Paul Makonda Kuunguruma Kwa kishindo cha Simba katika mikoa 20 kuanzia Dar Tarehe 19 January, kusikiliza na Kutatua kero papo kwa papo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,300
9,727
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi,uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Mwamba Mwenyewe wa Siasa Mheshimiwa Paul Makonda ataanza kuunguruma kwa kishindo cha simba katika mikoa ishirini bila Kupoa wala kupumzika. ambapo ziara hizo zitaanza kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dar es salaam nzima Tarehe 19 mwezi huu kabla ya kuendelea mikoani anakosubiliwa kwa hamu kubwa na kiu kubwa mithiri ya watu walio jangwani.

Taarifa hiyo ambayo imetolewa na idara ya uenezi na kusambaa kwa kasi ya mwanga katika mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi Mpaka kule Washington DC Marekani, imeonekana kugusa na kuteka hisia za watu wengi sana ambao wana hamu kubwa sana kufikiwa na Mh Makonda ili kumsikiliza na kumpatia kero zao kutokana na kufahamu utamaduni wake wa kupokea kero na kutoa suluhisho la papo kwa papo.

Paul Makonda ambaye mitaani wanamwita mtetezi na sauti ya wanyonge ameonekana kugusa hisia za wengi sana kwa ratiba yake hiyo ambayo imefurahiwa na wengi sana , kutokana na kila mtu kuwa na kiu ya kuonana naye na kumuona akifika katika mkoa wake . mitaani na katika vijiwe vyote kwa sasa ni Makonda na CCM na namna Rais Samia alivyopanga safu matata yenye watu matata wenye uwezo matata na uchapakazi matata wenye kuleta matokeo chanya na matumaini kwa watanzania wanyonge wanaohitaji msaada wa serikali kuinuliwa kiuchumi.

Wakati haya yanafanywa na CCM Katika kuwafikia watanzania
popote walipo na mahali walipo na kuwasikiliza kero zao na kutatua kero zao zinazowatesa na kuwa kikwazo katika shughuli zao za kila siku. Imekuwa ni tofauti kwa upande wa vyama vya upinzani kama CHADEMA ambavyo vipo Bize kutoa na kuleta mapendekezo ya kirafi,kifisi na yenye kukosa uchungu na maisha ya watanzania kwa kutaka kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo bila kujali kuwa suala hilo litambebesha mzigo wa mateso mtanzania mnyonge .

lakini pia kukomba pesa zote kuwalipa wabunge pesa ambazo zingeweza kutumika kufanyia shughuli za maendeleo kama vile kujenga zahanati au vituo vya afya au shule au barabara au kununua madawa ,vifaa tiba n.k. wao CHADEMA wanataka fedha hizo zitengwe kwa ajili ya matumbo yao wakishaupata ubunge ambao wanataka waongezewe njia kubwa ya kuupata kirahisi.huo ndio ufisi wa CHADEMA na mawazo yao yalipoishia kuwaza matumbo yao tu badala ya maisha ya watanzania wanyonge.

Hii ndio maana watanzania wanaendelea kuwapuuza na kuvipuuza vyama kama CHADEMA kwa kuwa wanaona ni vyama kwa ajili ya kuneemesha matumbo yao wao na familia zao .ndio maana hawataki kusikiliza wala kuwaunga mkono kwa chochote kile.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Kelele za chura....

Awqdanganye watu wake wa kanda ya ziwa.

Wewe Lukas sukari unanunua kilo elf mbili??
 
Kelele za chura....

Awqdanganye watu wake wa kanda ya ziwa.

Wewe Lukas sukari unanunua kilo elf mbili??
Habari za sukari wala hilo lisikupe shida maana mwezi huu Tani Elfu Hamsini zinaingizwa nchini kuja kutatua changamoto ya upungufu wa sukari uliokuwa umejitokeza ,ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa umesababishwa na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha ambazo ziliathiri shughuli za uvunaji wa miwa na hivyo kukwamisha uzalishaji wa sukari viwandani.

Kikubwa kaa kwa kutulia Mheshimiwa Makonda anakuja muda siyo mrefu huko huko uliko atakuja kuwapeni ufafanuzi wa kina na kukata kiu ya maswali yenu yote.
 
20231112_004017.jpg
 
Akawapotezee muda mazombie, tatizo kubwa ni la mgao wa umeme, na Hana uwezo yeye na chama chake kulitatua. Huyo muhalifu apite kusaka kiki kwa wajinga.
Wala usipate presha wewe kaa kwa kutulia unakuja kupewa majibu yote ya changamoto mbalimbali na kilakitu utaelezwa na kuelewa mipango ya serikali katika kumaliza kero mbalimbali ikiwepo hizo ulizotaja za umeme
 
Habari za sukari wala hilo lisikupe shida maana mwezi huu Tani Elfu Hamsini zinaingizwa nchini kuja kutatua changamoto ya upungufu wa sukari uliokuwa umejitokeza ,ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa umesababishwa na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha ambazo ziliathiri shughuli za uvunaji wa miwa na hivyo kukwamisha uzalishaji wa sukari viwandani.

Kikubwa kaa kwa kutulia Mheshimiwa Makonda anakuja muda siyo mrefu huko huko uliko atakuja kuwapeni ufafanuzi wa kina na kukata kiu ya maswali yenu yote.
HIzo mvua linapokuja swala la kujaza Bwawa la Umeme huwa Haliguswi na Maji ila linalokuja swala la Sukari Miwa inapata Athari..

Eeh Mungu tunusuru
 
Hii style ya uandishi umeiiba kwa ERYTHROCYTE, anaweza kukudai hati miliki...😆😆
Acha mzaha ndugu yangu.tangia lini mimi nianze kuandika umbea umbea kama afanyavyo Erythrocyte. Hata hivyo namheshimu maana ni mtani wangu na ni mwana nyanda za juu kusini mwenzangu. Kwa hiyo ni watani kama ilivyo kwa simba na yanga.
 
Wameshawahonga wenzao WA hicho chama chao sasa n kwao kufika na kulala chin wapite juu Yao hovyo Kabisa
 
Mtu aliyewannyima watu HAKI YA KUISHI ndiye Katibu wa Taifa Itikadi na Uenezi wa Chama Tawala yaani CCM.

Roho yangu inaumia sana, ina maana viongozi wa CCM wakiongozwa na Mwenyekoti wa Chama wanatuona Watanzania ni Mazuzu!
 
Back
Top Bottom