Picha: Prof. Lipumba aanza kazi ofisini, aimarisha ulinzi

Piga kaz prof usiishie hapo fukuza mtatiro na seif wake mara moja
Akimfukuza Seif ndio mwisho wa CUF. 2020 hawapati hata mbunge mmoja. yeye mwenyewe na uenyekti wake hajawahi kupata hata kura laki tano nchi hii toka aanze kugombea urais.
mnamdanganya mlioko nyuma ya huu uhuni wa kulazimisha uenyekiti cuz baadae atajikuta yuko peke yake kma lyatonga na TLP.
 
Kuna vitu ambavyo ni mwiko kuviongea japo vinaonekana dhahiri: angalia jinsi alivyovaa Prof. na ujiulize Kama kuna kundi la watu ambao 'upagawa' wakiona mtu kavaa hivyo hata kama amekosea ni rahisi kwao kuona "wema" wake kuliko "ubaya" wake.

Vazi linalikufanya umchukie ndio vazi linalofanya wengine wampende!

Kofia tu ya Prof. Imekukereketa hivyo lakin hukumbuki Katibu Mkuu wa Chama cha Siasa kishawahi kuwa Padri na Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania na haikuwa na Tatizo kwako!
 
Mtatiro kajificha Mchambawima kwa Seif Sharif!

Mbona yupo Dar anaendelea na kazi.Hujasikia Le Professer analalamika hajakuta hata ream ya karatasi na hajui aanzie wapi zaidi ya kuongea na media namfukuza Maalim Seif,asubiri akisha mfukuza kama hata hicho kiti atakalia
 
Safi sana mwenyekiti wa ukweli!

Mwenyekiti wa ukweli kabisa aliyeletwa kwa Mtutu wa AK 47 chini ya ulinzi mkali na kuvunja mageti.Hebu imagine unatoa talaka halafu unapotaka kurudi na umekataliwa unaamua kuruka ukuta na kuvunja milango.
 
Ikiwa ni siku mbili tangu arudi ofisini na kuyazima maasi yalioandaliwa na kijana wake aliemlea na kumfundisha medani za siasa Julius Mtatiro, Mhafidhina Prof. Lipumba ameimarisha ulinzi nje ya ofisi ya CUF kuhakikisha nidhamu inakuwepo na akina Mtatiro hawaleti fyokofyoko za aina yoyote.

Dullu za intellegencia zinadai baada ya tukio hilo la le profeser kukaba penati kwa kubaki ofsini, kundi hasimu lipo mbioni kuanzisha ofisi nyingine hali itakayofanya kua na CUF mbili.

Mpaka sasa haieleweki hatima ya kijana Julius Mtatiro ambaye amekua akisingizia mgogoro wa chama hicho unatokana na external force kutoka Kitu alichokiita system, CCM na ACT wazalendo wapo nyuma ya profesa huyo nguli wa uchumi alietelekeza tasnia ya uchumi na kujishughulisha na siasa kwa miaka karibu robo karne.

Pichani na profesa akihudumia wanachama ofsini.

View attachment 406951
Hii Kali sana mmmh
 
Mbona yupo Dar anaendelea na kazi.Hujasikia Le Professer analalamika hajakuta hata ream ya karatasi na hajui aanzie wapi zaidi ya kuongea na media namfukuza Maalim Seif,asubiri akisha mfukuza kama hata hicho kiti atakalia

'Hajakuta hata ream ya karatasi...' Nashukuru umetambua kuwa yupo Makao makuu ya CUF
 
Ikiwa ni siku mbili tangu arudi ofisini na kuyazima maasi yalioandaliwa na kijana wake aliemlea na kumfundisha medani za siasa Julius Mtatiro, Mhafidhina Prof. Lipumba ameimarisha ulinzi nje ya ofisi ya CUF kuhakikisha nidhamu inakuwepo na akina Mtatiro hawaleti fyokofyoko za aina yoyote.

Dullu za intellegencia zinadai baada ya tukio hilo la le profeser kukaba penati kwa kubaki ofsini, kundi hasimu lipo mbioni kuanzisha ofisi nyingine hali itakayofanya kua na CUF mbili.

Mpaka sasa haieleweki hatima ya kijana Julius Mtatiro ambaye amekua akisingizia mgogoro wa chama hicho unatokana na external force kutoka Kitu alichokiita system, CCM na ACT wazalendo wapo nyuma ya profesa huyo nguli wa uchumi alietelekeza tasnia ya uchumi na kujishughulisha na siasa kwa miaka karibu robo karne.

Pichani na profesa akihudumia wanachama ofsini.

View attachment 406951
Safii, prof. alijiondoa mwenyewe kajirudish mwenyewe pia
 
Nafikiri hiki ni moja kati ya vitu vinavyofanya siasa za Tanzania kuwa za hovyo na kuvunja watu moyo waliokuwa na tumaini kuona siasa za Tanzania zikipata sura na mwamko mpya.
 
CCM inamuona sasa hivi ana thamani...ila kwa mgogoro huu wa pande mbili kuvutana, watamu"eliminate" Lipumba, ili kuaminisha watu kua ni kina-Maalimu wamefanya hivyo.
Ukweli, naona Lipumba, anacheza mchezo ambao utamgharimu sana huko tuendako...inaweza kumgharimu hata maisha.....
Ngoja tuone
 
Nafikiri hiki ni moja kati ya vitu vinavyofanya siasa za Tanzania kuwa za hovyo na kuvunja watu moyo waliokuwa na tumaini kuona siasa za Tanzania zikipata sura na mwamko mpya.

Na hawa ni wasomi wakituaminisha wako kwa ajili yetu kumbe wako kwa ajili ya MATUMBO yao
 
Back
Top Bottom