Poleni TISS tena... R.I.P "Dr"

Status
Not open for further replies.
Yo Yo, Du...! Hii kali!.
Humu ndani, umeweka facts and figures as if ni kweli!, kama ni kweli, its not fair ku mu unmask the masked oparatives, utahatarisha sio tuu usalama wa taifa lako, bali pia usalama wake mwenyewe.

Mode: Naomba hiki kipande cha Yoyo kifute haraka kabla hakijaleta madhara.

Nakumbuka mwaka jana, baada ya membe mmoja ku mua un mask FMES IN in black and white na kumuacha mtupu kabisa, kwa kifupi jamaa alifungasha rasmi never to return to jf na makali yake, siku hizi akiibuka ni kyutuma tuu salama that he/she is still alive!

Naomba usitupotezee Mzee Mwakijiji wetu!.
Sasa bahati mbaya wewe umekiquote, wakati unajua ni cha kumvua mtu privacy ya kazi yake...
Anza wewe kufuta ili umshawishi kirahisi!
Vinginevyo hata mimi nimekuwa overwhelmed na data hizo!
 
Hivi jaman hamjui kibunango na maswali yake? Anapenda sana kuichimba kiundani hii idara sijajua kama ni Agent wa nchi fulani au la na maswali na thread anazoanzisha Huwa za kichokonozi zaidi ya mtu anayetaka kujua kawaida na sidhani kama anajua kuna madhara ya kutoa cover ya mtu maana anaweza kuleta athari mbalimbali zikiwemo kuvuruga wale wanaoendelea na kazi alizoziacha na hata kujulikana madhara aliyosababishia mahali husika

I stand to be educated. Hivi wanafanya kazi zipi hawa watu??? mbona Taifa limekithiri kwa wizi wa mali ya umma - serikali imefisadiwa etc. au kazi yao ni kuchunguza wapinzania wa serikali???? au kazi yao ni kulinda maslahi ya wakubwa???? jamani sielewi - waliopo nje ya nchi - labda kuchunguza maadui wa Taifa - lakini waliopo humu ndani ya nchi............ maadui wa Taifa si wanaofuja mali za umma???? Anaejua anieleweshe hizo KAZI ZAO PLEASE.... Again I stand to be EDUCATED.:peace:
 
Kibunago, nimekupata vizuri lakini lengo langu kwa bahati mbaya ni kugusa hasa nafasi yake katika utumishi wa Taifa letu. Nafasi ambayo huwa hawatunzwi. Nataka familia na watu wa karibu wanaomjua wajue kuwa some of us tunaappreciate his service to the nation.

Hivi kumbe yule professor aliyeniambia ukitaka kupoteza "direction" ya maisha yako jiunge na usalama wa taifa alikuwa sahihi eeh?
 
Tatizo la wazee kama hao waliotumikia taifa kwa moyo na uadilifu wakifa basi wanaondoka na kila kitu (wanakufa nacho)................... vitu hivyo ni kujituma, uadilifu, uzalendo, haki, moyo wa uaminifu. Sote twajua kuwa vitu kama hivyo ni vigumu sana kuvirithisha kwa wengine kwa njia ya kawaida, kama tufanyavyo kwa mali kama nyumba. Hilo limepelekea kuwapo na vijana ambao vitu hivyo wamevikosa kabisa, yaani hawana uadilifu na uzalendo hata chembe. wao kazi ni moja tu, kuiba mali ya umma na kujifanya vibepari uchwara. kuna vijana wengi sana ambao wako mtaani na kujisifia kuwa wao ni wana TISS na wanatuonesha tuvitambulisho twao twekundu. sijui kwa faida ya nani!!???!!!??!?
 
I stand to be educated. Hivi wanafanya kazi zipi hawa watu??? mbona Taifa limekithiri kwa wizi wa mali ya umma - serikali imefisadiwa etc. au kazi yao ni kuchunguza wapinzania wa serikali???? au kazi yao ni kulinda maslahi ya wakubwa???? jamani sielewi - waliopo nje ya nchi - labda kuchunguza maadui wa Taifa - lakini waliopo humu ndani ya nchi............ maadui wa Taifa si wanaofuja mali za umma???? Anaejua anieleweshe hizo KAZI ZAO PLEASE.... Again I stand to be EDUCATED.:peace:
Naambiwa kuwa kuna watu TISS wamebobea kwenye Economic Espionage, hapo kweli naachwa hoi!..wanashindwa vipi kushauri serikali na kuchukua hatua juu ya utoroshaji uliokithiri wa madini nchini ambao unafanywa kupitia baadhi ya viwanja vya ndege!
Ni unazi upi wa kiuchumi na kizalendo walioufanya so far ambao umepelekea nchi kuinuka na tunaweza kujitapa kuwepo kwao?
CURIOUS!
 
