Wadau hapa, kwenye face book yako, unaweza kuandika ujumbe, kuhusu dr slaa, na marafiki zako wanapoingia kwenye profile yako wana kutana na ujumbe wa mabadiliko, kuhusu slaa
Kuna anko wangu mbishi huyo yupo kijijini alipewa kofia ya ccm na buku nimempa darasa sasa kaelewa anaelimisha wenzie nategemea kura nyingi sana bush maana hata akina bibi nao wameelewa.
Hakika Kiongozi Utahesabiwa Haki Mbele za Mungu, Maana umefanikiwa kumrudisha Kundini Kondoo aliyepotea, hata Mch Masa analitambua hilo
Kuna Watu wamekuwa wanajaribu kuufananisha Uchaguzi wa 2010 na ule wa mwaka 1995, wamekuwa wakijaribu kulinganisha Umaarufu alionao nao Dr. Slaa na Umaarufu aliokuwa nao Augustino Lyatonga Mrema alipokuwa anagombea Urais Kupitia NCCR-Mageuzi. Watu hao wanadiriki kutumia ufanano wa Umaarufu huo hata kujaribu kutabiri eti Dr. Slaa ataanguka kama alivyoanguka Mrema 1995.
Watu hao wamejivika upofu wa Kufananisha watu hao wawili huku wakikwepa ama kwa makusudi ama kwa kutojua Tofauti ya Kimazingira kati ya Mwaka 1995 na mwaka 2010
Kuna mambo ambayo inabidi yaangaliwe kabla ya kufananisha hali ilivyokuwa 1995 na 2010
Mwaka 1995 technolojia ya habari haikuwa imeenea sana kama 2010, Sasa hivi karibu kila Mzazi kijijini mwenye mtoto Mjini anatumia simu ya Mkononi. Nimekuwa nikifuatailia kura za mtandaoni ambazo zimekuwa zikimpa Ushindi mkubwa Dr. Slaa dhidi ya Wapinzani wake.
Japokuwa Baadhi ya Watu wamekuwa wakiziponda polls hizi ila kwa mtu makini hawezi kuzipuuzia hata kidogo na hata Wapinzani wa Dr. Slaa hawawezi kuzipuuzia hata kidogo kwa sababu wanatambua ni Ujumbe gani unaotolewa
Baadhi ya Watu wanaweza kuja hapa na kutoa Hoja kwamba ni Watanzania wangapi wana access na internet? Watanzania Wangapi wanajua JF? Hizi ni Hoja Mfu zinazofanana na Mgombea mmoja wa Urais aliyena kwamba kura 350000 ni ndogo sana kwake bila kuangalia ni watu wangapi wako nyuma ya hao watu 350,000
Ndugu wana JF wapenda Mabadiliko leo nina Ujumbe Muhimu sana kwenu
Wanaweza kutubeza kwa Uchache wetu, wanaweza kutubeza eti hatupigi kura, Wanaweza kutubeza eti kwamba sisi ni watu wa kulalamika kwenye Mitandao, wanaweza kutubeza kwamba tunaota ndoto za mchana
Lakini Ukweli ni Kwamba
Sisi wana JF tuna Wazazi, tuna Wadogo zetu na kaka Zetu na hata Ndugu zetu wale wanaobezwa kwa kukosa huduma hii ya Mtandao, Lakini ndugu zetu hawa asilimia kubwa wana Simu za Mikononi
Sasa Wana JF wote wapenda mabadiliko, wataopiga kura na ambao hawatapiga kura kwa sababu yeyote Nyanyua Simu yako Mpigie Shangazi yako, mama yako, bibi yako, babu yako, kaka yako dada yako, mjomba wako Mwambie tunahitaji mabadiliko.
PAMOJA NA UCHACHE WETU TWAWEZA KULETA MABADILIKO, PLAY YOUR PART
NyU
Leo nietoka kuongea na mama mdogo hakuwa na mpango wa kupiga kura eti kisa kachoshwa na CCM, nikamwambia kama amechoshwa na CCM dawa si kuzira kupiga kura bali ni kupigia chama kingine kura, kwa kweli amenielewa akatoa kauli hii " Kama wewe mwanangu msomi unaniambia Nimpigie kura Slaa nitafanya hivyo"
mimi nina kaka wa 2= watampigia slaa
baba na mama= watampigia slaa
wadogo zangu 2= watampigia slaa
Mimi mwenyewe slaa
ofisini kwangu kuna watu saba, wote wanataka mabadiliko, wamechoka maisha ni magumu, na watampigia slaa
kwahiyo nauakika kura hizi zote = 2+2+2+1+7=14, ni ZA SLAA
Hao , wanaodharau kura za maoni za JF, waendelee, october 31, usiku baada matokeo kuanza kutangazwa, watapigwa na bumbuwazi.
Kura ni siri ya mtu utajuaje kama kakubari ili kukuridhisha tu ili asije akakosa vile vijisenti unavyomtumia. Mtumikie kafiri upate mkate wako. sina chama nataka kujua tu na kujiridhisha.
sisi extended familia yetu ina watu kama 12 ukianza kushuka kwa watoto jumla twafika 35 zote dr slaa.
Bado ofisi kuna watu kama 12.
Ila kuna mccm mmoja alikuja rubuni vijana wangu kuwa akija akiona bendera ya ccm inaninginia atawapa mkwanja vijana si wakaninginiza bendera wakati niliposafiri nilyorudi ndo wakanipa huo mkasa tukaingoa.