotangulia kuuliza. Ahsante.
kuwa mwanzilishi si lazima niwe na kadi namba moja, yangu inaweza kuwa namba 1000 na pasiwe na tofauti yeyote.
Kwa heshima ya yeye na wowote watakaojitolea na kuamua kujiunga nami, basi watapata hizo nambari ambazo zitaonyesha kukuwa kwetu na kuwepo kwa demokrasia.
Mambo ya kujivunia kuwa mimi mwanzilishi, sijui kadi yangu ndiyo ya asili hayana manufaa ikiwa wale wanaojiunga kwa utashi na hiyari yao hawatapewa thamani na kujiona kuwa ni washiriki wakuu katika ujenzi wa chama na wa nchi!
Kwa mimi kutoa kadi ya kwanza kwa mtu wa kwanza kutamka rasmi anajiunga nami, ni heshima na kumwezesha huyu aliyeunganisha nguvu na mawazo yake na yangu atambue kuwa wote tuna nafasi sawa kutimiza umoja wa lengo letu.
Ya fikra sahihi, sijui mwenyekiti mwanzilishi au utukuzo usio na tija hauko katika moyo wangu na si na haitakuwa staha na mwelekeo wa chama chetu cha pppt.
Jina sio tatizo, watu wako result oriented, wanataka mabadiliko kwenda kwenye nchi ya ahadi. Kwao jina halitatui matatizo yao hata kidogo, ila matatizo ni mtazamo na malengo ya kweli ya chama. Mbona wananchi hao hao wanatamka majina magumu ya dawa eg klorofeniko ni kwa sababu dawa hio inawasaidia, hawataweza kusahau PPPT, kitu kinachokusaidia sawa na chama hicho wananchi hawawezi kusahau.
Siasa siziwezi mkuu.. mimi domo kaya tu, ni mmoja wa Watanzania waumini tunaosubiri Nabii!
Hapana mkuu wangu nitakwambia kitu kimoja, huko kwetu ukiwa unatembea usiku wa manane basi unajifanya kuimba kwa sauti kubwa ili mradi kuondoa woga..Kma mlevi vile, lakini ukiona Unyasi tu kutikisika unatoka timu ukifikiria nyoka..Ndo huyu ameletwa kutupeleka kwenye nchi ya ahadi, lakini makandara, domo kaya nayo ni sehemu ya siasa
Hapana mkuu wangu nitakwambia kitu kimoja, huko kwetu ukiwa unatembea usiku wa manane basi unajifanya kuimba kwa sauti kubwa ili mradi kuondoa woga..Kma mlevi vile, lakini ukiona Unyasi tu kutikisika unatoka timu ukifikiria nyoka..
Ndio mimi navyoziogopa Siasa za Bongo!
Mkuu wangu kwanza mnabidi mfikirie Watanzania walio wengi.. Huyo mama yangu mkulima nikimwambia Progressive People's Party of Tanzania, atauliza eeeh ndio nini hiyo Pogolesivu!..kaazi mpya!
Wakuu wapo wengi sana, jaribuni pia kutumia jina la kiswahili amini maneno yangu mna deal na Wadanganyika!