Pinda akubali kujiuzulu jioni hii

Status
Not open for further replies.
Kwa mara nyingine CCM inaendelea kupungua umaarufu na kuporomoka imani kwa wananchi na wanachama wake kwa kile kinachoitwa kudandia hoja za wapinzani sambamba na kuungana nao ili kuiangusha serikali yao. Hii imekuwa ikitokea hata katika nchi mbalimbali duniani hasa za kiafrika kwa vyama tawala kuingia mtegoni na kuja kutambua makosa hayo muda ukiwa umepita.

Kosa kubwa hapa ni kudandia hoja na misimamo ya vyama vya wapinzani hivyo kuwapunguzia kazi ya kufanya. Kwa uchambuzi wangu wa kina nimeona hili likitokea Kenya, Zambia, Malawi nk.

Pengine ni kasi ya Vijana wa vyama tawala barani Afrika kwa mfano Chama cha CCM nchini kwa Kutokuwa na umakini, tahadhari, na upeo wa kisiasa ambao wapinzani huupata toka nchi zilizobobea katika masuala ya kisiasa kama wadau wao wakuu wa mpango wa kuvivuruga na kuviangusha vyama vyote vilivyopigania uhuru barani Afrika ambapo vyama vingi vya upinzani hutumiwa kama vibaraka (puppets) kwa maslahi ya nchi za magharibi.

Mawazo na mikakati binafsi kwa wanasiasa wakongwe ndani ya chama pia hupelekea kuwavuta vijana na kujikuta wanakuwa na mawazo ya Chama lakini baadae maslahi kwanza, hili limejionesha na kujidhihirisha Dodoma hasa kwenye sakata la ESCROW kwani majina kadhaa ya viongozi waandamizi wa Serikali pamoja na wastaafu au kwa maana ile niliyoeleza awali (wakongwe) wamesemwa kuendesha kampeni na mikakati mingi ya kuwatumia wabuge vijana wa CCM na kuunganisha nguvu zao ili kuiangusha Serikali ya CCM. Orodha ya majina ya viongozi wa serikali wanaotajwa kuhusika na mikakati hiyo michafu ni ndefu lakini wamo Wiliam Lukuvi, Edward Lowassa (Waziri Mkuu aliyejiuzuru) Apson Mwang’onda (Mkurugenzi Mstaafu wa TISS), Andrew Chenge (AG Mstaafu), Job Ndugai (Naibu Spika), Godfrey Zambi, Kagasheki, Ngeleja na Sophia Simba. Kundi la wabunge linaongozwa na Ole Sendeka, Kange Lugola, Esther Bulaya, Filikunjombe, Peter Serukamba kwa kushirikiana na wabunge wa vyama vya Upinzani wakiongozwa na Zitto Kabwe na David Kafulila.

Aidha taarifa za ndani kutoka bungeni Dodoma zinasema kuwa tayari wabunge wa CCM wamegundua njama za Lukuvi na wenzake kuiangusha serikali. Taarifa zinaonyesha kuwa William Lukuvi na Job Ndugai wamelipwa na kina Nimrodi Mkono, Mengi na Rostam Milioni 500 kila mmoja. Juzi jioni Mhe Lukuvi alitoroka bungeni na kurudi Dar es Salaam kwa ajili ya kuchukua mgao wake wa mwisho milioni 200 kwa lengo la kuiangusha serikali ya Kikwete hasa kwa kutumia sakata la IPTL.

Lukuvi apewa hadidu za rejea.
Katika kuhakikisha mpango huu unatimia Lukuvi amepewa Maagizo ya nini anachotakiwa kufanya.
1. Kuhakikisha kwamba anampotosha Waziri Mkuu na hasa kwa kumuonyesha kuwa ishu ya IPTL ni ndogo na hivyo hakuna haja ya kufanya vikao na wabunge pamoja na Mawaziri ili kutafuta Suluhisho la Sakata la IPTL.
2. Kumchonganisha Waziri Mkuu na viongozi wengine wa Serikali ili aonekane hafai na hawezi kuisimamia Serikali Bungeni
3. Kuhakikisha vyombo vya habari vya Mengi na Rostam (ITV, Radio one, gazeti la Mtanzania, Rai, Nipashe ) vinaichafua na kuibomoa Serikali kwa namna zote. Mkatkati huu pia umeshirikisha vyombo vya hanbari kama Mwananchi na The Citizen, Mawio, Fahamu na Raia Mwema.

