Prof. Benson Bana: Maandamano ya UKUTA ni ndoto ya mchana

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
MSOMI maarufu nchini, Profesa Benson Bana na mwanasiasa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, Leticia Mosore wamesema maandamano yaliyopewa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), hayawezekani kwani ni ndoto ya mchana na hayana msingi wowote wala tija kwa wahusika hata kwa Taifa.

Aidha, maandamano hayo ya nchi nzima imeelezwa kuwa ndio kifo cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwani kila chama kimekuwa kikihangaika kivyake.

“Wanaotaka kuandamana wanajidanganya na kuwalaghai wenzao kwani kufanya operesheni ni suala la dola na si la mtu au kikundi cha watu, hivyo maandamano hayo hayawezekani kabisa,” alisema Profesa Bana katika mahojiano maalumu na Idara ya Habari (MAELEZO).

Mhadhiri huyo Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliongeza kuwa wanaojiita Ukuta ni kwamba Rais John Magufuli amewanyima ajenda, kwani utendaji wake umezidi fahamu zao na kuwafanya waanze kutapatapa wasijue nini cha kufanya.

Alisema kama viongozi wa Ukuta ni waungwana, inabidi watamke wazi kuwa wametafakari na kuona kuwa maandamano hayana maana hivyo wameamua kuyasitisha nchi nzima.

Kuhusu utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano, Profesa Bana alisema ni serikali yenye maamuzi ya uhakika na inayowajali watu wote bila kujali itikadi zao za vyama, dini wala makabila hivyo inabidi Watanzania waipende na kuiheshimu.

“Rais Magufuli utendaji wake ni wa kuigwa na viongozi wengi duniani kwani anafanya maamuzi ya uhakika ikiwemo kukuza uchumi kwa kukusanya kodi na kuziba mianya ya ubadhirifu wa mali ya umma,” alisema Profesa Bana.

“Pamoja na kuwa Rais Magufuli amekuwa madarakani kwa kipindi kifupi, viashiria vyote vinaonesha kuwa ni kiongozi imara na shupavu kutokana na mambo makubwa ambayo ameyafanya kwa kipindi hiki kifupi. Katika kipindi hiki kumekuwepo na nidhamu katika utumishi wa umma, kodi inakusanywa kwa kiwango kikubwa na elimu ya msingi inatolewa bure kama Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala inavyosema,” alisema Profesa Bana.

Aidha, Profesa Bana alisema kuwa wanaomlaumu Rais Magufuli ni wale ambao hawajitambui na labda wanaona mianya ya ubadhirifu anayoendelea kuiziba, wao wanakosa mapato, vinginevyo Rais anafanya vizuri katika kuliongoza Taifa.

“Rais Magufuli yuko sahihi kwa jinsi anavyosimamia vipaumbele vya serikali ikiwemo elimu bure, kukusanya kodi na kuzuia mianya ya rushwa pia dhamira ya kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda,” alifafanua Profesa Bana.

Aliitofautisha Serikali ya Awamu ya Tano na awamu nyingine zilizopita kwa kutokuwa na kigugumizi katika kufanya maamuzi ikiwemo ya kuhamia Dodoma, kuondoa wabadhirifu katika utumishi wa umma na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na fedha hizo kutumika kwa miradi ya maendeleo kama miundombinu, afya na elimu.

Kwa upande wake, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR Mageuzi, Leticia Mosore amesema vyama vilivyoko katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimepoteza mwelekeo na vinashindwa kwenda na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Mosore alisema ujio wa maandamano ya nchi nzima yaliyopewa jina la Ukuta, ndio kifo cha Ukawa kwani kila chama kimekuwa kikihangaika kivyake.

Kuhusu Ukawa kupoteza mwelekeo, alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dk Magufuli inayafanyia kazi kivitendo yale yote ambayo yalikuwa ni kero na matatizo yaliyokuwa yakipigiwa kelele na upinzani, na hivyo ingewapasa sasa kufurahia na kumpongeza kwa dhati kwa hatua hizo.

Alisema Ukawa hivi sasa imekuwa ikitoa matamko ya ajabu, imekuwa kama umoja wa kufanya vituko bungeni kila siku wanatoka na kususa, kufunga midomo, mara wavae nguo nyeusi, na hata kuwatimua wale wanaotofautiana nao.

Katika hatua nyingine, Mosore alisisitiza kwamba hatambui kusimamishwa uanachama na uongozi katika chama hicho na ataendelea kufanya majukumu yake kama kawaida kwa kuwa barua aliyopewa haijatoa sababu za hatua hiyo. Alisema hakupewa haki ya kujitetea kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho ya mwaka 1992.

“Ninachoweza kusema kwa ufupi, sitambui kusimamishwa uanachama kwa sababu sijaelezwa sababu za kusimamishwa kwangu wala barua haielezi vifungu vya kikatiba au kanuni zilizotumika kufikia maamuzi,” alisema Mosore.

Uongozi wa wafanyabiashara ndogo maarufu kama ‘wamachinga’ wa soko la Mwenge jijini Dar es Salaam, umesema hauungi mkono maandamano ya Ukuta kwa kuwa maandamano hayo si halali kisheria. Uongozi huo, umesema maandamano hayo hayana uhalali wa kisheria kwa kuwa tayari Jeshi la Polisi nchini limeyazuia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa soko hilo, Omari Hamisi alisema hawapo tayari kuumizwa na askari Polisi kwa sababu ya maandamano hayo ya Ukuta.

Alisema wafanyabiashara hao wanamuunga mkono Rais John Magufuli kwa kutojihusisha na maandamano hayo na badala yake wataendelea na kazi yao ya kufanya biashara ikiwa ni njia ya kutekeleza kaulimbiu ya rais huyo ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Kiongozi huyo, alibainisha kuwa Dk Magufuli tangu aingie madarakani, amekuwa akiwatetea wanyonge hasa wafanyabiashara ndogo hivyo kujihusisha na maandamano hayo ni sawa na kumsaliti. Alisema rais huyo alionesha wazi nia yake ya kutetea wanyonge alivyozungumza hivi karibuni na wananchi wa Mwanza na baadaye Dar es Salaam ambako alielezea mikakati na mipango ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwasaidia na kuwakomboa wanyonge.

“Dk Magufuli ameonesha nia ya dhati kutetea wanyonge sasa leo hii tukiandamana na kuunga mkono maandamano yaliyozuiwa na Polisi ni sawa na kumsaliti,” alisema.

“Ukuta ina maana gani na faida gani kwetu? Nchi yetu ni moja, taifa letu ni moja, sisi ni wamoja hivyo hatukubali kufanya maandamano yasiyo na tija kwetu na taifa pia,” alisisitiza na kueleza kuwa wafanyabiashara hao wameshtuka na kuchoshwa na kitendo cha wanasiasa kuwatumia vijana wachache kwa faida yao binafsi.

Maandamano ya Ukuta yaliyoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yakilenga kupinga kile wanachokiita udikteta wa Serikali ya Rais Magufuli yanatarajiwa kufanyika kesho nchi nzima. Polisi na vyombo vingine nchini vimetangaza kuwa maandamano hayo si halali.

Chanzo: Habari Leo
 
Bana is nonsense of all wasomi in Tanzania. Jitu zima linajikomba kama jike! Hopeless Haya guy- !
 
S͢o͢u͢rc͢e͢ y͢e͢n͢y͢e͢w͢e͢ J͢a͢m͢b͢o͢ L͢e͢o͢, m͢w͢o͢n͢g͢e͢a͢j͢i͢ m͢w͢e͢n͢y͢e͢w͢e͢ B͢a͢n͢a͢n͢a͢!!?
 
Profesa bana bado anatazama vitu in one dimension ngoja na hao machinga siku wakitiwa dol* la udukuzi ndo wataelewa naona sasa hivi wanajifanya wanajua sheria.
 
Hivi chuo cha CCM kilichokuwa Kivukoni bado kipo ? Huyu msomi anaelekea amekunywa maji ya bendera ya CCM.
Enzi za Chama kushika hatamu tukiwa shuleni walipita pita kutupasha upupu wa zidumu fikra za Mteuliwa namba mmoja.
Poor Professor wakati mwingine inakubidi japo useme NO COMMENT haitakupunguzia mshahara wako wala posho yako,bali utapunguziwa lawama zisizo za lazima.
 
Proffesaa mzima lakini hajui kusoma namba za Ukuta.
Hawezi kujua kuwa ukuta tayari unafanya kazi
Jina la ukuta hakuna neno maandamano
Ni umoja wa kupinga udikteta tanzania.
Ni slogan ambayo imezagaa
Na watu wameicheza ngoma
Kila mtu kataharuki
Hivyo ukuta tayari tayari wameandaman kwa njia za ajabu na ajenda kujulikana
Wasomi wamekaa kujadili ukuta kama huyo Bana
Masheikh na Makasisi wamekaa kujadilili ukuta
Wanasiasa wamekaa
Wazee wamekaa
Kila mtu kashughulika na ukuta....na masage yao tayari imejulikana kutokana na reaction zake na hatua zinazo chukuliwa na walalamikiwa...
Sidhani kama kuna maandamano ya kutrmbea mitaani ....hilo halipo...ni maandamano ya aina yake ambayo yamebuniwa kisayansi.
 
Dah
Kwa kihaya mtu akiwa anaitwa bana inamanisha Mtoto tumuache akikua atakuwa mkweli kwa sasa bado anataka pesa za pipi na chocolate
Kunawatu uwa wanachwnganya Dr bana sio mhaya hukuna mhaya mwenye mawazo mgando kama huyu...
 
Shida ya nchi hii ni kwamba kila mtu anaweza kuwa Profesa. Bana ambaye alijulikana kwa uwezo mdogo, ambaye kwaajili ya urahisi alikimbilia kusomea DS (development Studies) pale University of Dar es Salaama, leo ni professor ambaye hata waandishi wa habari wanaona anafaa kuhojiwa kwaajili ya kuwakilisha mawazo ya wasomi.

Kwa kipimo chochote, kama nataka kupata wazo lolote la hekima, Bana hawezi kuwa ni mtu ambaye naweza kumfikiria, ni aheri nikawaulize wazee wenue hekima kijijini kuliko a comedian professor.
 
Back
Top Bottom