Kwa nini Pasco?ni maoni yangu tu nionavyo.kwani kuna ukweli?
Zion Daughter, yes hapa jf uko huru kutoa maoni yako kadri unavyopenda, ila inapokuja kwenye majina ya members wengine, hairuhusiwi, mathalani mimi natumia jina la Pasco, mtu ukiibuka na kusema Pasco anafanya kazi Umoja House, kama ni kweli, then its name calling unastahili ban. Au kama sijajitambulisha kuwa mimi ni mwandishi wa habari wa PPR, mtu akiibuka na kusema Pasco ameajiriwa PPR, kama ni kweli, ni name calling na anastahili ban. Sio vizuri, kutoa comments zinazokaribiana na ukweli kwenye majina ya watu, au kazi za watu!.
 
Hivi, kama TISS huficha majina ya viongozi wake, ilikuwakuwaje siku ile Zoka akajitokeza hadharani kukanusha madai ya Dr. Slaa? Kwa kawaida ingekuwa hapa Marekani CIA wangesema "no comment." Sijawahi sikia popote pale mkuu au afisa wa ngazi ya juu wa usalama wa taifa kujitokeza hadharani kujibu shutuma zilizoelekezwa kwenye serikali. Wangesema tu no comment tungejiondokea zetu. Na kwa nini hakutokea mwenyewe RO akajificha nyuma ya mgongo wa Zoka?

it is a disgrace to service. halafu issue yenyewe alivyoielezea alikuwa very unprofessional. sikumtofautisha na chiligati au makamba
 
Naambiwa kuwa kuna watu TISS wamebobea kwenye Economic Espionage, hapo kweli naachwa hoi!..wanashindwa vipi kushauri serikali na kuchukua hatua juu ya utoroshaji uliokithiri wa madini nchini ambao unafanywa kupitia baadhi ya viwanja vya ndege!
Ni unazi upi wa kiuchumi na kizalendo walioufanya so far ambao umepelekea nchi kuinuka na tunaweza kujitapa kuwepo kwao?
CURIOUS!

UwT ni Watanzania sisi hawahawa. Sote tumeoza nje ndani.
 
Kibunago, nimekupata vizuri lakini lengo langu kwa bahati mbaya ni kugusa hasa nafasi yake katika utumishi wa Taifa letu. Nafasi ambayo huwa hawatunzwi. Nataka familia na watu wa karibu wanaomjua wajue kuwa some of us tunaappreciate his service to the nation.
Yes MM, they have a right to professional recognition for their work and accomplishments, both with fair monetary remuneration, and non-monetary forms of recognition.
 
jamani mi namtaja jina maana sioni sababu ya kuendelea kuficha jina lake anaitwa

DR. HERI LUPEMBE alifaliki ghafla akiwa ofisini kwake kwa kweli ni pigo. na asante mwanakijiji nilikuwa najiuliza mbona hawatangazi kifo chake. du R.I.P Dr. Lupembe

I thought jina lake likitajwa ndo itakuwa mwisho wa dunia. Naona bado tunadunda tu. RIP DR pamona na kwamba ni mara yangu ya kwanza kukusikia. :sad:
 
Naambiwa kuwa kuna watu TISS wamebobea kwenye Economic Espionage, hapo kweli naachwa hoi!..wanashindwa vipi kushauri serikali na kuchukua hatua juu ya utoroshaji uliokithiri wa madini nchini ambao unafanywa kupitia baadhi ya viwanja vya ndege!
Ni unazi upi wa kiuchumi na kizalendo walioufanya so far ambao umepelekea nchi kuinuka na tunaweza kujitapa kuwepo kwao?
CURIOUS!

PakaJimmy, tatizo kuna watu wanashindwa kutofautisha kati ya TISS ya mtaani na TISS ya ukweli, ndio maana vitu vingine tunavyosikia vinachekesha.....eti economic espionage?.....vere fane.
 
Naambiwa kuwa kuna watu TISS wamebobea kwenye Economic Espionage, hapo kweli naachwa hoi!..wanashindwa vipi kushauri serikali na kuchukua hatua juu ya utoroshaji uliokithiri wa madini nchini ambao unafanywa kupitia baadhi ya viwanja vya ndege!
Ni unazi upi wa kiuchumi na kizalendo walioufanya so far ambao umepelekea nchi kuinuka na tunaweza kujitapa kuwepo kwao?
CURIOUS!

Economic Espionage my foot!! It is so funny to hear this. Ndio maana tumeletewa RICHMOND, DOWANS na mikataba ambayo haistahili hata kuitwa mibovu bali UOZO!!!.
 
Economic Espionage my foot!! It is so funny to hear this. Ndio maana tumeletewa RICHMOND, DOWANS na mikataba ambayo haistahili hata kuitwa mibovu bali UOZO!!!.

Tuko pamoja Chief. Kwa jinsi uchumi wetu ulivyo ovyo ovyo na shamba la bibi, hakuna spy yeyote hapa Tanzania anaweza kutembea kifua mbele kwamba ni bingwa wa economic espionage kwa manufaa ya taifa; labda kwa maslahi ya mafisadi.

Sasa mkitaka kumpa sifa zilizotukuka huyo mzee, msiingize hiyo kitu ya economic espionage. Naye ataonekana fisadi tu.
 
Zion Daughter, yes hapa jf uko huru kutoa maoni yako kadri unavyopenda, ila inapokuja kwenye majina ya members wengine, hairuhusiwi, mathalani mimi natumia jina la Pasco, mtu ukiibuka na kusema Pasco anafanya kazi Umoja House, kama ni kweli, then its name calling unastahili ban. Au kama sijajitambulisha kuwa mimi ni mwandishi wa habari wa PPR, mtu akiibuka na kusema Pasco ameajiriwa PPR, kama ni kweli, ni name calling na anastahili ban. Sio vizuri, kutoa comments zinazokaribiana na ukweli kwenye majina ya watu, au kazi za watu!.
Asante,ngoja nikajikumbushe tena sheria za JF .naamini mode hataiona hii...
 
Kwa mara nyingine, ninakuja na kutoa rambirambi kwa Idara ya Usalama wa Taifa kwa kumpoteza mmoja wa viongozi wa waandamizi ambao kwa kweli walikulia ndani ya Idara hiyo. Ni pigo kubwa kwa idara hasa kuondokewa na watu wenye weledi na waliojitahidi kufanya kazi yao licha tofauti ambazo zimekolezwa miaka hii michache iliyopita.

Bahati mbaya kutokana na kazi zao watu kama Dr. ni vigumu kuwaona viongozi wa kitaifa wakijitokeza kwenye misiba yao kwani wanalindwa na sheria ya TISS ya 1996. Ni hawa ambao majina yao na sifa za utumishi wao haziandikwi magazetini au hawawezi kuja na kulalamika hadharani jinsi mambo yalivyo magumu kitaifa. Ni hawa ambao huwa wanajikuta wananyong'onyea katika kuta za nyumba zao wasijue wafanye nini. Hawa wasio na watetezi wa wazi.

Na hii ndio sababu siwataji hawa wazee wetu ambao wametumikia taifa katika nafasi mbalimbali na hawakukubali kuwa corrupted kama kundi la baadhi ya vijana ambao wameingia kwenye idara siku za karibuni na sasa wamegeuka kuwa mabepari uchwara.

Natumaini siku moja idara hii itakuja kufanyiwa maboresho yanayohitajika haraka ili watu kama marehemu wazidi kuvutiwa kulitumikia taifa.

RIP - Amezikwa makaburi ya Kinondoni katikati ya mwezi wa kwanza baada ya kulitumikia taifa kwa muda mrefu na kwa uadilifu.

RIP Dr..

RIP Dr. Iko wazi sasa kwamba waliobaki wa kariba hiyo nao wanafahamika! Mazingira haya ni hatarishi.
 
Ni siku nyingi kidogo simsikii Dr Hassy Kitine akizungumzia lolote nchi.

Hivi yupo Tanzania hii hii na wala asiseme neno kuhusu upepo wa mabadiliko nchi ninavyomjua msimamo aliyonayo juu ya mambo mengi yanayogusa jamii kitaifa????????

Huyu yupo, sikuwa namfahamu kwa sura, lakini wiki iliyopita alikuwa mahali nikakonyezewa na rafiki yangu kwamba ni yeye, na hapakuwa na shaka, kwani rafiki yangu huyo alikwenda kumsalimia wakazungumza kwa muda tu. Sio yeye!

Lakini TISS kumbe si chochote! Wanajificha kwa sababu kazi wanayoifanya si njema. Sioni kwa nini watu kama hao, wafanye kazi kwa kificho namna hio. Wamekuwa Gestapo!?
 
RIP Dr. Iko wazi sasa kwamba waliobaki wa kariba hiyo nao wanafahamika! Mazingira haya ni hatarishi.
Mpui Lyazumbi, Tanzania tuko piece, hakuna mazingira yoyote hatarishi kwa watu watu maana wengi wao tunajichanganya nao, tena kwa kujulikana ndio wanaona sifa.

Sijawahi kusikia maofisa hawa wamedhurika kutokana na kujulikana, sana madhara makubwa ni jinsi tuu wanavyolipuana wenyewe kwa wenyewe pale Kijitonyama!.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom