Prince Bagenda ashambulia vikali M4C ya CHADEMA

Pia ni mjinga sana mbona asitetee wahaya na wao walipwe fidia ya migomba yao kama wakuleeeee wanaolipwa Ng'ombe baada ya kufa kwa ukame anakuja na agenda za kizamani tena za mkoloni kweli wameshikwa pabaya mbaka 2014 watakuwa wamechanganyikiwa
hivi kabla ya kuandika kitabu cha 'Tumaini lililolejea' alishawahi kabla ya hapo kuandika hata makala kuelezea ni jinsi gani jamii yake imeporomoka kimaendeleo (uchumi/elimu) na ni jinsi gani ya kurudisha (restoration) hiyo hali!?
 
Aina ya Prince na uandishi uliojaa hoja njaa za kinafiki na kujipendekeza nj kudharilisha taaluma ya uandish.prince arudi akakalie kiti cha utwana enzi za wafalme
 
Kada wa chama cha mapinduzi na mwanasiasa mkongwe nchini Prince Bagenda amekishambulia chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kwa operesheni yake ya M4C inayotishia uhai wa CCM.
Katika makala yake ndani ya gazeti la RAI Prince Bagenda amedai M4C ni chama kipya cha siasa ndani ya CDM na kusema hali hiyo ni hatari kubwa kwa ukuaji wa chama hicho na amesema utatokea mvutano mkubwa kati ya wafuasi wa CDM na wafuasi wa itikadi ya M4C.
Bagenda pia amesema kampeni ya M4C wanayoongoza nchi nzima inatangaza sera za shari na chuki.Pia amesema CDM walipata kura nyingi uchaguzi mkuu uliopita kutokana na vita ya makundi ndani ya CCM na kamwe si kutokana na chama hicho kuwa na sera nzuri.Amesema CDM hawana Itikadi inayoeleweka hadi sasa ndiyo maana mpaka sasa wajanja kama yeye wako CCM.

Source:RAI Alhamisi

My Take:
Prince Bagenda alishiriki kusambaratisha chama cha NCCR Mageuzi baada ya kuongoza mgogoro mkubwa huku akikimega chama vipande viwili na yeye akiwa Katibu Mkuu kambi ya Mrema.Baada ya kufanikisha kusambaratisha NCCR,Prince Bagenda alihamia CCM ambapo hadi leo yeye ni kada mwaminifu wa CCM.

Ana ujanja gani? kaishiwa tu kama yeye ni kada wa CCM basi aache kuongelea ya CDM! Pilipili hajaila anawashiwa nini?
 
Huyo ni mganga njaa tu dat why yupo RAI mpaka leo..!! Akili yake ishanunuliwa long time i doubt now anafikiria kwa kutumia kiungo gani cha mwili...!!
 
Pia ni mjinga sana mbona asitetee wahaya na wao walipwe fidia ya migomba yao kama wakuleeeee wanaolipwa Ng'ombe baada ya kufa kwa ukame anakuja na agenda za kizamani tena za mkoloni kweli wameshikwa pabaya mbaka 2014 watakuwa wamechanganyikiwa....................................


Ulichoandika umenitonesha kidonda maana anawapa watu faida ya bure.

Kwanza anajisahau badala ya kutumia chombo cha habari kutetea mambo ya maana yanayosumbua Watanzania yeye anaponda mkakati unaowatoa Watanzania kwenye usingizi wa pono na wale ambao kidogo wameuona mwanga wanatambua haki zao through M4C.

Lakini kikubwa anatuangusha watu tunaotoka Bukoba, as he has joined the bandwagon of Salva Rweyemamu.

Just imagine yule Salva wa Habari Corporation ya Jenerali Ulimwengu na sasa hivi. Ukisoma makala za kabla mwaka 2000 na ukamwangalia Salva wa kueleka uchaguzi wa 2005 na wa leo unaweza ukafikiri unadanganywa.

Wahaya wanamsemo "enaku ozitelaho akashweko", tafsiri isiyo rasmi kuwa njaa jaribu kuisetiri kidogo.

Napata tabu hawa wazee wameshindwa kuivalia shuka. Sasa ujumbe huu labda umfikie kuwa kwenye jamii ya Tanzania ambayo CCM imewafanya watu kuangukia value judgement hata ajikombe namna gani ataendelea kuhukumiwa kwa vigezo ambavyo watu wamejiwekea tayari japo sio rasmi.

Doa la kuwa na double standards na kuiua mbegu ya mageuzi ambayo ilikukweisha pandwa litamwandama kokote atakokokwenda.

CDM through M4C imelenga kuifufua mbegu iliyouawa na kina Bagendas badala ya kuona nyota njema yeye anabeza. Watanzania mdharau mtu wa aina na watu wa aina yake
 
Huyu Bagenda anataka tumtukane then JF ionekane ni forum ya matusi au tupigwe ban ili tuikose movie ya Ulimboka.
najitoa rasmi kwenye uzi huu
 
Bila kuingia katika siasa za kushambulia mtu, tuliomfuatilia Bagenda siku nyingi tunajua yuko ndani ya CCM kama mtumikia ajira (si kama mwanasiasa). Mwenyewe haamini hicho anachokisema. Anaujua ukweli lakini anatimiza wajibu. Mchangiaji Deus Mallya hapo juu amemuelezea vizuri kwa kiasi kikubwa. Hivyo kauli zake si za kupotezea muda sana labda kama mtu una kipaji (au dau kubwa zaidi la fedha) kiasi cha kumshawishi mnafiki abadili "mtazamo".
 
Hivi huyu alishaacha kazi kule TISS?? Au naye anaendelea kama mzee wa Kiraracha?

Hata hivyo, hana jinsi zaidi ya kutumikia wale wanamuweka mjini!!

Ila ingekuwa bora akajikita kujadili yale mambo anayoyajua vizuri kuliko kudandia treni kwa mbele. Na hata hivyo, inaonesha ana hang over ya kutisha....Anaposema kuwa makundi ndani ya lichama lao la CCM yalinufaisha CHADEMA, ana maana kuwa kwa sasa makundi hakuna??

Ni bora akakaa kimya ili tuzidi kumsahau.....Hivi hawa jamaa wa BKB wana matatizo gani??....au ndo mwendo wa kutafuta mkate kama ndugu zake Salva na Mhingo Rweyemamu?.................

Kama wanafikiria vizuri wanajuta maana huwezi mtu kufanya character assassination waliyofanya kwa kutumia magezi halafu ukazawadiwa kuwa mtu wa kufanya filtering ya habari mnaita censure wanahabari wakati wengine ambao hawakutumia nguvu tena sio ya kuchafua sifa za watu wapo wanakula kuku kama mawaziri, wakurugenzi, mabalozi nk.

Wakipita sehemu wanapata hata maji ya kunywa lakini hawa inabidi kwanza wajiangalie sana maana kuna wakati watapigwa mayai viza kwa kutuuzia Mbuzi kwenye gunia na wakaishia kupewa nafasi ya propaganda uchwara na kulipaka kabila lao matope wakiongezea kwenye value judgement and stereo type
.
 
M4C itawaunguza wengi, walisema wapinzani ni vyama vya msimu sasa wanahaha.

Ama kweli wameshikwa pabaya,yeye ni kada wa nyinyiemu na siyo msemaji wa CDM, so aezeke nyumba yake kwa jirani hapamhusu.
 
Masikini tanzania yangu, kila kada anaihofia cdm kuliko umasikini tulio nao, hakuna kada anayewasemea wakulima, wafanyakazi, wafugaji, wamachinga, wavuvi, walemavu, watoto wadogo kwenye migodi na makundi mengine yanayoyimwa haki. Nani alituloga?
 
Kada wa chama cha mapinduzi na mwanasiasa mkongwe nchini Prince Bagenda amekishambulia chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kwa operesheni yake ya M4C inayotishia uhai wa CCM.
Katika makala yake ndani ya gazeti la RAI Prince Bagenda amedai M4C ni chama kipya cha siasa ndani ya CDM na kusema hali hiyo ni hatari kubwa kwa ukuaji wa chama hicho na amesema utatokea mvutano mkubwa kati ya wafuasi wa CDM na wafuasi wa itikadi ya M4C.
Bagenda pia amesema kampeni ya M4C wanayoongoza nchi nzima inatangaza sera za shari na chuki.Pia amesema CDM walipata kura nyingi uchaguzi mkuu uliopita kutokana na vita ya makundi ndani ya CCM na kamwe si kutokana na chama hicho kuwa na sera nzuri.Amesema CDM hawana Itikadi inayoeleweka hadi sasa ndiyo maana mpaka sasa wajanja kama yeye wako CCM.

Source:RAI Alhamisi

My Take:
Prince Bagenda alishiriki kusambaratisha chama cha NCCR Mageuzi baada ya kuongoza mgogoro mkubwa huku akikimega chama vipande viwili na yeye akiwa Katibu Mkuu kambi ya Mrema.Baada ya kufanikisha kusambaratisha NCCR,Prince Bagenda alihamia CCM ambapo hadi leo yeye ni kada mwaminifu wa CCM.

Na yeye si aungane na nape kueneza sera za ccm? Watu wengine bwana wanabore tunataka kusikia sera za chama na sio malalamishi yasiyo ya msingi
 
Kwanza lile gazeti la fisadi Karamagi alilokuwa akilihariri liliishia wapi? gazeti hilo lilikuwa linamtetea Karamagi na mafisadi wengine. Nasikia alitafuna sh 80 milion za huyo fisadi halafu akamtimua. Amshukuru hakumpeleka polisi!

Inawezekana makala hiyo ni njia moja ya kumpigia honi mjamaa wa Magogoni kwamba amemsahau sana ukuu wa wilaya... kwi kwi kwi....

Kweli njaa kali -- inapoteza utu wa mtu!

halafu hapo alipo New habari nasikia yeye na AlShabab (Bashe) hawaelewani kabisa!
 
Back
Top Bottom