PPFT: Askofu Kakobe usitumie mwavuli wa dini kuhubiri chuki na uchochezi

Wakuu huyu mchungaji lkongo hana tofauti na yuda ninazo habari zake nyingi tuu kwanza Ikulu ni kama nyumbani kwake jukwaa la wakriso kunawakati walikuwa wakimtumia kupeleka maamuzi yao kwa Rais kufika kule akawageuka akasema jukwaa la wakriso linataka 2015 ccm isishinde Bali wachukue dola wapinzani. Huyu ni mchumia tumbo tuition.
Halafu huyu Pius Ikongo wala sio Mpentekoste. Ana wake wawili. Kaulize Kanisa la TAG Soweto Moshi watakueleza kuwa huyu ni muasi aliyeoa wanawake wawili. Aligombea ubunge mwaka 2010 katika kura za maoni CCM hapa Moshi mjini akatupwa nje. Kundi analolingoza la PPFT hawamjui sawasawa!
 
Huyo Ikongo ni kibaraka tu wa Interahamwe, wala hata hana Kanisa. Kikao hicho cha Moshi kiliitishwa na Mkuu wa Mkoa aliyesema kwamba anataka kuzungumza na Viongozi wa dini Jumatatu, na kwamba watakuwepo pia wageni kutoka Dar. Ajenda ya kikao haikutajwa, wala hao wageni kutoka Dar hawakutajwa kuwa ni akina nani. Wakati Viongozi wa dini wanamsubiri Mkuu wa Mkoa, ndipo ikaelezwa kwamba Mkuu wa Mkoa atakuja baadaye, lakini kabla hajafika, kuna Kiongozi wa dini kutoka Dar atakayekuwa mzungumzaji. Ndipo akasimamishwa Ikongo, ambaye muda karibu wote wa "semina" yake aliwaambia Viongozi wa dini wasiwe kama Kakobe ambaye amekuwa mstari wa mbele kuidai Tanganyika katika mahubiri yake ya "chuki na uchochezi". Mwisho wa hiyo "semina", Ikongo akamaliza kwa kuwaponda pia Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (PCT), Askofu David Batenzi; na Katibu Mkuu wa PCT, Askofu David Mwasota.

Baada ya Ikongo kumaliza ndipo aliposimama Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa, aliyesema kwamba anamuwakilisha Mkuu wa Mkoa, ambaye eti amepata majukumu muhimu yaliyomfanya alazimike kwenda Same. Katibu huyo pia akawaambia Viongozi wa dini kuilinda amani, kama vile kuzungumzia Tanganyika ndiyo kuiondoa amani. Viongozi wengi wa dini waliohudhuria, walisikitika sana kuona kwamba wamedanganywa kwamba Mkuu wa Mkoa atazungumza nao, kumbe ni propaganda za "Kiongozi wa Dini" Ikongo, ambaye hataki Viongozi wa dini kuzungumzia kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika. Interahamwe wanataka Viongozi wote wa dini wawe kama yule mpuuzi Askofu Mtetemela, na yule Sheikh Jongo aliyelia kwenye Bunge la Katiba kutokana na kukolewa na mahaba ya Interahamwe, na pia Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, aliyesema watu wameitafsiri vibaya kauli ya Lukuvi aliyosema Kanisani Dodoma, kama vile alizungumza lugha ya Kichina, tusiyoielewa!!!
Huyu sio Mpentekoste ndio maana anapinga PCT. Huyu ameoa wake wawili!
 
Kakobe weka Biblia chini kamata katiba.
Hivi ile yakuondoa lile jengo pale iliishia wapi.
 
Huyo yeye anayelaumu kuwa watumishi wa Mungu kazi yao ni kuomba tu! Anayajua maombi? Kama yeye anafanya hivyo atuambie anaombea nchi hii mara ngapi kwa siku na anatumia muda gani kuliombea taifa hil? Hiyo PPFT ni nini? Nina wasiwasi kuwa hawa PPFT wanatumiwa na watu ambao wameipoteza Tanganyika. Nina wasiwasi na mleta uzi kwa kuwa ni wale wale wanaotumiwa na walioiua Tanganyika.
 
Umesema kweli,watu hawamjui Askofu Kakobe bali wanamsikia kwa viumbe wengine tu,baada ya kumsikia mwenyewe baba askofu Kakobe !!! Vizuri zaida kutembelea tovuti yake >>> www.bishopzacharykakobe.org
Watu hawamwelewi Kakobe hata chembe. Wanamwona kwa nje nje tu. Wazungu wanasema don't judge a book by its cover. Mimi naamini Kakobe ni mtumishi wa Mungu ambaye anatumika kufikisha ujumbe kwa watawala ambao hata kama wameweka pamba masikioni utawafikia tu.
 
