STEIN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,770
- 553
Ndugu zangu naomba niwapongeze wapenda mabadiliko bila kuisahau CDM na viongozi wake kwa kuwaelimisha waTZ kuhusu katiba mpya kwani waTZ wote sasa wanaelewa hata chanzo cha umasikini wao unatokana na Katiba iliyoko sasa kwani inampa rais na serikali madaraka makubwa makubwa mno ambayo kwa miaka 49 sasa yamekuwa yakitumiwa vibaya sana ndio maana nhi hii na rasilimali zote ni masikini na watu wake ni masikini ile hali viongozi wakiwa matajiri wa kutupwa.
Pili nawapongeza wanaJF kwa kuzidi kuongeza kasi katika kudai haki, na katiba mpya ya nchi naomba mijadala hii iendelee hadi tutakapowashinda mafisadi nchi hii maana kama alivyosema mtoto wa mkulima mafisadi wana hela nyingi sana na wana nguvu sana kama ambavyo wamekuwa wakiwarubuni viongozi machachari nchi wakitaka kupanga safu ya viongozi watakao watetea hadi kwenye vyama vya siasa kama tuliyona siku za hivi karibuni.
Tatu naomba kumpongeza kamanda mbowe akisaidiwa na Dr. Slaa kwa misimamo yake kwani amekuwa mwiba kwa Mafisadi na ndio waTZ tunataka mtu wa namna hiyo, mapambano daima hadi kieleke wananchi wapo pamoja nanyi. watu wamechoka kimsingi na wako tayari kwa mabadiliko kwa gharama yeyote.
Kwa kweli mwaka huu nafikiri mafisadi wametumia mbinu zote hadi zimekwama kwa chadema, tuendellee na moyo huo na kama vipi watu wako tayari kugharamikia Democrasia.
Peoples Power.