Poleni TISS tena... R.I.P "Dr"

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Kwa mara nyingine, ninakuja na kutoa rambirambi kwa Idara ya Usalama wa Taifa kwa kumpoteza mmoja wa viongozi wa waandamizi ambao kwa kweli walikulia ndani ya Idara hiyo. Ni pigo kubwa kwa idara hasa kuondokewa na watu wenye weledi na waliojitahidi kufanya kazi yao licha tofauti ambazo zimekolezwa miaka hii michache iliyopita.

Bahati mbaya kutokana na kazi zao watu kama Dr. ni vigumu kuwaona viongozi wa kitaifa wakijitokeza kwenye misiba yao kwani wanalindwa na sheria ya TISS ya 1996. Ni hawa ambao majina yao na sifa za utumishi wao haziandikwi magazetini au hawawezi kuja na kulalamika hadharani jinsi mambo yalivyo magumu kitaifa. Ni hawa ambao huwa wanajikuta wananyong'onyea katika kuta za nyumba zao wasijue wafanye nini. Hawa wasio na watetezi wa wazi.

Na hii ndio sababu siwataji hawa wazee wetu ambao wametumikia taifa katika nafasi mbalimbali na hawakukubali kuwa corrupted kama kundi la baadhi ya vijana ambao wameingia kwenye idara siku za karibuni na sasa wamegeuka kuwa mabepari uchwara.

Natumaini siku moja idara hii itakuja kufanyiwa maboresho yanayohitajika haraka ili watu kama marehemu wazidi kuvutiwa kulitumikia taifa.

RIP - Amezikwa makaburi ya Kinondoni katikati ya mwezi wa kwanza baada ya kulitumikia taifa kwa muda mrefu na kwa uadilifu.

RIP Dr..
 
Thanks Mzee Mwanakijiji for this info.
Japo niko curious kumjua ni nani huyu lakini naungana nawe kuwapa pole wafiwa na naamini kwa kufuata sheria ya nyaraka za taifa, naamini watakuja jitokeza waandishi ambao watawaenzi watu hawa baada ya kupita ile miaka ya nyaraka za siri kugeuzwa sio siri tena!
Umenikumbusha Dr. Who na Dr. No !.
RIP Dr...!.
 
Poleni sana wafiwa ingawa hii habari imechelewa kutufikia. Mwenyezi mungu atawapa nguvu na siku za usoni mtaona mafanikio ya kazi iliyoifanya kwa taifa hili. RIP Dr.
 
Poleni sana wafiwa ingawa hii habari imechelewa kutufikia. Mwenyezi mungu atawapa nguvu na siku za usoni mtaona mafanikio ya kazi iliyoifanya kwa taifa hili. RIP Dr.

Ole.. ingefika mara moja watu wengine wangeweza kuhisi ni nani tunamzungumzia.... Natamani kuwa TISS na wenyewe wanasehemu ambayo wanaweka "nyota" or something in memory of mashushu wetu ambao hawawezi kutajwa kama CIA wanavyofanya...
 

Mkuu Mie kuna mmoja nimekuwa nikisali nae msikitini alikuwa ni mzee mmoja mwadilifu sana na mzalendo mwenye uchungu wa kweli na nchi. Kwa kweli nilikuwa namuadmire sana kama ndio huyo basi tumeondokewa na kifaa na wengi walikuwa hawamjui kweli.
 
angalau wewe umefunguka na kutambua mchango wa marehemu
kwa taifa hili. wengine wako mmhh wanafikiria jinsi ya kuendeleza
ubepari uchwara wao na kujificha katika kivuli cha "taratibu za kikazi"

rip dr.
 
Hivi, kama TISS huficha majina ya viongozi wake, ilikuwakuwaje siku ile Zoka akajitokeza hadharani kukanusha madai ya Dr. Slaa? Kwa kawaida ingekuwa hapa Marekani CIA wangesema "no comment." Sijawahi sikia popote pale mkuu au afisa wa ngazi ya juu wa usalama wa taifa kujitokeza hadharani kujibu shutuma zilizoelekezwa kwenye serikali. Wangesema tu no comment tungejiondokea zetu. Na kwa nini hakutokea mwenyewe RO akajificha nyuma ya mgongo wa Zoka?
 
Hii kazi ni ku-eliminate wengine,vp alikuwa dabo ajenti nini?(Walaa Tajasasu)wala msichunguzane.hiki ndicho ktengo hatari nakiogopa
 
Hivi, kama TISS huficha majina ya viongozi wake, ilikuwakuwaje siku ile Zoka akajitokeza hadharani kukanusha madai ya Dr. Slaa? Kwa kawaida ingekuwa hapa Marekani CIA wangesema "no comment." Sijawahi sikia popote pale mkuu au afisa wa ngazi ya juu wa usalama wa taifa kujitokeza hadharani kujibu shutuma zilizoelekezwa kwenye serikali. Wangesema tu no comment tungejiondokea zetu. Na kwa nini hakutokea mwenyewe RO akajificha nyuma ya mgongo wa Zoka?

Jasusi.. hawa ni maoperative wenyewe siyo wale administrators; ndio maana hata CIA kuna watu ambao wanaweza kuja to the front ila kwenye ile ilikuwa ni mojawapo ya mambo ya kushangaza sana hadi kule ndani wenyewe walishangaana! Kulikuwa hakuna jinsi sasa maana the only other person ambaye angeweza kujitokeza ni RO ambaye credibility yake kwa kweli iko matatani.
 
Du hii sheria labda tuisome vyema sote na kuomba msaada wa tafsiri Mahakamani:

Ningekuwa mimi ningeminya tu kutamka kuwa alikuwa ktk TISS na badala yake ningetaja jina lake wazi hapa na watu wangeendelea kutoa pole zao na faraja kwa wafiwa kama kawa. Maana jina lake linabeba Utu wake unaostahili kutambuliwa pasipo kujali alikuwa wapi kikazi au mwajiri wake alikuwa nani.

Aidha kama mpaka anafariki kweli kwa ujumla hakujulikana katika jamii kuwa alikuwa Intelligence Officer or Agent wa TISS basi jina lake lingetajwa tu hadharani hapa na kazi yake (Cover Design) ambayo kwayo jamii ilimfahamu na kumwona alivyokuwa akiwajibika ipaswavyo katika hiyo huduma nyingine aliyokuwa akiitoa katika jamii kama Mwanasheria au Daktari au Mkufunzi au mfanya biashara n.k

RIP M
 
Kibunago, nimekupata vizuri lakini lengo langu kwa bahati mbaya ni kugusa hasa nafasi yake katika utumishi wa Taifa letu. Nafasi ambayo huwa hawatunzwi. Nataka familia na watu wa karibu wanaomjua wajue kuwa some of us tunaappreciate his service to the nation.
 
Ni siku nyingi kidogo simsikii Dr Hassy Kitine akizungumzia lolote nchi.

Hivi yupo Tanzania hii hii na wala asiseme neno kuhusu upepo wa mabadiliko nchi ninavyomjua msimamo aliyonayo juu ya mambo mengi yanayogusa jamii kitaifa????????
 
Hivi jaman hamjui kibunango na maswali yake? Anapenda sana kuichimba kiundani hii idara sijajua kama ni Agent wa nchi fulani au la na maswali na thread anazoanzisha Huwa za kichokonozi zaidi ya mtu anayetaka kujua kawaida na sidhani kama anajua kuna madhara ya kutoa cover ya mtu maana anaweza kuleta athari mbalimbali zikiwemo kuvuruga wale wanaoendelea na kazi alizoziacha na hata kujulikana madhara aliyosababishia mahali husika
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom