Picha: Ziara ya Rais Kikwete nchini Oman

Ngongoseke una makaratasi au ndiyo unangoja kusombwa kama samaki wafu? Sema wenzio tukusaidie maana hatuko huku kwa kubeba mabox bali kwa taaluma zetu kubwa tu mwanangu.
 
Another great thinker' haya wewe mtanzani pyua na uchungu na nchi yako unasubiri nini kwenda leba kujifungua?

Wakati najiunga jf mara kwanza kabla sijala ban ya life nlikuwa nampinga sana jk kwa mambo mengi, lakini nilikuja kugundua mambo mengine mnayakuza humu jf kwa chuki zenu zisizo na maana,watu gani nyie msio sifia hata kitu kimoja mnajua kukosoa tu, hata hatua za maendeleo mnaponda tu kama sio wivu na chuki ni nini?
Mkuu unataka mtu asifiwe just for the sake of it!? kanifurahisha alivyokuwa anashangaa kasri hadi aibu
 
Ngongoseke una makaratasi au ndiyo unangoja kusombwa kama samaki wafu? Sema wenzio tukusaidie maana hatuko huku kwa kubeba mabox bali kwa taaluma zetu kubwa tu mwanangu.

Hahhaa haya kawaida yetu wabongo kwa advitise'nlipokuambia nalinda minara usiamini hayo ni mbwembwe tu'nina miaka 7 napiga mzigo ughaibuni kwa taaluma zangu, mpaka sasa nimefungua miradi mi 3 huko home ya maana ambayo nimeajiri watz wenzangu kama 38 hivi na bado naendelea kuisaidi serikali yangu na ndugu zangu wa tz kwenye suala la ajira ambalo ni tatizo la kidunia'
Ndio maana nawasihi wa tz wenzangu siasa sio suluhishisho la matatizo yetu,na wala hakuna mwanasiasa ambae atakuja kubadili maisha yetu labda ya family yake' muhimu tuachane na kupoteza muda kwenye siasa na muda huo tutumie kufanya kazi mwisho wa siku tutayaona maendeleo kwa macho yetu
 
Mwanangu Precise Pangolin afadhali umemjibu huyo ngongoseke ambaye kama si mtoto wa Kikwete basi anajilengesha kwa mafisadi ili wampe mabaki. Sijui kama kiumbe huyo ni mtanzania. Mijitu mingine imezaliwa na wezi, ikafundishwa wizi na damu zao zimejaa wizi. Hii unaweza kuiona kwenye mawazo ya mijitu kama ngongoseke. Ushindwe na kuangamia wewe ushabikiaye unajisi wa nchi yetu. Akina ngongoseke hawana tofauti na yule mrundi issa ponda .

Ni Myanzania na kahesabiwa kwenye sensa ya watu na makazi. Ni miongoni mwa Watanzania watakaofika milioni 50+.
 
Mpuuzi ni wewe unayeshabikia Mali zetu kuibiwa. Kutwa Rais ni kudhurura Huku akiteketeza kodi zetu kisa kwenda kupeleka zawadi za picha za maeneo aliyemuuzia sultani mwenzake!!!!

...great thinker mwenzetu..kuna eneo lililokodishwa "kwa shughuli za uwindaji tu, na kwa kufuata sheria na taratibu za uwindaji za jamhuri ya muungano"...na halikukodishwa kwa sultan yeyote..tujuze...eneo lipi hilo lililouzwa kwa sultani, harakati za kupigania maslahi ya "motherland", kwa style ya mchungaji mt zianze...?au ndio uzushi mwingine unaoathiri harakati zetu za kukabiliana na ufisadi wa kweli...manake miongoni mwa vikwazo ktk vita vya ufisadi ni majungu, uzushi, na uongo, na "kujifanisha kujua kumbe....."
 
Angepewa zawadi hiyo PAPA PAUL III wangemsifia JK anatangaza utalii wa tanzania!subirini 2015 rais atakua mlutherani
 
kapeleka sample ya tembo alonao mbugan, soon watasafirishwa kama wale twiga.
 
sijaona kibaya kutoa zawadi ya aina hiyo kwa rais wakuu tumbane kwa vitu senstive sio vidogovidogo kama hivyo tunatiana aibu aisee
 
majungu kuliko aliyokalia mwenyekiti wa chama cha magaidi. Ameenda Oman kujifunza namna ya kurithisha vyeo kwa watoto ili kukamilisha huo usultani wenu 2015 yatawatokea puani gamba la mwisho wewe

Mimi nadhani Rais anatafuta pia mji mzuri wa kulia mafao yake ya uzeeni akistaafu. Sidhani kama bagamoyo, Chalinze au Dsm patamfaa tena. Si unajua alishakwenda nje tripu/safari zaidi ya 330 ambayo idadi yake ya siku ni zaidi ya 1000 na ni sawa na zaidi ya miaka 3. Amezoea zaidi maisha ya huko kuliko hapa. Ni mawazo tu.
 
Ni juzi tu twiga walikuwa wanatoroshwa kwenda uarabuni kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa KIA na leo rais wetu anamkabidhi picha za wanyama hao hao mfalme wa Oman wa huko huko Uarabuni, kama Wazalendo wa Tanzania lazima tuulize kulikoni. Mfalme ni mjanja sana anakabidhi nishani isiyo na effects kwa rasilimali za nchi yake lakini sisi bila kujali hilo tumeshajichanganya. Nasikitika kwa wengi wanaoshindwa kulitambua hilo.
 
Katika muendelezo wa madharau kwa kiongozi wetu,waarabu wamechora picha mbalimbali za wanyama walioibiwa kwenye mbuga zetu na kumkabidhi Rais wa Tanzania eti kama aksante,eti wamedai hiyo ni tamaduni ya kiarabu,wengi wetu tumeshangazwa na hatua hiyo kwani tulidhani Rais na ujumbe mzito wa watu karibu 50 waliokwenda huko kwa waarabu wamekwenda kurudisha wanyama wetu kumbe wamekwenda kukabidhiwa mapicha kibao kama aksante ya hao waarabu waliotesa sana babu zetu kwa kuwauza kama nguo!​
 
Ikiwa watu watakuwa na mawazo kama yako basi dunia isingekuwa na maana kuishi,yaani wewe unachoamini na wengine wataka waamini?ama kweli ukimhisi jirani yako mwizi basi wewe ndio utaambulia dhambi zote,maana hata kama wapita njia wanapita wewe utahisi ndio anasogelea mlango wako kuvunja,
Naamini huna kazi za kufanya maan aungekuwa nayo usingekaa kuwaza upuuzi huu

yani watu wamefikia mahala wanatafuta hata makosa ya kusingizia ili wapate kumsema jk. Huu ni uzi wa pili kthusu safari ya jk huko mascut ambao hauna kichwa wala miguu, wakwanza ulikua unasema jk mshamba, anashangaa kasri la sultan wa muscut.
Hivi watanzania tunaenda wapi?
Mbona wengi wetu tumepumbazika namna hii?
 
Mkuu hivi jk ndiyo katoa au kapewa? Kuna thread ipo humu ikisema jk ndiyo katoa picha hiyo.
 
Mkuu hivi jk ndiyo katoa au kapewa? Kuna thread ipo humu ikisema jk ndiyo katoa picha hiyo.

kwa taarifa tulizo nazo Jk alitoa wanyama hai ili wakatumike katika kuchora hizo picha,yeye ndiye kapewa baada ya kazi kukamilika
 
Ahlan wa Sahalan Kikwete.

Leo baada asr (saa 10.30) ujumbe wa Kikwete na mawaziri wake akiwemo Abdallah Kigoda, B Membe , Haroun Suleiman(Znz) watakutana na wafanya biashara wa Oman katika kuzungumzia suala la uwekezaji katika nyanja mbalimbali katika ukumbi wa Al Qurooum.

Karibuni sana
 
Sikujua, kumbe amesafiri tena? Aaha, Ulaya hua anaenda kutuombea chakula (though wale hawana ardhi ya kutosha kulima kama yetu) sasa Uarabuni ameenda kutombea nini?
 
Mawazo mgando.

Hilo ni tatizo kubwa sana na nafikiri kama waTz mtakuwa makini ni lazima mfanye mjadala wa Kitaifa kuzungumzia UDINI. Kwani kilichopandwa na wakoloni na kupaliliwa na marais wenu wote kwa siri lakin hawakuweza kufikiri kuwa hilo ni kama Pemba la Ng'ombe haliwezi kufichika.

Poleni sana.

Kwa Tuliokuwepo jana wakti akikaribishwa kwenye Kasri la Malik Qaaboos tulistahaajabu yeye na ujumbe wake walivyokuwa wakilishangaa Kasr Hilo na mapokezi yake hakukuwa na gari bali farasi tu.

Poleni sana

 
Back
Top Bottom