Press Release Leo: Serikali Isitishe Mara Moja Ujenzi wa Bomba la Gesi kwenda Dar- Wana Mtwara

Mponjoli

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
668
152
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MADAI YA WANAMTWARA KUSHINIKIZA KUCHAKATWA KWA GESI KATIKA MJI WA MTWARA NA KUTOSAFIRISHA GESI GAFI KWA BOMBA KWENDA DAR ES SALAM.
TAREHE 07-01-2013.

Ndugu waandishi wa Habari kwanza ningependa kuwashukuru sana kwa kuitikia wito wenu kuja hapa leo kuyasikiliza yale ambayo nimekusudia kuyaongea.
Pili ningependa kuwapongeza sana kwa namna mnavyoripoti habari hizi kila wakati bila kuchoka na kuyafuatilia matukio na kueleza hoja na hisia za wananchi wa Mtwara kila kunapokucha.

Najua ziko shutuma zilizotolewa na viongozi wa serikali kwamba wanaozungumzia jambo hili wanatafuta umaarufu wa kisiasa,nadhani hiyo ilikuwa mbinu ya kuziba mdomo tusizungumze.Swala hili ni nyeti na lina sura ya kitaifa ni wajibu wa kila mpenda maendeleo ya nchi hii kulizungumzia kwa ustawi wa watu wetu,ndicho ninachofanya leo,uzalendo unanitaka kufanya hivyo.Nikinukuu maneno ya mpigania haki za wanawake nchini Afghanistan Mama Malalai Joya aliyewahi kusema"The silence of Good people is worse than the actions of Bad people " Hivyo kukaa kwangu kimya ni kubaya zaidi kuleta matendo mabaya ya mtu yeyote yule,ili nisiwe kwenye kundi hilo naomba nivunje ukimya huo.

Nianze kwa kusema kuwa ningependa kutoa maoni yangu kama mwananchi wa kawaida ninayeguswa na jambo hili na ninatumia haki yangu ya kikatiba kwa mujibu ya ibara ya 18 kipengele (A).Ingawa ukweli utabaki kuwa mimi ni mwanachama wa chama cha mapinduzi na historia inajieleza kuwa -nimeshawahi kuwa katibu msaidizi wa CCM wilaya- na mgombea wa ubunge katika kura za maoni mwaka 2010 katika uchaguzi wa ndani ya chama kwa jimbo la Mtwara Mjini.

Tangu kuanza kwa vuguvugu la mradi wa ujenzi wa bomba la gesi nimetumia -muda mwingi kuwa Mtwara kuliko Dar es Salaam ambako hasa ndiko ninakofanya shughuli zangu.
Kabla vuguvugu hili halijachukua sura kubwa ya kitaifa yalikuwepo manun'guniko mengi kwa wananchi yaliyoonyesha kutoridhishwa na kufanyika kwa mradi huu.Ikumbukwe kuwa ingawa mkataba wa kupata mkopo wa ujenzi wa bomba kutoka benki ya Exim china(Takribani usd 1Bill) ulisainiwa nchini china tarehe 26 september 2011 na ujumbe uliiongozwa na waziri wa wakati huo wa Nishati na Madini William ngeleja,kujulikana kwa utekelezwaji wa mradi huu kwa watu wengi ulikuwa ni pale mheshimiwa Rais alipozindua mradi wa kujenga mtambo wa kufua umeme kinyerezi tarehe 8/November/2012 ambao ungetokana na gesi kutoka Mtwara ikiungana na bomba la songosongo,hapa ikiwa ni takribani mwaka mmoja kupita tangu kusainiwa.

Kwa kulitazama jambo hili kutokea mbali na kwa kutoridhishwa na ukimya uliotawala kwa viongozi wa serikali na wawakilishi wa wananchi,nilichukua hatua za makusudi kufanya ufuatiliaji mbalimbali.Hatua yangu ya kwanza ilikuwa kwenda TPDC ofisi ya mkurugenzi tarehe12 december 2012 ikiwa ndiyo mwakilishi wa serikali anayesimamia mradi huu ili kuhoji mambo kadhaa na kutoa mtazamo wangu wa umuhimu wa kusimamishwa kwa mradi huu ili kusikiiliza kilio cha wananchi.Ingawa sikufanikiwa kuonana na mkurugenzi nilifanikiwa kukutanishwa na wakuu wa kitengo cha malalamiko yanayohusu mradi huu ambao kwa ukweli ni kwamba walisisitiza tatizo kubwa ni kutokuelewa kwa wananchi na kupuuza hoja yangu ya msingi ya kutaka ujenzi wa bomba hili usimamishwe ili kusikiliza hoja za msingi za wananchi.

Baada ya hapo nilichukua hatua ya kuomba msaada wakisheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu ili kusitisha mradi huu kwa kuwasiliana na mkurugenzi wa kituo hicho Bi hellen Kijo bisimba mnamo tarehe 17dec 2012 ambaye alinieleza kuwa alishatuma ujumbe wake Mtwara na wako katika hatua za kuandika ripoti hivyo niisubirie.Kwa bahati mbaya sana bado sijafanikiwa kuipata ripoti yao. Sikuishia hapo,niliamua kuandika barua kwa ngazi za manispaa ya Mtwara mnamo tarehe 18 dec 2012 ikiwa na madai kadhaa na mapendekezo ya nini kifanyike kuhusiana na mradi huu.Kati ya madai yangu ilikuwa kumtaka meya wa manispaa kuitisha kikao cha haraka cha baraza la madiwani kulijadili jambo hili kama la dharura wakiwa ndio wawakilishi wa wananchi na kutoa msimamo wao kwa serikali kuitaka kusitisha mradi huu na kusikiliza kilio cha wananchi.Juhudi hii nayo haikuzaa matunda kwani sikupata jibu lolote la barua yangu wala utekelezaji wake hadi hii leo.

Baada ya hapo nilishiriki kikamilifu katika mijadala ya sera na vipindi mbalimbali vya redio nikihimiza kusitishwa kwa ujenzi wa bomba hili hadi pale hoja za wananchi zitakapojibiwa kama vile nilivyonukuliwa katika gazeti la mwananchi la tarehe 26 december 2012 ukurasa wa kumi ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika maandamano makubwa siku ya tarehe 27.
Nimeeleza haya yote ili kuonyesha kuwa kwa mtu yeyote anayeona mbali ni lazima alijua kuwa bila ya kusikilizwa kwa kilio hiki cha wananchi ni lazima tungefika hapa tulipo na kuna uwezekano wa kwenda mbali zaidi kuliko hapa kama hatua stahiki hazitachukuliwa.
Baada ya kusema hayo ningependa kutoa masikitiko yangu kwa kauli za kejeli,dharau na kukatisha tamaa zilizotolewa na viongozi waandamizi wa serikali Mh.Waziri Sospeter Muhongo na mkuu wa mkoa wa Mtwara(Joseph Simbakalia)- mara baada ya maandamano ya tarehe 27 dec.Pia napenda kueleza kusikitishwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kauli yake aliyoitoa kuhusu ujenzi wa bomba hili katika salamu zake za mwaka mpya,napenda kutumia nafasi hii kumshauri Mh.Rais,Waziri wa Nishati na Madini na Mkuu wa mkoa kupitia upya madai 9 yalisomwa siku ya maandamano ili kutoupotosha mjadala na madai ya watu wa Mtwara.
Nimetoa rai hiyo kwasababu ukipitia hotuba za viongozi hawa wote utagundua kuwa aidha wamepewa taarifa zisizo sahihi kuhusu madai ya wanamtwara ama wamefanya haraka kujibu au hawajaelewa kabisa madai ya wanamtwara.Kwani kilichofanyika si kujibu madai yao bali kuonyesha jinsi ambavyo hawako tayari kuwasikiliza,nadhani mtazamo huu ndio unaochochea jambo hili kuwa kubwa kila siku na kuwapa mtazamo wananchi kuwa kuna ajenda ya siri katika hili.

Naomba kuchukua nafasi hii kueleza kuwa WANANCHI WA MKOA WA MTWARA HAWAPINGI WANANCHI WA MIKOA MINGINE KUNUFAIKA NA FAIDA ZA GESI BALI KINACHOPINGWA NI KUSAFIRISHA GESI GAFI TOFAUTI NA AHADI YA SERIKALI YA KUJENGA MTAMBO WA KUZALISHA UMEME MKOANI MTWARA UTAKAOVUTIA WAWEKEZAJI WA VIWANDA.UMEME HUU UNAWEZA KUSAFIRISHWA KWENDA MAHALI POPOTE TANZANIA/NJE YA NCHI BAADA YA MTAMBO KUJENGWA MTWARA.
Naomba kukumbusha kuwa madai haya hayajotoka hewani,bali yametokana na sababu kadhaa:
1.---- Ni ahadi za mara kwa mara zilizokuwa zilizotolewa na Mh.Rais na mawaziri wa Nishati na Madini katika nyakati tofauti.Tangu mara ya kwanza Mh.Rais alipohojiwa clouds(kipindi cha power breakfast) tarehe 29 october katika- kampeni ya mwaka 2010,pia alipokuja kwenye kampeni Mtwara na hata alipokuja kushukuru baada ya kuwa Rais aliendelea kuahidi kuufanya Mtwara kuwa mji wa viwanda kwa kuupatia umeme wa uhakika kupitia ugunduzi wa gesi hii,pia alieleza katika kipindi hicho cha radio kusudio la serikali yake kujenga mtambo wa 300MW.Hii yote ilitengeneza matumaini makubwa kwa wananchi wa Mtwara wa kufaidika na gesi hii.Leo tunaposikia gesi ghafi inahamishwa na bado hakuna mtambo huo wala kiwanda sawa na ahadi zilivyotolewa,kuna kosa gani wananchi wakihoji?
2.---- Mpango wa Mtwara power project uliolenga kuufanya mradi huu kuwa sehemu ya National power Development plan(3920MW) ukilenga kuwa na mtambo wa kuzalisha 300MW Mtwara zitakazoingizwa katika gridi ya Taifa na kuondoa tatizo la umeme nchini uliokuwa umelenga kukamilika mwaka 2012.Ingawa ni wazi kuwa kampuni iliyokuwa itekeleze mradi huu Artumas ilishindwa kutokana na mtikisiko wa kiuchumi wa mwaka 2008,iliweka bayana kuwa ingepata dola za kimarekani milioni 7 ingeweza kuutekeleza.Kwa nini serikali haikuweka kama sharti mojawapo kwa kampuni ya Wentworthy resource Limited iliyoinunua artumas kuutekeleza mradi huu uliokuwa umekubalika kuingia katika mpango wa kitaifa?kwa nini uliachwa?Hili nalo hatuna majibu kama ilivyo kwa mipango mingine kama vile Mtwara Corridor.
3.---- Ikumbukwe kuwa kisiwa cha songosongo ndio eneo la kwanza kugunduliwa kwa gesi asilia mwaka 1974 na kampuni ya AGIP kukiwa na takriban cubic feet 783 billion.Kati ya mipango mingi iliyowekwa kwa wakati huo kuhusiana na kubadilisha maisha ya wanasongosongo na kilwa kwa ujumla ni kujenga kiwanda cha mbolea KILWA AMMONIUM COMPANY,kilicholenga kutatua tatizo la ajira na kutosheleza uzalishaji wa mbolea nchini.Waliambiwa wasiwe na hofu gesi kwenda Dar es Salaam kwani viwanda vitajengwa kilwa,Ingawa eneo lilitengwa kwa ujenzi wa kiwanda hicho na wataalamu kusomeshwa,hadi hivi leo kiwanda hakijajengwa. Hivi hali kama hii haitoshi kuleta wasiwasi kwa wananchi?kuna tatizo gani wakihoji jambo hili?Waswahili husema ukiona mwenzako ananyolewa,wewe tia maji.
Kama viwanda hivi vitafanikiwa vitaleta tija na ulazima wa kuifufua bandari ya Mtwara ambayo tangu mwaka 2006/2007 imekuwa ikitumika kwa 31% ya uwezo wake(Tani 122,862 kwa mwaka badala ya tani 400,000 kwa mwaka).Mbinu hii itasaidia kupunguza msongamano wa bandari ya Dar kama ambavyo nchi Jirani ya Kenya wamefanya kwa kuipanua bandari ya Lamu ili kupunguza msongamano bandari ya mombasa.

4.---- Hoja nyingine ni ya kihistoria,Tangu tupate uhuru watu wa kusini wamesota katika janga la kukosa nishati ya umeme -kwa muda mrefu na hawakuunganishwa na gridi ya taifa kwa sababu lukuki ingawa iliwezekana kuvusha umeme baharini kwenda Zanzibar ilishindikana kuuleta Mtwara.Kama wameweza kusahauliwa kwa miaka 51 katika swala la nishati,hofu ni kuwa gesi itakapoisha vizazi vyao vitasahauliwa tena kwa kubaki na bomba tupu,na hakuna atakayekumbuka tena kuunganisha mikoa hii na Gridi ya Taifa ili kuwa na umeme wa uhakika ambao ndio hitaji kubwa mojawapo la wawekezaji.Hoja ya gesi kuwa nyingi sana na itachukua muda mrefu kuisha- haina mashiko kwani hata dhahabu tuiyokuwa tunajivunia kuwa ni nyingi sana katika mgodi wa Nzega uliokuwa unachimbwa na kampuni ya Resolute umefungwa mwaka jana august,dhahabu imeisha,hivyo hata gesi itaisha tu,tufanye maamuzi ya busara.
5.---- Ilani ya chama cha mapinduzi(2010) katika ibara ya 63(h) na (k) ilianisha miradi ya kinyerezi(240MW) na mradi wa Mnazi bay(300MW) kama miradi miwili tofauti inayojitegemea.Hivyo tunashangaa leo inapoonekana kuwa ni mradi mmoja.Tunataka kila mmoja uendelee kama ulivyopangwa na si vinginevyo.Hii ndiyo itawezesha ahadi ya ujenzi wa kiwanda cha UREA kilichopangwa kujengwa Mtwara kama inavyoainishwa katika Ibara ya 49(e) kufanikiwa.Lakini hii pia itawezesha uhakika wa uanzishwaji wa kiwanda cha kubangulia korosho kama makubaliano(Memorandam of understanding) yaliyoingiwa kati ya TIB(80% Tanzania Investiment bank) na Tandahimba Newala Cooperative union(20%TANECU) kukamilika.Nadhani Kuyatekeleza tuliyoahid ndio njia bora ya kutimiza ahadi na kuboresha maisha ya watanzania.

6.---- Kwa kuwa kipaumbele cha watu wa Mtwara si kuwa na umeme majumbani ambao ni ongezeko la gharama la maisha kiuchumi(na kwa kuzingatia kuwa nyumba nyingi za mji wa Mtwara hazina sifa ya kuunganishiwa umeme kwani ni za nyasi,udongo na makuti na kipato chao cha sasa kinawanyima uwezo wa kuipa bili za kila mwezi)Kipaumbele kinabaki ni kupunguza makali ya maisha kwa kuwa na uhakika wa kipato kwa njia ya ajira kwa shughuli za uzalishaji viwandani na shughuli zitakazoambatana na hizo,Ni vema serikali ikazingatia kauli ya Mkurugenzi mkuu wa Wentworthy resource Limited Inayochimba gesi ya Mnazi Bay Bwana Bob Mcbean iliyoripotiwa tarehe -6 December- London mwaka 2012 kuwa watapata faida kubwa kwa kuwekeza katika kiwanda cha mbolea na kemikali nyingine,hivyo ni vyema mkazo ukawa katika -kuhimiza uwekezaji zaidi kupitia gesi hii na uhakika wa nishati ya umeme kutokana na mtambo wa kufua umeme utakaojengwa Mtwara.

TUJIFUNZE KWA WENZETU.
Tanzania si nchi ya kwanza kuchimba gesi katika dunia wala Afrika.Katika bara la afrika tunazo nchi kama Algeria,Misri na Nigeria ambazo husafirisha gesi nje ya nchi.Tukiwa nchi ya 66 duniani tukizalisha 658,000,000cubic metres,jirani zetu msumbiji ni wa 50 wakizalisha 3,600,000,000cubic metres(takwimu za mwaka 2012).
Tanzania kwa sasa inasadikika kuwa na kiasi cha 43 Trillion Cubic feet (TCF) ukilinganisha na kiasi cha 2.8Trillioni cubic Metres(98.896Trillion cubic feet) za msumbiji ambazo ni zaidi ya mara mbili ya kiwango tulichonacho hivyo si vibaya tukijifunza kwao.
Kwa sababu ya mipango mizuri ya kiuchumi ya Msumbiji haikuwa lazima kujenga kila kitu Maputo/beira ambayo ni miji ya biashara lakini mtambo wa kuzalisha gesi ya 107.5MW umejengwa na kampuni ya Aggreko katika mji wa pembeni wa Ressano Garcia utakaopeleka umeme -Maputo na miji mingine ya Afrika kusini ambako katika miji hii umeme huu utasafirishwa -na kutumika kwani ndio miji mikubwa ya kibiashara kama ilivyo Dar Es Salaam .Ingawa umbali wa Maputo na Ressano Garcia ni 1/5 ya umbali wa Dar-Mtwara,tunaweza kujifunza kwao katika hili.
-Akizindua mradi huo mwezi July 2012 Rais wa msumbiji Mh.Armando Guebuza alieleza kuwa wanakusudia kujenga mitambo ya kuweka gesi katika hali ya kimiminika ipatayo 10(liquefied natural gas (LNG) plants) katika maeneo mbalimbali ya msumbiji.Hii yote ni kutawanya uchumi na kutengeneza fursa mbalimbali kwa wananchi wa kawaida wa Msumbiji.Hili nalo linaweza kufanyika Tanzania.

NINI KIFANYIKE?
1.---- Kwa sababu bomba hili halisafirishi chakula cha dharura kwamba likisitishwa watu watakufa katika jiji la Dar Es Salaam,Serikali itangaze rasmi kusitishwa kwa mradi huu wa ujenzi wa bomba mara moja kutokana na kilio cha wananchi na izijibu hoja 9 za wananchi zilizotolewa katika maandamano ya tarehe 27 december 2012.
2.---- Mkuu wa mkoa na waziri wa nishati na madini wawaombe radhi wananchi wa Mtwara kwa maneno yao ya kuudhi kwa kuita maandamano yao kuwa ni ya kipuuzi,wahaini na wasioelewa ili kuonyesha kuwa walikosea.Wasipofanya hivyo ni kusema walikusudia kuyasema hayo na kwa jinsi hiyo ni kuchochea mikutano na maandamano yanayoendelea,hivyo kwa lolote litakotokea watastahili kuwajibishwa.
3.---- Uwekwe mpango maalumu wa viongozi waandamizi wa serikali kuja mtwara na kukutana na wananchi wa mtwara Haraka ndani ya siku 14 zijazo.Nia sio kuwaambia gesi lazima itoke bali ni kuwasikiliza na kufanyia kazi hoja zao.
4.---- Wabunge wa mkoa wa Mtwara na Lindi waache malumbano kati yao bali wajitokeze hadharani na kueleza msimamao wao wa pamoja kuhusiana na jambo hili.

ANGALIZO
Swala la gesi linalenga kuwafaidisha wananchi wote wa Tanzania kama vile sera ya serikali inavyosema.Wananchi wa Mtwara ni sehemu ya Taifa hili nao wanahaki ya kuhoji na kutathmini utekelezwaji wa- yale waliyoahidiwa na viongozi wao.Kuwanyima fursa hiyo ni kuwatenga na utajiri wa Taifa lao.
Ningependa kurudia kwa kusema kuwa,wananchi wa Mtwara hawasemi wananchi wa maeneo mengine ya Tanzania hawapaswi kufaidika na gesi inayozalishwa Mtwara,hoja yao ni kuhusu faida zilizozungumzwa na viongozi hapo kabla kuhusiana na viwanda na umeme.Hili ndilo linalotakiwa kufanyiwa kazi kwa sasa.Ingawa ni kweli kwamba sio serikali inayojenga viwanda hivi lakini ndiyo yenye dhamana ya kufanya hivyo kama ilivyoahidi.
Ikumbukwe kuwa kufanikiwa kwa ujenzi wa mtambo wa kufua umeme Mtwara utatoa mwongozo wa utekelezaji wa miradi kama hii katika maeneo mengine ya Nchi yetu ambako gesi inaendelea kugundulika.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Mtwara,
Mungu Ibariki Gesi Asilia isaidie kuinua maisha ya watanzania Maskini,
Ahsanteni Sana.
JOEL NANAUKA
0713-243 244
MDAU WA MAENDELEO.

Fungua attachment
 
Attachments

  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MRADI WA UJENZI WA GESI[1].pdf
    76.4 KB · Views: 889
Asante Joel kwa kuwa mzalendo....sasa unaweza kuamini kuwa mabadiliko hayaji kwa kubembeleza bali kwa kuyadai. Mmedekeza sana viongozi wenu sasa wanadhani kila maamuzi wanayotoa yametoka kwa Mungu kwa hiyo tunapaswa kuwapigia magoti.

Haya shime wana Mtwara tupiganie haki za mkoa wetu na rasilimali zetu
 
mkuu kwa faida ya wanaJF wa mobile nakuomba uweke hii press release hapa

Wenye simu ambao ni wachangiaji wakubwa hawawezi kusoma ulicholeta

Nakala Kwa Fang, Invisible
 
Last edited by a moderator:
Nadhani Joel mwenyewe alikuwa ameiweka hii habari hapa mchana kimaandishi kabisa...sijui hii thread imeenda wapi kwa sasa..tafadhali fungua attachment
 
mmmhuhh... mpaka kieleweke! hakuna kulala! just thinking outloud hivi kwa nini walikunyima ubunge? umeflow kitaalam mpaka basi! karibu cdm utimize ndoto zako!
 
Mods. Hii issue ya pdf kwenye mobile phones inakuwa ngumu kidogo. Please angalieni namna ya kutuwekea hii taarifa hapa juu. Tunaihitaji sana, please...
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MADAI YA WANAMTWARA KUSHINIKIZA KUCHAKATWA KWA GESI KATIKA MJI WA MTWARA NA KUTOSAFIRISHA GESI GAFI KWA BOMBA KWENDA DAR ES SALAM.
TAREHE 07-01-2013.

Ndugu waandishi wa Habari kwanza ningependa kuwashukuru sana kwa kuitikia wito wenu kuja hapa leo kuyasikiliza yale ambayo nimekusudia kuyaongea.
Pili ningependa kuwapongeza sana kwa namna mnavyoripoti habari hizi kila wakati bila kuchoka na kuyafuatilia matukio na kueleza hoja na hisia za wananchi wa Mtwara kila kunapokucha.

Najua ziko shutuma zilizotolewa na viongozi wa serikali kwamba wanaozungumzia jambo hili wanatafuta umaarufu wa kisiasa,nadhani hiyo ilikuwa mbinu ya kuziba mdomo tusizungumze.Swala hili ni nyeti na lina sura ya kitaifa ni wajibu wa kila mpenda maendeleo ya nchi hii kulizungumzia kwa ustawi wa watu wetu,ndicho ninachofanya leo,uzalendo unanitaka kufanya hivyo.Nikinukuu maneno ya mpigania haki za wanawake nchini Afghanistan Mama Malalai Joya aliyewahi kusema"The silence of Good people is worse than the actions of Bad people " Hivyo kukaa kwangu kimya ni kubaya zaidi kuleta matendo mabaya ya mtu yeyote yule,ili nisiwe kwenye kundi hilo naomba nivunje ukimya huo.

Nianze kwa kusema kuwa ningependa kutoa maoni yangu kama mwananchi wa kawaida ninayeguswa na jambo hili na ninatumia haki yangu ya kikatiba kwa mujibu ya ibara ya 18 kipengele (A).Ingawa ukweli utabaki kuwa mimi ni mwanachama wa chama cha mapinduzi na historia inajieleza kuwa -nimeshawahi kuwa katibu msaidizi wa CCM wilaya- na mgombea wa ubunge katika kura za maoni mwaka 2010 katika uchaguzi wa ndani ya chama kwa jimbo la Mtwara Mjini.

Tangu kuanza kwa vuguvugu la mradi wa ujenzi wa bomba la gesi nimetumia -muda mwingi kuwa Mtwara kuliko Dar es Salaam ambako hasa ndiko ninakofanya shughuli zangu.
Kabla vuguvugu hili halijachukua sura kubwa ya kitaifa yalikuwepo manun'guniko mengi kwa wananchi yaliyoonyesha kutoridhishwa na kufanyika kwa mradi huu.Ikumbukwe kuwa ingawa mkataba wa kupata mkopo wa ujenzi wa bomba kutoka benki ya Exim china(Takribani usd 1Bill) ulisainiwa nchini china tarehe 26 september 2011 na ujumbe uliiongozwa na waziri wa wakati huo wa Nishati na Madini William ngeleja,kujulikana kwa utekelezwaji wa mradi huu kwa watu wengi ulikuwa ni pale mheshimiwa Rais alipozindua mradi wa kujenga mtambo wa kufua umeme kinyerezi tarehe 8/November/2012 ambao ungetokana na gesi kutoka Mtwara ikiungana na bomba la songosongo,hapa ikiwa ni takribani mwaka mmoja kupita tangu kusainiwa.
Kwa kulitazama jambo hili kutokea mbali na kwa kutoridhishwa na ukimya uliotawala kwa viongozi wa serikali na wawakilishi wa wananchi,nilichukua hatua za makusudi kufanya ufuatiliaji mbalimbali.Hatua yangu ya kwanza ilikuwa kwenda TPDC ofisi ya mkurugenzi tarehe12 december 2012 ikiwa ndiyo mwakilishi wa serikali anayesimamia mradi huu ili kuhoji mambo kadhaa na kutoa mtazamo wangu wa umuhimu wa kusimamishwa kwa mradi huu ili kusikiiliza kilio cha wananchi.Ingawa sikufanikiwa kuonana na mkurugenzi nilifanikiwa kukutanishwa na wakuu wa kitengo cha malalamiko yanayohusu mradi huu ambao kwa ukweli ni kwamba walisisitiza tatizo kubwa ni kutokuelewa kwa wananchi na kupuuza hoja yangu ya msingi ya kutaka ujenzi wa bomba hili usimamishwe ili kusikiliza hoja za msingi za wananchi.
Baada ya hapo nilichukua hatua ya kuomba msaada wakisheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu ili kusitisha mradi huu kwa kuwasiliana na mkurugenzi wa kituo hicho Bi hellen Kijo bisimba mnamo tarehe 17dec 2012 ambaye alinieleza kuwa alishatuma ujumbe wake Mtwara na wako katika hatua za kuandika ripoti hivyo niisubirie.Kwa bahati mbaya sana bado sijafanikiwa kuipata ripoti yao.
Sikuishia hapo,niliamua kuandika barua kwa ngazi za manispaa ya Mtwara mnamo tarehe 18 dec 2012 ikiwa na madai kadhaa na mapendekezo ya nini kifanyike kuhusiana na mradi huu.Kati ya madai yangu ilikuwa kumtaka meya wa manispaa kuitisha kikao cha haraka cha baraza la madiwani kulijadili jambo hili kama la dharura wakiwa ndio wawakilishi wa wananchi na kutoa msimamo wao kwa serikali kuitaka kusitisha mradi huu na kusikiliza kilio cha wananchi.Juhudi hii nayo haikuzaa matunda kwani sikupata jibu lolote la barua yangu wala utekelezaji wake hadi hii leo.
Baada ya hapo nilishiriki kikamilifu katika mijadala ya sera na vipindi mbalimbali vya redio nikihimiza kusitishwa kwa ujenzi wa bomba hili hadi pale hoja za wananchi zitakapojibiwa kama vile nilivyonukuliwa katika gazeti la mwananchi la tarehe 26 december 2012 ukurasa wa kumi ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika maandamano makubwa siku ya tarehe 27.
Nimeeleza haya yote ili kuonyesha kuwa kwa mtu yeyote anayeona mbali ni lazima alijua kuwa bila ya kusikilizwa kwa kilio hiki cha wananchi ni lazima tungefika hapa tulipo na kuna uwezekano wa kwenda mbali zaidi kuliko hapa kama hatua stahiki hazitachukuliwa.
Baada ya kusema hayo ningependa kutoa masikitiko yangu kwa kauli za kejeli,dharau na kukatisha tamaa zilizotolewa na viongozi waandamizi wa serikali Mh.Waziri Sospeter Muhongo na mkuu wa mkoa wa Mtwara(Joseph Simbakalia)- mara baada ya maandamano ya tarehe 27 dec.Pia napenda kueleza kusikitishwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kauli yake aliyoitoa kuhusu ujenzi wa bomba hili katika salamu zake za mwaka mpya,napenda kutumia nafasi hii kumshauri Mh.Rais,Waziri wa Nishati na Madini na Mkuu wa mkoa kupitia upya madai 9 yalisomwa siku ya maandamano ili kutoupotosha mjadala na madai ya watu wa Mtwara.
Nimetoa rai hiyo kwasababu ukipitia hotuba za viongozi hawa wote utagundua kuwa aidha wamepewa taarifa zisizo sahihi kuhusu madai ya wanamtwara ama wamefanya haraka kujibu au hawajaelewa kabisa madai ya wanamtwara.Kwani kilichofanyika si kujibu madai yao bali kuonyesha jinsi ambavyo hawako tayari kuwasikiliza,nadhani mtazamo huu ndio unaochochea jambo hili kuwa kubwa kila siku na kuwapa mtazamo wananchi kuwa kuna ajenda ya siri katika hili.
Naomba kuchukua nafasi hii kueleza kuwa WANANCHI WA MKOA WA MTWARA HAWAPINGI WANANCHI WA MIKOA MINGINE KUNUFAIKA NA FAIDA ZA GESI BALI KINACHOPINGWA NI KUSAFIRISHA GESI GAFI TOFAUTI NA AHADI YA SERIKALI YA KUJENGA MTAMBO WA KUZALISHA UMEME MKOANI MTWARA UTAKAOVUTIA WAWEKEZAJI WA VIWANDA.UMEME HUU UNAWEZA KUSAFIRISHWA KWENDA MAHALI POPOTE TANZANIA/NJE YA NCHI BAADA YA MTAMBO KUJENGWA MTWARA.
Naomba kukumbusha kuwa madai haya hayajotoka hewani,bali yametokana na sababu kadhaa:
1.---- Ni ahadi za mara kwa mara zilizokuwa zilizotolewa na Mh.Rais na mawaziri wa Nishati na Madini katika nyakati tofauti.Tangu mara ya kwanza Mh.Rais alipohojiwa clouds(kipindi cha power breakfast) tarehe 29 october katika- kampeni ya mwaka 2010,pia alipokuja kwenye kampeni Mtwara na hata alipokuja kushukuru baada ya kuwa Rais aliendelea kuahidi kuufanya Mtwara kuwa mji wa viwanda kwa kuupatia umeme wa uhakika kupitia ugunduzi wa gesi hii,pia alieleza katika kipindi hicho cha radio kusudio la serikali yake kujenga mtambo wa 300MW.Hii yote ilitengeneza matumaini makubwa kwa wananchi wa Mtwara wa kufaidika na gesi hii.Leo tunaposikia gesi ghafi inahamishwa na bado hakuna mtambo huo wala kiwanda sawa na ahadi zilivyotolewa,kuna kosa gani wananchi wakihoji?
2.---- Mpango wa Mtwara power project uliolenga kuufanya mradi huu kuwa sehemu ya National power Development plan(3920MW) ukilenga kuwa na mtambo wa kuzalisha 300MW Mtwara zitakazoingizwa katika gridi ya Taifa na kuondoa tatizo la umeme nchini uliokuwa umelenga kukamilika mwaka 2012.Ingawa ni wazi kuwa kampuni iliyokuwa itekeleze mradi huu Artumas ilishindwa kutokana na mtikisiko wa kiuchumi wa mwaka 2008,iliweka bayana kuwa ingepata dola za kimarekani milioni 7 ingeweza kuutekeleza.Kwa nini serikali haikuweka kama sharti mojawapo kwa kampuni ya Wentworthy resource Limited iliyoinunua artumas kuutekeleza mradi huu uliokuwa umekubalika kuingia katika mpango wa kitaifa?kwa nini uliachwa?Hili nalo hatuna majibu kama ilivyo kwa mipango mingine kama vile Mtwara Corridor.
3.---- Ikumbukwe kuwa kisiwa cha songosongo ndio eneo la kwanza kugunduliwa kwa gesi asilia mwaka 1974 na kampuni ya AGIP kukiwa na takriban cubic feet 783 billion.Kati ya mipango mingi iliyowekwa kwa wakati huo kuhusiana na kubadilisha maisha ya wanasongosongo na kilwa kwa ujumla ni kujenga kiwanda cha mbolea KILWA AMMONIUM COMPANY,kilicholenga kutatua tatizo la ajira na kutosheleza uzalishaji wa mbolea nchini.Waliambiwa wasiwe na hofu gesi kwenda Dar es Salaam kwani viwanda vitajengwa kilwa,Ingawa eneo lilitengwa kwa ujenzi wa kiwanda hicho na wataalamu kusomeshwa,hadi hivi leo kiwanda hakijajengwa. Hivi hali kama hii haitoshi kuleta wasiwasi kwa wananchi?kuna tatizo gani wakihoji jambo hili?Waswahili husema ukiona mwenzako ananyolewa,wewe tia maji.
Kama viwanda hivi vitafanikiwa vitaleta tija na ulazima wa kuifufua bandari ya Mtwara ambayo tangu mwaka 2006/2007 imekuwa ikitumika kwa 31% ya uwezo wake(Tani 122,862 kwa mwaka badala ya tani 400,000 kwa mwaka).Mbinu hii itasaidia kupunguza msongamano wa bandari ya Dar kama ambavyo nchi Jirani ya Kenya wamefanya kwa kuipanua bandari ya Lamu ili kupunguza msongamano bandari ya mombasa.

4.---- Hoja nyingine ni ya kihistoria,Tangu tupate uhuru watu wa kusini wamesota katika janga la kukosa nishati ya umeme -kwa muda mrefu na hawakuunganishwa na gridi ya taifa kwa sababu lukuki ingawa iliwezekana kuvusha umeme baharini kwenda Zanzibar ilishindikana kuuleta Mtwara.Kama wameweza kusahauliwa kwa miaka 51 katika swala la nishati,hofu ni kuwa gesi itakapoisha vizazi vyao vitasahauliwa tena kwa kubaki na bomba tupu,na hakuna atakayekumbuka tena kuunganisha mikoa hii na Gridi ya Taifa ili kuwa na umeme wa uhakika ambao ndio hitaji kubwa mojawapo la wawekezaji.Hoja ya gesi kuwa nyingi sana na itachukua muda mrefu kuisha- haina mashiko kwani hata dhahabu tuiyokuwa tunajivunia kuwa ni nyingi sana katika mgodi wa Nzega uliokuwa unachimbwa na kampuni ya Resolute umefungwa mwaka jana august,dhahabu imeisha,hivyo hata gesi itaisha tu,tufanye maamuzi ya busara.
5.---- Ilani ya chama cha mapinduzi(2010) katika ibara ya 63(h) na (k) ilianisha miradi ya kinyerezi(240MW) na mradi wa Mnazi bay(300MW) kama miradi miwili tofauti inayojitegemea.Hivyo tunashangaa leo inapoonekana kuwa ni mradi mmoja.Tunataka kila mmoja uendelee kama ulivyopangwa na si vinginevyo.Hii ndiyo itawezesha ahadi ya ujenzi wa kiwanda cha UREA kilichopangwa kujengwa Mtwara kama inavyoainishwa katika Ibara ya 49(e) kufanikiwa.Lakini hii pia itawezesha uhakika wa uanzishwaji wa kiwanda cha kubangulia korosho kama makubaliano(Memorandam of understanding) yaliyoingiwa kati ya TIB(80% Tanzania Investiment bank) na Tandahimba Newala Cooperative union(20%TANECU) kukamilika.Nadhani Kuyatekeleza tuliyoahid ndio njia bora ya kutimiza ahadi na kuboresha maisha ya watanzania.

6.---- Kwa kuwa kipaumbele cha watu wa Mtwara si kuwa na umeme majumbani ambao ni ongezeko la gharama la maisha kiuchumi(na kwa kuzingatia kuwa nyumba nyingi za mji wa Mtwara hazina sifa ya kuunganishiwa umeme kwani ni za nyasi,udongo na makuti na kipato chao cha sasa kinawanyima uwezo wa kuipa bili za kila mwezi)Kipaumbele kinabaki ni kupunguza makali ya maisha kwa kuwa na uhakika wa kipato kwa njia ya ajira kwa shughuli za uzalishaji viwandani na shughuli zitakazoambatana na hizo,Ni vema serikali ikazingatia kauli ya Mkurugenzi mkuu wa Wentworthy resource Limited Inayochimba gesi ya Mnazi Bay Bwana Bob Mcbean iliyoripotiwa tarehe -6 December- London mwaka 2012 kuwa watapata faida kubwa kwa kuwekeza katika kiwanda cha mbolea na kemikali nyingine,hivyo ni vyema mkazo ukawa katika -kuhimiza uwekezaji zaidi kupitia gesi hii na uhakika wa nishati ya umeme kutokana na mtambo wa kufua umeme utakaojengwa Mtwara.

TUJIFUNZE KWA WENZETU.
Tanzania si nchi ya kwanza kuchimba gesi katika dunia wala Afrika.Katika bara la afrika tunazo nchi kama Algeria,Misri na Nigeria ambazo husafirisha gesi nje ya nchi.Tukiwa nchi ya 66 duniani tukizalisha 658,000,000cubic metres,jirani zetu msumbiji ni wa 50 wakizalisha 3,600,000,000cubic metres(takwimu za mwaka 2012).
Tanzania kwa sasa inasadikika kuwa na kiasi cha 43 Trillion Cubic feet (TCF) ukilinganisha na kiasi cha 2.8Trillioni cubic Metres(98.896Trillion cubic feet) za msumbiji ambazo ni zaidi ya mara mbili ya kiwango tulichonacho hivyo si vibaya tukijifunza kwao.
Kwa sababu ya mipango mizuri ya kiuchumi ya Msumbiji haikuwa lazima kujenga kila kitu Maputo/beira ambayo ni miji ya biashara lakini mtambo wa kuzalisha gesi ya 107.5MW umejengwa na kampuni ya Aggreko katika mji wa pembeni wa Ressano Garcia utakaopeleka umeme -Maputo na miji mingine ya Afrika kusini ambako katika miji hii umeme huu utasafirishwa -na kutumika kwani ndio miji mikubwa ya kibiashara kama ilivyo Dar Es Salaam .Ingawa umbali wa Maputo na Ressano Garcia ni 1/5 ya umbali wa Dar-Mtwara,tunaweza kujifunza kwao katika hili.
-Akizindua mradi huo mwezi July 2012 Rais wa msumbiji Mh.Armando Guebuza alieleza kuwa wanakusudia kujenga mitambo ya kuweka gesi katika hali ya kimiminika ipatayo 10(liquefied natural gas (LNG) plants) katika maeneo mbalimbali ya msumbiji.Hii yote ni kutawanya uchumi na kutengeneza fursa mbalimbali kwa wananchi wa kawaida wa Msumbiji.Hili nalo linaweza kufanyika Tanzania.

NINI KIFANYIKE?
1.---- Kwa sababu bomba hili halisafirishi chakula cha dharura kwamba likisitishwa watu watakufa katika jiji la Dar Es Salaam,Serikali itangaze rasmi kusitishwa kwa mradi huu wa ujenzi wa bomba mara moja kutokana na kilio cha wananchi na izijibu hoja 9 za wananchi zilizotolewa katika maandamano ya tarehe 27 december 2012.
2.---- Mkuu wa mkoa na waziri wa nishati na madini wawaombe radhi wananchi wa Mtwara kwa maneno yao ya kuudhi kwa kuita maandamano yao kuwa ni ya kipuuzi,wahaini na wasioelewa ili kuonyesha kuwa walikosea.Wasipofanya hivyo ni kusema walikusudia kuyasema hayo na kwa jinsi hiyo ni kuchochea mikutano na maandamano yanayoendelea,hivyo kwa lolote litakotokea watastahili kuwajibishwa.
3.---- Uwekwe mpango maalumu wa viongozi waandamizi wa serikali kuja mtwara na kukutana na wananchi wa mtwara Haraka ndani ya siku 14 zijazo.Nia sio kuwaambia gesi lazima itoke bali ni kuwasikiliza na kufanyia kazi hoja zao.
4.---- Wabunge wa mkoa wa Mtwara na Lindi waache malumbano kati yao bali wajitokeze hadharani na kueleza msimamao wao wa pamoja kuhusiana na jambo hili.

ANGALIZO
Swala la gesi linalenga kuwafaidisha wananchi wote wa Tanzania kama vile sera ya serikali inavyosema.Wananchi wa Mtwara ni sehemu ya Taifa hili nao wanahaki ya kuhoji na kutathmini utekelezwaji wa- yale waliyoahidiwa na viongozi wao.Kuwanyima fursa hiyo ni kuwatenga na utajiri wa Taifa lao.
Ningependa kurudia kwa kusema kuwa,wananchi wa Mtwara hawasemi wananchi wa maeneo mengine ya Tanzania hawapaswi kufaidika na gesi inayozalishwa Mtwara,hoja yao ni kuhusu faida zilizozungumzwa na viongozi hapo kabla kuhusiana na viwanda na umeme.Hili ndilo linalotakiwa kufanyiwa kazi kwa sasa.Ingawa ni kweli kwamba sio serikali inayojenga viwanda hivi lakini ndiyo yenye dhamana ya kufanya hivyo kama ilivyoahidi.
Ikumbukwe kuwa kufanikiwa kwa ujenzi wa mtambo wa kufua umeme Mtwara utatoa mwongozo wa utekelezaji wa miradi kama hii katika maeneo mengine ya Nchi yetu ambako gesi inaendelea kugundulika.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Mtwara,
Mungu Ibariki Gesi Asilia isaidie kuinua maisha ya watanzania Maskini,
Ahsanteni Sana.
JOEL NANAUKA
0713-243 244
MDAU WA MAENDELEO.
 
mmmhuhh... mpaka kieleweke! hakuna kulala! just thinking outloud hivi kwa nini walikunyima ubunge? umeflow kitaalam mpaka basi! karibu cdm utimize ndoto zako!

Haya madai yamekaa kisiasa sana kuliko kiuchumi zaidi. Wengi wetu tumekuwa wanasiasa kuliko kuangalia facts.

Kusema kwamba serikali iwape kampuni binafsi 7 million USD in order to subsidize ujenzi wa mtambo wa umeme nadhani hapa tunashindwa kabisa kuangalia business risk ambazo ziinatokana na mpango huu mzima. Tuwe wawazi jee Mtwara kuna mahitaji makubwa ya umeme mpaka isababishe serikali kuchangia ujenzi wa mtambo wa umeme? Au wengi tunaamini ile falsafa ya jenga kisha watakuja?

Nadhani serikali inatakiwa kujadili Mtwara economic growth forecast ( Makisio ya ukuaji wa uchumi wa Mtwara), kisha kutengeneza mpango endelevu kutokana na hayo makisio. Na sio kutengeneza mpango kutokana na Matakwa ya wagombea ubunge.

Kutokana na ukuaji wa gesi huko kusini ni ushauri wangu watu wa Mtwara wajikite kwenye masomo ya muda mfupi yanayohusu mitambo ya kuchimbia mafuta ( Gas Rigs). Wakae chini na serikali kuomba shinikizo liwekwe kwa E&P companies (Statoil, BG Group) kuajiri wakazi wa mtwara kwa asilimia fulani. Labda 10%.

Lakini kushinikiza serikali ijenge mtambo wa kufua umeme wenye uwezo wa 300 wakati matumizi ya mtwara kwa sasa na miaka kumi ijayo yanaonekana kuwa 50, hapa tutakuwa tunataka kukiuwa hichi kiwanda badala ya kukiendeleza.
 
Haya madai yamekaa
kisiasa sana kuliko kiuchumi zaidi. Wengi wetu tumekuwa wanasiasa kuliko
kuangalia facts.

Kusema kwamba serikali iwape kampuni binafsi 7 million USD in order to
subsidize ujenzi wa mtambo wa umeme nadhani hapa tunashindwa kabisa
kuangalia business risk ambazo ziinatokana na mpango huu mzima. Tuwe
wawazi jee Mtwara kuna mahitaji makubwa ya umeme mpaka isababishe
serikali kuchangia ujenzi wa mtambo wa umeme? Au wengi tunaamini ile
falsafa ya jenga kisha watakuja?

Nadhani serikali inatakiwa kujadili Mtwara economic growth forecast (
Makisio ya ukuaji wa uchumi wa Mtwara), kisha kutengeneza mpango
endelevu kutokana na hayo makisio. Na sio kutengeneza mpango kutokana na
Matakwa ya wagombea ubunge.

Kutokana na ukuaji wa gesi huko kusini ni ushauri wangu watu wa Mtwara
wajikite kwenye masomo ya muda mfupi yanayohusu mitambo ya kuchimbia
mafuta ( Gas Rigs). Wakae chini na serikali kuomba shinikizo liwekwe kwa
E&P companies (Statoil, BG Group) kuajiri wakazi wa mtwara kwa
asilimia fulani. Labda 10%.

Lakini kushinikiza serikali ijenge mtambo wa kufua umeme wenye uwezo wa
300 wakati matumizi ya mtwara kwa sasa na miaka kumi ijayo yanaonekana
kuwa 50, hapa tutakuwa tunataka kukiuwa hichi kiwanda badala ya
kukiendeleza.

prof muhongo alikuwa akihojiwa dakika 45 na amejibu mengi ya yanayoulizwa
 
Maelezo sahihi kabisa. Inaelimisha vizuri.

TUJIULIZE lini serikali yetu itajifunza kusema ukweli na kuacha kupotosha uma? Kweli hii serikali ni baba wa uongo. Ki biblia baba wa uongo ni Lusiferi mwenyewe.

Tuwaunge mkono wananchi wa Mtwara, umeme uzalishwe pale na matumizi ya msingi ya gesi ifanyiwe pale. Tujiulize ipi rahisi kusafirisha gesi au umeme. Ipi aghali kusafirisha gesi au umeme. Manufaa ya kuzalisha na kusafirisha umeme ni mkubwa sana.

Serikali ya kifisadi, kila kitu ni manufaa binafsi. Aibu yako sisiem
 
Haya ndo matokeo ya kuahidi halafu hutekelezi. Watatokwa povu sana kujaribu kutetea gesi iende Dar, lakini watapata shida sana. Tegemeeni maandamano mengi siku zijazo kwa ahadi za viwanja vya ngege, hospitali za rufaa, meli, mamachinga complex matano etc ect
 
Haya madai yamekaa kisiasa sana kuliko kiuchumi zaidi. Wengi wetu tumekuwa wanasiasa kuliko kuangalia facts.

Kusema kwamba serikali iwape kampuni binafsi 7 million USD in order to subsidize ujenzi wa mtambo wa umeme nadhani hapa tunashindwa kabisa kuangalia business risk ambazo ziinatokana na mpango huu mzima. Tuwe wawazi jee Mtwara kuna mahitaji makubwa ya umeme mpaka isababishe serikali kuchangia ujenzi wa mtambo wa umeme? Au wengi tunaamini ile falsafa ya jenga kisha watakuja?

Nadhani serikali inatakiwa kujadili Mtwara economic growth forecast ( Makisio ya ukuaji wa uchumi wa Mtwara), kisha kutengeneza mpango endelevu kutokana na hayo makisio. Na sio kutengeneza mpango kutokana na Matakwa ya wagombea ubunge.

Kutokana na ukuaji wa gesi huko kusini ni ushauri wangu watu wa Mtwara wajikite kwenye masomo ya muda mfupi yanayohusu mitambo ya kuchimbia mafuta ( Gas Rigs). Wakae chini na serikali kuomba shinikizo liwekwe kwa E&P companies (Statoil, BG Group) kuajiri wakazi wa mtwara kwa asilimia fulani. Labda 10%.

Lakini kushinikiza serikali ijenge mtambo wa kufua umeme wenye uwezo wa 300 wakati matumizi ya mtwara kwa sasa na miaka kumi ijayo yanaonekana kuwa 50, hapa tutakuwa tunataka kukiuwa hichi kiwanda badala ya kukiendeleza.

hivi kwani mtera walihamisha maji kuja dar kufua umeme? kihansi? etc si wamesafirisha umeme ambao ni finished good!!?? na sio maji ambayo ni raw material? issue hapa sio viwanda vya kutumia huo umeme! na sio kwamba umeme utumike kwa wananchi wa mtwara tu, kwani kijijini mtera kuna viwanda? issue ni kwa nini mitambo ijengwe dar/bagamoyo ya kufua umeme na sio mtwara? kwa nini dar wasipokee umeme uliozalishwa mtwara?? je kuna ulazima gani mpaka wajenge hiyo mitambo huko dar kwa gharama za trillions za walipa kodi? tena kwa mkopo?
tukifika hapo ndo tunaona ukondoo huu wa kukaa kimya sasa basi! viwanda havipelekwi kusini kwa vile hamna umeme wa uhakika, now the opportunity has been presented by nature itself hata hapo tuwanyime wanamtwara hiyo golden chance ya kuwaletea maendeleo!! no no no bana hata mungu hatapenda!
na hivi mtwara kuna bandari nina imani upatikanaji wa umeme wa uhakika eneo hilo kitakuwa kichocheo cha kuanzisha viwanda huko na bidhaa zake (finished goods) kusafirishwa kwa njia ya bahari ambayo ni cheap kuja dar na all-over the country. its about time wanamtwara waondokane na umaskini uliokithiri now! msijichumie dhambi kwa ajili ya kutimiza tamaa za mafisadi wachache!
 
Serikali yenyewe kwenye "National Natural Gas Policy" imeweka kifungu kisemacho:

Nyekundu msisitizo wangu mimi.
3.1.7 Local Content and Capacity Building

Issue: Empowerment of Tanzanians to benefit from the natural gas industry.

Local content in Tanzania context refers to added value brought to Tanzanians through activities of the natural gas industry. These may be measured and undertaken through employment and training of local workforce; investments in developing supplies and services locally; and procuring supplies of services locally. Currently, most goods and services are supplied by foreign companies due to inadequate capital and requisite skills to Tanzanians. Participation of Tanzanians in areas where natural gas activities are intensive is important for industry stability, integration into local economies and poverty reduction.

Tanzania can maximize these benefits through strategic participation in the natural gas value chain. Successful maximization of local content benefits require implementation of proper policies, strategies, action plans, continuous consultation with key stakeholders and strengthening capacity of various institutions such as Local Government Authorities (LGAs) and Community Based Organizations (CBOs).

Objective: To develop capabilities of Tanzanians to participate strategically in the natural gas value chain.

Policy Statements:
The Government shall:
(i) Ensure that opportunities for supply of goods and services, employment and investments are made available to Tanzanians and local companies;
(ii) Promote joint venture arrangements between Tanzanians and foreign companies in implementing projects in the natural gas industry;
(iii) Ensure that capabilities of Tanzanians are developed in the natural gas value chain through skills development, transfer of technology and applied research;
(iv) Strengthen capacity of national company responsible for development of petroleum to participate strategically in the natural gas industry;
(v) Establish oil and natural gas center of excellence and strengthen capabilities of the training institutions to impart requisite skills to Tanzanians; and
(vi) Review mandates of Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) to ensure effective management of the natural gas industry.
na hili
3.1.8 Corporate Social Responsibility

Issue: Addressing immediate needs of local communities

Companies implementing projects and activities in the natural gas industry are required to contribute in the development process of the local communities through their Corporate Social Responsibility policies. It is in the interest of both parties to avoid or mitigate the negative perceptions and maximize the positive effects. Currently, activities under Corporate Social Responsibility are not addressing the pressing needs of local communities due to lack of guidelines and little participation of local communities.

The Government will emphasize implementation of Corporate Social Responsibility through proper communication and supporting priority development projects and activities of the local communities to ensure timely achievements in the investments of the companies. The local communities will also participate effectively in protection of the natural gas infrastructure.

Objective: To strengthen Corporate Social Responsibility mechanism in the natural gas activities and projects areas, in order to maximize benefits to the local communities.

Policy Statements:
The Government shall:
(i) Ensure that there is a contractual obligation to all contractors in the natural gas activities to undertake community developmental programmes;
(ii) Ensure companies in the natural gas industry to submit credible Corporate Social Responsibility action plans to the national company responsible for development of petroleum; and
(iii) Ensure companies in the natural gas industry and local government authorities enter into agreement to implement projects as per agreed action plans.
Wanasema empowerment, lakini hata kuwasikiliza watu hawataki.

