Prof.Mshigeni: Namibia wanamuenzi, Tanzania haimtambui!!

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
wana JamiiForums,

..nimevutiwa sana na hii article kuhusu Dr.Keto Mshigeni.

..mchango wake ktk utafiti wa Marine Biology unatambulika dunia nzima.

..kazi aliyoifanya kama Vice Chancellor Univ of Namibia ni ya kupigiwa mfano.

..wa-Tanzania tuna underutilize vipaji vya wasomi wetu. Keto Mshigeni ni mfano mmoja wapo.

Kiangiosekazi Wa-Nyoka said:
MSHIGENI HONOURED THIS WEEK

A PERSON who does not know the inside of the Vice-Chancellor of the Dar es Salaam-based Hubert Kairuki Memorial University, Professor Keto Mshigeni, will consider him very lucky. I do not.

All the glamour he gets is meritorious. Some years ago he was invited the Founding President of Namibia, Dr Sam Nujoma, and spent his holidays with him at Hanties Bay, our skeleton shores of Atlantic Ocean. They lived in a lavish sea resort where pensioners, who have funds, spend some time before they join their ancestors.

Dr Nujoma invited Professor Mshigeni in recognition of his great work to the Namibian people; his contribution to the founding of Namibia’s highest institution of learning . He was Pro-Vice Chancellor of the Namibian University (UNAM) for more than ten years. Actually he was the founding Pro-Vice Chancellor of UNAM.

Prof. Mshigeni did a great job in creating and making this tertiary institution one of the best 20 universities in Africa. He pulled in the best academics from all over the world, recruiting --- naturally --- the fellows he knew very well to be serious workers. At one time he had more than ten professors from East Africa.

And not by coincidence but by academic excellence, when he left for Tanzania he was replaced, albeit briefly by another Tanzanian Pro-Vice Chancellor Prof. Geoffrey Kiangi. The latter was replaced by another Tanzanian, Prof. Osmund Mwandemele.

Professor Mshigeni left Namibia in 2006, but he has twice been invited in recognition of his work.

He is a respected man here and he is here with us this week at the invitation of Namibians for further recognition. Besides Namibian honours he was awarded the UN’s Boutros Boutros Ghali award in 1994. He is accompanied by his wife Grace Mshigeni.

One of the prominent halls of the Sam Nujoma Marine and Coastal Resources Research Centre has been named after him. It is called Prof Keto E. Mshigeni Mariculture Research Complex. When he saw it he said: “It is a kind of a complex I have never seen in Africa.”

The biblical adage: A prophet is never recognized in his own country. Tanzanians are admired for their work beyond Tanzania’s borders. At home?

Prof Mshigeni hails from Mamba, Same, Kilimnjaro Region. He is seen as a broad-minded scientist, author of over 150 scholarly papers, covering many themes, including marine and fresh water agae, edible and medicinal mushroom.

He is one of the founders of the Tanzania’s modern seaweed industry. He met his mentor, Professor Erick Jaasund, at the University of Dar es Salaam, who made him developed a special interest in seaweeds.

Mshigeni realised that Tanzanian coastal village communities exported species of seaweed genus Eucheuma to France, Denmark and United Kingdom, where products were boiled for a gel (carrageenan) that has a wide range of industrial applications.

He won a Rockefeller Foundation Scholarship in 1970, went to University of Hawii for his PhD on Hypnea, a seaweed genus whose species are found in both Hawaii and Tanzania. His findings and their publication led to being promoted to a full professor at the University of Dar es Salaam.

In the citation here we were told Prof Mshigeni is one of the new breed of African scientists. He has created work for Africa’s subsistence farmers. His work has enabled the emerging of the new mushrooms and seaweed industry, creating jobs for unemployed women in East and West Africa.

We were told seaweed is used in pharmaceutical and food products, including yogurt, shaving cream and ice-cream. In Zanzibar, 40,000 women are doing seaweed farming because the crop is sustainable. In the last 10 years, Tanzania is said to have earne 20 million US dollars annually in exports of seaweed. Optimists says Professor Mshigeni’s work will soon help coastal communities in all of Africa.

Tanzanians and Namibians are waiting to receive Prime Minister Mizengo on Monday. The premier should rest assured that Tanzanians in here are good ambassadors of our Motherland. A good example has been Professor Mshigeni.

Enjoy your Otjesomething.

kiangiosekazi@yahoo.com nyoka2006@hotmmail.com
 
......aisee jokakuu.......Prof Mshigeni ni moto wa kuotea mbali ktk field yake......nilipata kuhudhuria conference moja ya Mazingira ya marine........nilimkubali.......

wapo wengi tu wa kuenziwa.....kuna akina Erasto Mpemba katika field ya thermodynamics and the list goes on.......ndio hivyo ndg yangu........tatizo hawa vipanga wetu wakishaingia ktk system zetu mbovu zilizochanganywa na siasa wanaharibikiwa kabisa...............ndio maana watu kama akina Prof Kichuguu, wewe na wengi tu hapa JF wapo huko waliko
 
But, why do you say he is not being honoured in Tanzania? Don't you know that in Africa, and in Tanzania in particular,academics are not honoured, they honour themselves?

My friend, in Africa it is the politicians who are honoured. If you want recognition in Africa, go into politics, become a cadre of certain governing party and you will be honoured instantly!
 
Ndiye mwenye usemi niliouweka hapo chini...Hivyo mimi tayari namuenzi Profesa Mshigheni.
Wataalam wengi tu walihamia Namibia na Botwsana na wengine nchi za magharibi na Taifa likabakiwa na Mafisadi peke yake huku wakiwa na wananchi wajinga na masikini wenye hazina za kila aina za kifikra na material.
 
Na tatizo viongozi wetu wamekaa wala hawajui jinsi ya kuwatumia watalaamu kama hawa, kila siku tunaishia kupiga ramli tu bagamoyo
 
My friend, in Africa it is the politicians who are honoured. If you want recognition in Africa, go into politics, become a cadre of certain governing party and you will be honoured instantly!
ndio maana na wewe umetupa chaki ukakimbilia kwenye mahelkopta!
 
But, why do you say he is not being honoured in Tanzania? Don't you know that in Africa, and in Tanzania in particular,academics are not honoured, they honour themselves?

My friend, in Africa it is the politicians who are honoured. If you want recognition in Africa, go into politics, become a cadre of certain governing party and you will be honoured instantly!

But Namibia is in Africa, isn't it?
 
Inafika kipindi tuache kuilamu sana serikali na tuangalie jamii zetu. Kuna watanzania wengi hapa USA ni mameneja wa Subways, Mac Donald na mambo mengine.

Ukipima ufanisi wao unaona wanafanya kazi nzuri sana. Lakini kwa nafasi hizohizo wakipewa nafasi Tanzania watavurunda na kuboronga.

Huyu Professor ameweza kufanya vizuri nje ya nchi kwa sababu katika nchi za watu, wanataka waone kazi yako na ukishindwa wanampa mtu mwingine, Hivyo kuna check and balance ya kuona kazi yao imefanyika.

Lakini huyuhuyu professor angefanya kazi bongo basi angetaka pesa anazopewa kufanyia research ajengee nyumba kwao, awe na vimada watatu na ampe kazi ya maabara ndugu yake alifeli kidato cha nne.

Kwa maoni yangu, watanzania na waafrika wengi wakifanya kazi nje ya nchi zao wanajaribu kuwa responsible lakini wakiwa kwenye nchi zao porojo nyingi.

Tamati
 
Kitila.
Mbona unaji-contradict? Ulitaka jamaa azungumzie Afrika kwanza ndio achomekee Tanzania? Hata Afrika, kuna vinchi ambavyo ni exception to the rule. Nchi kama Mauritius, Botswana n.k. Na nchi hizi vile vile ndio exception to the rule when it comes to development issues!

