Pinda awasimamisha katibu mkuu wa wizara ya afya na mganga mkuu

..hao wametolewa kafara tu.

..Pinda mwenyewe ndiyo alijitia ubabe wa kuwatisha na kuwafukuza kazi madaktari.
 
hv si alishasema kuwa hana uwezo wa kumfukuza katibu mkuu kazi kama wakati wa jairo alisema ingekuwa uwezo wake angemsimamisha kazi jairo
 
This country is funny....

Pinda kabwabwaja weee kuhusu ulimboka, mpnda kabwabwaja wee kuhusu ulimbika, sasa kiko wapi? hahahaaaaaaa.jpg
 
Habari toka mkutanoni kati ya waziri mkuu na madaktari zinasema waziri mkuu kawasimamisha kazi katibu mkuu wa wazara ya afya na mganga mkuu huku akimuachia rais kuwatimua waziri na naibu wake.
Chanzo: madaktari walio katika kikao na waziri mkuu.
mi naoana kama danganya toto 2. ngoja tususubiri huo mwezi 1 waliopewa na ma dr. nahisi kama mchezo waliocheza pinda na na hao katibu mkuu na mganga mkuu. nahisi ilikuwa kama hivi" (waziri mkuu)- ndugu zangu wananchi wanaumia , hawa jamaa nishawapiga mkwara lkn bado wanagoma na wanataka ninyi muondoke. sasa mi naenda kuzuga kama nawafukuza kazi lkn msijali tupo pamoja , wakisharudi kazini tutajua huko baadae jinsi ya kuwashughulikia"
 
Fukuzaaaaaaa.....hadi waziri....then PM ajifukuzeee mwenyewe, why? 7bu alitaka kuwafukuza madaktari
na kuwaacha Katibu mkuu, mganga mkuu & waziris, sasa kaenda opposite meaning
hana msimamo, ajifukuzishe mwenyewe...
 
Tofauti ya Jairo na Nyoni ni nini? Au ndiyo matabaka yenyewe kwenye uongozi!! Nashindwa kuelewa kwa nini Pinda alishindwa kumshushia nyundo Jairo kama alivyofanya kwa Nyoni?

Ili swali inabidi tumuulize Pinda mwenyewe na atupe jibu kwa mahandishi.
 
Tofauti ya Jairo na Nyoni ni nini? Au ndiyo matabaka yenyewe kwenye uongozi!! Nashindwa kuelewa kwa nini Pinda alishindwa kumshushia nyundo Jairo kama alivyofanya kwa Nyoni?

Ili swali inabidi tumuulize Pinda mwenyewe na atupe jibu kwa mahandishi.
 
Hii nji imezidi bureacracy, Waziri Mkuu, Waziri, Naibu waziri, Katibu Mkuu, Mganga Mkuu, Directors kibao hapo wizarani na vitengo lukuki, wote maboss. Gharama za huduma na mahitaji ya mashangingi yao kwa mwaka yangetosha kulipa posho za madaktari wangapi.

Hebu tuwe cost conscious tunapotengeneza hizi institutional frameworks hasa katika karne hii ya ICT ambapo kazi ya watu 3 inaweza fanywa na mtu mmoja.
 
Madaktari wa jeshi. Wanaishi palm beach hotel full board, na posho ya 50,000/- tambarare.....
 
Sina hakika na hatua hizo zilizochukuliwa na PM kwani hata yeye alifanya makosa kwa kutoa maamuzi yasiyo ya busara mwanzoni bila kufikiria matokeo yatakuwaje. Pengine watu wengi wasingekufa kama ilivyotokea. Taarifa ya habari ya saa mbili usiku imesema wahusika wapewe likizo na serikali lakini je hiyo adhabu wanastahili, walikuwa wanatekeleza maagizo kutoka kwa nani? na kama wanastahili inalingana na thamani ya uhai wa waliopoteza maisha kwa uzembe huu wa watu wachache katika utumishi wa umma.
 
