Prof. Lipumba aiapia CHADEMA kutotawala nchi

Anayeamini Lipumba atakuja kuchaguliwa kwa kura za wananchi kwa ngazi yoyote ile aidha balozi wa nyumba 10 au zinginezo, basi huyo atakuwa mgonjwa na anahitaji kwenda Mirembe. Haitaji hata kwenda kwa Babu Ambi.
 
..nadhani CUF hawana mpango wa kuchukua utawala na kuongoza nchi hii.

..chama cha upinzani kinapaswa kushambulia na kukosoa utendaji wa serikali iliyoko madarakani.

..Prof.Lipumba anapokishambulia Chadema, tena ktk maeneo kama Tanga ambako hakina umaarufu, sijui anategemea nini haswa.

..nadhani Prof.Lipumba anatafute washauri wapya wa kisiasa wamsaidie kuijenga CUF. Inasikitisha kwamba toka uchaguzi mkuu uishe Prof hajafanya juhudi zozote zinazoeleweka za kukiuza chama chake kwa wananchi.

..kama all that Lipumba and CUF want, is to replace Chadema and become the main, but weak[wabunge 40] opposition party in the country, basi wanaweza kuendelea na hizi kampeni kwa mtindo huu waliokuja nao.
Relevancy, relevancy, ndiyo inayowasumbua. Prof anatambua kwamba CUF imepoteza relevancy hasa bara na kama mfa maji ameanza kutapatapa. Ukiangalia idadi ya waliojitokeza kumpokea Tanga na idadi wanayosomba viongozi wa Chadema basi utaelewa ni kwa nini Prof anaelekeza makali yake kwa Chadema badala ya CCM.
 
Hivi siku hizi common enemy ni cdm? Huyu mzee wa pumba ndo akanywe kikombe kwa babu!
 
Huyu sasa ndio yulee prof, ambaye nilikuwa simjui sasa naiona picha yake kamili!
Nimeamini ile methali isemayo;
TUMBO Linauponza Mkund**
Sasa amesha kuwa vuvuzela jinga jinga la mafisadi kabsaaa shaka hamna.
Sasa CDM huu ni usongo wanangu tumelishwa na cuf, tutumie njia yoyote iliyo mikononi mwetu lolote na liwe ikibidi kafara ni lazima kuwakomboa wananchi wanaoteseka na mfumo huu wa kikandamizaji.
Mtatiro toka huko haraka hao ni kunguru wa zenj wewe ni njiwa jiunge na waTanganyika wenzio walio vitani.
MPAKA KIELEWEKE!

Kieleweke nini, mpaka ifike 2015 mbona mtakoma na matusi yataisha tu...
 
Hayo ndio matatizo ya wanasiasa wengi wa tz, badala ya kuongea mambo ya sera za vyama vyao na matarajio yao ya nini wataifanyia nchi na dunia iwapo wataingia madarakani, wamebaki wanapambana wao kwa wao. Watu kama hao ni hatari sana kwa maendeleo ya tz, kwa kuwa tz tunahitaji viongozi wenye vision ya wapi tz tupo na tunatakiwa kwenda wapi tokea hapa tulipo ili tuweze kuendelea.Pia tunataka viongozi wawe wanajua siasa za dunia ya leo na ijayo kwa kuwa siasa ya dunia ina madhara sana kwa siasa ya tz na afrika kwa ujumla, kwa mfano bila kujua siasa za dunia huwezi kujua kinachoendelea libya, utafikiri kwamba uvamizi wa majeshi ya kigeni dhidi ya libya ni kuwasaidia wananchi wa libya kitu ambacho siyo kweli, wao wapo pale kiuchumi zaidi yaani kupata nafasi ya kujipatia mafuta ya libya free of charge,oh mungu ibariki afrika
 
SLAA-CUF inafadhiliwa na ccm kufanya mikutano ya kuishutumu cdm,cuf haiwezi kuwa chama cha upinzani,cuf ni chama popo,cuf haina uwezo wa kuongoza dola,


MBOWE- CUF ni mke wa ccm,cuf siyo chama cha upinzani,cuf ni ccm b, cuf ni wanafiki, cuf hawana mwelekeo,

LIPUMBA-Chadema ni chama cha wafanyabiashara na mafisadi nyangumi,chama cha wapiga disco,chama kisicho na uwezo wa kuwatoa watz kwenye umasikini,anayedhani cdm inaweza kuongoza nchi akanywe dawa ya babu loliondo,anaumwa.

Mtatiro- Tutajibu kila propaganda wanayosema cdm dhidi yetu, chama kinachotafuta dola hakiwezi kudhaminiwa na mafisadi(nyangumi) -sabodo,mengi na wenzie- siku kikipata dola kitawatumikia waliokifadhili,tutajibu hoja kwa kielelezo,propaganda kwa ukweli , mwisho wa siku ukweli utasimama,
MANENO YA VIONGOZI WENU HAYO,KATI YA HAO WOTE NANI MJINGA NO 1,2,3,4,
NANI MJINGA KULIKO WOTE,NANI TAAHIRA, NANI MJANJA?




.

...anaekuanza,mmalize...
 
CHADEMA ACHENI WANYANG'ANYI WA WAPARUANE WAMALIZANE WENYEWE
HUKU 'NGUVU YA UMMA' TUKIWASUBIRI NJIA PANDA YA KURA!!


Jamani siku zote mjue saikolojia hii rahisi ya kwamba kote dunia hakuna Mtu, Chama na au taifa KIDUME mpaka kwanza kuwepo na Mtu, Chama na Taifa linalojihisi K-INZI pinzi wote wajitokezapo mbele ya hadhara.

Hivyo nymbo zisizopata kituo toka kwa wenyeviti wa vyama nchini kama vile Mhe Kikwete, Mrema, Mbatia, Lipumba na hivi sasa Mzee Mapesa na santuri yake mpya ni ujumbe mzito wa ujumbe uliojificha nyuma ya ujumbe tuuonao kiharaka kwenye kelele hizo!!

Sana sana labda nichukue fursa hii kukiomba CHADEMA kiwatendee haki hawa watangazaji wa hiari waliojikita zaidi kwenye kujulisha Wa-Tanzania tulioamka akilini; juu ya uwepo, nguvu na shughuli thabiti za chama hiki kwa walalahoi, taifa, na dunia kwa ujumla!!

Nasema hivi kwa sababu nimeona muda mrefu waheshimiwa kama akina Mzee Makamba, mbali na ratiba zao ngumu kweli kikazi, wakijitolea hivi hivi na wala msitambue juhudi zake, Mhe Kikwete kufanya hivo kwa mapenzi makubwa kila apitako (na wala asifanye kwa CCM) huku nyie wala hamuoni. Mama Simba tena ndio usiseme katika juhudi hizi za hiari kukitangaza zaidi CHADEMA bila malipo.

Naongeza hiviii; acheni wakatutangazie zaidi chama hawa akina TBC1, Rweyemamu wa Magogoni, Chalii Ngoyayi, wakubwa kama Kepteni Chiligati, Benno Malisa, Riz1 Kikwete, Hamad Rashid, Haruna Lipumba a.k.a Mgombea wa Kudumu CUF ... listi ni ndefu sana mpaka najiuliza Dr Ali Mohamed Shein, Maalim Seif, Mzee Msuya, Mzee Warioba, ... wao kukibania CHADEMA matangazo ya hiari katika mkumbo huu wenzetu mnamaana gani??

Ukiniuliza mie ninavyoendelea kushuhudia mishale mbali mbali kwa CHADEMA hadi baadhi ya maafisa wetu serikalini nao kujichagulia kuwashambulia wapendwa wao tena bila aibu, yooote kwangu ni kichekesho kisicho na kituo!!

Mwenzenu ninavyoumwa mbavu hapa kuona watu mnavyojichosha pumsi ya gharama kwa kujadili MENDE zinapoigonga KABATI kiajali tu tena kule katika kuruka ruka kwao ovyo tu ndani jiko lilizoeleka kwa kwa mtaji wake wa uchafu kwa wezi na wanyang'anyi wengi tu ndani ya taifa hili, huku zikitafutia makombo ya wafalme baada ya kusaza na kuvimbiwa pia, mwenzenu mbavu katika na machozi ya furaha kusimama machoni!!!

Acheni hao watumwa wa hiari kwa MFUMO FISADI wajimalize wenyewe kwani kupayuka kwao ovyo ni salamu tosha kwamba kweli CHADEMA na 'Nguvu ya Umma' kote nchini kweli TUMEWASHIKA pachungu sana tena pasipoelezeka zaidi ya mtu mzi kusikika kuendelea tu kutoa gugumia tena wa masharikiiii.

Mwisho ningemuuliza Mzee Mapesa akawaeleze Wa-Tanzania mradi aliyonayo ndani ya Kamati ya Mahesabu Mapato na Matumizi ya serikali, hata asipende kubanduka mle, waka wenzake hali gumu balaa huku mitaani wakati yeye akiendelea kuchota 10% ya kila fungu la UFISADI kama vile RICHMONDI, DOWANSI, MEREMETA, MRADI WA RADA, EPA ... kabla ya kuzifumbi macho, lakini bora nisubiri siku nyingine.
 
Bepari, mpashe mlugaluga huyo. Mpaka kufikia 2013 watakuwa wamepoteza mvuto kabisa kwa umma wa watanzania wapenda amani

Weweee CDM maji marefu tupo gado.
nyinyi kafu endeleeni kutumwa markiti na kukuna nazi uwani si ndio zenu!
Nawaombea dua msife ili muone kwa macho yenu CDM Ikipeta mjengoni.
CDM a luta continua!
 
Kieleweke nini, mpaka ifike 2015 mbona mtakoma na matusi yataisha tu...

Hujui!! bado uko bongo au wapi mwenzetu, basi kama hujui mmebebeshwa junia la mawe ngata kifuu heya heya hiyo dogo manake; tutaiendesha sisiemu na kibanda chake kidogo kama mgari mbovu mwana.
Kama hutaki kunywa sumu xa mbewa upotelee mbali!
KIVYAKO DOGO.......
 
Lipumba bana ananifurahisha sana kwa kauli zake...SAsa kama CCM inawafanya watanzia wale mlo mmoja mbona wamekubali kufanya nao ndoa...hii mijamaa kweli haina akili hata kidigo
 
Ogopa sana kuugua ugonjwa wa njaa. Maana unashambulia seli za kufikiri na kufanya maamuzi ( Ndio ubinadamu/utu ulipo). Inafikia mahali unailazimisha hata nafsi yako kufanya yale ambayo haitaki ili mradi tu uendelee kuwepo kama ulivyo hata kama kwa kufanya hivyo unaukosea umma.
Mi nawashauri watu wa hivyo wakae kimya kulinda majina na taaluma zao. Kwani zilishaanza kuwa "kweshenabo!!!!!"

Ni aibu kwao (Indivijo), ni aibu kwetu (kama taifa mbele ya wenzetu), ni aibu ya Afrika (Kwa matumizi mabaya ya rasilimali - Profesa kuropoka bila kufanya utafiti) ili kuwafurahisha watu fulani kwa maslahi binafsi.

Shida ya Prof. Lipumba anaamini watanzania wote ni mabwege isipokuwa yeye. Nakumbuka kwenye kampeni za Uraisi 2005 nilihudhuria kampeni zake nikiwa pale Sumbawanga mjini. Alichofanya ni kujibaraguza na kujichelewesha kwa kwenda Intaneti kefu moja na baadae kuja kutuambia kuwa amegundua leo (siku hiyo) kuwa anatakiwa kuhudhuria mkututano wa kimataifa wa wachumi huko nchi za skandinavia wakati stori ilikuwa kwenye mitandano wiki nzima na midia kibao zilikuwa zimesharipoti hiyo kitu.

SHAME ON YOU PROF!!!!!!!!!!
 
Song:
mwombee adui yako aishi siku nyingi ili unapofanikiwa ajionee kwa macho!!
 
URAFIKI WA "MBUZI" na "CHUI" wanapokaribia kwenye MSITU MNENE...... ili waungane pamoja wasivamiwe.....:tape2:
 
Hii ilikuwa kabla ya UKAWA au baadaya UKAWA? Maana habari ya mjini kwa sasa ni UKAWA.
 
Hahahah Profesa Lipumba atuambie, ni Lini ameanza kuamini kuwa wafanyabiashara wa Chadema wanaweza sasa kuongoza nchi?.

Mbona basi ameungana na wafanyabiashara hawa kwenye hili genge la Ukawa?
 
Pale ukawa hakuna viongozi wenye nia ya kutatua matatizo ya wananchi, pale kuna wasaka madaraka na vyeo na wapiga dili tupu
 
Mnajitahidi kufukunyua vistory vya zamani, mnajidharaulisha kwa viujira mbuzi.
Mkuu hutaki historia? Hii ndio JF mkuu kila kitu kinabaki kama kumbukumbu. Mkiambiwa wekeni akiba ya maneno hamtaki. Siasa siku zote haina rafiki ama adui wa kudumu.
 
Back
Top Bottom