Polisi: Marehemu Ally Zona aligongwa na kitu kizito na sio Risasi

Ukweli anao mungu. Mungu hafichi kitu. Ipo siku itajulikana tu. Ee mola mrehem ally mpumzishe kwa aman. Damu yake imetumika na uonyeshe ukweli kwa kutumia damu yake. Amin.

Kama police huwa wanaingia nyumba za ibada basi wanamudhihaki Mungu.waoneshe hicho kifaa haraka.nyooooooo police.
 
Kitu kizito siajwaelewa!! Yale yale ya Ulimboka na Mkenya yajirudia tena. Ila Shilogela ametokea Dar. Kova atakuwa ndio Mwalimu wake
View attachment 63299
Hilo tobo linaweza kuwa la kitu gani jamani!!!!??? Polisi acheni kufanya watu wajinga

Sidhani kama risasi ikimpiga mtu inakuwa na uzito au unakuwa kama umepigwa na tunda ya ubuyu.
my take: kama bunduki inauwezo wa kulipiga pipa na likarushwa na bado ikaendelea kuwa nyepesi? basi tunahitaji jeshi la kisasa zaidi la hawa kina kova
 
Kwa mjibu wa ripoti ya madaktar 2 tofauti waliofanyia uchunguzi mwili wa marehemu ally ,aliyeuawa kwenye mandamano ya cdm morogoro wamebainisha kuwa kifo chake kimesababishwa na kupigwa na kitu kizito kichwani na kifo chake kimetokana na kuvuja damu nyingi kichwani. Maelezo hayo yalitolewa na kamanda wa polisi morogoro kufuatia matokeo ya uchunguzi wa madactari
Source tbc taifa
 
Nilisema humu JF, hao hao walioandamana kwa ukaidi ndio hao hao wauaji.
 
Habari nilizopta ambazo huyo RPC wa Moro hakuzisema ni kwamba alipigwa kwenye skull na ganda la bomu la machozi lililorushwa na askari polisi.

Mwanafalsafa wa China Confucius aliwahi kusema kuna vitu vitatu haviwezi kufichika daima -- jua, mwezi na ukweli!
 
Policcm wanachekesha kweli kweli. Wauwe wao, wasimamie uchunguzi wa madokta wao, waunde timu ya uchunguzi wao, watoe taarifa wao -- yaani full one-man show!!!
 
Haya,,,,,,,,, na yule aliyejeruhiwa? Alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali?
ulisikia wapi kesi ya nyani unampelekea ngedere?walishajipanga cha kufanya lakini ipo siku mambo yatabadilika haya mambo wanayofanya yanamwisho,wote pale hawakuwa wajinga kiasi kwamba hawajui risasi,na hapohapo hicho kitu kigumu kikawaporomokea nw wengine 2?acheni ushoga polisi!!!!!!!!
 
Kama kuna siku ambayo polisi waliwahi kutuhumiwa kisha wao wenyewe wakafanya uchunguzi na kujikuta wao wenyewe

wana hatia, nitaiamini habari hii. Otherwise garbage in garbage out!
 
Ni suala la muda tu. Lissu kishawaambia kuna siku tutawataka watuleleze ukweli wote, na siku hiyo haiko mbali sana. Ole wako Shilogile na baba yako Mwema.
 
Lengo lao wanataka kuonesha kuwa ameumia katika fujo kwa kupigwa na chadema kwa kitu kizito! Nadhani wana haja ya

kuonesha hivyo vitu vizito vilivyopiga, kuua na kujeruhi watu.
 
Ukweli anao mungu. Mungu hafichi kitu. Ipo siku itajulikana tu. Ee mola mrehem ally mpumzishe kwa aman. Damu yake imetumika na uonyeshe ukweli kwa kutumia damu yake. Amin.
Mungu wetu hapendi uonevu,ole wao wanaowaonea wanyonge,wataadhibiwa mchana kweupe. M4C inasonga mbele,
 
I hate polisi"Kwa sababu mko kama kadhi dhalimu Hamjali watu wala hammuogopi Mungu"
 
Wameua wao, wamechunguza wao na wanatoa ripoti wao! Tafakari!

Kule Arusha Chagonjwa alisema "CHADEMA walitaka kukichoma kiyuo cha police", huko Mtwara nako Chagonjwa akotoa pumba hiyo hiyo. Mabwepande (kwa Ulli) Kamanda KOVU akatoa pumba hiyo hiyo. Ulitegemea Moro waseme tafauti? hivi ndio vyombo vya dola ambaye waziri wake ni mtoto wa polisi na watumishi wake wengi ni watoto wa mapolisi.
 
Kamati aliyounda Dr Nchimbi ndio imetoa hiyo report? Na kama report ya tume maalum haijatoka, haki itatendeka kweli maana polisi wameshaonesha mwelekeo wao?

Kuuwa ni kosa kubwa, lakini kujaribu kupindisha ukweli ni sawa na kuuwa kwa mara ya pili - unforgivable.

Wakuu! Waziri "MCHIMVI" ni dokta hawezi kudanganya hasa akishirikiana na CHAGONJWA
 
Back
Top Bottom