Polisi wapiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika nchi nzima

Papasa

JF-Expert Member
Nov 2, 2018
1,947
4,131
Jeshi la Polisi Tanzania, limetoa onyo kali watu wanaotangaza mpango wa kuiangusha serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia akibainisha kuwa huu ni uhaini na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura ameeleza kuwa taarifa hiyo imekuwa ikisambaa tanga jana Agosti 10, 2023 kwenye mitandao ya kijamii ikihusu kundi la watu ambao wameeleza kwamba wanaandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025 huku hoja inayotajwa ikihusu masuala ya bandari.

IGP ametaka wananchi kuzipuuza taarifa hizo.

Chanzo: EastAfricaRadio
 
Miaka na miaka maandamo yanafanyika na hata yakipigwa marufuku sio kwa sababu hizi za uhaini.

Kuna nini kinaendelea awamu hii?
 
Kwani wanaopinga serikali kuhusu bandari si wanajuliakana? Kamata wote hao kimya kimya tu, wenyewe watapeana taarifa

Hawa kiboko yao alikuwa mjomba tu, viroba ndio stahiki yao.

Wahaini usipowashughulikia watakushughulikia
 
Back
Top Bottom