Umesema kweli,watu hawamjui Askofu Kakobe bali wanamsikia kwa viumbe wengine tu,baada ya kumsikia mwenyewe baba askofu Kakobe !!! Vizuri zaida kutembelea tovuti yake >>> www.bishopzacharykakobe.org[/QUOTE

Tatizo la hawa jamaa wanapenda kuongopewa,wakipata mtu anayewaambia ukweli ili wapone hawataki,ndio maana
wanaishia kukung'utwa na migogoro haiishi,mtumishi wa Mungu Kakobe huwezi mlinganisha na watumishi wachumia tumbo'
 
Huyu aliyeitoa tamko Ana hadhi gani katika jamii? Huu umoja unahusisha vijikanisa gani? CCM mnahangaika sana , Kinana leo huko Singida hakuna habari nini ?

No wewe unayehoji ndiye unauelewa finyu. Na si tatizo lako bali ndivyo akili yako ilivyo kijinga kijinga. Watu ka ninyi mnahitaji kuelimishwa. Waulize latin Amerika jinsi kanisa katoliki lilivyochangia kuleta hasira kwa watawala hatimaye mapadri waliuawa na yakafanyika mauaji zaidi ya raia kisa ni kuhubiri siasa makanisani. Kakobe ni mmoja ya watu wanafiki sana na ni wakukemewa kwani ana brain wash waumini wake.
 
habari leo mhariri wake alipata matokeo kama ya ole nanihii ........yule mbunge machachari wa chama cha majambawazi huku kaskazini
 
Kwani KAKOBE ana hadhi gani katika jamii? Kiongozi wa Dini anayetumia maandiko matakatifu kuwatawanya Kondoo hafai katika jamii ya wastaarabu.
Kama hana hadhi kwa nini Kikwete alimuarika Ikulu ?
Inamaana unapomuarika mtu unaona ana hadhi lakini anapokataa chai yake unasema hana hadhi Kamuulize Katibu Mkuu Yusufu Makamba alivyokuwa anamtafuta Kakobe
 
No wewe unayehoji ndiye unauelewa finyu. Na si tatizo lako bali ndivyo akili yako ilivyo kijinga kijinga. Watu ka ninyi mnahitaji kuelimishwa. Waulize latin Amerika jinsi kanisa katoliki lilivyochangia kuleta hasira kwa watawala hatimaye mapadri waliuawa na yakafanyika mauaji zaidi ya raia kisa ni kuhubiri siasa makanisani. Kakobe ni mmoja ya watu wanafiki sana na ni wakukemewa kwani ana brain wash waumini wake.
1.Kakobe ameunga Mkona hoja ya Tume ya Jaji Warioba wa CCM.
2.Jaji Warioba aliteuliwa na Kikwete(Mwenyekiti wa CCM) kukusanya maoni kwa Muujibu wa Sheria
3.Baada ya Kukusanya maoni Warioba alimufuata Kikwete Ikulu na kumupa ripoti na Kikwete akasoma na kusema ni nzuri na akaamua kusaini na kuendelea na mchakato
Jibu Maswali haya:
1.Hoja ya Tanganyika ni Maoni ya Wananchi na waliokusanya na Kuhakiki ni CCM je Kikwete na CCM ni wachochezi??
2.Kwa nini Kikwete kama ana uelewa alisaini Ripoti ya Tume ya Warioba wakati anajua ina Msimamo wa Serikali tautu na Tanganyika??
3.Watendaji wa serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu walikuwa na msimamo wa Serikali tatu je, Ikulu imemeguka??
4.Nilini Serikali ya CCM na Ikulu ya Kikwete wameanza kupinga kupinga serikali tatu? Kumbuka Zaidi asilimia 70% ya Wajumbe wa Tume ya Warioba ni CCM???
5.Ni kwa nini Kikwete alikubali ripoti ya Tume ya Warioba Ikulu wakati inawakilishwa lakini ghafla anakuja kupinga Bungeni??

KIKWETE ANAPOKEA RIPOTI YA WARIOBA KWA FURAHA IKULU NA KUISANI , LAKINI ANAMSHAMBULIA BUNGENI

Kwa tafsiri ya Ma-CCM, maneno ya chuki na uchochezi, ni maneno yoyote yaliyo kinyume na sera za CCM!!! Mpaka leo Ma-CCM haya, bado yana ndoto za Chama kimoja, na "Zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM!!! - ZIDUMU !!!" SHAME!!!!!
 
USHIRIKA wa wachungaji wa Kipentekoste nchini (PPFT) umemtaka Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zakaria Kakobe, kuacha tabia ya kutumia mwavuli wa dini kuhubiri chuki na uchochezi kwa wananchi.

Akizungumza juzi wakati wa kufunga semina ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika ukumbi wa Umoja Hostel, Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji nchini, Askofu Ikongo alisema kauli za Askofu Kakobe zimekuwa za hatari na zinaweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko ya kidini.

"Nchi yetu imekuwa na dalili za viashiria vya kutoweka kwa amani na utulivu, kutokana na baadhi ya viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa na kuanza kutoa kauli za kuashiria uchochezi na kupandikiza chuki kwa waumini…sasa umefika wakati sisi viongozi wa dini hatuwezi kunyamaza kwani tutaonekana na matamko yanayotolewa kiholela kwa kutumia mwamvuli wa upentekoste," alisema Askofu Ikongo.

Alisema Askofu Kakobe amekiuka uadilifu wake, kwani Aprili 20 mwaka huu katika kanisa lake la Mwenge, alitoa kauli kuwa atapambana hadi Tanganyika irudi hata kwa kukatwa kichwa, kauli ambayo inadhihirisha ugaidi.

Askofu Ikongo alisema kauli kama hiyo haistahili kutolewa na mtumishi yeyote wa Mungu, kwani mtu mwenye uwezo wa kusema hata akatwe kichwa sio wa kawaida bali ni mtu aliye na mafunzo ya kujitoa mhanga kama gaidi.

"Tunasikitishwa na kauli za Askofu Kakobe ambazo zinaweza kuliletea Taifa machafuko ya kidini…siku ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu aligeuza mimbari kuwa jukwaa la siasa, kwa kuhubiri uchochezi kwa kudai; kila mtu anayepigania kurudi kwa Tanganyika, ana Mungu ndani yake," alisema.

Kwa mujibu wa Askofu Ikongo, kauli hizo za Kakobe ni za kigaidi na zina nia ya kuvuruga amani ya Watanzania na kuliingiza taifa kwenye machafuko, ambayo yataharibu tunu iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema ni vyema viongozi wa dini wajikumbushe wajibu wao wa kuliombea Taifa, na kuwaongoza waumini wao kufuata yaliyo mema badala ya kugeuka sehemu ya kutumiwa na wanasiasa.

Akifunga semina hiyo Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Makiluli aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Leonidas Gama, alisema inasikitisha kuona viongozi wa dini kutumiwa na wanasiasa, kwa kutoa kauli zinazowafanya wananchi kuhoji kama viongozi hao hawatumii dini kutekeleza malengo ambayo sio mema.

Alisema Serikali bado ina imani na viongozi wa dini, kwa wale wanaozingatia maadili na utume wao wa kuhakikisha amani iliyodumu kwa miaka mingi inadumishwa.

Aliwataka waumini kutowaunga mkono wanaotumia mimbari kuwa jukwaa la siasa kwa kutoa maneno makali yanayohatarisha amani na kupandikiza chuki miongoni mwa waumini na wananchi.
Chanzo: Habarileo.
Kakobe Katoa maoni yake Juu ya Tanganyika. Jambo la Kushangaza CCM wanampinga hata Warioba aliyefanya Kazi ya kukusanya Maoni na kila mtu anaye changia anatuakanwa na kupandikizwa watalaamu wa Kutukana
Mimi naomba CCM na Kikwete mujibu maswali haya hapa:
MASWALI SABA KWA JK ANAYEPINGA TUME YA WARIOBA
Q1. Kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?

Q2. Wapeni majibu wananchi kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano?

Q3. Elezeni kwa nini Katiba imevunjwa, madaraka ya Rais kuchukuliwa na marais wawili katika nchi moja?

Q4. Tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi na kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?

Q5. Kwa nini mnamtuhumu Jaji Warioba na Joseph Butiku kuwa walikuwa wajumbe wa Tume za Kisanga na Nyalali zilizopendekeza serikali tatu?

Q6. Kwa nini hamtaki kuzungumzia yaliyomo katika rasimu bali wanadai imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba?

Q7. Waelezeni wananchi kwa nini mnadai Tume imeingiza maoni yake, wakati iliyakusanya kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?

CV ya JAJI JOSEPHY SINDE WARIOBA
1.Served as Attorney General (1976-83)
2.Attorney General and Minister for Justice (1983-85)
3. Prime Minister (1985-90).
4.He also served as a Judge on the International Tribunal for the Law of the Sea, (1996-99)
5. Judge at the East African Court of Justice (2001-06).
6.He was Chairperson of the UN Secretary General's advisory panel for the World Summit on Sustainable Development (2001-02).

CV YA JAKAYA KHARAFANI MRISHO KIKWETE
EDUCATION:
1958-61: Msoga Primary School
1962-65: Lugoba Middle Scholl
1966-69: Kibaha secondary School
1970-71 Tanga Secondary School
1972-75 University of Dar es Salaam, B.A (Economics)
1976-77 National Leadership Academy(TPDF) Officer cadet
1983-84 Company Commander's Course
APOINTMENTS:
1975-77 Assistant Regional TANU Secretary-Singida
1977-79 Lieutenant in the TPDF
1977-80 Assistant Secretary-CCM Sub-Head office Kisiwandui
1979-84 Captain in the TPDF
1980-81 Chief Administrative office CCM Head Quarters
1981-83 CCM Secretary ,TABORA Region
1983-86 Political Commissar and Chief Tutor, TPDF Leadership
1984-86 Major in the TPDF
1986-88 District CCM Secretary,Nachingwea and Masasi
1988-90 Deputy Minister for Energy and Minerals
1990-94 Minister for Energy,Mineral and Water
1994-95 Minister For Finance
1995-2005 Member of Parliament Chalinze
1995-2005 Minister of Foreign Affairs and International
2005-To Date President of URT.

ungejua kuwa huyo askofu yukoje kipesa usingesema hivyo?

Askofu Kakobe anaandaa sherehe kubwa ya kukata na shoka kwa kutimiza miaka 25 ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship ! Itakuwa ni kula na kunywa na washirika wake usiku na mchana !!!

ungejua kuwa huyo askofu yukoje kipesa usingesema hivyo?
 
Askofu Ikongo mbona ndio namsikia leo, halafu hao waliokuwa nao kwani sio wanasiasa? Anataka apewe shavu kama yule mwingine Mtetemela halafu hawa sijui wanawakilisha kina nani, nadhani wanawakilisha matumbo yao...

Huyu askofu Ikongo ni mwana ccm kwani alishindwa kwenye kura za maoni za kugombea ubunge Moshi mjini
 
USHIRIKA wa wachungaji wa Kipentekoste nchini (PPFT) umemtaka Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zakaria Kakobe, kuacha tabia ya kutumia mwavuli wa dini kuhubiri chuki na uchochezi kwa wananchi.

Akizungumza juzi wakati wa kufunga semina ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika ukumbi wa Umoja Hostel, Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji nchini, Askofu Ikongo alisema kauli za Askofu Kakobe zimekuwa za hatari na zinaweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko ya kidini.

"Nchi yetu imekuwa na dalili za viashiria vya kutoweka kwa amani na utulivu, kutokana na baadhi ya viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa na kuanza kutoa kauli za kuashiria uchochezi na kupandikiza chuki kwa waumini…sasa umefika wakati sisi viongozi wa dini hatuwezi kunyamaza kwani tutaonekana na matamko yanayotolewa kiholela kwa kutumia mwamvuli wa upentekoste," alisema Askofu Ikongo.

Alisema Askofu Kakobe amekiuka uadilifu wake, kwani Aprili 20 mwaka huu katika kanisa lake la Mwenge, alitoa kauli kuwa atapambana hadi Tanganyika irudi hata kwa kukatwa kichwa, kauli ambayo inadhihirisha ugaidi.

Askofu Ikongo alisema kauli kama hiyo haistahili kutolewa na mtumishi yeyote wa Mungu, kwani mtu mwenye uwezo wa kusema hata akatwe kichwa sio wa kawaida bali ni mtu aliye na mafunzo ya kujitoa mhanga kama gaidi.

"Tunasikitishwa na kauli za Askofu Kakobe ambazo zinaweza kuliletea Taifa machafuko ya kidini…siku ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu aligeuza mimbari kuwa jukwaa la siasa, kwa kuhubiri uchochezi kwa kudai; kila mtu anayepigania kurudi kwa Tanganyika, ana Mungu ndani yake,” alisema.

Kwa mujibu wa Askofu Ikongo, kauli hizo za Kakobe ni za kigaidi na zina nia ya kuvuruga amani ya Watanzania na kuliingiza taifa kwenye machafuko, ambayo yataharibu tunu iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema ni vyema viongozi wa dini wajikumbushe wajibu wao wa kuliombea Taifa, na kuwaongoza waumini wao kufuata yaliyo mema badala ya kugeuka sehemu ya kutumiwa na wanasiasa.

Akifunga semina hiyo Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Makiluli aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Leonidas Gama, alisema inasikitisha kuona viongozi wa dini kutumiwa na wanasiasa, kwa kutoa kauli zinazowafanya wananchi kuhoji kama viongozi hao hawatumii dini kutekeleza malengo ambayo sio mema.

Alisema Serikali bado ina imani na viongozi wa dini, kwa wale wanaozingatia maadili na utume wao wa kuhakikisha amani iliyodumu kwa miaka mingi inadumishwa.

Aliwataka waumini kutowaunga mkono wanaotumia mimbari kuwa jukwaa la siasa kwa kutoa maneno makali yanayohatarisha amani na kupandikiza chuki miongoni mwa waumini na wananchi.
Chanzo: Habarileo.

My God! Hata hawa nao ------------? Hii vita sio ya kitoto
 
Back
Top Bottom