Picha hii inatoa ujumbe Gani kwenu?

Babylon

JF-Expert Member
Feb 5, 2009
1,332
82
8D6U2314.JPG
 
Kwamba CCM ni chama twawala.

Mkuu nakuona Kiswahili Umesha kisahau na hiyo Lugha unayoizungumza hapo ulipo sijuwi kama unaielewa?nilikuwa namaa kuwa hao wakuu bodi lengweji zao zinatowa ujumbe gani ?kwani makamba anaonekana kumpa kicheko cha kikejeli karume na Ali Hassan mwinyi anaonekana mwenye furaha ya Kupindukia.inayoashiria kumdhalilisha Rais Karume..
 
Ujumbe upo wazi, Viongozi wote wa serikali ya Mapinduzi Zanzaibar hawakuvaa uniform ya kijani ya ccm.
 
Hata siku moja siwezi kusahau kiswahili Mkuu. Ninachoona katika hiyo body language ya hao waheshimiwa ni unafiki na ufisadi hakuna jingine.
 
Ujumbe upo wazi, Viongozi wote wa serikali ya Mapinduzi Zanzaibar hawakuvaa uniform ya kijani ya ccm.
Aisee, mimi pia niliishitukia hiyo tangu kwenye gazeti la habari leo. Hawa wazanzibari wamevaa nguo za maombolezo. sijui kulikoni hapo??!
 
Hata siku moja siwezi kusahau kiswahili Mkuu. Ninachoona katika hiyo body language ya hao waheshimiwa ni unafiki na ufisadi hakuna jingine.

lakini hao Waheshimiwa (Mnaowaita) wanafiki si mnawachaguwa nyinyi Wenyewe? sasa lawama za nini jamani?

Msiwatukane Viongozi wetu jamani kuweni na Heshima kama hamuwataki musiwachague tena kwenye Uchaguzi
 
Naona Benjamini kama alielazimishwa kuhudhuria, anawaza saa ngapi mtamaliza, Madili yananipita viwanja!

Hata siku moja siwezi kuwapigia kura viongozi ambao wanaweka maslahi yao mbele badala ya yale ya nchi. Mimi sioni kama hayo ni matusi bali ndiyo ukweli wa mambo. Kwa kufumbia macho ufisadi mkubwa unaoendelea nchini na kukaa nao meza moja mafisadi mbali mbali huko ni kuonyesha unafiki na ufisadi. Upane mmoja wanatwambia Watanzania kwamba wanapambana na ufisadi halafu mafisadi wanaojulikana na upo ushahidi wa kutosha dhidi yao hawachukuliwi hatua zozote za kisheria. Kama huo si unafiki na ufisadi sijui ni kitu gani!
 
Naona Benjamini kama alielazimishwa kuhudhuria, anawaza saa ngapi mtamaliza, Madili yananipita viwanja!

Alipotakiwa kujibu tuhuma dhidi yake kuhusu ufisadi alisema yeye kishastaafu siasa! Sasa kwenye hicho kikao sijui hajui kama kinahusu siasa! ndiyo huo unafiki ninaosema hapa na akitoka hapo si ajabu anapokea sitting allowance kubwa tu.
 
It is very very difficult to comprehend what it is in somebody's mind! All of them they know exactly know how terribly they have failed us! Imagine a country will all these human resource, political tranquillity, and the immense natural resources, Can you imagine we have not built even one meter railway apart from that was LEFT by colonial regime!

I like it you guys when you call em Wanafiki watupu, because that is the perfect description! Actually we furious, we are frustrated, and there is huge storm out there gaining speed and energy, it is coming to sweep single hypocrite politicians because this time we need results! We need outputs!
 
hapo wanasema tu jamani tunafanyaje ili nipate kula na mie miaka 5 tena nisaidieni au sio wanajamii anaomba msaada anajua kuwa ameharibu
Conquest
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom