Philip Mangula ateuliwa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM

CCM wamezidiwa sana kwenye kutafuta watu makini wa kuongoza chama;sasa wanawarudia wale wale akina Mangula ambao sera zao mbovu ndizo zimetufikisha hapa!

CCM hawana watu wapya wenye new ideas wakivushe chama hiki kwenye msukosuko huu wa ombwe la uongozi?
 
kuna mtu alijaribu kunieleza japo nimesahahu ila ni hivi kwa ufupi.....Katika Jeshi Mangula ni mkubwa kicheo kuliko JK, na hivyo JK hulazimika kupokea Order toka kwa Mangula maana kumbe vyeo vya kijeshi huendelea tu hata ukitoka nje ya system hio,,,,,,
Kikwete wanamwondoa? Mangula na Kikwete wanawezaje kufanya kazi pamoja? Uwezo na Mangula na Kikwete ni sawa na kulinganisha mlima kilimanjaro na Kichuguu. Sasa utawawekaje pamoja hawa? Lakini pia ikumbukwe kwamba Kikwete alimtosa vibaya sana Mangula, baada ya Mangula kueleza wazi kwamba Kikwete hana uwezo wa kuongoza nchi. Sasa leo watakaeje tena kujadili masuala ya mstakabali wa taifa ilihali ni mahasimu?
 
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CHAMA CHA MAPINDUZI CCM iliyokaa kikao chake jana tarehe 10 November 2012, imependekeza Ndugu. Phillip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara huku Rais wa Zanzibar Mweneyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, akipendekeza kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.


Nape Nnauye ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kizota,amesema majina hayo yatapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu siku ya jumanne.Hata hivyo ndugu Nape, amewaambia waandishi wa habari kuwa kikao cha NEC kimepitisha kwa kishindo jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti CCM Taifa.


Pia kikao cha NEC kimefanya Mabadiliko kidogo ambapo leo wajumbe wa NEC nafasi kumi bara,na kumi Zanzibar watapigiwa kura leo tarehe 11 Novemba badala ya kesho, na matokeo yatatangazwa mara baada ya uchaguzi kumalizika.Wajumbe wote wa mkutano kutoka mikoa yote wameshawasili.


Wakati huo huo Rais Jakaya Kikwete kabla ya kufungua mkutano mkuu ataweka jiwe la msingi la Makao Makuu mapya ya CCM eneo la Makulu.

 
Kikwete wanamwondoa? Mangula na Kikwete wanawezaje kufanya kazi pamoja? Uwezo na Mangula na Kikwete ni sawa na kulinganisha mlima kilimanjaro na Kichuguu. Sasa utawawekaje pamoja hawa? Lakini pia ikumbukwe kwamba Kikwete alimtosa vibaya sana Mangula, baada ya Mangula kueleza wazi kwamba Kikwete hana uwezo wa kuongoza nchi. Sasa leo watakaeje tena kujadili masuala ya mstakabali wa taifa ilihali ni mahasimu?

Hivi EL na Mangula wana ukaribu?
 
Hili ni chama kubwa lakini kwa nini mnajikita katika circle ya watu wachache wale-wale kila siku? Yaani Tanzania nzima hakuna mwingine mwenye sifa mpaka mnarejea kwa wale wale? kweli?? Anaweza kuwa alikuwa mtu mzuri na shupavu lakini lazima twende na wakati na pia kuwapa wengine nafasi. Ingekuwa ni hivi Bill Clinton angerudishwa kuwa Rais wa US!! CCM fungukeni muangalie nje ya hilo box.
 
Ndio maana nauliza, nikitegemea majibu yanayo sindikizwa na hoja; kwa maana hiyo wananchi wana kiu ya sura mpya zitakazosimamia sera mpya, au sera zile zile.
...lililowazi ni kuwa tunahitaji vyote sura na sera, lakini kwa upande wa sura, hatuhitaji ukale au upya wake, bali dhamira na uwezo.
 
JK ndie anaemtaka sasa...akijenge chama upya!amekuwa active kwa mwaka sasa kusaidia chama kwenye kazi za ndani nyingi sana hata majuzi nimemuona akiwakilisha chama Msumbiji kwenye sherehe za Frelimo

Kikwete ameshakamilisha kazi yake ya kujichotea rasilimali za nchi na kufanya utalii wa kutosha nje ya nchi hivyo kwa sasa anataka awaachie matatizo aliyoyatengeneza kwa takribani miaka saba tangu aukwae urais na uenyekiti wa chama. Mbali na hilo, ameweza kutimiza azma yake ya kuishi magogoni na kumtafutia mke wake pamoja na mwanae ulaji ndani ya chama.
 
How did you know that ? acha watu wachambue kila hoja hata kama siyo wana CCM , halafu aliyekudanganya kwamba ccm itashinda 2015 lengo lake umelijua ? nakushauri ujiandae kisaikolojia ! kwa taarifa yako tu ni kwamba Huyo Kikwete anajua kitakachotokea , mazoea yana tabu nyingi sana .

mwaka mzima wa m4c matunda yake nini? viti vitatu vya udiwani? kua realistic kidogo.dalili za ushindi uwa zinaanza mapema pamoja na ujinga wote wa ccm, cdm bado hawana support base kubwa wanategemea independent voters na kura za chuk za wana ccm/retaliation votes. assuming nothing drastically happens btn now and election date, ccm wanashinda. just a simple objective reasoning from an independent voter.
 
Wanabodi baada ya pendekezo la Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti je JK ataendelea kujutia makosa yake na kwenda kumuangukia Mzee Salim A Salim arudi kundini? Pengine ndiye mgombea Urais CCM 2015 kwa dhana ya "Ni zamu ya wa Zanzibari"
 
Mwaka 2006 nilishuhudia na machozi yalinilengalenga Mangula akigaragazwa katika uchaguzi wa mkoa wa Iringa nafasi ya uwenyekiti wa mkoa. Sikulia kwa sababu napingana na dhana ya demokrasia bali kiongozi nyota akisukumizwa gizani na nguvu ya fedha na campaign za hila ambazo ziliongozwa na wanamtandao.

Kwa mawazo yangu nilihisi ndio mwisho wa kisiasa wa Mangula. Kimsingi wanajamii kwamba leo Mangula amependekezwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama Taifa inanirudisha tena kwenye mawazo ya mwaka 2006 lakini leo katika mtizamo tofauti kabisa, namhurumia kwani huenda ameandaliwa kwenda kupigana vita ambayo hajui mipaka yake na pia hajui nani ni adui wa nani. Amebebwa kuwa ngao ya kundi ambalo limeshindwa kupigana na sasa limerudi nyuma kuomba msaada kwa mahasimu wao. Sijui ni pendekezo la nani? sijui ni nani anasema Mangula anatosha kuwa M/M ili afanye nini?

Mtizamo wangu ni kwamba Mwenyekiti anahisi CCM wanaweza kuingia uchaguzi 2015 wakiwa katika makundi. Kwa hiyo Makamu Mwenyekiti Ndugu Mangula analo jukumu la kuondoa makundi ambayo yatakuwa yamezaliwa na machungu ya misuguano ya mnyukano wa kutafuta madaraka na si kutumikia wananchi. Tujiulize kama kweli kazi hii Mangula wa leo na wa jana ataiweza sina hakika bali nina mashaka makubwa mno.

Mangula ambaye wanamtandao walimwita kila jina na kumtupia kila aina ya kejeli baada ya uchaguzi 2005 eti leo ni hazina kwa CCM, Mangula ambaye yeye mwenyewe alishindwa kusimamia wanamtandao wasijenga misingi ya kuibomoa CCM ya leo, aliachia wanamtandao wakakua ndani ya chama mithili ya nyoka mwenye vichwa viwili leo akapambane na nyoka alieyeko ndani ya CCM ambae sasa ana vichwa na midomo minne. Mangula ambaye alishindwa kuwaelewesha watu wa Iringa athari za rushwa na kuacha zimdhuru yeye mwenyewe, leo akaongoze kujenga misingi ya chama ambacho alama yake kuu ni uadilifu na upendo ili iwe rahisi kujinadi mbele za watu?

Namtakia kazi njema akimudu hii kazi leo na kesho anayohaki ya kuwa mgombea uraisi kupitia chama chake na kwa kweli mimi Mghaka nitazunguka nchi nzima kumwombea kura. Akipambana na kuondoa rushwa, akarudisha hadhi ya CCM ile ya miaka 80 na 70 nitamwombea awe mgombea pekee wa uraisi wa Tanzania na nahisi wanajamii mtakuwa pamoja namimi.

Wairinga nitawakumbusha leo kuwa waliwahi kupingana na Baba wa Taifa katika kumwangalia Daudi Ngelautwa Mwakawago wakati wa uhai wake, nafurahi Mwenyekiti wa Chama na Rais wa wakati huo alikubaliana na wanairinga na uchaguzi wao lakini baada ya muda kidogo Daudi akateuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tanu madaraka ambayo ni sawa na Katibu Mkuu wa chama leo. Kama CCM ya leo hawakuridhika na demokrasia katika mkoa wa Iringa walipaswa kwanza kumpa kazi Mangula mapema sana ili kuwapinga kwa vitendo badala ya kuacha miaka zaidi ya 6 kupita. Watu wa Iringa hawajifunzi na makosa ya hovyo wayafanyayo katika kuendesha demokrasia ya uchaguzi ndani ya chama mkoani.Siwalaani, lakini akili ya kawaida inanilazimisha kuwakumbusha kuwa demokrasia ni pamoja na kuwalinganisha wagombea katika vigezo ambavyo vinaweza kuwafanya kuwa viongozi bora, kimsingi mshindani wa Mangula alikuwa hatoshi kwa kila kigezo kushindana na Mangula

Mwisho nisema kazi aliyonayo Mangula ndani ya Chama Cha Mapinduzi ni kubwa mno na naomba asome maneno ya kipole lakini mazito ambayo Mwenyekiti ameyasema leo katika ufunguzi wa mkutano wa chama. Anapaswa kubeba taswira na maono ambayo J.K. ameiweka katika hotuba yake. Chama kinaonekana kuelemewa, na kuzidiwa maarifa na wale watafutao vyeo ndani ya chama. Wenzake wanaona wanaelekea kushindwa kiasi kwamba wanalazimika kuwakodi majenerali walioko mapumzikoni ili wapambane vita hiyo kwa manufaa ya Watanzania. Sasa angalizo kwake Mangula asipoangalia atashindwa kazi kabla hata hajaanza, nguvu ya mitandao ndani ya chama inanguvu kuliko mamba ndani ya maji, si tembo wala simba wala nyati awezaye kupambana na mitandao hiyo naye akabaki salama asipoangalia 2015 uchaguzi mkuu unaishia salama atakuwa nae ametafutiwa lorry lakubeba mizigo yake kwenda kijini kama ilivyomtokea 2006. Je yupo tayari kupitia njia hiyo tena na kwa gharama ya nani? Atambue kuwa katika nyumba ya shetani utakatifu ndio adui namba moja na dhambi kuu na uongo, udanganyifu, uovu, utoaji na ula rushwa ndio misingi ya ustawi wake.

Kwa kuwa nimekuwa mshabiki wako naogopa tena kul;engesha machozi eti nikuhurumie wewe tena kwa kushindwa kuwa mtume bora katika viwanja vya shetani.

Wasalaamu na nikutakie kazi njema kama mnampenda mzee huyu mpelekeeni salaamu hizi
 
  • Thanks
Reactions: Ame
can anyone help to explain this, is kind of strange! is it that the guy was too good for regional level? or the guy is too weak to handle matter at national level and may be EPA need weak people to easily control them?
 
Kikwete wanamwondoa? Mangula na Kikwete wanawezaje kufanya kazi pamoja? Uwezo na Mangula na Kikwete ni sawa na kulinganisha mlima kilimanjaro na Kichuguu. Sasa utawawekaje pamoja hawa? Lakini pia ikumbukwe kwamba Kikwete alimtosa vibaya sana Mangula, baada ya Mangula kueleza wazi kwamba Kikwete hana uwezo wa kuongoza nchi. Sasa leo watakaeje tena kujadili masuala ya mstakabali wa taifa ilihali ni mahasimu?

hasira huwa zinaisha mkuu then watu wanapatana na kuendelea na safari.
 
CCM wamezidiwa sana kwenye kutafuta watu makini wa kuongoza chama;sasa wanawarudia wale wale akina Mangula ambao sera zao mbovu ndizo zimetufikisha hapa!

CCM hawana watu wapya wenye new ideas wakivushe chama hiki kwenye msukosuko huu wa ombwe la uongozi?

hiyo ni kudanganyana tu ndugu yangu hebu niambie unavyosema "CCM hawana watu wengine" Ok ni chama gani chenye watu hao watu? mbona upinzani wamekuwa wanasubilia akina Mpendazoe, Shibuda nk na kuwaacha watu wao kwa sababu wanasema hawana uwezo? na sasa nimesikia Mbowe anasisitiza anamtaka Sumaye?
 
CCM wamezidiwa sana kwenye kutafuta watu makini wa kuongoza chama;sasa wanawarudia wale wale akina Mangula ambao sera zao mbovu ndizo zimetufikisha hapa!

Mwishowe kuna mtu kaongea jambo lenye busara.
Huyo Mangula mnayemwona ndiyo tiba ya matatizo sugu ya CCM si alikuwa kiongozi mkuu tu hivi majuzi? Kitu gani alifanya mpaka leo aonekane eti ni 'jembe'?!?

Sijaamini kama waumiza vichwa humu bado wana imani na mtu yeyote ndani ya CCM hii.

Kwa hali ilivyo sasa, CCM imefikia uwezo wake wote; hakuna lolote jipya iwe katika uongozi wala sera, ambalo litaletwa na CCM.

Hii CCM inapaswa ikae kando, ili chama kingine kiungoze dola. Ipumzike, miaka 50 ya kupiga mark time imetosha.
 
hiyo ni kudanganyana tu ndugu yangu hebu niambie unavyosema "CCM hawana watu wengine" Ok ni chama gani chenye watu hao watu? mbona upinzani wamekuwa wanasubilia akina Mpendazoe, Shibuda nk na kuwaacha watu wao kwa sababu wanasema hawana uwezo? na sasa nimesikia Mbowe anasisitiza anamtaka Sumaye?

Ng'azagala!
kwa sababu CHADEMA huwa wanashindwa kuleta watu wenye mawazo mapya ndiyo nao CCM waige?Mangula alikwisha kuwa hadi Katibu Mkuu-CCM sasa anarudishwa tena kama Makamu wa Rais;ni kitu gani kilimfanya ashindwe kuibadilisha CCM alipokuwa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu na leo hii ndiyo tuamini kuwa eti ataibadili CCM kwa nafasi hii mpya?

Mangula HANA JIPYA!
 
Back
Top Bottom