Karatu: Ngome imara ya upinzani (CHADEMA) kwa upande wa bara

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,306
Hapa nchini kumekuwa na fikra kwamba kaskazini kote ni ngome imara ya upinzani kwa majimbo karibu yote ila kwa tunaofahamu vizuri hiyo kanda tuko tofauti kidogo. Ni kweli wapinzani wamesimika mizizi kwenye baadhi ya majimbo ila mengi hayako imara kusimama na upinzani kwenye chaguzi zote.

Kwa mfano watu wengi wanaweza dhani kwamba jimbo la Arusha mjini ni ngome imara ya upinzani na labda huenda CCM ndo inaongoza kwa mara ya kwanza. Kihistoria Arusha mjini ni jimbo la CCM kwa muda mrefu sana hadi alipojitokeza Lema mwaka 2010. Mwaka 1995 lilishawahi kuwakilishwa na Mh Makongoro Nyerere. Na baada ya hapo akafuatia Felix Mrema hadi 2010. Jimbo la Hai pia limekuwa likipokezana CHADEMA na CCM tangu 1995. Angalau jimbo la Vunjo ndo limeonyesha kuwa kambi ya upinzani kwa muda mrefu chini ya Lyatonga na baadae Mbatia.

Kwa kaskazini ni jimbo la Karatu peke yake halijawahi kupokezana na CCM tangu 1995 hadi 2020. Watu wa hili jimbo ni wabishi na ni wapinzani kwelikweli wakishaamua. Walisimama na Dr Slaa tangu 1995 hadi 2010. Na 2010 -2020 bado wakachagua upinzani. Uchaguzi wa 2020 hauna haja ya kuuongelea kwasababu haukuwa huru wala wa haki kuanzia kwenye kura za maoni hadi kwenye uchaguzi wenyewe. Kihistoria wananchi wa Karatu kisiasa wako mbele sana ya muda. Mwaka 1961 wakati Karatu ikiwa kwenye jimbo la Mbulu walishiriki kikamilifu kumkataa mgombea wa TANU Chifu Dodo na kumchagua mgombea binafsi Chifu Sarwatt.. baada ya ule uchaguzi ndo mambo ya mgombea binafsi yakafutwa.

Pamoja na kuwa wapinzani ila wananchi wa Karatu mwanzoni hawakuwa na tatizo na CCM hadi pale jina la mgombea waliyemtaka (Dkt. Slaa) kukatwa Dodoma na kurudishiwa jina la mgombea wasiyemtaka. Kwa hasira wakamchagua Dr Slaa aliyeamua kuhamia CHADEMA huku akimsapoti mgombea urais kwa tiketi ya NCCR Mageuzi hayati Mrema mwaka 1995.

Nimeandika huu uzi kukikumbusha chama kuwa makini sana kwenye kuteua mgombea wa CCM anayekubalika Karatu ili kuepusha jimbo kuangukia mikononi mwa wapinzani. Nashauri CCM wamsimamishe Dkt. Slaa kwasababu yule mzee ni kipenzi cha wanaKaratu. Hakuna mwenye ubavu wa kisiasa kumzidi Dr Slaa pale Karatu.
 
Umeelezea vizuri sana, ila hapo kwenye mfano wa majimbo uliyotoa naona kidogo ndipo ulipokosea.

Kwa mfano, majimbo kama ya Arusha Mjini na Hai kwa wakati huu, kusema kwamba CCM na Chadema wanaweza kugawana nusu kwa nusu naona umekosea.

Tukumbuke wakati ule miaka ya nyuma ambapo CCM walikuwa wakishinda hayo majimbo, wapiga kura wengi wa hayo maeneo husika walikuwa bado hawajaamka, wazee wa sasa, ambao ndio walikuwa vijana wa wakati ule walioipigia kura CCM.

Lakini kwa sasa hali ya mambo ni tofauti, kuna wimbi kubwa la vijana wanaopenda mabadiliko walioamua kuwachagua wapinzani, hawa wanawazidi hesabu wale wazee wa CCM kwa mbali, hivyo kama uchaguzi ukiwa huru na haki, kuna uwezekano mkubwa mgombea wa upinzani kushinda kwenye majimbo husika.
 
Kwa jimbo la Arusha mjini CCM wakiweka mgombea anayekubalika wapinzani hawana chao... lile jimbo halitabiriki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom