Pinda ana uwezo wa kumsimamisha kazi Blandina Nyoni lakini Jairo hapana kweli?

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Nakumbuka rais akiwa safarini Pinda alishindwa kumuwajibisha Jairo, Leo hii Rais yupo nje ya nchi nasikia Pinda kamuwajibisha Blandina Nyoni. Hivi Jairo na Nyoni wanatofautiana nini? kama wapo sawa Pinda katoa wapi mamlaka ya kumuwajibisha Nyoni? Najaribu kutafakari kabla sijamdharau kabisa Pinda.
 
Waulize sisiemu. Wenye akili zao wanasubiri ishirini kumi na tano.usipate shida maumivu yataisha hiyo siku.pinda na j.k wake.
 
Waulize sisiemu. Wenye akili zao wanasubiri ishirini kumi na tano.usipate shida maumivu yataisha hiyo siku.pinda na j.k wake.

Wengi walioteuliwa na fulani wanafanya kazi kama maroboti; hawatumii taaluma zao kazini - bali wanamtumikia alowapenda na kuwachagua kuwa wasaidizi wao. Hata mwanamke ulomua mara nyingi hujitahidi kutokuwa against na wewe! Mume wao ni CCm na sasa kazeeka - wanapuyanga tu! 2015 watatwambia ni kwa nini walishiriki katika kuondoa roho za ndugu zetu wanaopoteza maisha kipindi hiki cha mgomo; na ... duH .... nina machungu!
 
Waulize sisiemu. Wenye akili zao wanasubiri ishirini kumi na tano.usipate shida maumivu yataisha hiyo siku.pinda na j.k wake.

Seriously imenichanganya kama kuna mtu ameelewa vema swali langu anisaidie
 
kwa kawaida Pinda hufanya mambo kama mpagazi, JK humtanguliza mbele kwakua anamjua hawezi kukataa, hahaaah , JK kwa remote control kamwambia Pinda nenda , yaani JK NI KAMA HUYU ALIEBEBWA, na huyo chini kibaunsa ndio PINDA
404306_365619276798937_100000526027202_1448331_1109016896_n.jpg

Kuna point hapa jamani....ila kwa hii tz kila kitu kinawezekana
 
Are we discussing issues or powers!!?. Ndugu zetu wanakosa huduma za matibabu na wanakufa tumeomba serikali ichukue hatua, angalau imechukua ni moja ya malalamiko ya ndugu zetu madaktari. Tufike mahali tutambue kuwa not everybody is a politician. There are people who discusses issues not powers!
 
Tumechagua viongozi walio 'street smart' na sio walio 'competent' na wao wameteua watu wanaofanana nao.
Waziri Mkuu alichofanya ni kukwepa jukumu katika incidence ya Jairo ili kukwepa kumfunga paka kengele.
Kwenye hii case ya Nyoni amebeba jukumu kwa sababu moto umekuwa mkali sana kwa hiyo hata 'buying-time technique' imeshindikana.
 
wangemwachia mzee wa kukata utepe angalau na yeye a-exercise powers kidogo kwenye hii mambo...
 
Kuna kitu kinanipa utata wandugu,ktk sakata la Jairo ambaye alikuwa katibu mkuu Nishati na Madini Waziri mkuu alisema kuwa hana mamlaka ya kumsaspend,hivyo asubiriwe rais aliyekuwa sauz,Mbona leo amefanikiwa KUMFURUSHA katibu mkuu Afya bi Blandina Nyoni,hebu nieleweshe bcose i see the contradiction in this actn.NAONA HAWA JAMAA 'WANAKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA'
 
Wengi walioteuliwa na fulani wanafanya kazi kama maroboti; hawatumii taaluma zao kazini - bali wanamtumikia alowapenda na kuwachagua kuwa wasaidizi wao. Hata mwanamke ulomua mara nyingi hujitahidi kutokuwa against na wewe! Mume wao ni CCm na sasa kazeeka - wanapuyanga tu! 2015 watatwambia ni kwa nini walishiriki katika kuondoa roho za ndugu zetu wanaopoteza maisha kipindi hiki cha mgomo; na ... duH .... nina machungu!

Tuanze na Uzini na Arumelu kwanza huko 2015 bado ni mbali.
 
nilivyomsikia mimi amemtumia katibu mkuu wake ambae ndio anamsaidia katibu mkuu kiongozi! but bado nna shaka na ilo kwani bado angeweza kufanya the same kwa jairo!!
 
Mi naona asamehewe bure handsome pinda, hajui alitendalo. Bahati mbaya zaidi kwa handsome huyu ni msahaulifu kupita kiasi, sijui ni wingi wa majukumu au ni mtindio wa ubongo!? Nadhani someone is right 'wamekubaliana kutokukubaliana'
 
Tatizo sio individual pipo,bali siasa.ukiitumia siasa na saikolojia ya siasa inakuwaga hivo,unazani personally makinda yuko harsh kama alivo bungeni?Siasa utasifu baazi ya watu ama kuwabania kwa sababu fulani fulani tu.
 
Taarifa ya vyombo vya habari inamnukuu Pinda akisema kuwa amewasimamisha kazi katibu mkuu wa wizara ya Afya na Mganga mkuu wa seikali, na kwamba waziri na naibu waziri wa wizara hiyo amemuachia rais awachukulie hatua.Hapa tunaona waziri mkuu akitumia madaraka yake (ambayo sidhani yapo kikatiba) akimtimua katibu mkuu ili kunusuru hali.Kinachonisumbua ni kuwa kama ameweza kwa Nyoni alishindwa nini kwa Jairo?? Maana kwenye sakata la Jairo(ambalo mpaka leo halina jibu kamili) alishindwa kuchukua hatua akisema Jairo angekuwa kwenye mamlaka yake angeshamtimua ikabidi ampigie rais simu.Je ni kwamba makatibu wakuu wa wizara wapo kwa madaraja kiasi kwamba kuna walio kwenye mamlaka ya waziri mkuu kama Nyoni na wengine wanategemea maamuzi ya rais kama Jairo?? karibu tujadili
 
Baada ya kuondoka Luhanjo ndio haya mazingaombe ya Pinda kumsimamisha kazi Permanent Secretary yanaonekana. Tafakari......
 
pINDA INAONESHA HAWEZI KABISAA KUFANYA KANZI NZURI KATIKA JAMII YA KIDEMOKRASIA. iLA YEYEY NI KAKULIA KUFANYA KAZI KATIKA JAMII YA KIKOMUNISTI TUU. oNA HATA MAVAZI YEKE NI YA KIKOMUNISTI TUU!
 
Back
Top Bottom