Mshume Kiyate
JF-Expert Member
- Feb 27, 2011
- 6,766
- 894
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema anayeamini kuwa Chadema, kitatawala nchi hii atambue ni mgonjwa na anatakiwa kwenda kwa Mchungaji Mwasapile Ambilikile, maarufu kama Babu kupata kikombe cha dawa.
Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha soko la Mitumba, wilayani Muheza hivi karibuni, Profesa Lipumba alisema viongozi wa Chadema ni wafanyabiashara hawawezi kuongoza nchi.
"Kama kuna mwananchi yoyote Wilaya ya Muheza anaamini Chadema inaweza kuongoza nchi hii, basi huyo akanywe kikombe kwa Babu huko Loliondo", alisema Lipumba.
Naibu Katibu Mkuu CUF, Julius Mtatiro, alisema CCM imewafikisha wananchi wanakula mlo mmoja kwa siku, huku watoto wakienda shuleni na njaa. Mtatiro alisema hali inazidi kuwa ngumu, lakini CCM ambayo imesababisha ugumu huo inaona kawaida vyakula kupanda bei.
Source: Mwananchi Machi 26, 2011