Hii tabia mbovu ya kuwaenzi wanasiasa tu imejikita sana hapa kwetu na inastahili kukemewa. Si academicians peke yao. Wanamichezo, wasanii (kwa maana nzuri na si hiyo ya siku hizi), wana-mazingira, activists wa kila aina n.k. wote hatuwajali. Wote hawa, kama ulivyosema, wakitaka kutambulika na kuneemeka kutokana na juhudi zao, inabidi waingie kwenye siasa!

Iko kazi.

Amandla............
 
Uko sahihi. Tatizo watanzania hawawezi kufanya kazi Indepently bila kusimamiwa vikali na mtu mkali ili wafanye vizuri.Kweli wakienda kufanya nje ya nchi hukutana na wasimamizi wakali na hufanya kazi vizuri ya kushangaza.

Ona mashirika kama Kampuni ya BIA,TTCL,NBC,NMB,TWIGA CEMENT N.K yalipokuwa chini ya menejiment za wasomi wa Kiswahili ilikuwa karibu yafe.Menejimenti ilipoletwa ya wageni ambao ni wasimamizi wakali wasiotaka mchezo kwenye kazi mashirika yanazalisha faida na yanafanya vizuri.

Watanzania tuna roho ya utumwa ambayo lazima awepo mnyapara mkali ndipo kazi ziende lakini akiwepo nyapara anayetabasamu wakati wote kama Kikwete basi ujue watu watu watafanya chini ya uwezo wao na kupata watu kama Mshingeni si kazi rahisi.
 
wana JamiiForums,

..nimevutiwa sana na hii article kuhusu Dr.Keto Mshigeni.

..mchango wake ktk utafiti wa Marine Biology unatambulika dunia nzima.

..kazi aliyoifanya kama Vice Chancellor Univ of Namibia ni ya kupigiwa mfano.

..wa-Tanzania tuna underutilize vipaji vya wasomi wetu. Keto Mshigeni ni mfano mmoja wapo.

Huyo Prof ngaebaki Bongo Bongo angeishia kuwa Mwanasiasa, tena Mkereketwa wa CCM! Si unawaona kina Prof. Wangwe, Dk. Kaburu, Prof. Kapuya, Dk. Msekela, Prof. Mwandyosa, Prof. Mwakyusa etc, etc the list is so long and hakuna walichotufanyia zaidi ya kujipatia mirija ya kunyonya ng'ombe wetu ambaye amekonda?
 
Jamani tanzania yetu ndivyo ilivyo, ukisha kuwa mwana siasa wewe ni profesa na mtaalamu wa kila kitu! maamuzi yote hata ya kitaalamu unafanya wewe bila kujali ushauri wa wataalamu!

Mangapi tumeshuhudia wataalamu wetu wakishauri juu ya vitu kama vile Mikataba mibovu mifano ya IPTL wana siasa wanapitisha tu?

Nani asiye jua kuyumba kwa uchumi wetu na mfumuko wa bei umetokana na mkuu wa kaya kukataa ushauri wa wasomi wa kutopandisha kodi ya mafuta kwa kudai kwamba hapo hapo ndo pataleta pesa chap chap?

Oh, one sad thing, sitokaa nisahau maafa ya MV BUKOBA pale mtaalamu alipo shauri meli isitobolewe, itazama lakini mkuu wa Mkoa akatoa amri kwamba itobolewe na ikazama instantly kama jiwe?

Kwa Tanzania wataalamu hawathaminiwi hata kidogo ni siasa tu hata kama za kuganga njaa kama za Rev. ndizo za kuenziwa period!
 
Uko sahihi. Tatizo watanzania hawawezi kufanya kazi Indepently bila kusimamiwa vikali na mtu mkali ili wafanye vizuri.Kweli wakienda kufanya nje ya nchi hukutana na wasimamizi wakali na hufanya kazi vizuri ya kushangaza.

Ona mashirika kama Kampuni ya BIA,TTCL,NBC,NMB,TWIGA CEMENT N.K yalipokuwa chini ya menejiment za wasomi wa Kiswahili ilikuwa karibu yafe.Menejimenti ilipoletwa ya wageni ambao ni wasimamizi wakali wasiotaka mchezo kwenye kazi mashirika yanazalisha faida na yanafanya vizuri.

Watanzania tuna roho ya utumwa ambayo lazima awepo mnyapara mkali ndipo kazi ziende lakini akiwepo nyapara anayetabasamu wakati wote kama Kikwete basi ujue watu watu watafanya chini ya uwezo wao na kupata watu kama Mshingeni si kazi rahisi.

Hicho ndicho ninachokiamini. Angalia safu ya wanasiasa wa juu Tanzania. Zaidi ya nusu ni ya watu wenye digrii wa utaalamu fulani. Hivyo wangeweza kutuonyesha ufanisi wao wa kazi ata katika nafasi za kisiasa.

Kuna kitabu fulani kama sikosehi " Fimbo ya Mnyonge": Kilitoa mfano kuwa wakati wa ukoloni kuna jamaa kutoka Kigoma aliyekwenda kufanya kazi kwenye mashamba ya mkonge kama manamba. Kutokana na usimamizi wa kinyapara katika mashamba haya, jamaa alikuwa anamaliza kazi ya manane katika kipindi cha masaa manne.

Uhuru ulipopatikana na kodi ya kulazimishwa kufutwa, jamaa alirudi kwao Kigoma. Na kazi aliyofanya kama mtu huru ni kishamba cha robo heka cha mihogo na kucheza bao.

Hivyo tuache kukemea sana siasa kwa sababu wanasiasa wengi ni haohao wasomi.
 
Jamani tanzania yetu ndivyo ilivyo, ukisha kuwa mwana siasa wewe ni profesa na mtaalamu wa kila kitu! maamuzi yote hata ya kitaalamu unafanya wewe bila kujali ushauri wa wataalamu!

Mangapi tumeshuhudia wataalamu wetu wakishauri juu ya vitu kama vile Mikataba mibovu mifano ya IPTL wana siasa wanapitisha tu?

Nani asiye jua kuyumba kwa uchumi wetu na mfumuko wa bei umetokana na mkuu wa kaya kukataa ushauri wa wasomi wa kutopandisha kodi ya mafuta kwa kudai kwamba hapo hapo ndo pataleta pesa chap chap?

Oh, one sad thing, sitokaa nisahau maafa ya MV BUKOBA pale mtaalamu alipo shauri meli isitobolewe, itazama lakini mkuu wa Mkoa akatoa amri kwamba itobolewe na ikazama instantly kama jiwe?

Kwa Tanzania wataalamu hawathaminiwi hata kidogo ni siasa tu hata kama za kuganga njaa kama za Rev. ndizo za kuenziwa period!

Rwabugiri:

Huyo mkuu wa mkoa angekuwa anafanya kazi nje ya nchi kwa kazi hiyohiyo angefanya vizuri.

Lakini Tanzania mkuu wa mkoa alimpigia kampeni rais kwenye uchaguzi. Vilevile ameoa nyumba moja na waziri mkuu. Na vilevile ni mjumbe wa NEC. Hivyo nafasi aliyonayo inalindwa na watu anaowafahamu na koneksheni zake na sio ufanisi.

Hata wasomi wakifanya kazi kwenye mazingira ambayo hayana uwajibikaji wanasahau kuwa walikwenda shule.
 
Prof Mshigeni alifanya kazi Tanzania kwa ufanisi sana kabla ya kwenda Namibia. Nafasi aliyopewa Namibia (Pro Vice Chancellor, sio Vice Chancellor) iliipita kidogo nafasi aliyokuwa nayo UDSM ya Director of Postgraduate Studies.

Namfahamu vizuri Prof. Mshigeni. Nilikuwa mwanafunzi UDSM wakati akiwa Botany, na nikaanza ualimu pale wakati alipokuwa Director of Postgraduate Studies. Ni mtu mwenye roho nzuri mno! Hana makuu, na analelea, kwa upendo na kwa dhati, wale wanaokuja nyuma yake.

Prof. Keto Mshigeni angekuwa VC mzuri wa UDSM. Lakini baada ya Chagula, aliteuliwa Pius Msekwa kuwa VC. Wakat huo Msekwa alikuwa na BA tu. Aliamua kusoma MA wakati akiwa VC. Yaani alikuwa mwanafunzi wa mmoja wa maprofesa wa chuo ambacho yeye ni VC.

Baada ya Msekwa, walifuatia ma VC wengine walioteuliwa kisiasa hivyo hivyo. Alifuatia Ibrahim Kaduma, kisha Nicholaus Kuhanga. Sifa kubwa walizokuwa nazo ni ukereketwa wa CCM. Kaduma aliwahi kututamkia wanafunzi UDSM kwamba yeye alikuwa na damu ya CCM!

Nirudi kwa Mshigeni. Napendekeza jengo la Idara ya Botany UDSM liitwe Keto Mshigeni Building. Arts Tower ibatizwe iitwe: Geofrey Mmari Arts Tower. Jengo la Kitivo cha Sheria liitwe Isa Shivji Building. Library iitwe Isaria Kimambo Library. Bureau of Resource Assessment iitwe Mascarenhas Bureau of Resource Assessment.

Hizi ndizo namna za kuwaenzi. Au mnasemaje?
 
Kitila.
Mbona unaji-contradict? Ulitaka jamaa azungumzie Afrika kwanza ndio achomekee Tanzania? Hata Afrika, kuna vinchi ambavyo ni exception to the rule. Nchi kama Mauritius, Botswana n.k. Na nchi hizi vile vile ndio exception to the rule when it comes to development issues!

Hii tabia mbovu ya kuwaenzi wanasiasa tu imejikita sana hapa kwetu na inastahili kukemewa. Si academicians peke yao. Wanamichezo, wasanii (kwa maana nzuri na si hiyo ya siku hizi), wana-mazingira, activists wa kila aina n.k. wote hatuwajali. Wote hawa, kama ulivyosema, wakitaka kutambulika na kuneemeka kutokana na juhudi zao, inabidi waingie kwenye siasa!

Iko kazi.

Amandla............

Kuna kamchezo kabaya nchi hii, hata ukifanya mazuri vipi kwenye fani yako, hutojulikana wala kuenziwa huko, ni mpaka uingie kwenye siasa. Mifano mingi:
1. Prof Juma Kapuya alifundisha Botany pale mlimani, lakini kinachomtambulisha sasa ni ubunge wa Urambo huko na uwaziri wa elimu, michezo, kazi,vijana, ulinzi nk.
2. Prof Philemon Sarungi alikuwa mzalendo wa kwanza kuwa bingwa wa fani ya mifupa, lakini hiyo haikumsaidia "kula nchi", badala yake "kilichomtoa" ni ubunge, uwaziri, ukuu wa mkoa, ujumbe wa halmashauri kuu ya CCM.
3. Dr Mohamed Bilal ni mtaalam wa nuclear physics, lakini bado hakuonekana wa maana katika fani hiyo, hadi alipoingia siasa za ukatibu mkuu, uwaziri kiongozi, kugombea urais nk
4. Dr Ali Mohamed Shein ni mwanasayansi mahiri tena katika fani yenye wataalamu wachache sana ya "molecular genetics", akiwa ameandika PhD thesis yake kuhusu "inborn errors of metabolism", lakini huko hakuona "utamu" hadi alipoingia kula nchi na wenye meno wengine kwenye siasa
5. Ukifanya search ya jina "Mark Mwandosya" kwenye google scholar utadondoshewa hits kibao za machapisho ya kisomi, na utashangaa kwa nini profesa kama huyu hayuko chuo kikuu kufundisha na kuendeleza fani hiyo, badala yake yuko kwenye siasa!
6. Wako wengine kibao kina Profesa David Mwakyusa, Prof Joseph Mbwiliza, Prof Daimon Mwaga (huyu alishawahi hadi kuwa mkuu wa wilaya sawa na akina Betty Mkwasa, na uprofesa wake!)

