Paul Makonda Kuunguruma Kwa kishindo cha Simba katika mikoa 20 kuanzia Dar Tarehe 19 January, kusikiliza na Kutatua kero papo kwa papo

Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi,uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Mwamba Mwenyewe wa Siasa Mheshimiwa Paul Makonda ataanza kuunguruma kwa kishindo cha simba katika mikoa ishirini bila Kupoa wala kupumzika. ambapo ziara hizo zitaanza kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dar es salaam nzima Tarehe 19 mwezi huu kabla ya kuendelea mikoani anakosubiliwa kwa hamu kubwa na kiu kubwa mithiri ya watu walio jangwani.

Taarifa hiyo ambayo imetolewa na idara ya uenezi na kusambaa kwa kasi ya mwanga katika mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi Mpaka kule Washington DC Marekani, imeonekana kugusa na kuteka hisia za watu wengi sana ambao wana hamu kubwa sana kufikiwa na Mh Makonda ili kumsikiliza na kumpatia kero zao kutokana na kufahamu utamaduni wake wa kupokea kero na kutoa suluhisho la papo kwa papo.

Paul Makonda ambaye mitaani wanamwita mtetezi na sauti ya wanyonge ameonekana kugusa hisia za wengi sana kwa ratiba yake hiyo ambayo imefurahiwa na wengi sana , kutokana na kila mtu kuwa na kiu ya kuonana naye na kumuona akifika katika mkoa wake . mitaani na katika vijiwe vyote kwa sasa ni Makonda na CCM na namna Rais Samia alivyopanga safu matata yenye watu matata wenye uwezo matata na uchapakazi matata wenye kuleta matokeo chanya na matumaini kwa watanzania wanyonge wanaohitaji msaada wa serikali kuinuliwa kiuchumi.

Wakati haya yanafanywa na CCM Katika kuwafikia watanzania
popote walipo na mahali walipo na kuwasikiliza kero zao na kutatua kero zao zinazowatesa na kuwa kikwazo katika shughuli zao za kila siku. Imekuwa ni tofauti kwa upande wa vyama vya upinzani kama CHADEMA ambavyo vipo Bize kutoa na kuleta mapendekezo ya kirafi,kifisi na yenye kukosa uchungu na maisha ya watanzania kwa kutaka kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo bila kujali kuwa suala hilo litambebesha mzigo wa mateso mtanzania mnyonge .

lakini pia kukomba pesa zote kuwalipa wabunge pesa ambazo zingeweza kutumika kufanyia shughuli za maendeleo kama vile kujenga zahanati au vituo vya afya au shule au barabara au kununua madawa ,vifaa tiba n.k. wao CHADEMA wanataka fedha hizo zitengwe kwa ajili ya matumbo yao wakishaupata ubunge ambao wanataka waongezewe njia kubwa ya kuupata kirahisi.huo ndio ufisi wa CHADEMA na mawazo yao yalipoishia kuwaza matumbo yao tu badala ya maisha ya watanzania wanyonge.

Hii ndio maana watanzania wanaendelea kuwapuuza na kuvipuuza vyama kama CHADEMA kwa kuwa wanaona ni vyama kwa ajili ya kuneemesha matumbo yao wao na familia zao .ndio maana hawataki kusikiliza wala kuwaunga mkono kwa chochote kile.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Unatengeneza matatizo, watu wanataabika halafu unaleta suluhisho kwa matatizo uliyoyatengeneza
 
Back
Top Bottom