Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 62
- 1,246
Inadaiwa hapa ni Sinza polisi waliingia Bar inaitwa Boardrom wakatishia wateja kwa bunduki kisha wakampiga risasi mlinzi. I tell you Rais Samia kuna siku hasira zitafumuka raia wataangusha serikali yako kutokana na uonevu polisi ambao kila uchwao wanalalamikiwa na huchukui hatua. Mark my words.
Inadaiwa polisi hao walikuwa wakiwatafuta wanawake wanaojiuza. Swali la msingi kabisa tangu lini wanawake wanaojiuza wakatafutwa kwa bunduki? Yani kwamba tuna jeshi la polisi ambalo linapambana na nyege kwa kutumia bunduki? Seriously? Kila siku nasisitiza kuwa jeshi hili la polisi limeharibiwa mfumo mzima kuanzia sifa za wanaoajiriwa, mafunzo na weledi.
Leo askari polisi wanaotegemea mishahara inayotokana na bia wanavamia bar na bunduki kutisha walipakodi wanaowawezesha wao kulipwa mishahara? Ni ubumunda kiasi gani?
Binafsi napendekkeza ifuatavyo:
1. Askari hawa wachukuliwe hatua kali mara moja zikiwemo za nidhamu na kufikishwa mahakamani.
2. Napendekeza maboresho ndani ya jeshi la polisi kuanzia sifa za wanaoajiriwa kwamba angarau wawe na cheti chochote cha sheria ili kuwasaidia katika uelewa mpana wa sheria.
3. Kwamba mitaala ya mafunzo pia iangaliwe upya. Hatuwezi kuwa na mafunzo ya kutumia zaidi bunduki na maguvu hata sehemu ambazo hazitakiwi nguvu au bunduki. Vifaa vya kisasa na mafunzo ya kisasa yanahitajika zaidi kuliko bunduki na miguvu.
4. Wahitimu wa chuo cha polisi wafanye mitihani ambayo 80% iwe inahusu uelewa wa sheria. Utungaji wa mitihani hiyo ihusishwe ofisi ya DPP , Chama cha wanasheria TLS na wakufunzi wa polisi. Atakayefaulu ndio aajiriwe.
Tofauti na hapo tutaendelea kulia na kulalamika ndugu zetu wakifia mikononi mwa polisi.
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.