Pinda: Dowans hatuirudishi bungeni

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Na Baraka Kimwanga

SERIKALI imesema mjadala kuhusu fidia ya kampuni ya Dowans hautarudishwa bungeni na badala yake itafuata taratibu za kisheria kwa kwenda mahakamani ili mkondo wa sheria uchukue mkondo wake.

Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara hivi karibuni ililiamuru shirika la uzalishaji na ugavi wa umeme nchini (TANESCO) kuilipa Dowans fidia ya shilingi bilioni 94 baada ya kulitia hatiani kwa kuvunja mkataba baina yake na kampuni hiyo kinyume cha taratibu za kisheria.


Msimamo mpya kuhusu Dowans ulitolewa jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika mkutano wake na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika semina ya siku tatu kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), iliyofanyika Blue Peal Hotel, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam ambapo alisisitiza kwamba suala la fidia ya Dowans halina ujanja kwani ni la kisheria na kwa hiyo ni lazima tulishughulikie kisheria.


"Hatutalipeleka suala hili bungeni….kulipeleka huko itakuwa ni kwenda kujadili siasa na si sheria. Na kwa hili tayari kuna timu ya wabunge wa CCM ambao ni watalaamu wa sheria pamoja na timu itakayoundwa na serikali, timu hizo zitakaa na kupitia kwa makini suala hili ili twende tukatafute ufafanuzi huo wa kisheria," alisema Pinda.


Alisema mjadala huo wa hukumu ya Dowans umeibua hisia za watu mbalimbali nchini na hata kupelekea baadhi ya viongozi wa serikali kuingilia kati na kutoa misimamo yao hali ambayo haikuleta taswira nzuri kwa taifa.


"Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake, na hata mawaziri waliopishana kauli ni ugeni wa masuala ya serikali tu, lakini jambo hili ni letu sote kama serikali na hivi sasa tumejiweka sawa ili kuepusha hali kama hii isijirudie tena," alisema Pinda.


Akisoma maazimio ya semina hiyo Kaimu Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama, alisema kamati yao imeishauri serikali kutafakari kwa makini hukumu hiyo na kutumia njia za kisheria kuangalia uwezekano wa kutolipa fidia hiyo.


"Kuhusu deni la Dowans kwa TANESCO la sh 94 bilioni kamati ya wabunge wa CCM wameitaka serikali kupitia njia za kisheria itazame upya suala hilo kwa nia ya kutafuta uwezekano wa kuwaepushia Watanzania mzigo huu," alisema Mhagama.


Alisema wabunge wa CCM wametakiwa kutumia kamati ya wabunge kwa ukamilifu kujadili masuala yote na hata kukosoana ndani ya vikao vya kamati kwa uwazi ili kulinda maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.


Hata hivyo Mhagama alisema semina hiyo imewapa uhuru kamili wabunge hao kuikosoa serikali na kutoa mawazo yao kuhusu masuala yote yenye maslahi kwa taifa ili mradi watumie lugha ya ufasaha.


"Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, imetupa uhuru wa kuikosoa serikali na vyombo vyake ili mradi tu lugha ya ufasaha itumike katika kutoa maoni," alisema Mhagama.


Alisema wabunge hao wameunda kamati ndogo ya kufanya marekebisho ya kanuni za wabunge wa kamati wa CCM na kuwa na wajumbe kumi ambao wataongoza timu hiyo.


Aliwataja wajumbe wa kamati ya marekebisho ya kanuni za CCM kuwa ni Jenista Mhagama, Dk. Maua Daftari, Pindi Chana, Bernadeta Mushashu, Christopher Ole Sendeka na Andrew Chenge.


Wengine ni Dk. Harison Mwakyembe, Gosbert Blandes, Mshadhi Maalim na George Simbachawene.


Kuhusu migomo ya vyuo vikuu

Pinda alisema serikali imepitia kwa makini na kuunda kamati na kugundua matatizo ya mawasiliano baina ya utawala, wafanyakazi na wanafunzi waliopo masomoni hali inayopelekea kutokea migomo ya mara kwa mara.

Alisema njia ambazo serikali imeshauri ni kuhakikisha kunakuwa na ujenzi wa miundombinu ya uhakika katika vyuo vyote vya umma pamoja na kuwa na utaratibu wa kufanya ukaguzi wa mahesabu kupitia ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali.


Mgao wa Umeme

Alisema kwa mujibu wa Waziri wa Nishati na Madini imebainika hivi sasa Tanzania inakabiliwa na uchavu na uduni wa miuondombinu katika vyanzo vya umeme nchini.

Alisema kukosekana kwa maji ya uhakika kumepelekea kutokea mgao wa mara kwa mara nchini hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya taifa na watu wake.


"Utafiti unaonyesha kuwa matumizi ya umeme nchini yameongezeka kuliko uwezo wetu lakini serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na tatizo hili ili limalizike kabisa," alisema Pinda.


