nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Kada wa chama cha mapinduzi na mwanasiasa mkongwe nchini Prince Bagenda amekishambulia chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kwa operesheni yake ya M4C inayotishia uhai wa CCM.
Katika makala yake ndani ya gazeti la RAI Prince Bagenda amedai M4C ni chama kipya cha siasa ndani ya CDM na kusema hali hiyo ni hatari kubwa kwa ukuaji wa chama hicho na amesema utatokea mvutano mkubwa kati ya wafuasi wa CDM na wafuasi wa itikadi ya M4C.
Bagenda pia amesema kampeni ya M4C wanayoongoza nchi nzima inatangaza sera za shari na chuki.Pia amesema CDM walipata kura nyingi uchaguzi mkuu uliopita kutokana na vita ya makundi ndani ya CCM na kamwe si kutokana na chama hicho kuwa na sera nzuri.Amesema CDM hawana Itikadi inayoeleweka hadi sasa ndiyo maana mpaka sasa wajanja kama yeye wako CCM.
Source:RAI Alhamisi
My Take:
Prince Bagenda alishiriki kusambaratisha chama cha NCCR Mageuzi baada ya kuongoza mgogoro mkubwa huku akikimega chama vipande viwili na yeye akiwa Katibu Mkuu kambi ya Mrema.Baada ya kufanikisha kusambaratisha NCCR,Prince Bagenda alihamia CCM ambapo hadi leo yeye ni kada mwaminifu wa CCM.
Nilikuwa nawaza Amekwenda wapi PRINCE BAGENDA? Kumbe kaanzisha Chama kingine
Ndani ya CCM; kwahiyo yeye ni M4C copy upande wa CCM; CCM wajichunge asiwasambaratishe
kama NCCR Mageuzi... Ana Chuki Kweli...