Pinda: Serikali kuunda jopo kuchunguza madai ya katiba mpya

Niliandika hapa kwamba moto kuhusu katiba mpya uliowashwa na CHADEMA hakuna wa kuuzima. Sasa ni kuendelea kuishinikiza Serikali kwamba hatutaki kuongeza viraka kwenye katiba mpya ambavyo vinavyoulizana mwenzangu umekuja lini, bali tunataka katiba mpya ambayo itaendana na hali halisi ya siasa za vyama vingi nchini na pia kuhakikisha katiba hiyo inapatikana kabla ya uchaguzi ujao 2015. Hongera sana CHADEMA juhudi zenu taratibu zinazaa matunda.

Lazima kuwe na time frame kwamba katiba mpya itapatikana lini, vinginevyo wadanganyika watasubiri kama wazee wa jumuiya ya afrika mashariki
 
Lazima kuwe na time frame kwamba katiba mpya itapatikana lini, vinginevyo wadanganyika watasubiri kama wazee wa jumuiya ya afrika mashariki

Naam NN, CCM hawaoni kama kuna haraka yoyote ya kuwa na katiba mpya wako tayari kusubiri hata 2050 maana wanajua wazi kwamba katiba iliyokuwepo inawapa mianya mingi ya kuendelea kuwepo madarakani na hata kupata kiburi cha kutamka kwamba, CCM itatawala milele.
 
Bila samahani Mkuu. Ni kweli kabisa hili la katiba mpya ni swala linalohusu umma wote wa Watanzania ambao wana mapenzi ya kweli na nchi yetu na si la CHADEMA au CCM tu. na sikutaka kumaanisha kwamba issue hii inaihusu CHADEMA tu. Pamoja na Watanzania wengi kuipigia kelele katina iliyopo na kutaka iundwe katiba hii, safari hii chokochoko hizi za kuishinikiza Serikali kuhusu katiba mpya zilianzishwa rasmi na CHADEMA mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa. Hivyo sioni ubaya wowote wa kuipongeza CHADEMA kama waanzilishi wa chokochoko hizi ambazo taratibu zinaanza kuzaa matunda.

Mkuu,

Wakati wa kupongezana bado, ni mapema sana. Asante kwa ufafanuzi.
 
Naam NN, CCM hawaoni kama kuna haraka yoyote ya kuwa na katiba mpya wako tayari kusubiri hata 2050 maana wanajua wazi kwamba katiba iliyokuwepo inawapa mianya mingi ya kuendelea kuwepo madarakani na hata kupata kiburi cha kutamka kwamba, CCM itatawala milele.

kibaya zaidi kuna project 2015 nyingi tu ndani ya ccm ndio maana wata dilly dally tu, lazima watanzania tushupalie katiba mpya haraka sana.
 
Baada ya kilio cha muda mrefu cha madai ya Katiba, hatimae hii leo serikali ya Tanzania imekiri kuwa ipo haja ya kuifanyia mabadiliko Katiba ya sasa ili iweze kukidhi mahitaji na mabadiliko ya sasa.


Akiongea na wahariri wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema serikali itaunda jopo la wataalam kupitia mapendekezo ya awali na ya sasa yaliyotolewa kuhusiana na mabadiliko ya Katiba.


Hata hivyo Mh. Pinda amesema serikali bado haina jibu iwapo yafanyike mabadiliko makubwa ama mabadiliko madogo kutokana na mapendekezo yaliyokwishatolewa, au suala hilo lipelekwe bungeni ama lirudishwe kwa wananchi kwa maamuzi.


Source-Mimi

Ni hatua na maamuzi yaliyochelewa sana na uharibifu wa kutisha umeshafanyika kwa nchi yetu na wananchi wake kwasababu ya katiba hiyo ya kijima.Ni nani atalipia uharibifu ambao umeshafanyika kwa ajili ya katiba hiyo?Inasikitisha kwamba watu waliohusika na kuchelewesha katiba mpya tena kwa makusudi kabisa na kwa maslahi yao binafsi wanaendelea kupeta kana kwamba hakuna lililotnkea.Ni nani atawafuta machozi wananchi hawa walio-onewa na kunyimwa haki zao kwa ajili ya katiba hiyo uchwara iliyopitwa na wakati?
 
Wakuu, mnafikiri ni busara kwa CCM ku-lead hii process ya mabadiliko ya katiba?
Mnafikiri tupo tayari kwa sasa? mnafikiri wananchi wanajua katiba ina matatizo gani?
CCM ipo very strategic, mnafikiri itajitengenezea kaburi lake yenyewe?

Nipo skeptic kidogo on this one. Sorry.
Kweli ndugu si busara kumkabidhi fisi kulinda Bucha!
 
@THE DREAMER ambaye amesema "wanatafuta kupachika OIC na kadhi kama Kenya. Sitaki katiba mpya kwa sababu hiyo".

Ili mchakato wa kupata katiba mpya uende vizuri compromise and "give and take" ni muhimu. Kama si hivyo katiba inaweza kuchukua muda mrefu kuliko Kenya, na huenda isipatikane kabisa.

Lakini pia DREAMER why do you hate Islam too much!? I am sure unatamani ndugu zetu hawa wasinge exist kabisa. Ndo UPENDO HUO ALIOHUBIRI YESU BWANA WETU YESU KRISTU?
 
Naomba nirudie maneno yangu tena. Chini ya utawala wa CCM hakutakuwa na katiba mpya hiyo ya pinda ni danganya toto tu. watakachofanya ni kuiwekea viraka tu, ili kuwatuliza wananchi. CCM will never dig is own grave.
Kumbuka kwamba
kila jambo lina wakati wake.Kuna wakati wa kulima na wakati wa kupanda.Tena kuna wakati wa palizi na wakati wa kuvuna.Naomba pia ukumbuke kwamba utakula matunda ya kinywa chako.
 
Naomba nirudie maneno yangu tena. Chini ya utawala wa CCM hakutakuwa na katiba mpya hiyo ya pinda ni danganya toto tu. watakachofanya ni kuiwekea viraka tu, ili kuwatuliza wananchi. CCM will never dig is own grave.
Hapana tunaweza kupata katiba MPYA kabisa chini ya uongozi wa CCM! lakini lazima kutakuwa na vifungu vitakavyoilinda CCM au viongozi wake!
 
Don't wait until people start to puke. If you dare wait, see what is going to unfold before you!
Katiba mpya si kama EPA for the organs to dilly-dally! It needs a concrete actions to set its wheels into a go object.
 
Bado tuendelee kutafakari dhidi ya tamko la PM, je hilo jopo linateuliwa na nani maana yasije yale yale ya tume ya uchaguzi kuchaguliwa na wakuu wa serikali.Tuendelee kutafakari.
 
JOPO BILA UTEUZI TOKA KWA WADAU WOTE WA KATIBA WALA HADIDU-ZA-REJEA YAO NI KUJIFURAHISHA TU KILIONI!!!

Mtoto wa Mkulima,

Hatutaki MADALALI wa kuteuliwa na kuwakilisha MASLAHI ya MTAWALA kwenda kuchunguza mambo ya Katiba wakati sisi WATAWALIWA hatujashiriki kwenye kuwateua watu hao. Mheshimiwa Pinda, ni nyinyi watawala ndio HATURIDHIKI na utendaji wenu kazi tulizowapa na kutaka TUPITIE KWA PAMOJA NA KUANDIKISHA UPYA mkataba mpya ya utawala, iweje tena ukaniteulie jopo wewe wewe???????????????????

Hapa leo hatukubaliani hata kidogo!! Majibu watakayokuletea jopo lako hilo la kujiteulia tayari tunaweza tunaweza kukujatia hata kabla hawaanza kazi yako hiyo lakini kwa kodi zetu. Utasikia wanaotaka KATIBA MPYA ni asilimia 2.001% kwa nchi nzima na kwamba matakwa yao ni madogo madogo sana kiasi kwamba VIRAKA TU inatosha. Kwa hapo ndipo mawasiliano na wananchi yatakapoanza kupotea moja kwa moja na serikali na watu kulazimika kutafuta katiba mtaani.

Mwenye JUKUMU LA KUUNDA JOPO HILO SI WEWE, SERIKALI WALA Chama chchote kile!! Lenu ni kuanzisha mchakato, na kuifadhili kwa kodi zetu na kutoa ushauri mnapoombwa full stop. Nyinyi kama serika ni sehemu ndogo sana ya WADAU WA KATIBA hivyo kamwe haiingii akilini kwa mdau mmoja tu KUJITEULIA JOPO bila kushirikisha WADAU WOTE WA KATIBA na kuweka wazi zaidi misingi itakayotumika kufanya hiyo kazi yao na wao kuwajibika kwa nani.

Kumbuka hapa hatuzungumzii harakati za kuanzishwa kwa sheria pengine ya kuwalinda ndugu zetu walemavu wa ngozi au wazee wanaouawa kwa tuhuma za uchawi ambapo SERIKALI inaweza ikajikalia tu chumbani na kuibuka asubuhi moja kuteua teua watu kwenda kuangalia namna gani sheria hizo zitungwe.

Wadau wate wa KATIBA amkeni, ndio hivyo madai yetu halali YANAANZA KUTEKWA na serikali kuanza kuandaa taifa kwa michafuko ambayo hatuyapendi hata kidogo.

Kwa kupenda kwetu AMANI ndio maana tumeporwa ushindi na tukajinyamazia mpaka leo. Sasa Kutupora tena na madai ya KATIBA MPYa, NO NO NO!!! Hata mmbwa ukimfukuza sana atakimbia lakini ukiendelea kumkabili hadi akafiki ukutani na hana pa kwenda, kitakachofuata ni kwamba mmbwa huyo ataanza moja kwa moja KUKUKABILI WEWE ili akaokoe roho yake!!!

Mtoto wa Mkulima, huu ni ushauri tu kwa sababu ni muhimu sana TUSIFIKE HUKO.
 
Wananchi wapewe muda kuielewa iliyopo ili wapate kutoa maoni. juu ya tume kuundwa napata wasiwasi nani atawateua hao wajumbe wa tume?
 
Uwezo Tunao, Kwanza kinachotia wasi wasi sana ni kusema suala la kumshauri rais kuunda jopo na kuleta mapendekezo litafanywa ndani ya miaka mitatu!!!

Hii ni dana dana tu ili watutulize muendelee na kutafuna keki yetu wote...

Pinda suala la katiba si ombi ni lazima kwa sasa la sivyo tunakoelekea siko....!!!
 
Pinda: Serikali kuunda jopo kuchunguza madai ya katiba mpya
uongo, kasema:

1) binafsi haoni tatizo la Katiba

2) lakini atamshauri Rais

a) kuunda jopo la wataalam kutoka asasi mbalimbali kuliangalia swala hili, au
b) kuhusisha maoni ya wananchi, au
c) kutumia utaratibu wa ndani ya serikali, kutumia wataalam wa serikali.

3) yeye Pinda anadhani jopo la wataalam ndio njia bora zaidi
___________________________________

PINDA HAJAAHIDI SERIKALI ITAUNDA JOPO
 
Alichokisema Pinda sidhani kama ndio Mwanzo wa Katiba mpya, ni vigumu sana kutabiri mapendekezo ya CCM, wao wanaamua leo hili na kesho lile. Kwanza ni lazima wakubali tujadili kwanza tatizo lipo wapi katika katiba hii, baada ya wao kuhusika katika mahojiano ya nini kimekosewa na ni nini iwe frame work ya katiba then tunaweza kusema tunaanza kuandika katiba mpya.

Vingenevyo CCM wataandika katiba nyingine ambayo ina wafavor wao, na itachukua miongo na miongo kuibadili. I hope wote tunaona hili, CCM ni wajanja na ili ushindane nao lazima uwaze mbele ya uwazo wao.
 
Hapana tunaweza kupata katiba MPYA kabisa chini ya uongozi wa CCM! lakini lazima kutakuwa na vifungu vitakavyoilinda CCM au viongozi wake!
Yes kama wakiweza kuandika katiba still itailinda CCM 100%. Jamani kama waliweza kucheza na akili zetu wakati wa uchaguzi na kuonyesha kama matokeo yalikuwa poa. ndivyo hivyo itakavyokuwa hata katiba watakuja na lugha tamu na laini, Na kwa sababu watanzania wengi si watu wakuchambua mambo kwa undani na ni watu wa 'NDIYO MZEE'
Mfano wa kuthibitisha hili ni wakati CHADEMA walipotoka nje ya bunge kipindi the so called Dr. kikwete akihutubia, hakuna mtanzania yoyote aliyesema au kutoa sababu za msingi za kupinga kitendo chao, zaidi ya kusema tu kwamba WAMEMVUNJIA HESHIMA MHESHIMIWA DR. Hii inaonyesha kuwa atakapo sema raisi jambo lolote mathalani kuhusu katiba hata kama ni baya tutakubali hili tusimvunjie heshima
 
Back
Top Bottom