Kirode
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 3,566
- 82
Mabwepande kwetu...
Title ya kitabu?
Title ya kitabu?
wewe ndiyo ufikirie vizuri mkuu. Kama ameyaona hayo kwa nini bado yuko kwenye serikali ya ccm? Kwa nini asijiuzulu uwaziri na badala yake anaendelea kutumikia serikali hiyo hiyo iliyoingia kwa siasa hizo hizo? Nyerere aliandika kitabu cha kukosoa baada ya kuondoka serikalini je usingeshangaa raisi wa nchi aandike kitabu cha kuikosoa serikali anayoiongoza? Mawazo yako ni "mepesiiii" mkuu. Jipange upya ndiyo ujibu hoja yangu.
wewe mzee umekalia kupiga kelele tu kwenye jamiiforums hata huelewi unacho andika kwani tatizo ni serikali au chama chao? Kama alitoka serikalini mbona alikua bado ccm? Hamna ulicho andika hapo hujui hata tatizo la nchi yako nini!kwa taarifa yako tatizo ni ccm! Chama legelege huzaa serikali legelege!HIYO NDIYO TUITION NIMEKUPA YA BURE!
Je yeye hakuwa sehemu ya hizo siasa za rafu na rushwa? Je angeshinda uchaguzi wa kumtafuta mgombea wa CCM 2005 leo hii angesema haya? Na je kama mwanaCCM amechukua hatua gani kuhusu tatizo hilo? Maana bado ni waziri kwenye serikali hiyo hiyo iliyoingia madarakani kwa siasa hizo hizo.
Hivi huwa una proof read kabla ya kusoma? Nimesema bado anatumikia serikali hiyo hiyo ambayo imeingia madarakani kwa siasa anazo zipinga. Sasa hiyo serikali imeundwa na chama gani? Do you think my friend? Utatofautishaje CCM na serikali wakati saa nyingine hata kabla ya maamuzi kufanywa na serikali wanajadili kwenye vikao vya chama? Tatizo unasema ni CCM fine no problem sasa serikali ni ya chama gani? INABIDI UJIPE MWENYEWE HIYO TUITION YA BURE