Polisi wajikoroga kuhusu kifo cha mwenyekiti wa CHADEMA Usa River

Nadhani kwa sasa ingekuwa bora JWTZ wachukue kazi zote za polisi ya Tanzania
 
Hivi wale mafedhuli waliowakatakata wabunge Mwanza walishakamatwa?Au ni upepo tu?
 
Mtu anaposema kifo hiki hakihusiani na hiki, maana yake umeshajua kinahusiana na kile.

Polisi watuambie kifo cha mbwambo kimetokana na nini!
 
Mimi binafsi sijui kama jahazi hili la ukombozi tutafika nalo salama! Hivi hii Tanzania ni ileile ya miaka ya baba wa taifa?
 
Baada ya kutafakari mauaji ya mbwana kule igunga, mauaji ya mwenyekiti CDM Usa river, mauaji ya wale vijana wa Arumeru na kukatwakatwa mapanga wabunge wa CDM mwanza. Nimegundua kuwa kukaa kimya kwa Mbowe na Slaa ktk mambo mazito kama haya kutawagharimu nafasi zao za uongozi huko mbele. Sioni kama wako serious hawa viongozi wakuu wakati wanajua wanaweza kuandaa maandamano yatakayoweza kubadili sura ya mchezo. Nadhani wanatakiwa waoneshe kuwa wanajali maisha ya wafuasi wao na sio kwenda kufanya kama mojawapo ya ajenda ktk mikutano ya hadhara kama alivyoongelea slaa kule Geita kuhusu wabunge amesahau kabisa kama kuna wengine wameuwawa kutokana na uaminifu wao kwa chadema.
 
Baada ya wananchi kuamka na kuamua kuchukua mashamba yao Hakuna hata wiki mbili waliuwawa kinyama vijana wanne.
Jana kabla ya saa tatu usiku kauwawa Mbwambo kinyama, Chap polisi wanatoa tamko kabla ya uchunguzi kukamilika.

Haihitaji degree wala nini kuunganisha dots. Kuna kitu.
 
Typical policcm...hivi utaratibu wa kuengage scotland yard upoje hapa nchini.Sina imani na hawa akina Andengenye kufanya uchunguzi wa tukio hili maana tayar ashatoa msimamo wake
 
nimemshangaa sana andenganye anasema kifo hicho hakihusiani na masuala ya kisiasa wakati uchunguzi bado unaendelea. Cha ajabu ikitokea vurugu mahali fulani hawakawii kusema kuna uchochezi wa kisiasa kabla hata uchunguzi haujafanyika. Mtu wa upinzani akiuawa hawakawii kusema hakuna njama za kisiasa
 
Mimi sina imani na polisi hata mmoja, kuanzia waziri mwenyewe, ambaye kwanza siyo mtanganyika hadi polisi wa mwisho. Na polisi vijana muamke, mnafukuzwa nyiye tu kila siku kwa rushwa wakati viongozi wenu wanakula rushwa ya mabilioni na wanapeta tu, chngamkeni, badilikeni, acheni ujuha.
 
Kibona, uliyoyasema ni kweli kabisa lazima waonye kukerwa na unyama huo mfano swala la wakala wa chadema kuuwawa kinyama kule igunga sikulisikia viongozi wangu wakilishikia bango juzi wabunge mamechalangwa mapanga, siku chache baadae vijana wanne wakauwawa kwa kunyongwa halafu wakatupwa sehemu ambapo kuna ungomvi wa mashamba na wawekezaji hapa huhitaji elimu ya chuo kikuu kujua lengo la wa husika leo tuna sikia mwenye kiti kachinywa..chadema vijana tupo tena wngi chadema watoe tamko tuanze na mabalozi
 
Baada ya kutafakari mauaji ya mbwana kule igunga, mauaji ya mwenyekiti CDM Usa river, mauaji ya wale vijana wa Arumeru na kukatwakatwa mapanga wabunge wa CDM mwanza. Nimegundua kuwa kukaa kimya kwa Mbowe na Slaa ktk mambo mazito kama haya kutawagharimu nafasi zao za uongozi huko mbele. Sioni kama wako serious hawa viongozi wakuu wakati wanajua wanaweza kuandaa maandamano yatakayoweza kubadili sura ya mchezo. Nadhani wanatakiwa waoneshe kuwa wanajali maisha ya wafuasi wao na sio kwenda kufanya kama mojawapo ya ajenda ktk mikutano ya hadhara kama alivyoongelea slaa kule Geita kuhusu wabunge amesahau kabisa kama kuna wengine wameuwawa kutokana na uaminifu wao kwa chadema.

well said mkuu! Ni wakati sasa wa viongozi wa CDM kulitolea tamko swala hili kwani si la kupuuzwa hata kidogo na linagharimu utu wa mtu.
Viongozi wa cdm fungukeni jamani.
 
Mtu anaposema kifo hiki hakihusiani na hiki, maana yake umeshajua kinahusiana na kile.

Polisi watuambie kifo cha mbwambo kimetokana na nini!

kama sikosei siku wale vijana wameokotwa nilikwambia kama polisi imehusika hii issue itapotezewa lakini akifa askari mmoja tu utaona watakavyo haha na kutuomba ushirikiano na kubandika mapicha kila ona a zawadi za ilini lakini watu watano wamekufa hakuna hatua yyte ya maana iliyo chukuliwa zaidi ya kauli za kipumbavu...
 
Back
Top Bottom