Polisi: Marehemu Ally Zona aligongwa na kitu kizito na sio Risasi

Kuna siku yataisha yote hayo, kuna siku. tatizo udanganyika wetu ndiyo unatuumiza.

Hili sio suala la kwisha na kusahaulika. Wote ambao wamehusika na kutenda uovu dhidi ya WaTZ, wanaojihusisha au waliojihusisha na kuficha maovu hayo, kwa kipindi chote cha utawala wao watashitakiwa nchi itakapokombolewa. Umuhimu kwa sasa uwe kwenye kuweka ushahidi na kutunza mashahidi wa uovu huo. Hawa akina Shilogile watatuambia walijua nini na walihusikaje.

Hata Polpot alishitakiwa miaka 30 baada ya uovu wake. Hatutataka kusikia kuwa serikali itakayokuja inafanya "witch hunting" kwani wanaotenda haya wanafanya kwa makusudi. Hatutegemei kuwa na "Truth and Reconciliation commission" ya kusamehe madhambi haya. Nachelea kusema hata CCM itabidi ifutwe kama chama na viongozi wake kupelekwa mbele ya sheria kwa kutumia madaraka ya serikali yake vibaya.

Raisi anaapa kuilinda Katiba ya nchi, na yeye anakuwa wa kwanza kuivunja! Haya yote tunayoyasema ambayo CCM na serikali yake inafanya yanayokiuka Katiba lakini hawaonekani kusikia wala kustuka kwa kuwa wanayo dola tutayakumbusha. Iwe ni serikali yenyewe itakayowashtaki au Wanasheria binafsi walio na ushahidi lakini tutawapeleka mahakamani kujibu shutuma zao. Hakutakuwa na yeyote atakayekuwa na kinga ya kushtakiwa kwa uvunjaji wa Katiba.

Ya Misri na Tunisia yatakuja hapa.
 
Wanaficha siri, bila shaka iligundulika alipigwa risasi na polisi. Kwani polisi wanakataa nini? si kawaida yao kuuwa, kwani wakikubali hili kutaleta badiliko lolote katika tabia myao hiyo?

Mkuu, inaelekea hawajaona ile picha ya marehemu inayoonyesha jeraha kichogoni na tundu la risasi likiwa wazi. Wanafikiri enzi hizi ni zile za miaka ya 70.

Kwa daktari yeyote atakayefanya autopsy atagundua risasi kwenye ubungo wa yule kijana. Technilogy itaonyesha chembechembe za risasi kwenye jeraha. Wasiwasi wangu uko kwenye watu waliofanya autopsy hiyo.

Kama hawakuchukua sampuli sahihi na kuzitunza ipasavyo, ama hawakuwa makini kuchunguza mwili ili kuondoa uwezekano wa muathirika kupoteza maisha kwa sababu nyingine yoyote, Mwanasheria mzuri anaweza kuwasafisha wahusika, sio kuwa hawakuua bali kwa ushahidi finyu.
 
Back
Top Bottom