PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Huyu kamanda wa polisi ni mnene mpaka vishikizo vya shati vinakataa.. Wao wanaendekeza mavitambi yao tu na kuua raia..

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hapa hakuna cha kutaka kujua nani aliua ua la. Kama wananchi wanamechoshwa na vitendo vya askari kuwaua kama wadudu basi nao wajihami na kumshughulikia kila askari bila kujali aliua au la. Maana wakati wao wakiua huwa hawaangalii nani ana kosa au la. Jino kwa jino na jicho kwa jicho na hawa wauaji ili kuweza kuleta ulinganifu na kuheshimiana. Choma moto askari mtakayempata iwe kichochoroni au kwenye baa hata nyumbani kwake muone kama hawataacha upuuzi wao.

Hii nimeipenda sana!
 
ukitizama kwa umakini hiyo picha yenye askari aliyelenga mwandishi ni dhahiri amefyatua hiyo bunduki yake na moshi bado unafuka kutoka kwenye mtutu, hebu jiulize kwa nini amlenge mtu ambaye yuko chini na hana aina yeyote ya silaha na amezungukwa na maaskari? Je ni madhara gani angeweza kufanyia watu ambao wamepitia mafunzo kwa aklili yangu tu siwezi pata jibu la kuniridhisha tofauti na walinzi wa usalama kuwa wauaji

attachment.php


Someni ***** wa gazeti HABARI LEO linavyopindisha habari kisha linganisha na ukweli huu.

Habari leo limeandika kwamba Mwandishi Daud Mwangosi aliuawa kwa kutupiwa bomu wakati akiwa mikononi mwa polisi bomu ambalo lilimjeruhi pia mmoja wapo wa polisi cheo cha juu.

Picha hiyo ni kielelezo ambacho wanashindwa pakuficha aibu.
 
Unacheza na hawa policeCCM eeh.....utasikia alikuwa anapambana na police na katika police kujitetea wakamuua kwa bahati mbaya!

R.I.P Mwangosi.
 
RIP youngman.

happen to know and work with him and his folks. Mjengwa, najua wewe, akina Malembeka, na wanahabari nguli wote hapo hiki ni kipindi kigumu sana kwenu LAKINI I hope hamtanunuliwa kirahisi ili kuziba harakati na hasira zenu kupinga unyama huu. I know Ken, ambaye simuamini kabisa kwa jinsi alivyokuwa ananunuliwa kwa bei rahisi sana na hao mafisadi mabulushi, waarabu na hata akina Lukuvi. Mwenzenu ameuawa kinyama sana, sana na nyie lazima muongoze mapambano haya magumu kuwakomboa wanahabari, wapenda amani na wananchi wa Tanzania kwa nguvu zote. Tunawaangalia na tutawafuatilia kwa karibu (nilitegemea kuona na kusikia mengi kutoka ktk blogu zenu hasa wewe na Francis, lakini as I mentioned earlier ) tunajua jinsi ambavyo chama na serikali inavyowatuliza watu kama nyie..

DM hakustahili kabisa unyama huu... Ohhhh god, msipoangalia sasa watu wataanza na hizo kopta za polisi, ambazo at times zinatumika kubeba familia na ndg wa hao hao tena kwa safari za matanuzi...!

sijui kama maggid anaweza kuliongelea hilo na pamoja na anko fransis maana watalitupia kiana kama habari za tbc zinavyowekwa hasa zinazo husu govt yetu..

RIP Dm
 
Wadau mwangalieni Issa michuzi alivyoandika hii habari kwenye blog yake. Jamani haki iko wapi? Nini hasa tunataka na tunakwenda wapi.
Issa michuzi nilikuwa namfagilia sana lakni kwa hili amenitoka. Kujifanya kwamba polisi sio waliokusudia. Shame on you michuzi.
 
Mungu wangu, huyu wamemkatakata kwa panga au ni risasi tu? Ee Mungu, inusuru nchi yako hii!!!!!!!!!!!!!

Huyu jamaa inaonekana wamemlipua na bomu la kuchimbia madini, inasikitisha, hawa polisi walio fanya hivi lazima warukwe na akili!
 
duh, pumbavu kabisa hawa polisi ni wajinga sana, ukisikiliza RPC anasema eti kunakitu kimerushwa toka kwa wananchi.....hii picha lazima waandishi iwekekeni front page magazeti yote
 
Sasa hivi nimesikiliza mahojiano kati ya RPC na mwandishi wa WAPO radio, anadai mwandishi DM alikuwa anafukuzwa na wananchi (wanachama wa Chadema) ambao walikuwa wanapambana na polisi kwa kutumia mawe. Na amepigwa na bomu ambalo polisi hawakuwa nalo, Polisi wanawashikilia watu saba kuhusiana na mauaji hayo.

Shuhuda mwingine aliyekuwepo kwenye tukio, anasema Polisi walimfyatulia bomu marehemu ambapo polisi aliyekuwa nyuma ya marehemu alijeruhiwa, maelezo ya shuhuda yanaendana na picha ya kwanza hapo juu. Na kwa mujibu wa shuhuda, kamanda wa Polisi wa mkoa alikuwa anashuhudia wakati unyama huo unatendeka.

Vifo vya watanzania wenzetu vinavyohusishwa na jeshi la polisi vinaanza kuwa matukio ya kawaida, hivi tunavyosikia ni kwavile kuna mkono wa siasa ndani yake, lakini polisi wetu wamekuwa wakiua wananchi kwa visingizio mbalimbali as if wao ni mahakama na wako juu ya sheria.

Sidhani kama wanaharakati au vyama vya siasa pekee wanaweza kupiga kelele ya kuleta mabadiliko, ni sisi wananchi wote bila kujali tofauti zetu za kiitikadi kupiga kelele na kuomba hatua stahiki zichukuliwa dhidi ya wote waliohusika na matukio ya vifo vya wananchi. Zaidi kushinikiza reform kwenye jeshi la Polisi. Lazima kuwa na jeshi litakalofanya kazi kwa uadifu na kutokuwa tayari kufanyia kazi maslahi binafsi ya wanasiasa
 
Ee Mungu endelelea kulivumilia taifa lako wanyonge utunusuru na majanga haya ya utawala huu mbovu
 
Nimemfahamu huyu bro Daudi Mwangosi since akiwa anafanya kazi pale CRDB akiwa inaitwa Co-operative Rural Development Bank miaka ya 90, baada ya hapo akaanzisha biashara ya kupiga picha. Na baadae akaingia kwenye uandishi.

Kwangu mimi ni msiba mkubwa, nimehuzunika sana, na hasa baada ya kuona kafa kifo cha kinyama, utumbo na viuongo vingine kumwagika hadharani. Hakika ni kifo kibaya, familia yake watamkosa, Iringa watamkosa, wanahabari watamkosa.

Je, huzuni hii yote haitoshi kuwa laana kwa polisi na serikali? Je, huzuni hizi na malalamiko haya ya wanaomkosa sasa, hayatoshi MUNGU kuwaadhibu wahusika?
 
duh, pumbavu kabisa hawa polisi ni wajinga sana, ukisikiliza RPC anasema eti kunakitu kimerushwa toka kwa wananchi.....hii picha lazima waandishi iwekekeni front page magazeti yote
iko kwenye gazeti la Mwananchi la leo
 
So sad, naumizwa na watu wanaitwa polisi hata nafikia kuwalaumu ndugu zangu waliomua kujiunga na kazi hii, ni heri hata wangekwenda kulima kuliko kazi hii ya laana.

Ni watu gani ambao mnakosa ubinadamu kabisa kiasi hiki!!!!

Ee Mungu tuhurumie watanzania na ingilia kati mateso ya watanzania!
 
n00B

Mgonja anadai Mwangosi alikimbia kutoka kwa waandamanaji akiomba msaada wa Polisi ni kweli ndugu yangu? Na kama sivyo tutaisubiria video tujionee ukweli, nakushauri disseminate hizo evidence ulizonazo kabla hawajakuvamia na wewe!

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kama ni kweli hao askari ndio wali Open fire hii itakuwa mojawapo ya scandal na blunder kubwa sana ya jeshi la polisi!!!
 
Jamani jamani jamani,polisi karibu kumi wnegine na bastora ,mabomu nk wanamdhibiti mtu mmoja asiye na silaha na kumuua kikatili hivyo,inatisha na haiitaji tume wala nini,ingekuwa ni nchi yenye haki hao wote wanaoonekana kwenye picha wangepelekwa mahakamani mara moja,hapo hakuna cha flying object,ukisikia excesive and unreasonable force in practise basi ndio hii.
 
Asante noob kwa taarifa iliyowazi!....

...Polisi wamesema Mwangosi alikimbilia waliko polisi kuomba msaada na kumkumbatia polisi ndipo kitu ambacho hakijulikani kilikotoka kikamlipua! ......Hizi bangi!..
 
Back
Top Bottom