Haiwezekani kuwasimamisha tu
ni kuwafukuza kazi na kushitakiwa kwa kosa la mauaji na kutowajibika
pia rais, w/mkuu na bi kiroboto wote wajiuzuru
Heko madaktari mnaweza
 
huu ni upumbavu tu kama alikuwa an maamuzi hayo tangu mwanzo mbona alishindwa kuyafanya tangu cku ya kwanza? watu wamefariki ndo anakuja tena kujishaua kwa kuwasimamisha kazi hao itasaidia nini? huo nao ni unafiki tu kama ungemsikia wakati anaongea ndo ungejua kuwa aina ya viongozi tulionao ni mboga tu hamna busara wala hekima kila mtu anaamka na lake hata wenyewe hawajui wanafanya nin bora JK ALIYEAMUA KUJIENDELEZEA NA ZIARA ZAKE ZA UTALII NCHI ZA WATU.
 
KATIBU MKUU, MGANGA MKUU WANG’OLEWA, VYOMBO VYA DOLA VYAWACHUNGUZA KWA UFISADI, MADAKTARI WAREJEA KAZINI
Waandishi Wetu
WAKATI madaktari nchini wakiafiki kusitisha mgomo wao na kukubali kurejea kazini leo, sakata hilo limeacha jeraha kubwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa, kwa kusimamishwa kazi.

Hatua hiyo ilitangazwa jana na Waziri Mkuu , Mizengo Pinda alipokutana na madaktari hao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), huku akiweka bayana kuwa hatima ya Waziri wa Wizara hiyo, Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya, inabaki mikono mwa Rais Jakaya Kikwete.
Pinda, alisema watendaji hao wa ngazi ya juu ya Wizara ya Afya, wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa vyombo vya dola, dhidi ya tuhuma mbalimbali zinazohusishwa na utendaji wao.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu aliweka wazi sababu kuu tatu za Serikali kuwasimamisha kazi vigogo hao wa wizara.

Pinda aliyelazimika kuacha kikao cha Bunge mjini Dodoma na kurejea Dar es Salaam juzi kushughulikia mgomo huo, alisema sababu ya kwanza ya kuwasimamisha watendaji hao, ni tuhuma za kuingiza nchini robo tatu ya vifaa bandia vya vipimo vya Ukimwi kutoka Korea Kusini.


Alitaja sababu zingine kuwa ni tuhuma za kuanzisha kampuni ya kusambaza nguo kwa madaktari na kuiingiza kinyemela kampuni ya kufanya usafi ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbil.Pinda alisema tuhuma hizo ni nzito zinazoidhalilisha Serikali na kamwe haitakuwa busara kuzifumbia macho huku Serikali ikiendelea kudhalilika.


“Nimeamua kuwasimamisha kazi Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wa Serikali, ili kuweza kupisha uchunguzi maana hizi tuhuma zinafedhehesha taifa."
Aliongeza; “Kwa upande wa Waziri na Naibu Waziri wa Afya, nimeshapeleka ushauri kwa Rais kutokana na yeye kuwa mwenye dhamana, siwezi kuliongelea hili hapa ila yule aliyewateua, atafanya maamuzi, najua kitakachofuata mnakijua,” alisema Pinda huku madaktari wakilipuka kwa shangwe na kuimba nyimbo ya mshikamano.

Alisema malalamiko ya madaktari ni makubwa na kwamba, yana msingi wa kusikilizwa na kusihi kamati iliyoundwa kuorodhesha kila kitu ili Serikali iweze kuyafanyia kazi.
Alisema baada ya madaktari mabingwa kumweleza hali ilivyo katika hospitali hiyo ya Muhimbili, ndipo aliweza kujua kwa undani matatizo yao makubwa.
source: Madaktari waangusha mbuyu
 
PM naye ajisimamishe kwa kufanya maamuzi bila uchunguzi......imagine kwa uamuzi ule wa awali watu wangapi wameathirika wakati majibu alikuwa nayo..............
 
Back
Top Bottom