Profesa Magembe aanza kupingwa!

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,617
Kauli ya waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi kuwa vijana wanaomaliza darasa la saba wataendelea moja kwa moja na kidato cha kwanza bila mchujo wa mtihani mara tu CCM ikipewa ridhaa mwaka huu imepatiwa changamoto na makundi mbalimbali katika jamii.Walimu na wanaharakati wameionya serikali kuacha kufanya majaribio kwenye elimu.
1. Mfumo huo utawagawa wanafunzi katika tabaka tawala na tabaka tawaliwa.
2. Mfumo huo utapunguza ushindani wa kitaaluma na kupunguza wataalam nchini.
3. Utafiti wa kina Rakesh unaonyesha kuwa nusu ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hawawezi kusoma na kuandika hivyo ni bora mfumo wa sasa ukabireshwa kuliko kukurupukia mfumo huo wa Magembe.
 
Its too sad, prof mzima anakurupuka bila kutafakari, wakati wanafunzi kibao hawawezi hata kusoma. Achilia mbali wanaojua kusoma lakini wengi ni vichwa tupu kabisa kabisa, hakuna mwamko wa kujisomea vitabu hata wanaokuwa busy wanakuwa busy kukariri midude ya ajabu ajabu. ukitunga mtihani toka studio mtu achomoki inakuwa kilio.
 
hiyo yote ni uchu wa madaraka ambao utasababisha elimu duni kwa watanzania
 
Jamani hawa kina BORA LIENDE hebu wakae pembeni kwanza waachie watu wenye utaalamu wa kutafiti mambo. Huyo mzee MKURUPUKO si wote mnamjua. unajua hapa bongo tunao MAPROFESA WA MAFISADI. msiumize vichwa trh. 31/ tutapanga elimu bora zaidi siyo maneno ya MZEE MKURUPUKO.
 
Hii Majembe naomna imepotea njia, si kwaajili ya shamba imeingiaje kwenye utawala wa elimu!
 
Kauli mbiu ya kweli ya Dr Slaa kuhusu elimu ya bure ndiyo chanzo cha kuweweseka kwa bwana Magembhe-si hiyo tu vilevile tumeona mkanganyiko mwingine kuhusu bei ya cement. Wenzetu walikuwa wapi?. Mwenye macho haambiwi tazama! watanzania tuamke
 
Hapa hakuna Prof. Hizi ni zile za kununua hizi...na sina hakika kama alithibitisha vyeti vyake kufuatia kashfa ya "Mafisadi wa Eimu-Msemakweli" Huyu ni professor wa wapi mjinga kiasi hiki, anayeweza kukurupuka na kuongea utumbo tuuuuuuuuuuu bila hata chembe ya kufikiri. Wawadanganye wana sisiem wenzao waliofilisika fikra, mawazo na uwezo wa kufikiri.....My word! Nitabaki kuwa M-Tanzania na raia wa nchi hii so long Dr.Slaa awe rais, otherwise bora nikaombe urai Chile.
 
kauli mbiu ya kweli ya dr slaa kuhusu elimu ya bure ndiyo chanzo cha kuweweseka kwa bwana magembhe-si hiyo tu vilevile tumeona mkanganyiko mwingine kuhusu bei ya cement. Wenzetu walikuwa wapi?. Mwenye macho haambiwi tazama! Watanzania tuamke
nashangaa tbc sijui wanaongea nini, wanazungumzia nauli ya kusafilishia badala ya kuzungumzia kwenye kuzalisha kama dr anavyosema, ninachoona ccm wanajikanyaga saana kweli kishindo cha kuanguka mti mkubwa tunakiona!
 
Kauli mbiu ya kweli ya Dr Slaa kuhusu elimu ya bure ndiyo chanzo cha kuweweseka kwa bwana Magembhe-si hiyo tu vilevile tumeona mkanganyiko mwingine kuhusu bei ya cement. Wenzetu walikuwa wapi?. Mwenye macho haambiwi tazama! watanzania tuamke
Sure....hawa ni watu wa kudesa na kuvuruga!
Huu mpango tuukatae, nia yake ni kuonyesha watu kuwa wanashughulika kwenye elimu, kumbe ni kuangamiza taifa!
 
Sure....hawa ni watu wa kudesa na kuvuruga!
Huu mpango tuukatae, nia yake ni kuonyesha watu kuwa wanashughulika kwenye elimu, kumbe ni kuangamiza taifa!

Na nadhani haijatosha kiasi amnacho kimechakachuliwa na mh mungai kwenye elimu sasa hivi ndo wanataka kuharibu zaidi....