Serikali jipange upya suala hili si dogo.
 
Tuache upotoshaji.
Kuna gesi ghafi (LG) nyingi tu tumeelezwa kuwa itaweza kuchukuliwa / kuuzwa huko huko kado mwa bahari ; Viwanda vimepangwa kujengwa huko kikiwemo cha mbolea, Wamepewa concessions za kuungiwa umeme, wanafanywa kuwa ukanda (Zone) maalumu ya kibiashara. Hivi wanataka wabwebwe vipi wakati katiba yetu inaeleza kuwa rasilimali ni umma?

Ni upuuzi kulilia bomba badala ya kuzungumzia faida zaidi itokanayo na uzwalishwaji na uuzaji wa gesi.

Halmashauri zako zingejikita kudai kodi ya uzalishaji na hata ya mitambo itakayojengwa. Hata mikoa mingine nasi hatukubali basi fedha zinazotokana na mazao au madini yetu zigawanywe kitaifa. Tupate sisi kwanza na wao baadaye.

Kwanza sasa tuna demand tujue serikali imeshatumia kiasi gani cha keki ya Taifa inayochangiwa na sisi sote (au tumeingia deni kiasi gani katika nchi hii kwa ajili ya utafiti uliokwisha fanyika maana sijasikia mtu yeyote mpuuzi anaandamana akisema TUNAOMBA HILO DENI KWANZA LILIPWE NA WATU WA MTWARA NA WATOTO WAO KABLA YA WENGINE KUCHANGIA KULILIPA!!

Katika kikao cha bunge lijalo naanzisha mjadala kuwa ukitaka zaidi kuliko wengine basi nawe uwe tayari kutoa zaidi hivyo deni lote la utafiti wa gesi kwanza liwekewe wazi na watu wa Mtwara wagawiwe gawio kubwa kabisa kwanza kabla ya wengine!!

Halafu ujinga mwingine ndio huu; Mbona hakuna mbunge hata mmoja wa CCM wala upinzani alipinga hotuba ya huyu Waziri ambayo ilielezea mipango ya Wizara ikiwemo ujenzi wa bomba hilo la gesi au watu huwa hawasomi na sisi ndio wawakilishi wa wananchi?
 
Haya madai yamekaa kisiasa sana kuliko kiuchumi zaidi. Wengi wetu tumekuwa wanasiasa kuliko kuangalia facts.

Kusema kwamba serikali iwape kampuni binafsi 7 million USD in order to subsidize ujenzi wa mtambo wa umeme nadhani hapa tunashindwa kabisa kuangalia business risk ambazo ziinatokana na mpango huu mzima. Tuwe wawazi jee Mtwara kuna mahitaji makubwa ya umeme mpaka isababishe serikali kuchangia ujenzi wa mtambo wa umeme? Au wengi tunaamini ile falsafa ya jenga kisha watakuja?

Nadhani serikali inatakiwa kujadili Mtwara economic growth forecast ( Makisio ya ukuaji wa uchumi wa Mtwara), kisha kutengeneza mpango endelevu kutokana na hayo makisio. Na sio kutengeneza mpango kutokana na Matakwa ya wagombea ubunge.

Kutokana na ukuaji wa gesi huko kusini ni ushauri wangu watu wa Mtwara wajikite kwenye masomo ya muda mfupi yanayohusu mitambo ya kuchimbia mafuta ( Gas Rigs). Wakae chini na serikali kuomba shinikizo liwekwe kwa E&P companies (Statoil, BG Group) kuajiri wakazi wa mtwara kwa asilimia fulani. Labda 10%.

Lakini kushinikiza serikali ijenge mtambo wa kufua umeme wenye uwezo wa 300 wakati matumizi ya mtwara kwa sasa na miaka kumi ijayo yanaonekana kuwa 50, hapa tutakuwa tunataka kukiuwa hichi kiwanda badala ya kukiendeleza.

hujui ulisemalo ndiyo maana umeandika ujinga huu wewe acha ujinga nchi hii inaliwa na wachache na huu mradi ni wa watu furani furani ndiyo maana unaona serikari ina shindwa kukaaa na kujadili hoja bali wanatoha maneno yasiyo kuwa na mantiki.
ikumbukwe kuna siku zito kabwe aliuliza bungeni kuhusu kujenga viwanda vya kuzalisha umeme wa dharura dodoma na mwanza na Mantiki ya Zito ilikuwa kwa nini visijengwe Dar ambapo mafuta yanapatikana kwa haraka na hakutakuwa na cost kubwa ya kusafirisha mafuta mazito? Ngereja alijibu hivi kama hii mitambo itajengwa dar itakuwa ni hasara kwa Tanesco kwa sababu umeme mpaka ukafike Mwanza unapote mwingi njiani, kiukweli lilikuwa ni jibu dhaifu sana kwa jinsi nijuavyo mimi natolea mfano wa Afrca kusini wananunua umeme ktoka msumbiji napale umeme walipochukua mpaka capetown ni zaidi ya km 3500 lakini umeme umefika na wanatumia na si kweli kwamba umeme umepotea sasa kwa taarifa tulizo nazo ni kwamba huu mradi wa kuzalisha umeme Dodoma na Mwanza kuna watu wananufaika nao kwa kuwekeza maroli ya kusafirisha mafuta na siku ukitaka mkuu tumwage hayo majina na makampuni yao inawezekana.
sasa hili la mtwara nalo ni vile vile kuna mkono wa mtu kulikuwa hakuna sababu ya kuleta gesi mjini badara ya umeme ni sawa na mtoto anaanza kukimbia kabla ya kutambaa kwa maana umeme tulio nao hautoshi tunawaza kusambaza gesi majumabani huu ni upuuzi sana wa serikari yetu.
kwa tathimini ya wataaramu bomba ni ghari kuliko kuleta nguzo za umeme
 
Kama hawakujua kupanga uchumi 50 yrs back leo hawana la kutudanganya, wananchi wana akili kuliko viongozi siku hizi.
 
Watu wakishajua siasa ni biashara rahisi ya kutengeneza pesa basi urahisi huu wa siasa uko katika kila nyanja. Watu wanajua siasa ni biashara ya kupiga domo basi chochote kinachotoka mdomoni mwao ni sehemu ya siasa hata kama ni uozo uliokithiri.

*Nadhani viongozi wetu sio serious vya kutosha katika jambo lolote. Wanasoma habari kwenye magazeti na blogs na ni taarifa hizo hizo za kwenye blogs na magazeti ndio wanazozitumia kujibia hoja nzito zinazohusu uhai wa nchi na wananchi wake.

*Kila mtu anajitahidi kueleza hisia zake na ni wachache wanaotoa mawazo.

*Viongozi wamekuwa kama kambale - wote wana sharubu. Huwezi jua jike ni lipi na dume ni lipi. Ni vigumu kujua hata watoto ni wepi maana wote wana sharubu.

*Hakuna mahali rasmi pa kupata habari rasmi maana kote ni wanasiasa tuuuuuuu, wanajibu kisiasa masuala ya kitaalamu. Wataalamu hawana sauti kwenye hili na wala hawasikilizwi. Kuna haja ya kurudisha heshima ya wataalamu wetu kwa wao kuwajibishwa na taarifa za kitaalamu kama hizi za gesi.

*Tukitaka taarifa rasmi za gesi (hasa takwimu na mchanganuo wa kibiashara/kiuchumi juu ya mradi huu wa gesi tunazipata wapi?

*Tukitaka msemaji juu ya taarifa za kitaalamu juu ya gesi twende wapi?? May be University of Dar?? au?

Inachoooooosha!
 
Kwani hata muhongo si ametoka udsm?
 
Back
Top Bottom