Tujiulize, ni matatizo ya mfumo (hauwatunzi wataalamu wake) au ya elimu ya wataalamu hawa (wanashindwa kuitumia kuleta mabadiliko kwenye fani zao?) Maana kipimo cha kwanza cha elimu kuwa inafaa au la, ni jinsi inavyoweza kuleta mabadiliko kwa msingi wa malengo ya elimu ile. Sasa hawa wasomi wetu ni kwamba elimu imewatupa au wao ndio wameitupa elimu?

Mfano mwingine ni jinsi wasomi wetu wanavyowekeza hela wanayopata. Mtaalamu wa kilimo anakwenda kuanzisha bar, guest house na club ya kuchezea pool, mhandisi anaanzisha kijiwe cha kukopesha kwa riba (kisichosajiliwa!), mkurugenzi wa benki ana biashara ya teksi na gereji bubu, na profesa electrical engineering ana genge la kuuzia kitimoto na bia! Kwa nini hawa hawaanzishi biashara kwenye fani zao ambako ni authorities, wanakoaminika? Lawyers peke yao wanajitahidi, wanaanzisha kampuni za uwakili au ushauri, lakini hata kule Dar nilikuwa napishana na Dr Lamwai akiwa na double cabin yake amebeba magudulia ya maziwa kutoka nyumbani kwake anakwenda kusambaza kwa wateja wake! Sasa jamani hii nini? Matokeo yake ni kuwa kile wataalamu wetu walichosomea wanashindwa kufanya vizuri maana wameelekeza nguvu kwingine. Na huko walikoelekeza nguvu wanafanya vibaya kwa sababu si fani zao. Kwa hiyo kila kitu hakiendi sawa, ni hovyo tu. Ni sawa na kununua tai yako ya bei mbaya halafu unaitumia kama mkanda wa suruali, utaonekana kituko licha ya hela nyingi uliyotumia!

Kuna mifano ya wasomi mahiri wanaotumia elimu yao kufanya kazi za ushauri na miradi inayoendana na elimu hizo, lakini bado ni wachache sana. Je wasomi wetu elimu imewatupa au wao wameitupa elimu na kukimbilia siasa na mengine? Je elimu haiwafai au wao hawaifai elimu, wanaitenda elimu yao visivyopasa. Tutafakari.
 
Kithuku,

Naona unashangaia biashara wanazofanya wasomi wanapong’atuka. Kuanzisha shughuli ya maana kunahitaji mtaji mkubwa. Wengi hawana mtaji wanapong’atuka.

Vile vile, uzeeni mtu hupenda kufanya biashara inayoendana na hobby zake . Sasa mtu mwenye hobby ya kunywa bia jioni kwa nini asifanye grosari ya bia ndiyo biashara yake ya kung’atukia? Kuna mbaya gani akiiuza kama kreti 5 na kuku 6 kwa siku? Sii ndio biashara ndogo ndogo?
 
Nadhani sababu kubwa ya watu kufanya mambo yasioeleweka ni kuwa mfumo mzima wa pensheni au mafao kwa wastaafu wetu hauelewiki. Kama watu wangeweza kuishi kwa mafao basi nani angetaka auze bia au kulima mchicha?

Nadhani professor Shivji wakati anastaafu alipewa kama 40 Milioni kwa kipindi chote. Wakati mbuge analamba 30Milioni katika kipindi cha miaka mitano kama mafao.

Tukirudi kwenye mada. Hapa Marekani kuna title wanapewa wastaafu maprofessor -- emeritus. Anapewa ofisi, anaudhuria mikutano lakini kazi za kufundisha hafanyi. Lakini mshahara anavuta.

Nadhani waliofikia ngazi ya uprofessor wakifikia umri wa kustaafu waendelee kuwa maprofessor wa heshima na wavute mishahara kama kawaida na wapewa ofisi katika idara zao kwa sababu mchango wao ni mkubwa.
 
Back
Top Bottom