Hivi kila mtu ana uwezo wa kusoma hadi form IV?
 
sijawahi ona WAZIRI wa elimu bogus kama huyu. alinunua u proff wake nini huyu grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Ninajiuliza sana juu ya hili na jibu ninalolipata ni kwamba haliwezekani isipokuwa ni mbinu ya kudanganya wapiga kura kwamba watawala wanalifanyia kazi suala la elimu.Hivi ni kweli Tanzania tuna madarasa na nyenzo nyinginezo za kuweza kuchukua wanafunzi wote wanaomaliza darasa la saba?Kwa uelewa wangu nadhani hatuna.Na kwa nini hili lisemwe wiki hii ya mwisho ya uchaguzi?Walikuwa wapi hawa siku zote?Nadhani sera za Dr.Slaa zinaanza kuchakachuliwa taratibu!!
 
Prof. huyu ameiba ki aina sera ya CHADEMA ila akaichakachua kisanii kwa mtindo wa bora liende tupate kura kwanza.
Wanacho taka hapa ni kupata kura hata ikiwabidi kudanganya wananchi ila mambo mengine watarekebisha mbele kwa mbele hata kama mpango wenyewe hautafanikiwa.

Hivi jiulize kwa nini huu mpango unakuja kipindi hiki ambacho CCM maji yako shingoni, pia jiulize ni kwa nini hata kwenye mpango wa badget ya wizara ya elimu ya mwaka 2010/2011 hilo halipo kabisa wala kutajwa sehemu yoyote.

Hizi ni kauli za mfa Maji na DAWA YAKE HUYU NI KUWAZAMISHA KWA NGUVU YA KURA ZETU TAREHE 31/10/2010

CHADEMA HOYEEEEEEEEEEEEE
 
Mankind will never see an end of trouble until... lovers of wisdom come to hold political power, or the holders of power... become lovers of wisdom. ~

Plato, The Republic
 
Wanajf juzi nilimsikia prof maghembe akisema serikali itafuta mitihani ya darasa la saba, mi kwa upande wangu naona sasa serikali inazika elimu yetu na ndio wanazalishwa vilaza, majambazi na machangudoa nchini na ndio kwanza tunazidi kushusha dhamani ya elimu yetu kimataifa. Mi najiuliza kuna mwanafunzi anayesoma bila mitihani? Kama kusingekuwa na mitihani hata yeye maghembe asingekuwa hapo alipo kwani alisoma kwa bidii ili afaulu na kujua mambo na sasa ni prof, naanza kuwa na wasiwasi na uprof wake kwa hili.

Tuliharibu elimu yetu wakati wa mungai kwa kubadili mitaala na sasa linakuja lingine la kuondoa mitihani ya maana kama ya darasa la saba,zamani tulikuwa tunapiga paper kuanzia darasa la nne, saba, form two na form four na ukifeli huendelei na kidato au darasa la juu, na watu hao ndio wanaendesha nchi mpaka sasa.NINA WASIWASI MTATOA MITIHANI YA FORM 4,FORM 6 NA VYUO NYINYI MAANA AKILI ZENU NI MGANDO.

Hili swala la kuwa elimu ya umuhimu iwe form four ni nzuri ila si kwa kisai hiki cha kuburuza watoto hata kama uwezo hawana, hivi tutazalisha aina gani ya wataalamu au watanzania, na je tutaweza kweli kupambana na soko huria la elimu la afrika mashariki?Mi sijui nchi hii watendaji wake wanatumia nini kufikiria.dr slaa chukua nchi maana sasa tunapotea live.

DAWA YA KUNYANYUA ELIMU SIO KUONDOA MITIHANI ILA NI KUBORESHA ELIMU KWA KUWA NA WALIMU WAZURI NA KUWAPATIA VYENZO NZURI ZA KAZI NA MISHAHARA MIZURI, VITABU VYA KIADA NA ZIADA, MAABARA ZA KUTOSHA MASHULENI NA KUBORESHA SHULE ILI WANAFUNZI WASOME KATIKA MAZINGIRA BORA N.K.
 
hivi hata ukimwangalia alivyokaa kama ana mtindio wa ubongo vile!!
kuna watoto hawana uwezo wa kusoma/kuandika unawapeleka vipi huko?
 
maghembe ni umbumbu au msukumo wa wakubwa, kwanini mnawakosea watz heshima kiasi hicho km alivyosema mbunge pale mwembeyanga?....kwweli kwa uamuzi huu ambao hata wewe maghembe hutapelaka mtoto wako afuate huo mtaala una maana gani?..........hii nchi anatakiwa mtu mmoja tu kutukombo kutoka fikra na akili mgando za ccm yaani DR.SLAA
 
Hii kauli inakasirisha sana Prof unatakiwa kupembua mambo kwanza, kwani kuna watu kibao wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika, na hawa wataendelea na elimu ya sekondari kama hakuna mchujo? je ni shule hizo hizo za msingi zitatumika au ni hizi za kata wanazojenga? je walimu wapi watafundisha hayo masomo ya sekondari kwa wanafunzi wote au ni walewale wa Ualimu pasipo Elimu? Chichiemu acheni kukopy kama hamjui kupaste
 
Back
Top Bottom