Lukuvi ndumi la kuwili

Ikumbukwe kuwa Wiliam Lukuvi sio mara yake ya kwanza kuhujumu Wagombea viongozi wenye nia ya kutaka kugombea Urais. Mwaka 1995, inasemekana kuwa Lukuvi alikuwa timu moja na Kikwete, lakini baadaye akamgeuka na kumuunga mkono Mkapa. Mwaka 2005 pia Lukuvi alikuwa anamuunga mkono Fredrick Sumaye, lakini ghafla dakika za mwisho akahamia kambi ya Kikwete na kumhujumu Sumaye. Mwaka huu pia inasemekana Lukuvi alikuwa bega kwa bega na Waziri Mkuu Pinda lakini leo hii ghafla anaonekana kushirikiana kwa karibu na Lowassa katika vikao vyao vya ndani na kuweka mikakati ya kumuangusha Pinda na kumtoa kwenye kinyang'anyiro cha Urais.

My take
Hii inaashiria nyakati mbaya kwa CCM kama Chama Tawala kwani tayari Wapinzani wamefanikiwa katika mtego huu na sasa mashambulizi makubwa ni kati ya baadhi ya wabunge wa CCM dhidi ya Serikali na sio wapinzani dhidi ya Chama Tawala. Ili kufanikisha mkakati huu Ahadi kadhaa zimekuwa zikitolewa kwa makundi mbalimbali ya wabunge Vijana wa CCM, hasa ahadi za vyeo, ahadi za kutoingiliwa na wapinzani katika majimbo ya wabunge wa chama tawala ambao wanaonesha msimamo mkali dhidi ya Chama chao. Aidha mkakati huu unaonekana kuwapa nguvu wapinzani na hata Oparesheni mbalimbali zinazofanywa na wapinzani wamekuwa wakiruka kwa makusudi majimbo ya wabunge wa CCM ambao wana msimamo nao wa pamoja.
 
Taarifa zilizonifikia japo sijazibitisha ni kwamba waziri mkuu pinda amekubali yaishe kwenye kikao cha uongozi bungeni kilichodumu kwa zaidi ya masaa matatu. Stay tune

Mara hujazibitisha, mara kakubali,mara umepata taarifa. Kama hujui kaa kimya. Unapandisha watu midadi bila sababu za msingi.
 
kujihudhuru sio mpaka atake hata asipotaka tutamhudhurisha mshenzi huyu! Hatuwezi kumpa mwizi ajichagulie adhabu huu utakuwa wendawazimu! Kwanza hapaswi kufunua domo lake kuongea, yeye fact ziongee!!

NA AKIKATAA KUJIHUDHURU ATAPIGWA TU, NA MIMI NASEMA APIGWE TU.


Ndugu acha kuharibu lugha yetu adhim ya Kiswahili!!!!:teeth:
 
Pinda ajiuzulu kwa kosa lipi kwenye hii suala la Escrow?manake kipindi kile tuliona Lowasa alivyojiuzulu kutokana namna alivyoshiriki kuiba pesa za umma kupitia kwa kampuni feki ya Richmond ripoti ya Mwakyembe ilidadavua namna zote ambavyo Lowasa alishiriki kukwapua pesa za umma,sasa je katika sakata hili la ESCROW waziri mkuu Mizengo Pinda amehusikaje,ebu fafanua hapo?
 
Taarifa zilizonifikia japo sijazibitisha ni kwamba waziri mkuu pinda amekubali yaishe kwenye kikao cha uongozi bungeni kilichodumu kwa zaidi ya masaa matatu. Stay tune

mimi waziri Mkuu Mizengo Pinda nijiuzulu kwa msala upi?
Hakatwi mtu hapa, mpaka ripoti ya CAG iletwe na kusomwa mjengoni.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimesikia pia Tibaijuka, Muhongo na Beno Nduru wataachia ngazi hivi punde sasa najiuliza CCM ndo munataka kucheza kalata ipi kwa kuwatoa kafara hao? sisi tunataka waende Mahakamani wafilisiwe hapo ndipo tutaona aki imetendeka, lasivyo hata hao watateuliwa na Mkulungwa wataiba tu.

Achana na mambo ya kusikia,tunataka useme umeona wakiwa wanakabidhi makabulasha ya ofisi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom