Paul Kagame: An African role model?

Nafikiri kuwa ili kuondoa non-sense zinazoendelea ktk nchi nyingi za Afrika, mtazamo wa Kagame ni sahihi kabisa. Tunahitaji maendeleo, na dikteta ambaye atatusaidia kuyapata hayo maendeleo ni bora kuliko kuendelea kukaa na 'uswahili" usiokwisha na maneno tele bila maendeleo.

Namsifu Kagame kwa kuweza kutumia strength yake ya kupanga mikakati ya kijeshi kuhakikisha Rwanda inaendelea kusonga mbele kimaendeleo tena kwa mkono wa chuma.Hataki kulea rushwa na wapinga maendeleo kwa kigezo cha demokrasia.Mbona hata Putin anafanya hivyo na Rusia imeweza kurudi taratibu pale inapotaka kuwa?

Nchi yetu hii tunapenda wapiga hadithi kuliko watekelezaji sasa tumekwama.Mambo hayaendi.Kila siku sound nyingi bila utekelezaji.

Pengine sijaifahamu vizuri Rwanda, lakini nahisi tuna utajiri mkubwa kuliko wao. Sidhani kama wana mali nyingi tulizonazo kama dhahabu, gas asilia, vito, bandari etc? Mara nyingine ili mambo yaende tunahitaji mtu kama Kagame.Demokrasia inayodhidi kutupeleka kwenye umaskini haitatusaidia mana tutaishia kupigana bila sababu.Imetuzalia ufisadi na rushwa isiyokwisha.

Lakini hata JK ni askari..tumpe muda atumie uzoefu wa kupanga mikakati ya kijeshi kutuletea maendeleo. Tatizo ni mpaka lini tutamsubiri?

Kazi kwelikweli

Hali ya Rwanda ni tofauti sana na watu wanavyoiona kwa nje, na Kagame sio role model kama watu wanavyofikiria. Tatizo la Africa ni kuwa lile suala la kufanya kazi au kuitumikia nchi kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote hakuna. Nyerere tu ndio alikuwa na mtazamo wa namna hiyo. Ukiona kiongozi ana onyesha kuwa mkali na kuonyesha kuwa analinda maslahi ya nchi basi ujue ni kwa ajili ya wachache. Rwanda kuna rushwa nyingi na michezo michafu mingi sana. Ila wanaoruhusiwa kuifanya ni wachache waliokaribu na utawala, na wanaotoka kabila fulani. Wengine hata uhuru wa kufanya maombo yao na kutoa maoni yao hawana. Mchezo mchafu alioufanya DRC Congo na anaoendelea kuufanya ni kielelezo tosha cha jinsi Kagame alivyo.

Bado Kagame hajaweza kuwa role model wa Africa, bado sana.
 
quote=SOPHIST;416972]Nadhani ni muhimu kuelewa kuwa fursa haisubiriwi itokee kutoka kwa akina fulani..,bali hutengenezwa. Dola letu ni chaka la wazembe! Mathalani, fikiria zipo fursa kiasi gani iwapo serikali itaweka sheria ya kutaka kila mikataba yote ya biashara na uwekezaji, ikiwa ni pamoja na nyaraka rasmi \(pamoja na sheria) ziandaliwe/zitafsiriwe kwa ligha ya Kiswahili. Hiyo si fursa tosha Mama?

yawezekana kabisa na ni kweli kuwa fursa haitokei tu ( japo huwa kuna windows of opportunity zinajitokeza japo mara chache na ukishindwa kuziona zikapita ndo imetoka hairudi tena).Tukitegemea sana Serikali kuleta fursa tunaweza tukasubiri sana.Serikali hata ikiweka sheria, utekelezaji wake utakuwa vipi?Sidhani na wala haijawahi kuwa kwamba Sheria ndiyo suluhisho la matatizo.
In the meantime nadhani Watanzania tukubali ukweli kuwa bado hatuko competitive na hii inatokana na uzembe na kubweteka kwetu kama wananchi! Hutegemei serikali kwa kila kitu hata kujifunza lugha! Hata serikali ikatafsiri mikataba na makabrasha yote kwa kiswahili, bado tatizo litabaki pale pale.Kuna sheria nyingi ziko kwa kiswahili ikiwa ni pamoja na Katiba ya Nchi, kwa sababu nina uhakika si wengi wameisoma Katiba ambayo ndiyo sheria mama yenye kubeba pia Haki za Binadamu ( Bill of Rights).Hapa kumekuwepo na mijadala mathalani ya Dhamana, kuwekwa rumande, uhuru wa mawazo, etc.Maswali mengi yameulizwa na nina uhakika kama watu tungekuwa tunajishughulisha kufahamu na kujisomea basi tungekua na uelewa mpana zaidi.[/QUOTE]

Nadhani sikueleweka au kuna tatizo la elimu ya uraia!
Ni kwamba kinachoitwa maendeleo ya Rwanda au kilichokuwa kinaitwa maendeleo ya Tanzania hadi mwishoni mwa miaka ya 80, ni kutokana na jukumu la serikali kutengeneza 'fursa za maendeleo' kwa wananchi. Maendeleo ya nchi hayatokani na juhudi tu za mtu au familia binafsi. Lazima kuwe na central command ya 'sera kuu ya taifa' inayoelekeza mipango yote ya maendeleo. Mifano halisi ni juhudi za sasa za serikali za Ulaya(hasa UK), Amerika (USA) na Mashariki ya mbali (hasa Japan) kuanza kusimamia mipango ya uchumi (siyo kuliachia soko huria kama ilivyokuwa zamani) wa nchi husika.
Nilichomaanisha niliposema mipango ya kutafsiri nyaraka rasmi kwa Kiswahili ni fursa za kazi, kwa maana kila Mtanzania anayejua Kiswahili atajifunza ufundi wa kazi ya kutafsiri. Hivi ndivyo ilivyo kwa nchi nyingi, hususan za Uarabuni, ambapo waendao huko kwa shughuli za kibiashara hulazimika kupata huduma za kulipia (fursa/ajira) kutafsiriwa nyaraka zao kwa Kiarabu ili zikubalike kama nyaraka rasmi. Hii ni kwa mujubu wa sheria na kanuni zao. Sheria na kanuni hizo husimamiwa na serikali zao. Vinginevyo fursa hizo zitapotea. Hili ndilo jukumu ambalo Serikali yetu ya Tz inalikwepa!
Juhudi za mtu mmoja mmoja haziwezi kuweka mitahala, miundombinu ya maji, usafiri wa nchi kavu/anga/majini, usalama na amani, na kadhalika. Ingawa mtu mmoja anaweza kununua gari, ndege, meli elimu na kadhalika.
Pasaka njema.
 
..Kagame siyo role model, ni MUUAJI.

..Kagame,Kabarebe,na Nkunda, wanahusika na mauaji ya wananchi milioni 3 wa DRC.
 
Inategemea kwa wakati huo uko wapi.Wakati kundi linaweza kuonekana ni terrorists na upande mmoja, kundi hilohilo ukiwa upande wa pili linaonekana ni wapigania haki/uhuru.
Likewise bila kuangalia mengine, Kagame anaweza kuonekana role model kwa jinsi anavyoisukuma nchi yake ielekee kwenye maendeleo.
 
WomanofSubstance said:

..kuna mambo fulani ukiyafanya ktk jamii yanaweza ku-overide mazuri yote uliyoyafanya ktk maisha yako.

..mfano: muuza madawa ya kulevya hawezi kuwa role model hata kama atatumia baadhi ya fedha zake kujenga zahanati.

..kwa hali hiyo hiyo Kagame,Kabarebe,na Nkunda, wamehusika na vifo vya wananchi wasio na hatia DRC.

..wako viongozi wa Kiafrika wa kupigiwa mfano kama Maraisi wa Mauritius,Seycheles,Namibia,Botswana, lakini siyo hawa waliotapakaa damu kwenye miili yao kama Kagame.

NB:

..Tanzania tuna eneo kubwa sana na watu wengi, hivyo challenges za uongozi na utawala za Tanzania, ni tofauti kabisa na zile za Rwanda.
 
Nafikiri kuwa ili kuondoa non-sense zinazoendelea ktk nchi nyingi za Afrika, mtazamo wa Kagame ni sahihi kabisa. Tunahitaji maendeleo, na dikteta ambaye atatusaidia kuyapata hayo maendeleo ni bora kuliko kuendelea kukaa na 'uswahili" usiokwisha na maneno tele bila maendeleo.
Namsifu Kagame kwa kuweza kutumia strength yake ya kupanga mikakati ya kijeshi kuhakikisha Rwanda inaendelea kusonga mbele kimaendeleo tena kwa mkono wa chuma.Hataki kulea rushwa na wapinga maendeleo kwa kigezo cha demokrasia.Mbona hata Putin anafanya hivyo na Rusia imeweza kurudi taratibu pale inapotaka kuwa?
Nchi yetu hii tunapenda wapiga hadithi kuliko watekelezaji sasa tumekwama.Mambo hayaendi.Kila siku sound nyingi bila utekelezaji.
Pengine sijaifahamu vizuri Rwanda, lakini nahisi tuna utajiri mkubwa kuliko wao. Sidhani kama wana mali nyingi tulizonazo kama dhahabu, gas asilia, vito, bandari etc? Mara nyingine ili mambo yaende tunahitaji mtu kama Kagame.Demokrasia inayodhidi kutupeleka kwenye umaskini haitatusaidia mana tutaishia kupigana bila sababu.Imetuzalia ufisadi na rushwa isiyokwisha.
Lakini hata JK ni askari..tumpe muda atumie uzoefu wa kupanga mikakati ya kijeshi kutuletea maendeleo. Tatizo ni mpaka lini tutamsubiri?
Kazi kwelikweli

Point taken mkulu. Ila hiyo ya JK nafikiri miaka mitatu aliyokaa madarakani inatosha kutuambia tutegemee nini kwa rais wetu kwa miika 7 ijayo. Ndiyo maana mleta hoja amem-single out Kagame kwa vile hana imani na JK kwa hili. Ndiyo maana nimeamua kukubali kuwa Watanzania Kweli Tumerogwa!!!
 
Nimekuwa nikijaribu kufuatilia habari za huyu mtu anayeitwa Paul Kagame, rais wa Rwanda. Habari nilizopata hivi karibu ni kuwa huyu ndiye rais pekee wa Afrika anayefanya kazi ya kuendeleza nchi kwa mtazamo wa mbali sana. Nimeambiwa anafanya maajabu makubwa sana. Kwamba Rwanda hakuna ufisadi na hata rushwa ndogo ndogo za kijinga zinaelekea ukingoni. Mbali ya hayo jamaa anasisitiza uwajibikaji katika utumishi wa umma. Je, ni kweli anastahili kuwa role model ya viongozi wa Afrika??

Sidhani kama Paul Kagame ni kiongozi ambaye inabidi aangaliwe kama "Role Model" katika masuala ya Utawala Afrika,Ni kweli kwamba ni Kiongozi Mzuri na amenyoosha mambo mengi Rwanda,Lakini pia ni Mtu ambaye si rahisi kukubali ushauri na kwa upande Mwingine ni mtu asiyependa kupingwa hata kama yupo nje ya Mstari,kuna baadhi ya watu Rwanda wanamuona Kagame ni Muuaji!

Ni hivi majuzi,nilipata nafasi ya kuonana na Dr.Dambisa Moyo,ambaye alikuwa katika mkutano wa kutangaza kitabu chake "DEAD AID"(Why Aid is not working and How there is better way for Africa).Katika Mazungumzo yetu nae alimtaja Rais Kagame kama ndiye Rais bora na mwenye wazo la kuindeleza Nchi tofauti na viongozi wengi wa Africa,Nilibishana na Dr.Moyo (mzaliwa/raia wa Zambia) lakini aliniambia takwimu zinaonyesha hivyo.Dr Moyo ni Mchumi katika shirika la Goldman Sachs.Katika mazungumzo yetu aliwataje marais Abdoulaye Wade wa Senegal na Seretse Ian Khama wa Botswana kwamba nao wapo kundi moja na Rais kagame.

Katika kitabu chake "Dead Aid" amezungumzia kwa kirefu ni namna gani ya kuinua Uchumi wa Africa kwa kutumia rasilimali za Africa bila kukodolea macho misaada kutoka ng'ambo ambayo mara nyingi huwa ni short term solution.Ili kujua mengi mtembelee Dada Dambisa Dead Aid: Why Aid is Not Working and How There is a Better Way for Africa na utaelewa mengi mazuri kuhusu Rais Paul Kagame.
 
..kuna mambo fulani ukiyafanya ktk jamii yanaweza ku-overide mazuri yote uliyoyafanya ktk maisha yako.

..mfano: muuza madawa ya kulevya hawezi kuwa role model hata kama atatumia baadhi ya fedha zake kujenga zahanati.

..kwa hali hiyo hiyo Kagame,Kabarebe,na Nkunda, wamehusika na vifo vya wananchi wasio na hatia DRC.

..wako viongozi wa Kiafrika wa kupigiwa mfano kama Maraisi wa Mauritius,Seycheles,Namibia,Botswana, lakini siyo hawa waliotapakaa damu kwenye miili yao kama Kagame.

NB:

..Tanzania tuna eneo kubwa sana na watu wengi, hivyo challenges za uongozi na utawala za Tanzania, ni tofauti kabisa na zile za Rwanda.

Sasa unataka kusema sababu za kushindwa kwetu challenges blah blah blah...??? CCM wanafurahi kweli wakisikia haya..............!!!

Tukabali tusikubali Kagame anafanya kazi na ana vision kuliko viongozi wetu wabinafsi. Sasa wewe unataka kusema mtu mtumia madawa, akiuwa hawezi kwenda mbinguni hata kama akitubu na kuongoka (kama tuaminivyo sis wenye dini)?? Anyway, mwezetu ulitaka wahutu wawamalize watutsi?? Hiyo Namibia imekombolewa kwa kumwaga damu sasa sijui hao akina Nuyoma na Pohamba nao wako kwenye nafasi gani???
 
Kagame is an agent of change, and is taking his country towards development.

Tanzania does NOT have such an agent. JK is no where near to one.
 
Ameua Opposition na Civil Society!

Kuna a lot of resentment over him!

Anaongoza kwa 'Either on our way or or against us!

Wengi wana hofu kubwa..sema hakuna anayedhubutu kuongea!

May be tunahitaji mtu kama huu Tz!

Yes sir,

kama anaongoza vizuri,, ana mipango mizuri, then this is kind of man that is needed in Tz. asiwe dictator kama amin, but awe ana kaudictator ka kichina!

Rostam, EL,Chenge wangekuwa wameshanyongwa tungekuwa tunajadili mambo mapya, kwenye internet though!
 
....Kagame hataki mchezo,hapendi rushwa na anapenda maendeleo sana,waliofika Kigali wanajua jinsi mji ulivyo clean,safe & most green na kila kitu kiko orderly,utashangaa kuna Drs na Profs watanzania wamejaa kwenye Rwandans universities kuliko Tanzania,huko ukiwa unatoka East Africa Kagame anakupa kazi na free work permit,police Rwanda wanaheshimu raia kuliko wanavyoheshimu bosses wao
 
Zero said:
Sasa unataka kusema sababu za kushindwa kwetu challenges blah blah blah...??? CCM wanafurahi kweli wakisikia haya..............!!!

Tukabali tusikubali Kagame anafanya kazi na ana vision kuliko viongozi wetu wabinafsi. Sasa wewe unataka kusema mtu mtumia madawa, akiuwa hawezi kwenda mbinguni hata kama akitubu na kuongoka (kama tuaminivyo sis wenye dini)?? Anyway, mwezetu ulitaka wahutu wawamalize watutsi?? Hiyo Namibia imekombolewa kwa kumwaga damu sasa sijui hao akina Nuyoma na Pohamba nao wako kwenye nafasi gani???

Zero,

..kuna nchi ambazo tunashabihiana nazo kidogo kwa ukubwa wa eneo na idadi ya watu. Ghana na Mozambique ni kati ya nchi hizo.

..sikuwa na nia ya kuwapa CCM visingizio vya kushindwa kazi. FRELIMO, ambao wamelelewa na Tanu na CCM, wameweza kurekebisha uchumi wao kwa haraka sana baada ya kuhujumiwa na Makaburu na vibaraka wao wa Renamo. sasa kwanini CCM wameshindwa pamoja na amani na rasilimali zote tulizonazo?

..Mauritius na Seychelles wanalingana lingana na Rwanda. viongozi wao wameweza kuinua uchumi na hali ya maisha ya wananchi wao, tena hawana rekodi chafu za mauaji kama aliyonayo Kagame. kwanini tusiwakubali hao kama role models, badala yake tunamng'ang'ania muuaji-nduli-Kagame??

NB:

..kwani Kagame ametubu kuhusu kuhusika kwake na vifo vya wa-Congo zaidi ya milioni 3?

..kama ametubu na ameokoka basi ni vizuri "akapumzishwa" kwenye selo ya wauaji wanaofanana naye kama Charles Taylor, General Mosquito wa Sierra Leone, wakati akisubiri safari yake kuelekea "akhera."

..kuna tofauti kubwa sana kati ya vita vya ukombozi wa Namibia na mauaji ya kinyama ya wananchi wa Congo yaliyofanywa na vikosi vya jeshi la Kagame.
 
..nimeangalia data za USAID Tanzania imeizidi Rwanda kwenye per capita income, literacy rate,primary school enrolment, life expectancy, na pia infant mortality rate zetu ni ndogo kuliko za Rwanda.

..ningekuwa na muda ningeangalia data za mashirika kama UNDP,WHO,UNICEF,na FAO.

..pia ningependa kujua tangu Kagame aingie madarakani amejenga barabara za lami za urefu gani, shule za sekondari ngapi, vyuo vya ufundi, vyuo vikuu, hospitali za rufaa, etc etc.

..budget yake inategemea wafadhili kwa kiwango gani? pia amekuwa akikiteremsha kiwango hicho kila mwaka kwa kiasi gani.
 
Sasa sisi tanzania tumvamie nani na to plunder dhahabu za nani?

Maendeleo ya rwanda yanayozungumziwa hapa yamekuja kwa cost gani na ya aina gani? au ndio
masuala ya " the end justifies the means"?

Inawezekana kagame kafanya mazuri kwa nchi yake lakini hili la kuwa role model sidhani kama ni sawa.
 
zero,

..kuna nchi ambazo tunashabihiana nazo kidogo kwa ukubwa wa eneo na idadi ya watu. Ghana na mozambique ni kati ya nchi hizo.

..sikuwa na nia ya kuwapa ccm visingizio vya kushindwa kazi. Frelimo, ambao wamelelewa na tanu na ccm, wameweza kurekebisha uchumi wao kwa haraka sana baada ya kuhujumiwa na makaburu na vibaraka wao wa renamo. Sasa kwanini ccm wameshindwa pamoja na amani na rasilimali zote tulizonazo?

..mauritius na seychelles wanalingana lingana na rwanda. Viongozi wao wameweza kuinua uchumi na hali ya maisha ya wananchi wao, tena hawana rekodi chafu za mauaji kama aliyonayo kagame. Kwanini tusiwakubali hao kama role models, badala yake tunamng'ang'ania muuaji-nduli-kagame??

Nb:

..kwani kagame ametubu kuhusu kuhusika kwake na vifo vya wa-congo zaidi ya milioni 3?

..kama ametubu na ameokoka basi ni vizuri "akapumzishwa" kwenye selo ya wauaji wanaofanana naye kama charles taylor, general mosquito wa sierra leone, wakati akisubiri safari yake kuelekea "akhera."

..kuna tofauti kubwa sana kati ya vita vya ukombozi wa namibia na mauaji ya kinyama ya wananchi wa congo yaliyofanywa na vikosi vya jeshi la kagame.

....hater!
 
Kagame ni Criminal au War Criminal kama walivyo viongozi wengine wengi watumiao damu nyingi za watu kukidhi wafikiriavyo au mitazamo yao kisiasa, kiuchumi, kidini au hata kikabila. kwangu binafsi sikuzote nitamwona kama viongozi wauwaji wengine ambao weshawahi kuongoza nchi au vikundi vya watu kwa vitusho na kumwaga damu kupita kiasi.
Watu wa aina hii ni wazuri pale tu fikra zenu zinapokubaliana au unapokubali kuwa mtu wa ...."...ndiyo bwana..." Ukibadilisha tu mtazamo wako au ukitofautiana nao kimtazamo ujuwe ndo utaiga dunia..nothing more nothing less. Au pia uwe wa kabila lao au dini yao, ukitofautina nao basi ujuwe utamalizwa.

Nakubali kuwa anawaiba watu ambao siye tulidhania ni watanzania wenzetu siku zote kumbe wao walikuja kuchuma nchini Tz, sasa mtu wa kabila lao yu madarakani basi wanaamua kurudi kwao, hawa hawakuwa watanzania asilani bali walikuwa wazamiaji tu, kama vile leo au kesho mtanzania halisi anavyozamia uswazi, botswana, canada, UK au USA na kuchukua pasipoti ya huko, huyu siku zote atakuwa Mtz tu! na Tz itakapochanganya yeye atarudi tu!, roho yake siku zote inatazama Tz kama promised land yake!
 
Kwa Statistics za BBC Tz tuko bora zaidi ya Rwanda!

Full name: Republic of Rwanda
Population: 10 million (UN, 2008)
Capital: Kigali
Area: 26,338 sq km (10,169 sq miles)
Major languages: Kinyarwanda (official), French (official), English (official), Swahili
Major religions: Christianity, indigenous beliefs
Life expectancy: 45 years (men), 48 years (women) (UN)
Monetary unit: 1 Rwandan franc = 100 centimes
Main exports: Coffee, tea, hides, tin ore
GNI per capita: US $320 (World Bank, 2007)

Full name: United Republic of Tanzania
Population: 41.5 million (UN, 2008)
Capital: Dodoma (official), Dar es Salaam (commercial)
Largest city: Dar es Salaam
Area: 945,087 sq km (364,900 sq miles)
Major languages: English, Swahili
Major religions: Christianity, Islam
Life expectancy: 51 years (men), 54 years (women) (UN)
Monetary unit: 1 Tanzanian shilling = 100 cents
Main exports: Sisal, cloves, coffee, cotton, cashew nuts, minerals, tobacco
GNI per capita: US $400 (World Bank, 2007)
 
All,

Tujifunze mazuri ya Kagame mabaya yake tuyaache.

Kagame so far ame prove kuwa kiongozi mwenye vision Africa yetu ya leo. Hivi wanaomponda Kagame? Are you real au basi ni zile stereo type tumeshajazwa kichwani kwamba jamaa ni mtusi sijui muhutu? Nenda Kigali uangalie uone...The guy is matching and seriously matching! Wakati wengine wamelala.. Sisi si tunakumbatia akina Lowassa na Karamagi? You cant do that nonsense in Rwanda....The best is to ask him..how did he do it?

Hivi mnakumbuka tulipokuwa shule za sekondari? It was possible mtu kukuchukia kwa sababu wewe unasoma usiku yeye kalala! Ndo linalotokea hapa..the guy is matching,..tunaanza kumtafutia sababu za human rights ohh sijui nini.... The fact is Tanzania we should be ashamed! We are poor. The best we can do is to reinvent ourselves tufanye kazi tuache longo longo...za kuhate wanaojikwamua..au mnataka wote tubaki hapa hapa kwenye marktime ya umasikini?......

Harafu Jokaa Kuu ni aibu..aibu..kubwa......kwa Tanzania nchi kubwa kama sisi kuanza kujicompare na nchi kama Rwanda! Nchi ndogo kuliko zote..imetoka kwenye Genocide ambapo raia zaidi ya million walikufa..nguvu kazi yote ilipotea.....leo Tanzania (more than 40M heads!) unajilinganisha naye eti..tunamzidi? huoni kwamba tuna tatizo somewhere? Ni kama libaba la miaka 50 au 60..lianze kushindana na mtoto wa miaka 20..kisa wote ni graduates... TANZANIA HAS NEVER HAD A WAR WALA UKABILA so we say......Kagame aliichukua nchi ikiwa katika hali mbaya sana..wasomi watakwambia kwamba it was not worthy the name of the state itself...leo tunadiriki kumbeza Kagame? Of all countries..TANZANIA?? Give me a break! Tuache wivu..tukubali kwamba jamaa anafanya kazi na anajua analolifanya kuliko viongozi wetu! ITS SAD BUT TRUE..

Kwamba aliua Congo..that is a contested matter...hatujawahi kupata independent report kwa watu wasio biased..kama unaiamini UN..si wote..ni hiyo hiyo UN iliyokimbia ikaacha watu wanachinjwa..harafu leo wanapata courage ya kuwanyoshea vidole watu? Congo is just a sickman of Africa...hawawezi kujitawala...mara mia wamrudishe mbeligiji awatawale..(perhaps even we could think the same)...

Hivi wewe jiulize..raia million moja TANZANIA wafe (GOD FORBID)..Na huu ufisadi si tutarudi kwenye stone age? maana akina Rostam wataiba hata chakula cha msaada!

All, mwacheni Kagame..haters watazidi kukimbilia hizi minimalist approach oohh..human rights...ohh democrasia..ohh sijui nini...kwa hiyo TANZANIA tuna demokrasia zaidi ya Rwanda? Zanzibar wanaochaguliwa viongozi wana democrasia kuliko Rwanda? Kwa hiyo Putin ni democrat zaid ya Rwanda? Kwa hiyo Belarus ni democrat kuliko Rwanda? Tuache mawazo mufilisi..tumuangalie Kagame..kafanya nini kupambana na ufisadi na kuwainua watu wake..tuchukue mawaidha..yale ambayo hayatufai tumuachie..kila mtu ana matatizo yake! so is Kagame..Hata yeye ana matatizo yake..like any other developing country..but he doing fine and he will succeed.

Inanikumbusha ya Obama...he isnt black enough..Lol!
 
Back
Top Bottom