Paschal Mayala atoa Ushauri wa bure kwa wana JF

Tofauti ya kimaendeleo kati yetu Sisi v/s China, Singapore au Malaysia za miaka hiyo ya sitini.
Na tofauti yetu kwa miaka hii ya sasa ikoje?
Miaka hiyo tulikua wote sawa au tuliachana kidogo tu, sasa ikoje?
Wao walikua na nini kutuzidi?
Ukijiuliza hili swali ndio utathubutu kusema tanaendelea?? Au lah!!!!
ni kweli tunahitaji kua na shule ambazo wanafunzi wanakosa madawati na kukaa chini katika karne hii??

Shark umesema vizuri lakini akili za watu kama Paschal siyo rahisi kukuelewa.
 
Sasa kama Tz inakuwa ranked sawa na Iraq na Afughanistani kwa kuomba omba bado unadiriki kusema tumesonga mbele?
CCM wameua viwanda,wameua ATC,unemployment rate iko juu,madini yanachimbwa kwa wingi faida hatuioni.
Mayala tupe mchanganuo wa hayo wanayosema tumesonga mbele tukupe facts za kujustify criticisms
 
Huyu Pascal anatakiwa atambue watu wanapinga nini. Hatua zilizopigwa zinaendena na rasilimali/uwezo wa nchi yetu? Kwa nini hatuna reli ya uhakika? Kwa nini huduma za afya na sasa wakubwa wameamua kukimbilia India? Tanzania tulipata uhuru pamoja na nchi kama za Malaysia na Singapore. Na hizi nchi (zote kwa pamoja) hawana natural resources hata nusu ya Tanzania. Leo hii Malaysia na Singapore wako wapi?

Pascal anaongelea barabara? Aende Kuala Lumpur halafu alinganishe na Dar es Salaam! Pascal akaangalie vyuo vikuu vya Malaysia. Ni vizuri Pascal aelewe nini hasa kiini cha watu kulalamika.
 
Baada ya miaka 50, nchi ya tatu duniani kwa kupewa misaada, tumepitwa kimaendeleo na hata nchi ya 'Vanuatu' !!?
 
Asante mtoa mada, asante Mayala, ni kweli member wenzangu humu wengi wao ni kupinga tu, matusi tu, bila ya kupima na kujenga hoja ya hali halisi
Acha utani.Hali halisi ni ngumu sana.Binafsi nimelima kwa jembe la mkono.Mbolea nitaishia kuisiki kwa wenzangu.Mfuko 1 ni 65000.vp hapo?njoo huku uswahilini uone jins watu wanavyokula mlo 1.
 
Mwacheni Pascal ajineemeshe na vitumbua anavyopewa Tatizo ukiwa kilaza Mjini na unataka kuishi Sifia uchafu wa CCM basi utaishi fresh Pascal Kaza Buti Kuna nafasi za wakuu wa wailaya nyingi tena wale wanaozishikilia kwa kukaimu wameshatangaza kuchoka.

Mkuu wa walaya ya Kinondoni anakaimu Ilala na Temeke. Jana Nilikusikia japo Ulinipa Kichefu chefu kama Uttoh
 
Kituko zaidi tangu mwezi June kunafanyika maonesho ya kila idara za serikali kuonesha maendeleo yaliofikiwa baada ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, je hivi ni maendeleo gani yasioonekana kwa macho mpaka yafanyiwe maonesho?
Cha kusikitisha mambo haya yanafanywa na watu wazima wenye akili zao timamu ambao Watanganyika wanaamini ndio walipaswa kuonesha dira.
 
Yeye mwenyewe alivyopata ajali,alikwenda india kutibiwa.KUNGEKUWA NA Maendeleo si angeendelea kutibiwa Muhimbili,Pasco bwana.
 
kinachotumaliza ni UFISADI na POSHO otherwise tungekuwa mbali sana

Haya munayoita maendeleo ukilingasha na umri [miaka 50] wa nchi, rasilimali zilizipo haviendani ndiyo maana tunasema hakuna maendeleo

ni kweli!kwa kweli hakuna uwiano wa eti maendeleo yetu leo ukulinganisha na umri huo wa miaka50 ni kujidanganya changamoto ni nyingi mno kuliko tunavyosheherekéa
 
wala ushauri wake hautuhusu,kumbe tunafyopiga kelele humu jamvini inawauma sana na bado hatutakaa kimya ndio wataendelea kutuibia wananchi lakini wataiba kwa mateso ya nafsi kama ilivyo sasa.
Wanaweza kutaja km za barabara na vyuo lakini maendeleo hata kama yapo hayaendani na miaka 50.maendeleo yaliopo ni ya miaka 10 ya uhuru,hilo lazima wakubari hata kama watasifia upumbavu ili mradi tu wapate ugali wa watoto wao na mademu zao
 
Ahaa nimeshaelewa maendeleo wanayoyazungumzia. Ni kweli Tz tumepiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Nyie mnadhani ni mchezo nchi kuwa miongoni mwa "best three ombaombaring countries". Jk endelea kutuletea maendeleo zaidi kwa kuongeza safari za nje za kuomba misaada ili tuwe na maendeleo zaidi.
 
Hata mimi nataka kujua anatumia ID gani maana huwa namkubali sana huyu jamaa

Ahsante DA,
Ukweli baada ya hii mada na maelezo kwamba ni Member Mwebzetu nimevutiwa sana kuangalia michango mengine ya huyu Paschal Mayala ili nimjue ni mtu wa aina gani.
Public Figure kama yeye kuongea utumbo kama ule "publically" inanipa mashaka na hawa wanahabari wetu tulio nao.
Dena, Inakua vigumu kumtenganisha Paschal na Takrima!!!
Paschali Mayala as our fellow member, unajiteteaje katika hili??
 
Sasa kama Tz inakuwa ranked sawa na Iraq na Afughanistani kwa kuomba omba bado unadiriki kusema tumesonga mbele?
CCM wameua viwanda,wameua ATC,unemployment rate iko juu,madini yanachimbwa kwa wingi faida hatuioni.
Mayala tupe mchanganuo wa hayo wanayosema tumesonga mbele tukupe facts za kujustify criticisms

Tunasonga mbele sawa kwa maana ya kwamba tulikua 1 na sasa tupo 4,
Lakini je kwa miaka yote hii ni hii 4 tu ndio tulitakiwa kuwepo??
Singapore na Malaysia tuliokua nao 1 miaka hiyo kwa sasa wako 30, sisi tukiwemo na kina Paschal Mayala bado tunafurahia kabisa kuwepo kwenye hii 4 yetu!!!
 
Kwanini yasemwe mazuri tu, na mabaya yaachwe, nyie hamnazo kweli. Bila kuyataja mabaya na kuyakemea nchi itawezaje kukabiliana na changamoto? Mmezoea kusifiwa ujinga tu, zama hizo zimepita. Ukweli ni lazima usemwe ili watu wajisahihishe.
 
Back
Top Bottom