Paul Chizzi amuumbua Mwakyembe

Namjua Dr Mwakyembe;ni
Mbunge wangu!Watz tujiandae kumlipa Chizi mamilion ya pesa akienda
mahakamani;Dr Mwakyembe ni mtu wa kupenda sifa zisizo na msingi!Yeye na
Magufuli hamna aliyemzidi mwenzake!

Kusitishwa kwa ajira ya mtu kuna utaratibu wake inabidi ufuatwe na sio
kuwaita waandishi wa habari na kutangaza fulani nimemfukuza kazi!Kwa
ufupi Dr Mwakyembe ni abuser mkubwa wa haki za binadam!

Kyela 2015 tumekwisha mkataa na analijua hilo!

Lkn Chizi, chizi kweli! Si alishastaafu 2002 hilo mbona hasemi? Anang'ang'ania nini! Wasomi wengi tu hawana kazi! Pumb..v.u zake...
Kweli Mwakyembe mnafiki kwani ndie alie mlea rais mbovu tulie nae kwa kumfichia udhaifu wa ktk richmond skendo...lkn chizi pia hafai kabisa.
 
kwani hizo dola 18,000 ni kidogo? wakati shirika halina hata ndege moja? Tusiwaonee haya wahalifu kama hawa ni hatari kwa nchi yetu

Hivi wewe ulitaka wavae magunia ndio uone raha? Hiyo ni ndege inayowakilisha utaifa wetu. Hivyo, uniform za watumishi wake zinatakiwa kuwa zenye hadhi hiyo. Piga hesabu rahisi, watumishi 20 wa ndege wakipewa pair tatu za uniform ni nguo 60. Hapo unapata dola 300 kwa nguo. Mbona Mlimani City akina mama wananunua nguo za zaidi ya Dola 500 ambazo hata hazifanani na zile walizonunuliwa watumishi wa ATCL? Naona una lako jambo na Chizi. Kaa kimya mwanafyale huna sera.
 
Sijasoma yote nitasoma baadaye lakini huu ni wizi na uhuni. Amekansha nini sasa hapo kihusu uniform? Anasema hela zingine zilitumika kununua other materials; yapi? Uhuni tu. Hivi angekuwa mbunifu si angewapa wanamitimdo wetu washone nguo zinazofanana fanana na Tanzania badala ya kukimbilia China. Ati CEO hivyo ana mandate; mandate y wizi?

Amesema wabunifu wa ndani walikuwa gharama zaidi. Na ukisoma gazeti limesema kabisa bei ya uniform moja ni dollar 200-600. Mbona watu tunamkubalia Mwakyembe moja kwa moja bila ushahidi halafu maelezo ya Bwana Chizi hatuyakubali?
 
kama mtu anaonekana mbadhilifu si ashitakiwe,tuondoleeni hapa nyinyiemu longolongo.com
 
Kumbe uniform 2 mpaka china,kwan hzo uniform zinakua na mwanvul ya kusaidia ispate ajali?serikal yenyewe bomu mda wowote linalpuka,ww unajua m2 anaitwa chiz hta kma n timamu lazma kuna cku zinaruka.
 
Kumbe uniform 2 mpaka china,kwan hzo uniform zinakua na mwanvul ya kusaidia ispate ajali?serikal yenyewe bomu mda wowote linalpuka,ww unajua m2 anaitwa chiz hta kma n timamu lazma kuna cku zinaruka.Ona thatha sare 2 chna,ataagiza na kahawa kwa ajir ya abiria dubai.
 
Aliyekuwa mtendaji mkuu wa ATCL ameibuka na kusema kwamba Dr Mwakyembe alidanganya umma kutokana taarifa alizopewa kuwa ni za uongo na zisizokuwa na ukweli wowote.

Kwa mfano uniform ziligharimu dola 18,000 tu na sio dola 50,000 kama alivyosema mwakiembe, Bwana Chizi alisema pia tatizo ni kwamba kuna watu hawajui chochote kuhusu sekta ya anga lakini wanajidanganya kuwa wanajua mbele ya umma.

Chanzo: The Guardian on Sunday


...Njia rahisi ya kujisafisha weke Payment Receipts with detailed breakdown......don't be like layman
 
Kama anasema $18k za uniform na zingine material zingine basi total inaweza kuja kwenye aliyosema Mwakyembe. Kwanza kama Chizi anajitetea basi angesema na hizo materials zingine ni zipi na walitumia how much.

Anataka kujisafisha kwangu mimi bado hajanifanya nimuamini. Mwakyembe lazima amepewa paperwork walizozipangaga sasa analalamika nini?

Nahisi anajisafisha kutafuta cheo kingine.

Ila jamani ndege moja, $18k. Labda pia kuna wafanyakazi bubu.
 
Si ajabu anaitwa chizi....utatumiaje dola 18,000 kushona nguo ambazo zaweza shonwa kwa batiki za hapa hapa na hata Millioni 2 isifike.....

na kwanza huzo nguo za bei yote hiyo zilikuwa zinatumika wapi maana hawakuwa na ndege kwa kuda mrefu sana
 
jiandaeni kulipa bil zingine na fidia juu kwa hawa madirector.......hivi zile za dowans bil 94 mlishalipa ee!!....
 
Napata shida sana Kutamka Jina na huyu Mkurugenzi aliyefukuzwa, Nashindwa pia kushangaa hata aliye mpa hiyo nafasi ndiyo maana hata haliyoyafanya sishangai sana coz jina lake speeks more Than words......
 
Kama aliyekanusha ana ushahidi basi Mwakyembe shule haijamsaidia au nitaamini kuwa hata ukiwa msomi na intergrity yako ukiingia CCM unakuwa juha .

Mkuu Chizi ni Chizi tu, lakini ni vizuri tukumbuke pia kuwa hakuna shule au chuo kinachoelimisha watu kuwa na busara, shule huwa wanafundisha nadharia tu. Ndio maana mtu asiye na elimu anaweza kuwa na busara na mwenye elimu anaweza kutokuwa na busara. Kwa hiyo ni vitu viwili tofauti, kama maji na mafuta.
 
aiseee huyu kweli chizi.....kwa hiyo $18K anaona sawa kabisa kushona nguo za watu 15??
 
Ndugu yangu ukishangaa ya Musa ya Firauni itakuwaje? Wadanganyika nawaogopa sana tena sana wengi wetu tunajiita tumesoma ila wengi sana wamefika hapo walipo kwa sababu ya madesa hawana weledi wowote ule ndani mwao. Wapo watu humu wanajiona wenye uwezo wa kufikiri lakini kamwe sivyo walivyo. Mashirika yetu yanakufa kwa sababu ya watu kama waliopo humu JF. Mwangalie mtu aliyepewa madaraka na kupewwa heshima ya kusimamia nchi yote ya Tanzania ndugu JK alivyo hajui umasikini wa Watanzania. Je wana Jamii humu wanajua umasikini wetu umetokana na nini? Wengi humu ni wezi tu watu wa misheni Town ndio maana kamwe hawezi kutuonea huruma wakulima na wafanyakazi wa kima cha chini. Yote hii inatokana na kuwa CCM imewalea sana baba zao na sasa kizazi chao na wengine wengi wanatamani waingie kwenye mfumo ili wazidi kuiibia Tanzania yetu.
Ndiyo maana nimewafurahia sana Watu wa Jamhuri ya Zanzibar wamechoka kutokana ukazuzu huu wa watu wa Tanganyika wa kulinda wezi.
Humu JF tumevamiwa na majuha, ni nani asiyejua ubadhirifu unaofanyika katika sekta ya umma? kitu chaweza kuwa dola 200 lakini kikaandikiwa invoice ya dola 2500 bila aibu, kuna sehemu kwa sekta ya umma mwanzoni mwa mwaka 2000 nilikutana na invoice amboya one of the price ya RJ45 iliwekwa dola 250. Sasa kama unashangaa alichosema Mwakiyembe basi fuatilia hata bajeti zetu uone wanatenga mamilioni mangapi kwa chai na entertainment na kila mwaka hela za fenicha, Chizi mwizi na Mwakiyembe nae mwizi tu, maana mwizi afukuzwi kazi tu na ashitakiwe na kufilisiwa, mshatuona WATZ mabwege sanaaa. Mnakera
 
Chizi anapoongelea bei iliyotumika kununulia uniforms pekee anachanganya mambo, sisi tunajali gharama iliyotumika ktk hizo uniforms, including usafiri, na hizo "other materials" anazodai; pamoja na kujitetea lakini bado inaonyesha pesa ililiwa tu! Hata kama waziri amesikia tetesi na akachukua hatua kwangu mimi ninaona ni vizuri kuliko angesubiri uchunguzi ambao ungeendeshwa na Chizi akiwa ofisini na kuchukua muda zaidi ya mwaka na kutoa ripoti (pengine ya kumuosha Chizi),kwa kuwa cheo hicho hakina hati miliki ya Chizi na wapo wengine wanaoweza kufanya kazi hiyo ni muhimu Chizi kupisha!!!
 
“Administrative matters are quite different from those of a technical or executive nature. There is no way a chief executive could seek approval from the parent ministry about every single matter. “The leasing of an aircraft is a technical matter. What isimportant is to inform them (minister), for if you act the way the ministry wants you to, you might end up doing entirely nothing because they do not respond to letters in time on the pretext of attending a series of endless meetings,” he said..

Kwa hili nimemkubali Chizi!
 
Back
Top Bottom