Elections 2010 Piga kampeni kwa simu

Kuna anko wangu mbishi huyo yupo kijijini alipewa kofia ya ccm na buku nimempa darasa sasa kaelewa anaelimisha wenzie nategemea kura nyingi sana bush maana hata akina bibi nao wameelewa.
 
Kiukweli tuna machungu sana na awamu ya nne hasa sie vijana. Mhe. wetu wa awamu ya nne alituharibia sana watu wangu. Aliingia kwa mikwara ya kutudanganya atazalisha ajira kibao hususani kwetu sisi vijana matokeo yake si ndo tunayaona leo twamaliza vyuo twaranda randa mitaani kutafuta kazi! Tujiulize zile ajira aliwapa watu wa pwani? Mazidisha mkwazo wa upatikanaji wa mikopo elimu ya juu! Wao wamesoma kirahisi enzi zao sie twapata shida wakati watoto wao wanatumia mikopo ya watoto wa watanzania duni. Yale mahela ya UFISADI waliyokula kwanini wasingetunisha mikopo ya kusoma watanzania wasome jamani?
Guys we need changes! Tumpatie DR. SLAA atujali jamani!
 
Wadau hapa, kwenye face book yako, unaweza kuandika ujumbe, kuhusu dr slaa, na marafiki zako wanapoingia kwenye profile yako wana kutana na ujumbe wa mabadiliko, kuhusu slaa
 
Wadau hapa, kwenye face book yako, unaweza kuandika ujumbe, kuhusu dr slaa, na marafiki zako wanapoingia kwenye profile yako wana kutana na ujumbe wa mabadiliko, kuhusu slaa

Asante PayGod, Kimsingi Bado kuna Kazi kidogo inatakiwa kufanyika na wanaaotakiwa kuifanya ni sisi, Ndugu zetu wa vijijini wako Vulnerable sana, tusiache kuwaimbia huu Wimbo wa mabadiliko, Tukiumba sana hakika utakaa kichwani nao wataapa kuzilinda shahada zao mpaka siku ya kupiga kura

Asante sana
 
Kuna anko wangu mbishi huyo yupo kijijini alipewa kofia ya ccm na buku nimempa darasa sasa kaelewa anaelimisha wenzie nategemea kura nyingi sana bush maana hata akina bibi nao wameelewa.

Hakika Kiongozi Utahesabiwa Haki Mbele za Mungu, Maana umefanikiwa kumrudisha Kundini Kondoo aliyepotea, hata Mch Masa analitambua hilo
 
Hakika Kiongozi Utahesabiwa Haki Mbele za Mungu, Maana umefanikiwa kumrudisha Kundini Kondoo aliyepotea, hata Mch Masa analitambua hilo

Tayari nimefanya kampeni sana kwa cmu kuhamasisha mabadiliko katika nchi yetu.

Mch Masa nae yupo busy kweli huko kijijini kuhamasisha waumini wake
 
Kuna Watu wamekuwa wanajaribu kuufananisha Uchaguzi wa 2010 na ule wa mwaka 1995, wamekuwa wakijaribu kulinganisha Umaarufu alionao nao Dr. Slaa na Umaarufu aliokuwa nao Augustino Lyatonga Mrema alipokuwa anagombea Urais Kupitia NCCR-Mageuzi. Watu hao wanadiriki kutumia ufanano wa Umaarufu huo hata kujaribu kutabiri eti Dr. Slaa ataanguka kama alivyoanguka Mrema 1995.

Watu hao wamejivika upofu wa Kufananisha watu hao wawili huku wakikwepa ama kwa makusudi ama kwa kutojua Tofauti ya Kimazingira kati ya Mwaka 1995 na mwaka 2010

Kuna mambo ambayo inabidi yaangaliwe kabla ya kufananisha hali ilivyokuwa 1995 na 2010

Mwaka 1995 technolojia ya habari haikuwa imeenea sana kama 2010, Sasa hivi karibu kila Mzazi kijijini mwenye mtoto Mjini anatumia simu ya Mkononi. Nimekuwa nikifuatailia kura za mtandaoni ambazo zimekuwa zikimpa Ushindi mkubwa Dr. Slaa dhidi ya Wapinzani wake.

Japokuwa Baadhi ya Watu wamekuwa wakiziponda polls hizi ila kwa mtu makini hawezi kuzipuuzia hata kidogo na hata Wapinzani wa Dr. Slaa hawawezi kuzipuuzia hata kidogo kwa sababu wanatambua ni Ujumbe gani unaotolewa

Baadhi ya Watu wanaweza kuja hapa na kutoa Hoja kwamba ni Watanzania wangapi wana access na internet? Watanzania Wangapi wanajua JF? Hizi ni Hoja Mfu zinazofanana na Mgombea mmoja wa Urais aliyena kwamba kura 350000 ni ndogo sana kwake bila kuangalia ni watu wangapi wako nyuma ya hao watu 350,000

Ndugu wana JF wapenda Mabadiliko leo nina Ujumbe Muhimu sana kwenu

Wanaweza kutubeza kwa Uchache wetu, wanaweza kutubeza eti hatupigi kura, Wanaweza kutubeza eti kwamba sisi ni watu wa kulalamika kwenye Mitandao, wanaweza kutubeza kwamba tunaota ndoto za mchana

Lakini Ukweli ni Kwamba

Sisi wana JF tuna Wazazi, tuna Wadogo zetu na kaka Zetu na hata Ndugu zetu wale wanaobezwa kwa kukosa huduma hii ya Mtandao, Lakini ndugu zetu hawa asilimia kubwa wana Simu za Mikononi

Sasa Wana JF wote wapenda mabadiliko, wataopiga kura na ambao hawatapiga kura kwa sababu yeyote Nyanyua Simu yako Mpigie Shangazi yako, mama yako, bibi yako, babu yako, kaka yako dada yako, mjomba wako Mwambie tunahitaji mabadiliko.

PAMOJA NA UCHACHE WETU TWAWEZA KULETA MABADILIKO, PLAY YOUR PART

NyU

Fantastic analsis.Hoping you are a mathematician arn't you???
Fikiria JF ina wanachama kwa uchache 1500 hao ni wapiga kura.Kwa kuwa nao ni wanamaharakati wa mageuzi watatafuta wapiga kura 20 kila mmoja utapata wapiga kura 300,000+1500=301,500 multiplier effect ya wapiga kura 301500 kwa uchache iwe wapiga kura 10 utapata jumla ya wapiga kura 3,010,500.Kumbuka hawa watakuwa wamehamasishwa sana maana ni kampeni ya kichwa kwa kichwa, kitanda kwa kitanda na meza kwa meza.Taarifa za waliojiandikisha ni 17ml. Fraction ya 3/17 ni sawa na 17% Je hiyo ni kidogo????
Nawaomba wa JF KILA MMOJA WETU APATE WAPIGA KURA 30 NDUGU WA KARIBU NA SIKU YA KUPIGA KURA WAPIGIE SIMU WAAMBIE WAKAPIGE KURA UTAONA MADHARA YAKE.
 
Leo nietoka kuongea na mama mdogo hakuwa na mpango wa kupiga kura eti kisa kachoshwa na CCM, nikamwambia kama amechoshwa na CCM dawa si kuzira kupiga kura bali ni kupigia chama kingine kura, kwa kweli amenielewa akatoa kauli hii " Kama wewe mwanangu msomi unaniambia Nimpigie kura Slaa nitafanya hivyo"

Kura ni siri ya mtu utajuaje kama kakubari ili kukuridhisha tu ili asije akakosa vile vijisenti unavyomtumia. Mtumikie kafiri upate mkate wako. sina chama nataka kujua tu na kujiridhisha.
 
Fanya kuwa wanJF wako 1500 kwa uchache.
  • JF 1500 watawashawishi wapiga kura 20 kila mmoja utapata wapiga kura 300,000+1500=301,500
  • Wapiga 301,500 wakiwashawishi wapiga kura 10 utapata wapiga kura 3,015,000+301,500=3,316,500
  • Taarifa za waliojiandikisha ni zaidi ya 17million kwa hiy kwa asilimia utapa 3/17=17%
  • Wana-JF tunayo nafasi ya make the difference kwa ukubwa sana.
Tujitahidi kila mmoja wetu apate kwa uchache wapiga kura na ambao ni jamaa wa karibu 30 na uhakikishe siku ya kupiga kura wanapiga.Utafurahi na roho yako baada ya matokeo
 
mimi nina kaka wa 2= watampigia slaa
baba na mama= watampigia slaa
wadogo zangu 2= watampigia slaa
Mimi mwenyewe slaa

ofisini kwangu kuna watu saba, wote wanataka mabadiliko, wamechoka maisha ni magumu, na watampigia slaa

kwahiyo nauakika kura hizi zote = 2+2+2+1+7=14, ni ZA SLAA

Hao , wanaodharau kura za maoni za JF, waendelee, october 31, usiku baada matokeo kuanza kutangazwa, watapigwa na bumbuwazi.

ni vigumu kuamini kwamba ndugu zako wote 14 wamekuambia ukweli wakati kura ni kitendo cha siri. Mtu anaweza kufika pale na akampa kura yake Kikwete au mgombea mwingine yeyote. Ningekuwa mimi kwa kutumia hesabu za yamkini (probability) hapo ungesema una kura 8 na zingine sita huna uhakika nazo kwa sababu ya tabia ya binadamu usiri na kubadilikabalika( kigeugeu).
 
Sisi extended familia yetu ina watu kama 12 ukianza kushuka kwa watoto jumla twafika 35 zote Dr Slaa.
Bado ofisi kuna watu kama 12.
Ila kuna MCCM mmoja alikuja rubuni vijana wangu kuwa akija akiona bendera ya CCM inaninginia atawapa Mkwanja vijana si wakaninginiza bendera wakati niliposafiri nilyorudi ndo wakanipa huo mkasa tukaingoa.
 
Kura ni siri ya mtu utajuaje kama kakubari ili kukuridhisha tu ili asije akakosa vile vijisenti unavyomtumia. Mtumikie kafiri upate mkate wako. sina chama nataka kujua tu na kujiridhisha.

Ndiyo maana inaitwa Kampeni, hata Wagombea wanatambua kwamba si wote wanaokuja kwenye Mikutano watawapigia Kura, lakini hiyo si sababu ya kuwafanya waache kupiga Kampeni

Wana JF Wapenda Mabadiiko Maadui wanatambua Nguvu ya Kampeni kwa Njia ya Simu Watakuja hapa ku discourage watu, Waambieni hatudanganyiki



KAMPENI KWA NJIA YA SIMU NI KIBOKO, UNANGOJA NINI? FANYA ASUBUHI, FANYA MCHANA FANYA USIKU
 
Mke wangu ndiye alikuwa mbishi na ccm lakini nilipiga darasa la kufa m2 sasa hivi ni mgombea udiwani kwa tiketi ya chadema kata ya ipagala dodoma mjini.sasa nyumba yangu yote na kwa wakwe ni dr slaa.habari ndiyo hiyo
 
Tarehe 30 september katika mchango fulani niliandika hivi na hapa najinukuu:
"Jambo la msingi hapa ni kuwa hawa watanzania wamejitoa mhanga kuweka mbele maslahi ya Taifa kwanza.Na kila siku mamia kama si maelfu ya watanzania wanadefy the powers that be kwa kusimama katika principles.Hivi sisi wengine tunajitoa kwa vipi na kwa kiasi gani ili tuweze kupata hayo mabadiliko tunayoyalilia?
Ni wangapi kati yetu tumejitoa kuchangia harakati hizi za ukombozi wa nchi yetu?Kwa fedha,muda,mali,kushawishi ndugu na jamaa zetu wasioelewa?Ni kwa kiasi gani tumeshiriki katika kufichua mauozo katika serikali na chama twawala?
Kwa kifupi I challenge us to exarmine ushiriki wetu katika struggle.Hakuna serikali duniani inayopenda kuachia madaraka,hususan serikali corrupt kwa vile mabadiliko yanamaananisha kupoteza madaraka,ukwasi,opportunities na political clout!
CCM hawataachia ngazi hivi hivi ndugu zangu,Believe me,They will put up a fight to the end!
Struggles are not won by wishful thinking!They are won by sacrifice,by self denial,by persistence and by strategic planning and execution coupled by commitment to succeed!
Be part of the change!!!"


Huu ni mfano halisi wa jinsi tunavyoweza kushiriki kuleta mabadiliko.Thanks kwa posts karibu zote(Isipokuwa zile za kutukatisha tamaa!) zilizotolewa kwenye thread hii.


"True freedom must be expressed through the human ability to think critically, to analyze and to make informed decisions about oneself, his society and the world "- Sidanganyiki2010
 
Mpaka sasa SLAA ana kura zaidi 21 kutoka huku..
Naendelea kumtafutia..
 
Nimesoma hizi jumbe na mwisho kabisa nikataka kutokwa na machozi mimi ni student wa udsm, ila nitapiga kura kwani nimejiandikisha dar, na nitakuwepo wakati wa kupiga kura dar, mara baada ya kumpigia kura dr slaa nitaenda kijijini,
nimefurahishwa sana na message hizi, naenda kununua line ya zaini ili niwasambazie jumbe za kumpigia dr slaa watu wa kijijini kwetu am sure watakubaliana nami,
ebu tushirikiane kuleta mabadiliko katika nchi yetu.
Naona jua limewaka tanzania .
Thanks wana jf,
ukombozi ni lazima tushiriki kuleta ukombozi kwa kutuma sms kwa ndugu na marafiki zetu.
 
sisi extended familia yetu ina watu kama 12 ukianza kushuka kwa watoto jumla twafika 35 zote dr slaa.
Bado ofisi kuna watu kama 12.
Ila kuna mccm mmoja alikuja rubuni vijana wangu kuwa akija akiona bendera ya ccm inaninginia atawapa mkwanja vijana si wakaninginiza bendera wakati niliposafiri nilyorudi ndo wakanipa huo mkasa tukaingoa.




nimeipenda sana hii imatia moyo , nitaendelea kuwashawishi wengi zaidi ili wote tumpe kura dr slaa
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom