Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda amebainisha kuwa Tundu Lissu ni mjanja ndio maana ameamua kuwakimbia CHADEMA baada ya kuona hakuna haja ya kufanya maandamano yasiyo na tija wala maana yoyote na kuamua kwenda zake Nchini Ivorycoast kuangalia mpira katika mashindano ya AFCON.
Mwenezi Makonda ameyasema hayo leo tarehe 19 Januari, 2024 kwenye Mkutano wa hadhara akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Kawe Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Wananchi hao, Mwenezi Makonda amewataka Watanzania kuwauliza CHADEMA kwanini wanamkimbia kwenye kuitisha mdahalo na badala yake wanaleta masharti na sababu ambazo haziingiliani kwenye mdahalo juu ya kile wanachotaka kukifanya cha kuandamana.
Makonda amesema kuwa CHADEMA wamekuwa wakifanya vikao ambavyo hawatoi mrejesho kwa wanachama wao wala wananchi na tafsiri yake hata maoni yao wanayosema wametoa kwa wananchi si ya wananchi bali ni yao wenyewe Mbowe, Lissu na Mnyika.
Pia, Mwenezi Makonda amewataka tena Mbowe, Lissu na Mnyika kufanya mdahalo wa kuzungumza ilikusudi wananchi kuelewa na kuchagua upande wao kuandaman au kutoandama na kukemea tabia ya Chadema kuwabuluza Wananchi kwa ajenda zao binafsi.
PIA, SOMA:
Uteuzi wa Uenezi wa CCM
Kauli nyingine za Paul Makonda
- Makonda: 2024 na 2025 tutakupima kwa kazi; sio kwa maneno, sio kwa kugawa kanga kipindi cha uchaguzi
- Makonda: Yetote mwenye sifa atasimamia uchaguzi
- Paul Makonda: Tumechoka na ahadi za treni za umeme
- Makonda: Ningeteuliwa kuwa Mwenezi kipindi cha Magufuli wangenyooka hawa
- Sifanyi mikutano ya kujaza watu kwa kutumia wasanii kwasababu tunataka kuona uhai wa CCM na jumuiya zake - Mwenezi Makonda
- Mwenezi Makonda amuagiza Meya na Mkurugenzi Halmshauri ya Pangani kuhakikisha kituo cha afya cha mwenbeni kinajengwa - Pangani
- Mwenezi Makonda ampatia tsh milioni 2 kijana mjasiriamali mwenye kujiendeleza kibiashara
- Makonda: Siasa imemlipa Mbowe kajenga kasri
- Mwenezi Makonda amuagiza Meya na Mkurugenzi Halmshauri ya Pangani kuhakikisha kituo cha afya cha mwenbeni kinajengwa - Pangani
- Makonda ambananisha meneja TANROADS Geita: Ahoji ni lini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kahama - Kakoro (km 60) utasainiwa ili ujenzi kuanza
- Makonda: Mbinguni walimchukulia fomu Rais Samia. Adai Mbowe anajua kama Samia ametumwa na Mungu
- Makonda: Wafanyabiashara huichangia CCM kwa kuogopa wasiletewe TRA, TAKUKURU, uhamiaji ama Polisi
- Makonda: Stendi mpya Iringa ipewe jina la Chongolo