Press Release Leo: Serikali Isitishe Mara Moja Ujenzi wa Bomba la Gesi kwenda Dar- Wana Mtwara

Ha ha ha
Tazara about 1860 km dollar 200 million
Pipeline about 500 km dollar one billion

Dr , economist, billionaire, president, honorable Jakaya Mrisho Kikwete

...........wee unafikiri tutaendeshaje vyombo vyetu vya dola.........au unafikiri tutasafiri vipi na delegation kwenda kuomba misaada.........
 
Wanaosema bomba la gesi lisijengwe kwenda Dar na huku wanasema kuwa dai lao siyo wananchi wengine wasifaidi faida za gesi ya Mtwara, wanaelewa wanachoeleza? Bomba la kupeleka gesi Dar es Salaam siyo tu kwaajili ya kuzalishia umeme tu bali ni pamoja na gesi inayoweza kutumika kuendeshea magari, gesi ya kupikia majumbani, gesi ya kuendeshea jenereta za umeme kwa viwanda vinavyotaka kuzalisha umeme wao, n.k.

Kama bomba halijengwi kwenda Dar, hiyo gesi ya matumizi mengine zaidi ya kuzalishia umeme itasafirishwa kwa njia gani? Iende kwa malori mpaka Dar, halafu kwa malori mpaka Sumbawanga? Tuna matatizo Watanzania, tunaongea mengi lakini yenye ukweli na faida za kiuchumi ni machache sana. Tuzungumzie wananchi wa Mtwara kunufaika na ugunduzi wa gesi huko Mtwara lakini siyo lazima faida hiyo iendane na kutojengwa kwa bomba la gesi kwenda Dar.

Maelezo sahihi kabisa. Inaelimisha vizuri.

TUJIULIZE lini serikali yetu itajifunza kusema ukweli na kuacha kupotosha uma? Kweli hii serikali ni baba wa uongo. Ki biblia baba wa uongo ni Lusiferi mwenyewe.

Tuwaunge mkono wananchi wa Mtwara, umeme uzalishwe pale na matumizi ya msingi ya gesi ifanyiwe pale. Tujiulize ipi rahisi kusafirisha gesi au umeme. Ipi aghali kusafirisha gesi au umeme. Manufaa ya kuzalisha na kusafirisha umeme ni mkubwa sana.

Serikali ya kifisadi, kila kitu ni manufaa binafsi. Aibu yako sisiem
 
Wanaosema bomba la gesi lisijengwe kwenda Dar na huku wanasema kuwa dai lao siyo wananchi wengine wasifaidi faida za gesi ya Mtwara, wanaelewa wanachoeleza? Bomba la kupeleka gesi Dar es Salaam siyo tu kwaajili ya kuzalishia umeme tu bali ni pamoja na gesi inayoweza kutumika kuendeshea magari, gesi ya kupikia majumbani, gesi ya kuendeshea jenereta za umeme kwa viwanda vinavyotaka kuzalisha umeme wao, n.k.

Kama bomba halijengwi kwenda Dar, hiyo gesi ya matumizi mengine zaidi ya kuzalishia umeme itasafirishwa kwa njia gani? Iende kwa malori mpaka Dar, halafu kwa malori mpaka Sumbawanga? Tuna matatizo Watanzania, tunaongea mengi lakini yenye ukweli na faida za kiuchumi ni machache sana. Tuzungumzie wananchi wa Mtwara kunufaika na ugunduzi wa gesi huko Mtwara lakini siyo lazima faida hiyo iendane na kutojengwa kwa bomba la gesi kwenda Dar.

Nilielewa hivyo, na hiyo ni sahihi kabisa kama lengo ni hilo.

Kufuatana na maelezo ya serikali yenyenyewe lengo la msingi kupeleka gasi Dar si hiyo, ni umeme. Sasa tuweke ushabiki nyuma tusimamie ukweli, Je ni manufaa kuzalishia umeme Dar au Mtwara. Umeme uzalishwe Mtwara na gesi ipelekwe Dar kwa matumizi mengine.

Tatizo serikali ni ONGO

 
Safi sana. Majibu ya serikali saa zote inapokosa hoja huwa ni kejeli na kusingizia wanasiasa kana kwamba wanasiasa sio raia wenye haki ya kuhoji au kutoa maoni yao. Serikali hailimi korosho lakini ndio inayosimamia na kuamua juu yake. Wananchi kusini wanateseka. Reli iling'olewa! Barabara toka nimezaliwa mpaka sasa nazeeka haiishi! Nyingine zinajengwa na kuzinduliwa ndani ya miaka mitatu tu! Kusini wamekosa nini? ya bagamoyo msata itaisha hivi karibuni lakini ya Mtwara - Dar hadi Yesu arudi! Barabara ya mabasi yaendayo kasi inajengwa kwa kasi itakwisha hivi karibuni lakini ya Mtwara ni tamithiliya isiyoisha kama Egoli na Isidingo!
 
Halafu kuna watu wanaweza kuja kutetea watu wanaokuja na kejeli kama hizi kwa serikali iliyochaguliwa na watanzania kuwafanyia na kuwategenezea mipango ya maendeleo, kama si sawa wasubiri uchaguzi ujao wasiwapigie kura hawa wasasa kwakuwa hawatimizi au angalia maslahi yao lakini hawana haki ya kuiamuru serikali.

sawasawa wasepwe kunako husika on cubic walls.
 
Wahenga walinena "Haki haiombwi bali watu wanadai Haki". Ndg zetu wa kusini kazeni misuli ama sivyo mtaachwa kama wenzenu walio katika migodi ya madini wanaachiwa Mahandaki na milima isiyo na tija kwao.
Suluhisho la kudumu ni kubadilisha utawala mwaka 2015 na kuingiza Chama chenye sera ya Majimbo ambayo ndiyo mwarubaini wa matumizi ya Rasilimali za kila maeneo ya nchi yetu.
 

Fungua attachment[/LEFT]

kwani mtwara hakuna kiwanda cha kuzalisha umeme au hakuna mtambo wa kuzalisha umeme???na je umeme unaotumika mtwara ,lindi,masasi,nachingwea,ruangwa na sasa unasambazwa katika wilaya liwale etc ..unavuliwa na maji au gas hiyo ya mtwara????....
naona sasa mnakuja ambapo serikali inataka ..safi jk... tatizo moja wanaharakati na wanasaisa wa tz wanakurupuka sana hawasomi hata kidogo.... hivi bandari ya mtwara,kilwa,lindi inapanuliwa kwa ajili ya nini??... hivi kujenga mtambi wa uzalishaji umeme mtwara ndo kunaleta maendeleo ???au kuna takiwa kuanzishwa viwanda vingi etc... na umeme si tayari upo mtwara na unafuliwa kwa gas hiyo hiyo ba bado inatumika kwa kiwango kidogo sana...
 
kwani mtwara hakuna kiwanda cha kuzalisha umeme au hakuna mtambo wa kuzalisha umeme???na je umeme unaotumika mtwara ,lindi,masasi,nachingwea,ruangwa na sasa unasambazwa katika wilaya liwale etc ..unavuliwa na maji au gas hiyo ya mtwara????....
naona sasa mnakuja ambapo serikali inataka ..safi jk... tatizo moja wanaharakati na wanasaisa wa tz wanakurupuka sana hawasomi hata kidogo.... hivi bandari ya mtwara,kilwa,lindi inapanuliwa kwa ajili ya nini??... hivi kujenga mtambi wa uzalishaji umeme mtwara ndo kunaleta maendeleo ???au kuna takiwa kuanzishwa viwanda vingi etc... na umeme si tayari upo mtwara na unafuliwa kwa gas hiyo hiyo ba bado inatumika kwa kiwango kidogo sana...

My question exactly!! Artumas walishatengeneza kiwanda cha kubadili gas kuwa umeme long time!!! Lindi na Mtwara na vitongoji vyake vina MW12 kati ya uwezo wa MW18 tayari in place!! Wakati watu Dar na TZ yote kwa ujumla wanalalamika kukatwa umeme mara kwa mara hawa ndugu zetu Mtwara na Lindi hawajui wala kuielewa situation kama hii!!

Hii "Press Release" ninaweza kuijibu hivi (in red):

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MADAI YA WANAMTWARA KUSHINIKIZA KUCHAKATWA KWA GESI KATIKA MJI WA MTWARA NA KUTOSAFIRISHA GESI GAFI KWA BOMBA KWENDA DAR ES SALAM.
TAREHE 07-01-2013.


Ndugu waandishi wa Habari kwanza ningependa kuwashukuru sana kwa kuitikia wito wenu kuja hapa leo kuyasikiliza yale ambayo nimekusudia kuyaongea.
Pili ningependa kuwapongeza sana kwa namna mnavyoripoti habari hizi kila wakati bila kuchoka na kuyafuatilia matukio na kueleza hoja na hisia za wananchi wa Mtwara kila kunapokucha.

......................................

Naomba kuchukua nafasi hii kueleza kuwa WANANCHI WA MKOA WA MTWARA HAWAPINGI WANANCHI WA MIKOA MINGINE KUNUFAIKA NA FAIDA ZA GESI BALI KINACHOPINGWA NI KUSAFIRISHA GESI GAFI TOFAUTI NA AHADI YA SERIKALI YA KUJENGA MTAMBO WA KUZALISHA UMEME MKOANI MTWARA UTAKAOVUTIA WAWEKEZAJI WA VIWANDA.UMEME HUU UNAWEZA KUSAFIRISHWA KWENDA MAHALI POPOTE TANZANIA/NJE YA NCHI BAADA YA MTAMBO KUJENGWA MTWARA.
Naomba kukumbusha kuwa madai haya hayajotoka hewani,bali yametokana na sababu kadhaa:
1.---- Ni ahadi za mara kwa mara zilizokuwa zilizotolewa na Mh.Rais na mawaziri wa Nishati na Madini katika nyakati tofauti.Tangu mara ya kwanza Mh.Rais alipohojiwa clouds(kipindi cha power breakfast) tarehe 29 october katika- kampeni ya mwaka 2010,pia alipokuja kwenye kampeni Mtwara na hata alipokuja kushukuru baada ya kuwa Rais aliendelea kuahidi kuufanya Mtwara kuwa mji wa viwanda kwa kuupatia umeme wa uhakika kupitia ugunduzi wa gesi hii,pia alieleza katika kipindi hicho cha radio kusudio la serikali yake kujenga mtambo wa 300MW.Hii yote ilitengeneza matumaini makubwa kwa wananchi wa Mtwara wa kufaidika na gesi hii.Leo tunaposikia gesi ghafi inahamishwa na bado hakuna mtambo huo wala kiwanda sawa na ahadi zilivyotolewa,kuna kosa gani wananchi wakihoji?
Mtambo ulishajengwa kuhudumia Mtwara & Lindi na vitongoji vyake
http://www.wentworthresources.com/pd...%20Project.pdf.

2.---- Mpango wa Mtwara power project uliolenga kuufanya mradi huu kuwa sehemu ya National power Development plan(3920MW) ukilenga kuwa na mtambo wa kuzalisha 300MW Mtwara zitakazoingizwa katika gridi ya Taifa na kuondoa tatizo la umeme nchini uliokuwa umelenga kukamilika mwaka 2012.Ingawa ni wazi kuwa kampuni iliyokuwa itekeleze mradi huu Artumas ilishindwa kutokana na mtikisiko wa kiuchumi wa mwaka 2008,iliweka bayana kuwa ingepata dola za kimarekani milioni 7 ingeweza kuutekeleza.Kwa nini serikali haikuweka kama sharti mojawapo kwa kampuni ya Wentworthy resource Limited iliyoinunua artumas kuutekeleza mradi huu uliokuwa umekubalika kuingia katika mpango wa kitaifa?kwa nini uliachwa?Hili nalo hatuna majibu kama ilivyo kwa mipango mingine kama vile Mtwara Corridor.

refer to this link: http://www.wentworthresources.com/pd...ual_Report.pdf



  1. Refer to FIG 3. PROPOSED CONNECTION FROM MTWARA ENERGY PROJECT TO NATIONAL GRID Artumas is engaging the Government of Tanzania and the state electricity utility, TANESCO, on a fast tracking of this power project and high voltage connection to the National Grid. Discussions have commenced with large industrial customers that would support a significant share of this new electricity supply. (Page 16 (18) Artumas Group Inc. Annual Report 2006)
  2. Refer to page 20 & 21 (22 & 23 of copied document) clearly shows what you are advocating i.e building a plant in Mtwara to join to the national grid


3.---- Ikumbukwe kuwa kisiwa cha songosongo ndio eneo la kwanza kugunduliwa kwa gesi asilia mwaka 1974 na kampuni ya AGIP kukiwa na takriban cubic feet 783 billion.Kati ya mipango mingi iliyowekwa kwa wakati huo kuhusiana na kubadilisha maisha ya wanasongosongo na kilwa kwa ujumla ni kujenga kiwanda cha mbolea KILWA AMMONIUM COMPANY,kilicholenga kutatua tatizo la ajira na kutosheleza uzalishaji wa mbolea nchini.Waliambiwa wasiwe na hofu gesi kwenda Dar es Salaam kwani viwanda vitajengwa kilwa,Ingawa eneo lilitengwa kwa ujenzi wa kiwanda hicho na wataalamu kusomeshwa,hadi hivi leo kiwanda hakijajengwa. Hivi hali kama hii haitoshi kuleta wasiwasi kwa wananchi?kuna tatizo gani wakihoji jambo hili?Waswahili husema ukiona mwenzako ananyolewa,wewe tia maji.
Kama viwanda hivi vitafanikiwa vitaleta tija na ulazima wa kuifufua bandari ya Mtwara ambayo tangu mwaka 2006/2007 imekuwa ikitumika kwa 31% ya uwezo wake(Tani 122,862 kwa mwaka badala ya tani 400,000 kwa mwaka).Mbinu hii itasaidia kupunguza msongamano wa bandari ya Dar kama ambavyo nchi Jirani ya Kenya wamefanya kwa kuipanua bandari ya Lamu ili kupunguza msongamano bandari ya mombasa.

Huwezi kujenga kiwanda wakati malighafi bado haijaanza kuvunwa!! Navyoelewa mimi ni gas kwanza na viwanda vya mbolea vinafuata - au? Kwa upande mwingine maendelezi ya bandari, kiwanda cha LNG, kilimo etc vyote vimetajwa humu:http://www.ecfa.or.jp/japanese/act-pf_jka/H21/JDI_tanzania/english.pdf.


4.---- Hoja nyingine ni ya kihistoria,Tangu tupate uhuru watu wa kusini wamesota katika janga la kukosa nishati ya umeme -kwa muda mrefu na hawakuunganishwa na gridi ya taifa kwa sababu lukuki ingawa iliwezekana kuvusha umeme baharini kwenda Zanzibar ilishindikana kuuleta Mtwara.Kama wameweza kusahauliwa kwa miaka 51 katika swala la nishati,hofu ni kuwa gesi itakapoisha vizazi vyao vitasahauliwa tena kwa kubaki na bomba tupu,na hakuna atakayekumbuka tena kuunganisha mikoa hii na Gridi ya Taifa ili kuwa na umeme wa uhakika ambao ndio hitaji kubwa mojawapo la wawekezaji.Hoja ya gesi kuwa nyingi sana na itachukua muda mrefu kuisha- haina mashiko kwani hata dhahabu tuiyokuwa tunajivunia kuwa ni nyingi sana katika mgodi wa Nzega uliokuwa unachimbwa na kampuni ya Resolute umefungwa mwaka jana august,dhahabu imeisha,hivyo hata gesi itaisha tu,tufanye maamuzi ya busara.
5.---- Ilani ya chama cha mapinduzi(2010) katika ibara ya 63(h) na (k) ilianisha miradi ya kinyerezi(240MW) na mradi wa Mnazi bay(300MW) kama miradi miwili tofauti inayojitegemea.Hivyo tunashangaa leo inapoonekana kuwa ni mradi mmoja.Tunataka kila mmoja uendelee kama ulivyopangwa na si vinginevyo.Hii ndiyo itawezesha ahadi ya ujenzi wa kiwanda cha UREA kilichopangwa kujengwa Mtwara kama inavyoainishwa katika Ibara ya 49(e) kufanikiwa.Lakini hii pia itawezesha uhakika wa uanzishwaji wa kiwanda cha kubangulia korosho kama makubaliano(Memorandam of understanding) yaliyoingiwa kati ya TIB(80% Tanzania Investiment bank) na Tandahimba Newala Cooperative union(20%TANECU) kukamilika.Nadhani Kuyatekeleza tuliyoahid ndio njia bora ya kutimiza ahadi na kuboresha maisha ya watanzania.

Really? Inawezekana hii ni kabla ya kugundulika gas nyingine ya kutosha tuu kule Mkuranga


6.---- Kwa kuwa kipaumbele cha watu wa Mtwara si kuwa na umeme majumbani ambao ni ongezeko la gharama la maisha kiuchumi(na kwa kuzingatia kuwa nyumba nyingi za mji wa Mtwara hazina sifa ya kuunganishiwa umeme kwani ni za nyasi,udongo na makuti na kipato chao cha sasa kinawanyima uwezo wa kuipa bili za kila mwezi)Kipaumbele kinabaki ni kupunguza makali ya maisha kwa kuwa na uhakika wa kipato kwa njia ya ajira kwa shughuli za uzalishaji viwandani na shughuli zitakazoambatana na hizo,Ni vema serikali ikazingatia kauli ya Mkurugenzi mkuu wa Wentworthy resource Limited Inayochimba gesi ya Mnazi Bay Bwana Bob Mcbean iliyoripotiwa tarehe -6 December- London mwaka 2012 kuwa watapata faida kubwa kwa kuwekeza katika kiwanda cha mbolea na kemikali nyingine,hivyo ni vyema mkazo ukawa katika -kuhimiza uwekezaji zaidi kupitia gesi hii na uhakika wa nishati ya umeme kutokana na mtambo wa kufua umeme utakaojengwa Mtwara.

Build it and they would come!! http://mitei.mit.edu/news/video/regional-economic-development-planning-east-africa. MIT wameoffer kushare technology katika kutayarisha wananchi wa huko wapate uelewa na kuhamisha technologia - soma hiyo link hapo juu.


TUJIFUNZE KWA WENZETU.
Hapa hata mie nakuunga mkono!


NINI KIFANYIKE?
1.---- Kwa sababu bomba hili halisafirishi chakula cha dharura kwamba likisitishwa watu watakufa katika jiji la Dar Es Salaam,Serikali itangaze rasmi kusitishwa kwa mradi huu wa ujenzi wa bomba mara moja kutokana na kilio cha wananchi na izijibu hoja 9 za wananchi zilizotolewa katika maandamano ya tarehe 27 december 2012.

Hii naipinga - tayari viwanda vinavyotumia gas asilia vimejengwa Dar - Wazo cement, TZ Breweries, Serengeti breweries and one major hospital etc zinatumia gas asilia. Sasa leo hii eti wasitishe mradi huo? Why? Mtambo mkubwa wa gas to electricity upo Dar ambao tayari unafeed into the national grid

2.---- Mkuu wa mkoa na waziri wa nishati na madini wawaombe radhi wananchi wa Mtwara kwa maneno yao ya kuudhi kwa kuita maandamano yao kuwa ni ya kipuuzi,wahaini na wasioelewa ili kuonyesha kuwa walikosea.Wasipofanya hivyo ni kusema walikusudia kuyasema hayo na kwa jinsi hiyo ni kuchochea mikutano na maandamano yanayoendelea,hivyo kwa lolote litakotokea watastahili kuwajibishwa.

Hakuna kuomba msamaha hapa! Why? Kwa watu na wabunge wao kuandamana wakati hali halisi ipo wazi kwamba tayari mambo haya yameanza kutekelezwa kunanishangaza kweli! Halafu wanasiasa wengine ambao wapo mbali na Mtwara nao wanadandia mkokoteni!! Come on!!!

3.---- Uwekwe mpango maalumu wa viongozi waandamizi wa serikali kuja mtwara na kukutana na wananchi wa mtwara Haraka ndani ya siku 14 zijazo.Nia sio kuwaambia gesi lazima itoke bali ni kuwasikiliza na kufanyia kazi hoja zao.

Wabunge wa huko walishaenda "Study Tour" kwenye nchi husika - wao kwa nini walivyorudi hawakutoa somo!!

4.---- Wabunge wa mkoa wa Mtwara na Lindi waache malumbano kati yao bali wajitokeze hadharani na kueleza msimamao wao wa pamoja kuhusiana na jambo hili.

Soma #3 hapo juu.

ANGALIZO
Swala la gesi linalenga kuwafaidisha wananchi wote wa Tanzania kama vile sera ya serikali ................................
...................................
........................................
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Mtwara,
Mungu Ibariki Gesi Asilia isaidie kuinua maisha ya watanzania Maskini,
Ahsanteni Sana.
JOEL NANAUKA
0713-243 244
MDAU WA MAENDELEO.

 
Back
Top Bottom