asha ngedere
Member
- Nov 6, 2009
- 92
- 11
Idara za ujasusi zinaweza kuficha jina halisi la mtu hata likitajwa hapa unaweza kukuta ni la kificho lakini ni kweli msiba wa jasusi mwenye elimu ya PHD na aliyeandika vitabu vingi vya mambo ya ujasusi aliaga dunia mwezi wa kwanza kwa habari ambazo zilizagaa katika mitaa lakini pasipo mtu yoyote kudhibitisha. Nasikia mazishi yake yalijawa na usiri wa hali ya juu sana ili marehemu asitangazwe kama ilivyo kwa wanasiasa, hata hivyo alizikwa kwa heshima kubwa ya kiongozi mwandamizi wa Idara hiyo nyeti ya Taifa. hata viongozi wakuu wa kitaifa waliokwenda kumzika hawakutangangazwa bali ni barabara tu zilikuwa zinasafishwa kuelekea makazi yake na mwisho mazishi yake. Hakuna mwandishi wa habari aliyeruhusiwa kupiga picha kwani picha zote zilikuwa zinapigwa na majasusi wenyewe kwa kumbukumbu zao. Tumesikia Ulinzi ulikuwa mkali kudhibiti habari za kuvuja au kumtambua jasusi mahili aliyeaga dunia baada ya kulitumika taifa kwa weredi wa hali ya juu na kwa kificho kikubwa hadi anakata roho ya kizalendo.
Hivi hao TISS kuna utaratibu gani wa kuzisaidia familia za watumishi wao waliojitolea moyo, mwili na akili kwa taifa hili? au ukishakufa ndio basi tena?