Inafika kipindi tuache kuilamu sana serikali na tuangalie jamii zetu. Kuna watanzania wengi hapa USA ni mameneja wa Subways, Mac Donald na mambo mengine.
Ukipima ufanisi wao unaona wanafanya kazi nzuri sana. Lakini kwa nafasi hizohizo wakipewa nafasi Tanzania watavurunda na kuboronga.
Huyu Professor ameweza kufanya vizuri nje ya nchi kwa sababu katika nchi za watu, wanataka waone kazi yako na ukishindwa wanampa mtu mwingine, Hivyo kuna check and balance ya kuona kazi yao imefanyika.
Lakini huyuhuyu professor angefanya kazi bongo basi angetaka pesa anazopewa kufanyia research ajengee nyumba kwao, awe na vimada watatu na ampe kazi ya maabara ndugu yake alifeli kidato cha nne.
Kwa maoni yangu, watanzania na waafrika wengi wakifanya kazi nje ya nchi zao wanajaribu kuwa responsible lakini wakiwa kwenye nchi zao porojo nyingi.
Tamati
Kwa ninavyomfahamu mimi Prof. Mshigheni ni mtu asiye na tamaa, yeye kani ni kazi tu. Na anapenda sana maendeleo na kusaidia watu. Akipewa nafasi atafanya makubwa mengi.