Prof. Kapuya atoweka ghafla nchini. Ni baada ya kufunguliwa mashataka Polisi

Huyo bint ni Taperi sana, safari hii anaenda gerezani, huwezi kuiaperi serikari, anamajina zaidi ya manne, mwanafunzi kisha anamtoto and so so! Amebugi, aliempanga na kumpa moyo atamkimbia, amehojiwa na mwandishi wa habari tu anababaika itakuwa mpelelezi?

Body without head
 
Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini Sweden miezi miwili hadi mitatu.
 
???????????????????????????????????????????????????/
 
Magazeti mengine njaa tupu. Wamehongwa vibukubuku hawaandiki kabisa hii habari ya unyanyasaji wa kijinsia

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Mkuu unakosea siyo bukubuku, wamelipwa some millions shillings
 
globo publisha na wenyewe wana kesi ya kujibu kutumika kumsafisha kp na kumdhalilisha aliyebakwa...

...Mkuu kumbuka globo pablisha nao wanamilikiwa na kada maarufu wa ccm Erick Shigongo, ambaye kulindana ni jadi yao!
 
SIKU chache baada ya Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kudaiwa kutoweka nchini kukwepa mkono wa sheria dhidi ya tuhuma za kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka, vigogo wa polisi wanadaiwa kuhusika kumsaidia kutimkia nje, Tanzania Daima limedokezwa. Habari ambazo gazeti hili limezipata, zinaeleza kuwa siku mbunge huyo akikamilisha taratibu za kusafiri, ndiyo siku ambayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni lilikuwa limekamilisha kufungua jalada la tuhuma zake na liliweka mtego wa kumnasa.
"Wakati Polisi Kinondoni wakiweka mtego wa kumnasa, baadhi ya polisi walimjulisha na hata kumsaidia kuhakikisha anasafiri nje ya nchi," alisema mmoja wa maofisa wa juu wa polisi nchini.
Hata hivyo, kuna utata na kauli zinazopingana kuhusu mbunge huyo. Taarifa nyingine zinasema kuwa mbunge huyo ambaye amepata kuwa waziri, anadaiwa kusafiri kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.
Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini humo miezi miwili hadi mitatu.
Hata hivyo, haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa safari hiyo imelenga kutuliza upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa.
Tayari Profesa Kapuya alishafunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam juzi

Habari hii imenukuliwa kutoka katika gazeti la Tanzania Daima.
 
SIKU moja baada ya binti anayedaiwa kubakwa na kutishiwa kuuawa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kufungua jalada polisi dhidi yake, inadaiwa mbunge huyo ametoweka nchini...

Vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na mbunge huyo, vinadai kuwa amesafiri juzi kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.

Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini Sweden miezi miwili hadi mitatu.

Hata hivyo haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa safari hiyo imelenga kumtuliza na upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa.

Wakati Profesa Kapuya anakimbilia nje ya nchi, tayari alishafunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam juzi.

Mtoa taarifa wetu anasema muda mchache baada ya Kapuya kushindwa kumshawishi binti huyo asimfungulie kesi ya ubakaji, wala kuogopa vitisho vya kuuawa, au kupokea pesa kiasi chochote aondoke nchini, Kapuya mwenyewe alipanga safari ya dharura na kwenda nje ya nchi.

Tanzania Daima lilifanya juhudi za kuwasiliana na ofisi ya Bunge kujua kama wana taarifa zozote za kuondoka kwa mbunge huyo kwenda nje ya nchi na kujua ni sababu zipi hasa zimempeleka huko, lakini simu ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai ilikuwa inaita bila kupokelewa.

Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila naye hakupatikana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) hakuujibu.

Hata hivyo, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu ambayo Kapuya ni mjumbe wake haina safari ya Sweden.

Tangu Tanzania Daima lianze kuandika tuhuma hizi nzito, kumekuwapo na kusuasua kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani na Jeshi la Polisi.

Harakati za kufungua jalada dhidi ya Kapuya zilianza juzi jioni na kuendelea hadi jana ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.

Akiwa polisi, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.

Polisi wanena

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema watamtafuta Kapuya nchi yoyote atakayokwenda iwapo tuhuma dhidi yake zitathibitika.

Alisema Jeshi la Polisi lina mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo si rahisi kwa mtuhumiwa yeyote kuukwepa mkono wa sheria endapo itahitajika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

"Sisi tunashirikiana na polisi wa nchi mbalimbali duniani, ndiyo maana inakuwa rahisi kwa mtuhumiwa aliyetoroka nchi fulani kukamatwa nyingine na kurejeshwa kwao.

"Nataka niwaondoe hofu wale wote wanaodhani polisi haiwezi kumkamata mtu akikimbia nchini, tuna mkono mrefu sana na hatufanyi kazi kinyume na taratibu zetu," alisema.

Kamanda Wambura pia alikiri polisi kufungua jalada la Kapuya huku akiweka wazi kuwa kinachofanyika hivi sasa ni uchunguzi wa tuhuma zake.

Alisema miongoni mwa maeneo wanayoyafanyia uchunguzi ni kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.

"Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo," alisema Wambura.

Tanzania Daima
Hata akae mwaka mzima huko nchini Sweden Pro. Kapuya atarudi na kesi yake ipo wazi inamngojea.cc@[URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=4026"]Power to the People[/URL]
 
Huyo bint ni Taperi sana, safari hii anaenda gerezani, huwezi kuiaperi serikari, anamajina zaidi ya manne, mwanafunzi kisha anamtoto and so so! Amebugi, aliempanga na kumpa moyo atamkimbia, amehojiwa na mwandishi wa habari tu anababaika itakuwa mpelelezi?

Body without head

Mbona unageuka hakimu!
 
wapenzi tunachezewa akiri message ya Airtel money na Mpesa wapi na wapi? hii namba ni airtel message hii ni ya Mpesa. amkeniiiiii huyu binti apimweee akili. (Note: im not in any side" regarding this bull shit saga)
 
SIKU moja baada ya binti anayedaiwa kubakwa na kutishiwa kuuawa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kufungua jalada polisi dhidi yake, inadaiwa mbunge huyo ametoweka nchini...

Vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na mbunge huyo, vinadai kuwa amesafiri juzi kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.

Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini Sweden miezi miwili hadi mitatu.

Hata hivyo haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa safari hiyo imelenga kumtuliza na upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa.

Wakati Profesa Kapuya anakimbilia nje ya nchi, tayari alishafunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam juzi.

Mtoa taarifa wetu anasema muda mchache baada ya Kapuya kushindwa kumshawishi binti huyo asimfungulie kesi ya ubakaji, wala kuogopa vitisho vya kuuawa, au kupokea pesa kiasi chochote aondoke nchini, Kapuya mwenyewe alipanga safari ya dharura na kwenda nje ya nchi.

Tanzania Daima lilifanya juhudi za kuwasiliana na ofisi ya Bunge kujua kama wana taarifa zozote za kuondoka kwa mbunge huyo kwenda nje ya nchi na kujua ni sababu zipi hasa zimempeleka huko, lakini simu ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai ilikuwa inaita bila kupokelewa.

Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila naye hakupatikana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) hakuujibu.

Hata hivyo, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu ambayo Kapuya ni mjumbe wake haina safari ya Sweden.

Tangu Tanzania Daima lianze kuandika tuhuma hizi nzito, kumekuwapo na kusuasua kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani na Jeshi la Polisi.

Harakati za kufungua jalada dhidi ya Kapuya zilianza juzi jioni na kuendelea hadi jana ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.

Akiwa polisi, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.

Polisi wanena

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema watamtafuta Kapuya nchi yoyote atakayokwenda iwapo tuhuma dhidi yake zitathibitika.

Alisema Jeshi la Polisi lina mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo si rahisi kwa mtuhumiwa yeyote kuukwepa mkono wa sheria endapo itahitajika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Sisi tunashirikiana na polisi wa nchi mbalimbali duniani, ndiyo maana inakuwa rahisi kwa mtuhumiwa aliyetoroka nchi fulani kukamatwa nyingine na kurejeshwa kwao.

“Nataka niwaondoe hofu wale wote wanaodhani polisi haiwezi kumkamata mtu akikimbia nchini, tuna mkono mrefu sana na hatufanyi kazi kinyume na taratibu zetu,” alisema.

Kamanda Wambura pia alikiri polisi kufungua jalada la Kapuya huku akiweka wazi kuwa kinachofanyika hivi sasa ni uchunguzi wa tuhuma zake.

Alisema miongoni mwa maeneo wanayoyafanyia uchunguzi ni kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.

“Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.

Tanzania Daima

Hivi hii nchi inatawaliwa na cartoon au kiongozi wa kiukweli? Toka lini mtu anayefunguliwa mashitaka kama haya anapewa fursa ya kusafiri? Huyu jamaa ni muuaji na evidences are there kuwa alitishia kuua mtu na kumpa ngoma...why the hell aliruhusiwa kuondoka nchini? kwa wenzetu anafunguliwa kesi na kwa kuwa ni kiongozi anayang'anywa passport yake na anasimamishwa kazi kwa muda kusubiri upelelezi dhidi yake. Tanzania, why huu upuuzi jamani?
 
Back
Top Bottom