Prince Bagenda ashambulia vikali M4C ya CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Kada wa chama cha mapinduzi na mwanasiasa mkongwe nchini Prince Bagenda amekishambulia chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kwa operesheni yake ya M4C inayotishia uhai wa CCM.
Katika makala yake ndani ya gazeti la RAI Prince Bagenda amedai M4C ni chama kipya cha siasa ndani ya CDM na kusema hali hiyo ni hatari kubwa kwa ukuaji wa chama hicho na amesema utatokea mvutano mkubwa kati ya wafuasi wa CDM na wafuasi wa itikadi ya M4C.
Bagenda pia amesema kampeni ya M4C wanayoongoza nchi nzima inatangaza sera za shari na chuki.Pia amesema CDM walipata kura nyingi uchaguzi mkuu uliopita kutokana na vita ya makundi ndani ya CCM na kamwe si kutokana na chama hicho kuwa na sera nzuri.Amesema CDM hawana Itikadi inayoeleweka hadi sasa ndiyo maana mpaka sasa wajanja kama yeye wako CCM.

Source:RAI Alhamisi

My Take:
Prince Bagenda alishiriki kusambaratisha chama cha NCCR Mageuzi baada ya kuongoza mgogoro mkubwa huku akikimega chama vipande viwili na yeye akiwa Katibu Mkuu kambi ya Mrema.Baada ya kufanikisha kusambaratisha NCCR,Prince Bagenda alihamia CCM ambapo hadi leo yeye ni kada mwaminifu wa CCM.
 
Aiseee baba yangu mwambie yeye si mjanja,mjanja yoyote awezi kufumbia macho wezi wa mabilioni

ngoja nianze na mbege kwanza
 
Huyo siyo mjanja. wajanja wanavua gamba na kuvaa gwanda
 
Ni bora hata angezungumzia operation vua gamba ya CCM na atupe tathmini yake kuliko kuzungumzia asiyoyajua wala hasiyomuhusu.

Mnafiki huyu hana lolote, aende zake akamshauri Mukama namna ya kufanya siasa.
 
M4C inatisha kwa kweli.Tutaona 'maiti' zote za kisiasa za CCM zinafufuliwa kuja kujibu mapigo maana wote walio hai CCM wameshindwa kukabili huu moto.

So CCM who is next,Mangula? Msabaha? Lamwai? Bring 'em on!
 
Huyu jamaa tunamfahamu sisi tunaotokea Mleba Rubya na siasa alizotufanyia na akatutelekeza wanamsalimia Ilambika.
 
Ni bora hata angezungumzia operation vua gamba ya CCM na atupe tathmini yake kuliko kuzungumzia asiyoyajua wala hasiyomuhusu.

Mnafiki huyu hana lolote, aende zake akamshauri Mukama namna ya kufanya siasa.

Namshangaa anahangaika nini na CDM.Anatoa povu jingi for nothing
 
Kipindi flani nilisafiri na Bagenda kwenda kwenye moja ya mikutano ya Wanaharakati wa umoja wa Afrika (Mkutano uliotengeneza Azimio la Tripoli-Libya).

Tulizungumza mengi lakini nakumbuka tukiwa kwenye hoteli moja Zurich, Uswiss aliniambia, "Siasa za Tanzania hazihitaji akili nyingi.

Mimi nina watu wangu nikiwalenga wananipa hela maisha yanaenda.Kwanza mimi mwenyewe mgonjwa (Sikuchunguza ni ugonjwa gani alimaanisha) kuna hoja ukiibua hata ukimfuata mtu anakupa hela".

From there nilimu dump Bagenda Prince totally.
Itanichukua miaka ya kuzimu kujadili hoja za huyu (Old man)
 
Huyu jamaa tunamfahamu sisi tunaotokea Mleba Rubya na siasa alizotufanyia na akatutelekeza wanamsalimia Ilambika.

Inadaiwa yeye ndiye aliongoza ile vurugu ktk halmashauri kuu NCCR pale Raskazone Tanga.
 
My Take:
Prince Bagenda alishiriki kusambaratisha chama cha NCCR Mageuzi baada ya kuongoza mgogoro mkubwa huku akikimega chama vipande viwili na yeye akiwa Katibu Mkuu kambi ya Mrema.Baada ya kufanikisha kusambaratisha NCCR,Prince Bagenda alihamia CCM ambapo hadi leo yeye ni kada mwaminifu wa CCM...........[/QUOTE]

I know this "PRINCE" when following his writings oftentimes you will doubt his SANITY!
 
Kipindi flani nilisafiri na Bagenda kwenda kwenye moja ya mikutano ya Wanaharakati wa umoja wa Afrika (Mkutano uliotengeneza Azimio la Tripoli-Libya).. Tulizungumza mengi lakini nakumbuka tukiwa kwenye hoteli moja Zurich - Swiss aliniambia "Siasa za Tanzania hazihitaji akili nyingi..Mimi nina watu wangu nikiwalenga wananipa hela;Maisha yanaenda.. Kwanza mimi mwenyewe mgonjwa..... (Sikuchunguza ni ugonjwa gani alimaanisha) kuna hoja ukiibua hata ukimfuata mtu anakupa hela".

From there nilim dump Bagenda Prince totally!.
Itanichukua miaka ya kuzimu kujadili hoja za huyu (Old man)

Thankyou for this useful post.......
 
Huyu mzee aliheshimika sana enzi akiwa mpinzani lakin njaa haina adabu.Naungana na wasemaji wengine, sijui anawashwa na nini kama ukizuka mgogoro ndani ya chadema unamuhusu nini.cjawahi ona wahaya wajinga huyu ni wakwanza
 
Huyu naye si aende kule kijijini ajue moja...bado yupo kwenye hizi siasa?
we, usicheze na njaa na ukichukulia kwa sasa migomba kule Rubya inaharibiwa na ugonjwa wa 'mnyauko'.
Lakini ninachokumbuka juu ya Price Bagenda alikuwa mtu mwenye akili sana ila inaonekana sasa kaamua 'kufaidika' nazo peke yake badala ya kushare na Watanzania wenzie
 
Back
Top Bottom