Source: Tanzania Daima
 
Mtoto wa mkulima keshaingia rasmi katika kundi naye amehakikishiwa mgao wa nguvu.If you cant fight them join them, there you are Mr. BEND
 
msimamo huo mpya unafuta misimamo ya Mh. Ngeleja na Mh. Werema au? Timu ya wanasheria wa CCM na wanasheria wa serikali inalipwa na nani?

Wanasheria hao wa CCM wamejitolea au inakuwaje? Mbona serikali inajikanganya kwa makusudi katika hili?

Kamati Kuu ya CCM ilisema uungwana ni kulipa. Ikasema kwamba kwa sababu wananchi wameenda mahakamani ni vyema serikali ikasubiri kidogo. Sasa Pinda ametoa tamko as if its a new thing anaongea!
 
...kwani ni nani mwenye mamlaka na swala lolote kwenda bungeni au kutokwenda? tunao wabunge mahiri wa upinzani tuliowapigia kura watalirudisha swala hili bungeni maana lilianzia huko, limalizikie huko huko huku wananchi tukifuatilia kwa karibu kwa shauku kubwa ya kujua nani ni nani,yupi ni nani na nani ni yupi.
 
hakuna jipya....wazo ni yale yale kutetea chama ...ndio dili kwa wanachama wa ccm!!!! sitakuwa tayari kudanganyika
 
Haya jamani..kumekucha. Aliyekuwa anajisingizia kuwa 'mtoto wa mkulima' ameamua kuonyesha 'true colours'.
Dowans itaumbua wengi..na wote watakwenda na maji!!
 
Pinda pinda pinda ulikuwa unalilia uwaziri mkuu ulidhani huko wanagawiwa pesa ukasema ngoja nijiite mtoto wa mkulima ili nipate mgao mkubwa
 
Is it just me or i happen to read that Chenge is among wateule wa kushughulikia hilo suala..? Kichefuchefu.
 
Ni Pinda huyu huyu aliyepigia debe kampuni ya kisheria kwamba isaidiane na serikali kuangalia upya mkataba wa Dowans. Hiyo kampuni ya Rex ikaishauri serikali kuvunja mkataba. Hiyo hiyo kampuni ikashiriki kwenye suala la usuluhishi na ikashindwa na ikaishauri serikali iilipe Dowans, ispinge. Pinda aliyeipigia debe bungeni kama kampuni yenye uzoefu kwenye mikataba ya kimataifa, ndiye anaekazania malipo haya.

Kuna nini hapo?
 
Kwa mara nyingine tena, Pinda amelikashifu Bunge letu..

Kama mtakumbuka kuna kipindi alienda kuzindua bwawa kwa Rostam na kumteteaya kwamba wanamsingizia mambo mengi na kwamba bungeni ni wazushi tuu.

Again, this time anasema suala la dowans halitarudi bungeni simply huko bungeni wanaongea siasa tuu, wakati issue hii ni ya kisheria!

Lissu et al., take a note..kwa uchache hii mitizamo miwili ya Pinda ni mahsusi kulidhalilisha Bunge letu..kwamba ni chombo cha hovyo hovyo tuu.

Anahitaji punishment huyu, nadhani this time hatalia hadharani kwa unafiki wake; Kwani tuliyemdhania kuwa ndiye, kumbe siye!!
 
Code:
Aliwataja wajumbe wa kamati ya marekebisho ya kanuni za CCM kuwa ni Jenista Mhagama, Dk. Maua Daftari, Pindi Chana, Bernadeta Mushashu, Christopher Ole Sendeka na Andrew Chenge.

Unatazamia nini kitafanyika ndani ya wajumbe wa kamati ya marekebishi ya kanuni za ccm wakati Chenge ni mmojawapo wa wajumbe?
 
UV CCM wanasema hakuna kulipa, baadhi ya mawaziri wanasema hakuna kulipa, CC ya ccm wasema kulipa ni lazima, wasubiri tu kesi iliyofunguliwa mahakamani.

Mimi nina swali: Hizi hela Chiligati anazosema uungwana ni kulipa zitatoka wapi? Au wanazo mifukoni mwao watachangishana, maana sisi ndo wenye hela, tunasema hatutaki kulipa, tunaona tunaibiwa au tuna tapeliwa wazi wazi. Hawa wanaolazimisha tulipe tu, labda wanazo mifukoni mwao. Nadhani tuwaulize kwanza.

Lakini kama ni kwenye fuko letu la jumla- HAZINA hakuna pesa ya mchezo hata Mkullo kesha sema
 
"Hatutalipeleka suala hili bungeni….kulipeleka huko itakuwa ni kwenda kujadili siasa na si sheria. Na kwa hili tayari kuna timu ya wabunge wa CCM ambao ni watalaamu wa sheria pamoja na timu itakayoundwa na serikali, timu hizo zitakaa na kupitia kwa makini suala hili ili twende tukatafute ufafanuzi huo wa kisheria," alisema Pinda.


Kama namwona Mzee wa Vijisent kwa mbali
 
Back
Top Bottom