Doji MD
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 1,223
- 2,414
Habari wakuu, natumaini mapambano ya maisha yanaendelea…
Mimi sio mwandishi mzuri ila nitajihidi nieleweke, bila kupoteza wakati, leo ningependa kushare jambo kuhusu pesa za moto’ (real story)
Jamaa tumuite Hassan’ alichukuliwa na boss mmoja kutoka kijiji nakuletwa mjini kuuza Duka, alifanya kazi kwabidii na miaka ikaenda huku akisave pesa mdogo mdogo…
To cut
Akafanikiwa fungua duka lake kwa mtaji mdogo aliopata na kama unavyojua biashara za uswahilini ikamlazimu atafute waganga kwa nia yake wamsaidie apate wateja wengi na ni jambo ambalo akafanikiwa kwa asilimia kubwa na kuweza kuongeza bidhaa za kutosha dukani lakini hilo halikumfanya atosheke.
Kasafiri mbali zaidi huko mkoani Mbeya kuelekea Songwe kufuata Wataalamu wa jadi na kupewa dawa za biashara na katika Stori za hapa na pale yule Mganga hakuwa nyuma kumdokeza pia kuwa hata pesa za moto anaiweza io kazi na kasaidia wengi kama anahitaji.
Basi bwana Hassan kwasababu hakuwa kwa lengo wakati huo ikabidi akajifakari,
Akaendelea na biashara zake.. asee biashara iliwaka sana wateja kama wote hahaa hakuwa mtu wa kujitegea isitoshe ni mtu katoka bush hukoo hivyo bata ilikuwa kama ugeni na watoto wa mjini..
Siku zikapita basi katika stori moja mbili tatu na rafiki yake kuhusu mambo ya pesa jamaa akaomba connection kwa Hassan kuwa ampeleke kwa huyo mtaalam kwakuwa kauchoka umasikini. Wakapanga siku na kukubaliana kuwa gharama zote atalipa mwenyewe yeye kama msindikizaji tu( jamaa tumuite John).
Siku ikafika, wakaanza safari toka mkoa X kuelekea Mbeya kama ilivyo kawaida kushuka gari kupanda gari na mwisho boda boda mpaka kufika kwa babu(Mganga).
Walipokelewa vizuri baada ya masaa kadhaa wakaingia kwenye Chumba maalumu(kilinge) huku jamaa akieleza Zaidi shida yake.
Ilipofika usiku wakiwa na stori za hapa na pale kibarazani babu akaagiza bia kama nne(bingwa moja) wakiwa katika mzunguko wa watu wanne yani Babu, Hassan, John na yule kijana wa mzee.. wakaanza kukata bia mzee akamimina bingwa kwa John nakumwambia lazima anywe huku Hassan akigoma kuwa safari inamtosha kwakuwa si mpenzi wa vilezi basi ilikua haina budi kwa John kuendelea kupiga bia huku akipigwa na mshangao wa kuwa mbona hakuna pale kwalengo la kunywa lakin ndio hivyo hakuwa na jinsi..
Stori na maelezo mengi yaliendelea toka kwa babu na baada ya kumaliza kunywa muda ulikuwa umeenda hivyo John akaonyeshwa Chumba cha kulala ambacho aliambiwa ni lazima alale na kijana wa yule mzee ambae hakuonekana kutoa hata neno wakati woote, huku Hassan nae akioneshwa chumba kingine alale pekeake….
ITAENDELEA………