Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

Hapa lazima chadema wakimbie hadi vimvuli vyao maana kaja mwamba mwenyewe anayezijuwa siasa za nchi hii na mwenye kujiamini kama komandoo wa vita.
Kumbe wewe mpuuzi kweli Chadema haikumuogopa Magufuli imuogope huyo div zero mwenzako. Unaona sasa tunapokuambia wewe ni takataka tu kwa walioko madarakani na kamwe huwezi kuteuliwa.
 
Niwe mkweli Makonda pamoja na udhaifu wake, mara 100 angerudishwa kuwa RC Dar.
Dar sasa ni:
1. Chafu kuliko wakati wowote
2. Katikati ya Jiji na kariakoo boda wanakera kuliko chovhote ni fujo na sio eneo salama tena.

Bora angerudishwa kule tu
 
Suala la mikono yake kuwa michafu haitaathiri safari yake ? US wana Data zake zote !! Kukatisha uhai wengine ?au sababu yiko chama sio Gov't?.....safari ......
Atajipendekeza ili aonekane ni zaidi ya Chongola; chama ndio inasimamia serikali, hicho ni cheo kikubwa kuliko cha awali. Sasa ataeeza kwenda kokote na kuongea lolote kuliko mwanzo. Mtegemee maandamano kila kona kuunga mkono Dpw, atakaegoma antachongewa ang'olewe.
 
View attachment 2789085

Ndugu Paul Makonda ameteuliwa na CCM kuwa Katibu Mwenezi.

===

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 22 Oktoba, 2023 mjini Dodoma, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Dokta Samia Suluhu Hassan, pamoja na masala mengine, imeridhia kwa kauli moja na kuielekeza Serikali kuendelea na hatua ya utiaji saini mikataba ya uendelezaji na uwekezaji wa bandari.

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kwa kumteua Ndugu Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya Ndugu Sophia Edward Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masala ya Wanawake, Watoto na Makundi Maalum.

Halmashauri Kuu ya CM Taifa pia imemteua Ndugu Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), akichukua nafasi ya Ndugu Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki.

Aidha katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dokta Hussen Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025.

===

Pia soma: Paul Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM!
Garbage in-garbage out!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom