Sababu ni nini?
Mbona yeye na Slaa wanataka tuzingua? Hivi hawa watu wamepewa nini hadi kutugeuka hivi.... walianza vizuri ila wanataka haribu mambo sasa
msiogope sasa ndio wamebaki wapinzani wa kweli hawa walikuwa sio wapinzani tukaze buti tunakwenda kuikomboa tanzania yetu
Ndio maana siamini habari za kwenye redio
Akili ya mbayuwayu changanya na ya kwako... usiropokeChona;
Ni roho mbaya tu kwani watu hudhani kuwa kama sote hatutagombea nafasi fulani basi hakuna tena mwingine. Tujiulize kwanza, nia ni kuonekana tu kuwa umegombea au nia ni kuingia Ikulu? Tangu kuanza vyama vingi amegombea na kutoka patupu, leo tujaribu tena? Ningetamani atulize kichwa ajue kuwa hata EL tumempa nafasi hii si kujaribu bali ni kuwa tuna hakika na ule umati alokuja nao. Tunatosha kiling;oa hili gogo litoke kule Magogoni. Mwenye nia nyingine UKAWA si pahala pake, Aende tuuu. Tukimaliza kazi, aweza kurudi:israel::israel::flypig::flypig:
1. Prof namuona ni mnafikiKila mtu anahaki ya kusimamia yale anayoyaamini yeye mwenyewe. Japokuwa Pro. Lipumba nae ana haki hiyo naomba wanajukwaa tulimulike swala hili kwa jicho la ndani na mbali.
- Pro. Ni mwenyekiti wa chama (High profile leader in CUF), angeweza kutumia vikao halali vya vyama kutoa mwelekeo kwa chama ili CUF ndio itoe mwelekeo wake ndani ya UKAWA. Kitendo cha katibu mkuu, makamu mwenyekiti na viongozi wengine kutojua ya PRO. ni dalili tosha inyoweza kuhitimisha mjadala huu kuwa kuna KITU PRO. AMEKIFICHA
- Kitendo cha gazeti la CCM kuwa la kwanza kulipoti habari hii hata kabla ya viongozi wengine wa CUF, UKAWA, na vyombo vingine vya habari hata kabla ya PRO. Hajatoa uamuzi huo unaonesha dhahiri nini LIPUMBA alichodhamilia
- Hali ya pro. kuwahadaa viongozi wenzake kuwa hakuna tatizo ndani ya UKAWA mpaka Juma Duni kubadili uanachama kwenda chadema ili awe mgombea mwenza akimuacha na katibu wake mkuu Maalim Seif kuhutubia mkutano mkuu wa CHADEMA wakati alikuwa nae jana yake mpaka saa nne usiku bila kuongea lolote, linatoa maswali mengi ambayo pro. hawezi kuyajibu.
- Pro. aliwaaminisha wenzake kuwa kumkaribisha LOWASSA Chadema, ni mafanikio makubwa na ushindi mkubwa, sijajua alimaanisha nini ukilinganisha na KAULI ZAKE ZA LEO
- Kama mwenyekiti hakupaswa kujiudhuru bali angesimamia hicho anachokiamini kwa vikao halali vya kichama na viongozi wenzake kuliko sasa ambapo anataka kutuaminisha kuwa VIONGOZI WENZAKE NDIO WASALITI NDANI YA CUF.
- Karibuni tutafakari wanajukwaa.
Mi naona wapinzani hawa bado hawajataka kuchukua hii nchi
Mbowe ni kiboko yenu. Mtawarubuni wengi sana ila kwa Mbowe mmegonga mwamba.Mbowe kawauza vyama vyote bila kujijuwa. Pale ambae kabaki ni mzee makaidi tu nadhani hata pesa hajapewa maana kwenye Chama yeye mwenyekiti na mkewe Katibu hawana mwanachama hata mmoja sasa ni faida kwa upande wake.
View attachment 273900
Prof. Lipumba akiongea na waandishi wa Habari kwenye Hoteli ya Peacock
Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti kwenye chama chake cha Wananchi CUF.
Ametangaza kuachia ngazi uenyekiti wa chama hicho mapema leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacok.
Amesema amechukua uamuzi huo kutokana na UKAWA kushindwa kusimamia makubaliano yao.
Chanzo: Nipo kwenye kikao
=======
Prof Lipumba akitaja sababu za kujiuzulu nafasi ya uenyekiti CUF
Sentensi za Prof. Lipumba akiwa na waandishi wa habari
waliopewa kitu kidogo akina mbowe,lema ,tundu lissu,na wengineo hamuwaoni? hujui chama kimeuzwa kwa mafisadi?
hongera lipumba kwa uamuzi huu wa busara!