Prof. Mwandosya azidi kuikoroga CCM aandika kitabu kuelezea rafu na rushwa ndani ya chama

Hivi una elimu gani?
Darasa la Nne la mkoloni "equivalent to Form 4" uliyohitimu wewe katika shule ya kata. Tofauti yetu ni kuwa mimi sijawahi kuchonga kinyago cha kukiabudu kama ulivyofanya wewe na mafisadi unao washabikia na kuwa abudu!
 
Profesa sasa kachoka kuishi ngoja Jack Zoka aagize vijana wake waongeze dozi ya ile sumu waliyomlambisha mara ya kwanza akanusurika.
 
Je yeye hakuwa sehemu ya hizo siasa za rafu na rushwa? Je angeshinda uchaguzi wa kumtafuta mgombea wa CCM 2005 leo hii angesema haya? Na je kama mwanaCCM amechukua hatua gani kuhusu tatizo hilo? Maana bado ni waziri kwenye serikali hiyo hiyo iliyoingia madarakani kwa siasa hizo hizo.

Nadhani hatua ndiyo hiyo kuandika kitabu hicho! hata nyerere aliandika kitabu cha kukosoa! hebu fikili vizuri maana umezuka tu na mawazo mepesiiii!
 
CCM kunarafu usiombe kuanzia ya pesa hadi ya ***no. tujikumbushe yaliyo tokea kule kawe kwenyeule uchaguzi wa matawi. Sijamsikia Nepi akisema au akitoa kauli yoyote.
Udhaifu ule ule
..Mkuu hebu tukumbushie kidogo ilikuwaje Kawe vie?
 
Kama nacho hiki ni kitabu cha proffesor. Basi hatuna proff nchi hii....mfano haya moja analaumu katibu wa kijiji hakwenda kula chakula baada ya kumaliza msiba wa Mwasanduku
 
Huyu professor wa electrical engineering. Bora hata angeandika kuhusu 'conservation of charge and energy in electrical circuits'
Level ya UDr. (Wa kusomea) na uprofessa wa kitaaluma ni kuwa na uwezo wa kuchanganua mambo katika nyaja mbalimbali za maisha ya binadamu. Ukikuta professa amefocus tu kwenye taaluma. basi huyo ni professa wa madesa tu na hao kwa kweli ni wachache sana.
 
je aliki-edit kitabu na kuongezea ya Dr Uli? au hiyo itakuwepo kwenye secind edition?
 
pole mwandosya. anayekataroho asemi uongo naamini uloaandika ni kweli mtupu ntakitafuta ntakisoma na ntaiishi msalimie mwalim
 
mwana JF unapoleta good nyuzi kama hii ya kitabu alichoandika Mc ni safi sana ,ili kuna ka kona kadogo tu umetuacha uchi ni wapi kinapatikana bana tupe hii kitu
 
He wants to put the records straight...things aren't the way we look at them. As a professor, the only way to communicate is to put the writings for generations to know what really transpired when he was involved in politics.

Well said,msomi ni msomi bwana.
 
Je yeye hakuwa sehemu ya hizo siasa za rafu na rushwa? Je angeshinda uchaguzi wa kumtafuta mgombea wa CCM 2005 leo hii angesema haya? Na je kama mwanaCCM amechukua hatua gani kuhusu tatizo hilo? Maana bado ni waziri kwenye serikali hiyo hiyo iliyoingia madarakani kwa siasa hizo hizo.

Hatua aliyo chukua ndiyo hiyo kaka! Jee wewe umechukua hatua gani? Ulitaka ajilipue au?
 
Nadhani hatua ndiyo hiyo kuandika kitabu hicho! hata nyerere aliandika kitabu cha kukosoa! hebu fikili vizuri maana umezuka tu na mawazo mepesiiii!

Wewe ndiyo ufikirie vizuri mkuu. Kama ameyaona hayo kwa nini bado yuko kwenye serikali ya CCM? Kwa nini asijiuzulu uwaziri na badala yake anaendelea kutumikia serikali hiyo hiyo iliyoingia kwa siasa hizo hizo? Nyerere aliandika kitabu cha kukosoa baada ya kuondoka serikalini je usingeshangaa raisi wa nchi aandike kitabu cha kuikosoa serikali anayoiongoza? Mawazo yako ni "mepesiiii" mkuu. Jipange upya ndiyo ujibu hoja yangu.
 
Hatua aliyo chukua ndiyo hiyo kaka! Jee wewe umechukua hatua gani? Ulitaka ajilipue au?
Mnasahau kuwa yeye bado ni waziri wa serikali iliyoingia madarakani kwa siasa hizo hizo anazo zikemea? Mimi hatua niliyo chukua ni kutokua part ya hiyo system anayo lalamikia. Je wewe?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom