Polisi: Marehemu Ally Zona aligongwa na kitu kizito na sio Risasi

Lakini wapendwa najiuliza, risasi ilibaki kichwani!? madactari wameshindwa kujua? kama haikutojea upande wa pili ingebaki ndani, risasi haiwezu kupiga na kudondoka chini kama jiwe!!!?
xp
 
sasa hiyo tume inachunguza nini ikiwa majibu yameshatolewa...polisi wetu bwana afadhali ya wanasiasa.!
 
Alhamisi, Agosti 30, 2012 05:12 Na Merina Robert, Morogoro

BAADA ya kufanyika kwa uchunguzi wa kitabibu kuhusu kifo cha mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ally Zona, matokeo ya madaktari yamebaini jeraha lililosababisha kifo chake limetokana na kugongwa na kitu kizito na si risasi kama ilivyokuwa inadaiwa.

Tukio hilo lilitokea Agosti 27, mwaka huu mjini Morogoro, wakati polisi wakitawanya maandamano ya wanachama wa chama hicho wakitokea eneo la Msamvu Lupila kuelekea Viwanja vya Fire kulikofanyika mkutano huo ambapo awali yalikatazwa na jeshi hilo.

Akieleza matokeo ya uchunguzi huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema jeraha hilo la marehemu lililokuwa kichwani lilitokana na kugongwa na kitu kizito kilichorushwa na si risasi kama ambavyo watu walikuwa wakidhani.

Alisema uchunguzi huo ulifanywa na madaktari wawili wa mkoani hapa pamoja na Dk. Ahmed Makata kutoka Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwanasheria wa CHADEMA, Amani Mwaipaja, pamoja na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi.

Alisema baada ya matokeo hayo ya daktari, polisi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kubaini kitu hicho kilichorushwa na kusababisha kifo cha mfuasi huyo.

Alisema baadaye watachukua hatua za kisheria kwa askari ama mtu mwingine atakayebainika kuhusika kurusha kitu hicho, ikiwa ni pamoja na kumkamata mtu ama kiongozi wa chama hicho aliyechochea ama kuandaa maandamano hayo yaliyozua vurugu.

Alisema katika kubaini mwenendo mzima wa tukio hilo, Serikali imeunda tume ya kuchunguza ambayo inahusisha askari polisi na watu wengine watakaosaidia kukamilisha uchunguzi huo.

Hata hivyo, alisema tume hiyo ambayo tayari imeshafika mkoani hapa, itatafuta maelezo na ushahidi kutoka kwa watu mbalimbali walioshuhudia tukio hilo, wakiwamo wanahabari na kuwaomba wote watakaohitajika kutoa ushirikiano.

Akielezea kuhusu majeruhi, Hashimu Seiph, aliyejeruhiwa mguu katika vurugu hizo, alisema uchunguzi umebaini kuwa alijeruhiwa na bomu lililomuangukia mguuni na anaendelea vizuri na bado yuko Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kwa upande wake, Mwanasheria wa CHADEMA, Aman Mwaipaja, ulikiri kupokea taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa madaktari hao na kusema wanafanya mawasiliano na viongozi wakuu wa chama hicho kuona hatua gani zitachukuliwa.

Alisema kwa sasa anafanya mawasiliano na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, aweze kumpatia taarifa hiyo na hatua zozote zitakazochukuliwa zitatolewa taarifa kwa vyombo vya habari.

Alisema mwili wa marehemu huyo unatarajia kusafirishwa baada ya familia kukaa na kupanga siku ya mazishi mkoani Tanga na mazishi hayo yatahudhuriwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoani Tanga na wengine.


[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Nilimshangaa sana yule RPC aliposema marehemu aligongwa na UFO( Unidentified flying Object). Polisi wakubali tu mapungufu yao haya. Wanapewa taarifa ya Maandamano kama sheria inavyotaka. Wanadai hawana polisi wa kutosha. Watu wakiandamana bila hicho "kibali" chao polisi wanamwagika mabarabarani kwa idadi karibu sawa na wanaoandamana!
 
niwazi kabisa vijana wa chadema ndo walio muua kijana ally muislam mwenzetu.hii ni mara ya pili kwa muislam kufa ktk maandamano ya cdm. Cdm imehusika iwaeleze wananchi

Unasema! muislam mwenzetu? eti nini? hainiingii akilini umefika huko? nani kakwambia vijana wa CDM sio waislam? alivaa nguo imeandikwa Islam? Tafadhali usilete mzaa kwenye majonzi ndugu yangu. Au wewe ndio RPC wa Morogoro umeamua kuja kwa namna hii. the blood of Ally with bear fruits and that fruit will bring revolution in the Country. RIP Ally,
 
Nimeona katika Channel Ten polisi wametoa ripoti kwamba marehemu Ally aliyeuawa katika maandamano ya Chadema Morogoro amefariki kutokana na kugongwa na kitu kizito sio risasi, hiyo ni baada ya uchunguzi wa madaktari

Hata Dr ulimboka watasema aling'atwa na Simba wa mwabepande...au alidondoka kutoka kwenye stool.....he he magamba...
 
Wameua wao, wamechunguza wao na wanatoa ripoti wao! Tafakari!

Jamani tusiamue kabla ukweli haujafika kwenye mahakama. Madaktari nao si wapo waliochunguza mwili? Au nao watakuwa wamehongwa au wanapendelea Polisi? Ni kweli wakati mwingine Polisi wanatenda kinyume na taratibu lakini sio wakati wote.
Tutoe hukumu kwa kila jambo kipekee sio hukumu inafuatana na matendo mengine ya nyuma.
Ngojeni tuone ukweli. Ndugu wapo, viongozi wa Chadema wapo, Wanachama wa Chadema Morogoro wapo, Vyombo vya kutetea haki za Binadamu vipo.
Jaziba haifai isije ikatupelekea kama yale yanayotokea Mombasa baada ya kuuwawa Mtuhumiwa wa Ugaidi.
 
halafu aliyepiga amepatikana ni mfuasi wa CHADEMA alienda kwa GWAJIMA kutubu, basi GWAJIMA akaona bora aripoti polisi
 
IKnashangaza sana, na ni katika nchi hii tu hilo laweza kutokea!! Jana RPC wa Moro, Faustine Shigolile alipora majukumu ya taaluma ya kimadactari na kuamua kuwatangazi Watz matokeo ya uchunguzin wa kifo (autopsy) cha kijana Ally.

Ndiyo -- Watanzania tumefikishwa hapa -- fani ya udaktari inaendelea kutukanwa na kunyanyasaw na jeshi la polisi kwa niaba ya serikali ya CCM -- kana vile ya Mabwepande hayakutosha!!

Na taaluma nzima ya udaktari na Watz wote kwea ujumla wanatakiwa kukubali hii outrage!

Kweli sisi ni wadangayika! Na kwa nini serikali hautaki kutumia Coroner's Act ambayo ipo katika kuchunguza vifo hivi vya utata, uchunguzi ambau hufanyika kimahakama, kwa uwazi zaidi/ Serikali inaogopa nini kama siyo kuwalinda tu mapolisi wauwaji na watesaji wakubwa wa raia?

Mods: Nakuomba usiitoe hii hapa kwani ni topic yenye uzito wa kipekee.
 
Serikali nzima ya CCM ni kinyaa kitupu -- ni udikteta unaoinyemelea kwa kasi! wanatafuta kila namna kujilinda kwa maovu yao!
 
IKnashangaza sana, na ni katika nchi hii tu hilo laweza kutokea!! Jana RPC wa Moro, Faustine Shigolile alipora majukumu ya taaluma ya kimadactari na kuamua kuwatangazi Watz matokeo ya uchunguzin wa kifo (autopsy) cha kijana Ally.

Ndiyo -- Watanzania tumefikishwa hapa -- fani ya udaktari inaendelea kutukanwa na kunyanyasaw na jeshi la polisi kwa niaba ya serikali ya CCM -- kana vile ya Mabwepande hayakutosha!!

Na taaluma nzima ya udaktari na Watz wote kwea ujumla wanatakiwa kukubali hii outrage!

Kweli sisi ni wadangayika! Na kwa nini serikali hautaki kutumia Coroner's Act ambayo ipo katika kuchunguza vifo hivi vya utata, uchunguzi ambau hufanyika kimahakama, kwa uwazi zaidi/ Serikali inaogopa nini kama siyo kuwalinda tu mapolisi wauwaji na watesaji wakubwa wa raia?

Mods: Nakuomba usiitoe hii hapa kwani ni topic yenye uzito wa kipekee.

Kuna siku yataisha yote hayo, kuna siku. tatizo udanganyika wetu ndiyo unatuumiza.
 
Mie kimenishangaza sana hicho kitu. Bila shaka Chama cha Madaktari (MAT) kitatoa tamko hivi punde.
 
wameshahau vijana walichukua picha eneo la tukio na pia ushahidi wa kielectronic na kimazingira utajitosheleza
wamedhani watanzania ni majuha.
kuna watu wa kufukuza kazi hapa, RPC,OCD, madaktari waliopima na magamba kwa ujumla
damu ya mtu haiendi bure majibu yake mtayaona soon.
kwanza balaa litaanzia kwa RPC mwenyewe,na wengineo watafuta.
 
Kwa nini yule daktari aliyoongoza jopo la autopsy asiruhusiwe yeye kutangaza? polisi mnakera kweli kweli!
 
Wanaficha siri, bila shaka iligundulika alipigwa risasi na polisi. Kwani polisi wanakataa nini? si kawaida yao kuuwa, kwani wakikubali hili kutaleta badiliko lolote katika tabia myao hiyo?
 
Back
Top Bottom