Prof. Kapuya atoweka ghafla nchini. Ni baada ya kufunguliwa mashataka Polisi

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
774
1,456
SIKU moja baada ya binti anayedaiwa kubakwa na kutishiwa kuuawa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kufungua jalada polisi dhidi yake, inadaiwa mbunge huyo ametoweka nchini...

Vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na mbunge huyo, vinadai kuwa amesafiri juzi kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.

Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini Sweden miezi miwili hadi mitatu.

Hata hivyo haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa safari hiyo imelenga kumtuliza na upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa.

Wakati Profesa Kapuya anakimbilia nje ya nchi, tayari alishafunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam juzi.

Mtoa taarifa wetu anasema muda mchache baada ya Kapuya kushindwa kumshawishi binti huyo asimfungulie kesi ya ubakaji, wala kuogopa vitisho vya kuuawa, au kupokea pesa kiasi chochote aondoke nchini, Kapuya mwenyewe alipanga safari ya dharura na kwenda nje ya nchi.

Tanzania Daima lilifanya juhudi za kuwasiliana na ofisi ya Bunge kujua kama wana taarifa zozote za kuondoka kwa mbunge huyo kwenda nje ya nchi na kujua ni sababu zipi hasa zimempeleka huko, lakini simu ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai ilikuwa inaita bila kupokelewa.

Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila naye hakupatikana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) hakuujibu.

Hata hivyo, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu ambayo Kapuya ni mjumbe wake haina safari ya Sweden.

Tangu Tanzania Daima lianze kuandika tuhuma hizi nzito, kumekuwapo na kusuasua kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani na Jeshi la Polisi.

Harakati za kufungua jalada dhidi ya Kapuya zilianza juzi jioni na kuendelea hadi jana ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.

Akiwa polisi, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.


Polisi wanena

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema watamtafuta Kapuya nchi yoyote atakayokwenda iwapo tuhuma dhidi yake zitathibitika.

Alisema Jeshi la Polisi lina mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo si rahisi kwa mtuhumiwa yeyote kuukwepa mkono wa sheria endapo itahitajika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Sisi tunashirikiana na polisi wa nchi mbalimbali duniani, ndiyo maana inakuwa rahisi kwa mtuhumiwa aliyetoroka nchi fulani kukamatwa nyingine na kurejeshwa kwao.

“Nataka niwaondoe hofu wale wote wanaodhani polisi haiwezi kumkamata mtu akikimbia nchini, tuna mkono mrefu sana na hatufanyi kazi kinyume na taratibu zetu,” alisema.

Kamanda Wambura pia alikiri polisi kufungua jalada la Kapuya huku akiweka wazi kuwa kinachofanyika hivi sasa ni uchunguzi wa tuhuma zake.

Alisema miongoni mwa maeneo wanayoyafanyia uchunguzi ni kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.

“Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.


Tanzania Daima
 
Mbona tulisikia biniti "keshatulizwa" na Prof.?
Hii movie inahitaji muda kuijua na kuifuatilia coz ukweli ni adimu sana na propganda za kupotosha ni nying mno.
 
Magazeti mengine njaa tupu. Wamehongwa vibukubuku hawaandiki kabisa hii habari ya unyanyasaji wa kijinsia

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
globo publisha na wenyewe wana kesi ya kujibu kutumika kumsafisha kp na kumdhalilisha aliyebakwa...
 
Mwanzo nayaona maelezo ya kipolisi kuhusiana na sakata hili, sielewi taarifa hii ya uchunguzi wa polisi imeishia wapi naona tu gazeti limefanikiwa kugundua..... Sasa hii ni taarifa kutokana na uchunguz wa polisi ama gazeti???
 
Ona sasa serekali ya wabakaji
Hii habari inabidi tuiweke kwenye mitandao ya kijami huu ni uzalilishaji kwa watoto
Shame on you Kapuya
 
Kwa hiyo walikuwa wanachelewesha kumkamata Kapuya ili apate muda wa kupanga na kukamilisha mipango ya safari yake nje ya nchi. Bila shaka kwa huyu atutaambiwa amefia huko kama Gavana Balali na kwamba atarudi mzima ili ajibu tuhuma zinazomkabili.

Tiba
 
Huu ni wakati wa Wanawake Tanzania kuonyesha kama mpo na mna akili. Hapa wanawake wanatakiwa waingie barabarani mfululizo mpaka Kapuya akamatwe na kurudishwa nchini haraka.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom