Prof. Ibrahim Lipumba atangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa CUF Taifa

Sababu ni nini?
Mbona yeye na Slaa wanataka tuzingua? Hivi hawa watu wamepewa nini hadi kutugeuka hivi.... walianza vizuri ila wanataka haribu mambo sasa

waliopewa kitu kidogo akina mbowe,lema ,tundu lissu,na wengineo hamuwaoni? hujui chama kimeuzwa kwa mafisadi?
hongera lipumba kwa uamuzi huu wa busara!
 
msiogope sasa ndio wamebaki wapinzani wa kweli hawa walikuwa sio wapinzani tukaze buti tunakwenda kuikomboa tanzania yetu

Mmh...
 

Attachments

  • 1438870449846.jpg
    1438870449846.jpg
    31.6 KB · Views: 1,027
CUF ni taasisi kama zingine.Uhai wake,ukuaji na uimara wake kamwe haukutokana na Lipumba bali ni matokeo ya upeo wa watanzania kuhitaji mageuzi,mshikamano na umoja wa wanachama wa CUF.Nitakuwa natenda dhambi kuamini kuwa eti Prof Lipumba kujiuzulu ni pigo kwa ukawa ktk kushinda uchaguzi wa oktoba.Aliamini ivo kuwa yeye ndie mhimili wa CUF Bara, ni haki yake kwa kuwa hakuwahi kuwa nje ya uongozi tangu awe Mwenyekiti.AMETOA NAFASI WENGINE WAONYESHE LEADERSHIP KTK WAKATI MUAFAKA NA WATA TENDA ZAIDI NA ZAIDI YAKE.ALUTA KONTINUA.
 
Chona;
Ni roho mbaya tu kwani watu hudhani kuwa kama sote hatutagombea nafasi fulani basi hakuna tena mwingine. Tujiulize kwanza, nia ni kuonekana tu kuwa umegombea au nia ni kuingia Ikulu? Tangu kuanza vyama vingi amegombea na kutoka patupu, leo tujaribu tena? Ningetamani atulize kichwa ajue kuwa hata EL tumempa nafasi hii si kujaribu bali ni kuwa tuna hakika na ule umati alokuja nao. Tunatosha kiling;oa hili gogo litoke kule Magogoni. Mwenye nia nyingine UKAWA si pahala pake, Aende tuuu. Tukimaliza kazi, aweza kurudi:israel::israel::flypig::flypig:
Akili ya mbayuwayu changanya na ya kwako... usiropoke
 
Prof IBRAHIM LIPUMBA sii mnawapa kuongea CCM na kwani msiijitowee UKAWA ukabaki na chama chetu CuF na ukasimama kma wwe pia naisii mlikulupuka kuunda UKAWa ila kila rakher kwenye shughuli zako za kimaendeleo , tunaeshimu mawazo yko ilaa mnatuweka kwenye wakati mgumu sanaa wanachamaa wenu N.k andaeni vitu kma wasomii jamaani . . .....
 
Kila mtu anahaki ya kusimamia yale anayoyaamini yeye mwenyewe. Japokuwa Pro. Lipumba nae ana haki hiyo naomba wanajukwaa tulimulike swala hili kwa jicho la ndani na mbali.
  1. Pro. Ni mwenyekiti wa chama (High profile leader in CUF), angeweza kutumia vikao halali vya vyama kutoa mwelekeo kwa chama ili CUF ndio itoe mwelekeo wake ndani ya UKAWA. Kitendo cha katibu mkuu, makamu mwenyekiti na viongozi wengine kutojua ya PRO. ni dalili tosha inyoweza kuhitimisha mjadala huu kuwa kuna KITU PRO. AMEKIFICHA
  2. Kitendo cha gazeti la CCM kuwa la kwanza kulipoti habari hii hata kabla ya viongozi wengine wa CUF, UKAWA, na vyombo vingine vya habari hata kabla ya PRO. Hajatoa uamuzi huo unaonesha dhahiri nini LIPUMBA alichodhamilia
  3. Hali ya pro. kuwahadaa viongozi wenzake kuwa hakuna tatizo ndani ya UKAWA mpaka Juma Duni kubadili uanachama kwenda chadema ili awe mgombea mwenza akimuacha na katibu wake mkuu Maalim Seif kuhutubia mkutano mkuu wa CHADEMA wakati alikuwa nae jana yake mpaka saa nne usiku bila kuongea lolote, linatoa maswali mengi ambayo pro. hawezi kuyajibu.
  4. Pro. aliwaaminisha wenzake kuwa kumkaribisha LOWASSA Chadema, ni mafanikio makubwa na ushindi mkubwa, sijajua alimaanisha nini ukilinganisha na KAULI ZAKE ZA LEO
  5. Kama mwenyekiti hakupaswa kujiudhuru bali angesimamia hicho anachokiamini kwa vikao halali vya kichama na viongozi wenzake kuliko sasa ambapo anataka kutuaminisha kuwa VIONGOZI WENZAKE NDIO WASALITI NDANI YA CUF.
  6. Karibuni tutafakari wanajukwaa.
1. Prof namuona ni mnafiki
2. Kwa alichofanya amejishushia heshima hata kama ni uwamuzi ni wake ila sitaki kuamini kama ameamua yeye there is something going on.
3. Ushindi kwa UKAWA bado upo pale pale asubuhi na mapema tunachukua nchi.
 
Mi naona wapinzani hawa bado hawajataka kuchukua hii nchi

Lowasa naye ni mpinzani amekwenda kuusaka uraisi tu. Tatizo la kutojiamini tu kwa Mbowe na baadhi ya viongozi wa Upinzani. Wanasema tatizo mfumo lakini mpaka sasa EL kashabadilisha mfumo wa CHADEMA badala ya kubadilishwa na mfumo wa CHADEMA:
1.Kashabadilisha ilani ya uchaguzi
2. Kabadilisha ratiba ya uchaguzi
3.Kabadilisha gharama za uchaguzi
4.Kasababisha viongozi malegendary kuondoka mf: Prof.Lipumba na Dr.Slaa
5. Kabadilisha kauli mbiu
 
Mbowe kawauza vyama vyote bila kujijuwa. Pale ambae kabaki ni mzee makaidi tu nadhani hata pesa hajapewa maana kwenye Chama yeye mwenyekiti na mkewe Katibu hawana mwanachama hata mmoja sasa ni faida kwa upande wake.
Mbowe ni kiboko yenu. Mtawarubuni wengi sana ila kwa Mbowe mmegonga mwamba.
 
View attachment 273900
Prof. Lipumba akiongea na waandishi wa Habari kwenye Hoteli ya Peacock

Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti kwenye chama chake cha Wananchi CUF.

Ametangaza kuachia ngazi uenyekiti wa chama hicho mapema leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacok.

Amesema amechukua uamuzi huo kutokana na UKAWA kushindwa kusimamia makubaliano yao.

Chanzo: Nipo kwenye kikao

=======


Prof Lipumba akitaja sababu za kujiuzulu nafasi ya uenyekiti CUF


Sentensi za Prof. Lipumba akiwa na waandishi wa habari



Nimejizuia kwa mengi, lakini kwa hili bora niseme nipate amani moyoni! Kwa hatua hii Prof. hukututendea haki! Tutakulaumu hadi dakika ya mwisho, na nakusihi jiandae kupokea tuhuma za "kutumika" kwa manufaaa ya kundi fulani!

Kwa msomi kama wewe, ulipaswa kupima hayo kabla! Umetuingiza mkenge, unakuja na hoja nyepesi, Sijashawishika! Ikiwa wasomi mnawezwa kirahisi namna hii, tusiokuwa na elimu itakuwaje?
 
Last edited by a moderator:
Dr.Slaa is caught kitendo cha Lipumba kujitoa CUF kinamuweka mzee pagumu for any decision kwa kuwa anaingia kundi la wasaliti wakati pengine haikuwa hivyo
 
Ndoto za kuitoa CCM madarakani naona zinaanza kufifia taratibu, ni vigumu sana kwa sasa kuwatoa CCM kwa hali inavyoendelea ndani ya UKAWA maana hawa viongozi wanaoachia ngazi wana wafuasi wao kibao kama ilivyokuwa kwa Lowassa kuhama na baadhi ya wafuasi wake. Watanzania tuna safari ndefu ya kuleta mabadiliko ya kisiasa.
 
Hizo ndo siasa za siasa, nasubir Dr naye aje afunguke likizo ya utawani ikiisha, nafsi inanisuta cc Prof
 
wale wanaoondoka wafanye fasta tunataka kufunga huu ukurasa tuanze mambo ya msingi UKAWA DAIMA
 
waliopewa kitu kidogo akina mbowe,lema ,tundu lissu,na wengineo hamuwaoni? hujui chama kimeuzwa kwa mafisadi?
hongera lipumba kwa uamuzi huu wa busara!

Kama ni kununuliwa,,, basi na lipumba keshachukua chake,,,,,SABABU ZAKE HAZINA MASHIKO,,, juzi kampokea Lowassa vizuri tu tena maneno flani amazing,,, LEO ANAKUJA NA NIMEJIENGUA KWENYE UENYEKITI SABABU UKAWA WAMEKIUKA MAKUBALIANO WAKATI WA MAHAMUZI YA KUJA KWA LOWASSA ALIKUWEPO NA ALIYAPITISHA,,,,,,,,,,AT THE SAME ANAKUJA LEO KUTWAMBIA OH NINAUBARIKI UKAWA NA NITASHIRIKI KAMPENI!!! Huu ni upumbavu mkubwa, UMEJIENGUA KWENYE UENYEKITI BEACAUSE OF UKAWA, kesho unashiriki kampeni hizohizo za ukawa.... HUYU JAMAA KACHUKUA CHAKE NAE,, tusiwe wapuuzi wakujaji wakina mbowe na wenzake wakati kuna wanaofuatia nyuma yao'
 
Back
Top Bottom